Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,658
- 4,866
Mtoto wa kiume kiongozi wa kundi la Hamas anayeitwa Mosab Hassan Youssef, amekuja wazi na kuonesha kutopendezwa na mienendo ya Kundi la Hamas, kitu ambacho kilipelekea kubadili dini na kuwa Mkristo na sasa anaishi kwa Amani. Mosab Hassan Youssef aliandaliwa kuwa kiongozi atakayerithi uongozi wa baba yake ila yeye akaamua kuachana na hayo mambo na kuwa Mkristo na badae kujikita kuandika vitabu mbalimbali ikiwemo kinachohusu kundi la Hamas, ikumbukwe kundi la Hamas linapigania kuchukua Palestina na kuifanya kuwa Nchi itakayoongozwa kwa misingi ya dini ya kiislam. Amesikika akisema
"HAMAS hawajali maisha ya wapalestina wala waisraeli au wamarekani, na hawajali maisha yao binafsi. Wanachojali ni kufa kwa ajili ya mitazamo yao na jinsi wanavyoabudu. Utaendelea vipi katika jamii ya namna hiyo?"
Aliongezea tena baada ya kuulizwa tena na mwandishi kuwa je utaweza kukaa sehemu moja na mtu anayetaka kumuangamiza; akajibu,
"Hamas hawataki kushirikiana kwa kuwa pamoja, wala mashauriano. Hamas wanachotafuta ni kupiga na kushinda, wanataka wao ndio wawe washindi kila mahali. Hata hivyo Hamas kuishambulia na kuipiga Israel sio lengo lao kuu la mwisho, lengo kuu la HAMAS ni kujenga utawala wa serikali ya kiislamu (Islamic Khilafah), kwa maana ya kuwa nchi nzima iwe ya kiislamu, na raia wote wawe chini ya dini ya kiislam. Hili ndilo lengo kuu la harakati zao"
Mtangazaji akauliza tena, Mosab kwenye kitabu chako umeelezea kuwa Hamas shabaha yao kuu ni kuwalenga Raia na kuwatumia kama dhana ya vita, tuambie Hamas unayoifahamu wewe toka ukiwa mdogo hadi unakuwa mkubwa huko West Bank;
Mosab akajibu "Ndani ya misikiti, Hamas walitufundisha bila kumwaga damu za wasio kuwa na hatia juu ya mitazamo yetu, tunataka kuwa na uwezo wa kutengeneza taifa litakalo kuwa chini ya uislamu. Na tulikuwa tunaandaliwa kabisa tukiwa wadogo sana, tukiwa na umri kuanzia miaka 5. Na haya ndio yalikuwa malengo yao ambayo walikuwa wakitulisha tukiwa wadogo. Na kiukweli ilikuwa ngumu au haiwezekani kwa mtu yeyote kutoboa na kuona ukweli juu ya nyuso za Hamas zisizokuwa za kweli, na kuweza kuachana nao kwa namna fulani. Na kama mnavyoona kwenye kesi yangu ilinibidi nipoteze kila kitu kwa ajili tu ya kuwakataa Hamas. Na leo nikiwatazama watoto wa Gaza, na ninajua nini wanalishwa, na ninajua hawana machaguo.
Hayo yalikuwa ni mahojiano yaliyofanyika na chombo cha habari za CNN dhidi ya Mosab Hassan Youssef. Tazama mahojiano hapo chini.