Israel yashukiwa kufanya mazungumzo na kiongozi wa Doghmush clan, Hamas yaua kiongozi wao

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,805
1,873
Hamas yavamia kikundi chenye msimamo mkali Doghumosh Clan Gaza city (13/3.2024) na kuua idadi kadhaa ya wapiganaji wao akiwemo kiongozi wao. Hamas walichukua hatua hii baada ya kikundi hicho kushutumiwa kuwa na mazungumzo na Israel. Hamas imeshawahi kuonya kuwa kikundi au mtu yeyote ndani ya Palestina atayeshirikiana na Israel atashughulikiwa.

Mpango wa afisa Usalama wa Israel "Shin Bet" ni kufanya mazungumzo na vikundi mbali mbali ndani ya Gaza, ili baada ya vita(kuitokomeza Hamas) kuigawanya Gaza na kuvipa vikundi hivyo jukumu la Usalama katika maeneo husika. Katika mpango huu Doghumush clan inatarajiwa kupewa Gaza kaskazini na kufanya kazi chini ya Israel.

Kikundi hiki kiitwacho "Army of Islam" ni kikundi shirikishi ndani/chini ya mwavuli wa Al-Qaida.

My take: Hapa Israel inaruka Mko...o na kukanyaga Mav. Eti unamkataa Hamas na unakwenda kumkumbatia Al-Qaida. Mwaka huu Israel imechanganyikiwa!

Chanzo: https://www.timesofisrael.com/hamas
 
Israel amechanganyikiwa wakati makobaz yametapakaa Gaza nzima mzee kuwa serious. Waoneeni wale watoto huruma aisee.
 
Gharama ya kutafuta uhuru ni kubwa. Wangoni laki 3 waliuawa wakipigana na Wajerumani mwaka 1905. Population ya Wangani wakati huo haikufika hata milioni 2.

Leo wewe unakaa, uko huru na kuandika bila kujua kuwa safari ya kusaka uhuru ilianzia huko. Afghanistani zaidi ya miaka 30 wakipigana na kuusaka uhuru, bila kujali idadi ya watu waliokufa katika vita. Niishie hapo bila kutaja Vietnam, na wahindi wekundu waliomalizwa huko Marekani.

Safari ya Gaza ni kupata nchi inayoitwa Palestina, hawana uchaguzi mwingine.
 
Hizo taarifa ni za uongo kabisa na hazina ushahidi wowote. Acheni kuleta habari za kuchuuza kutoka kwenye majengo yenu ya ibada maarufu kama "masjid" na kuzisambaza humu kwa lengo la upotoshaji.
Usiwe mvivu wa kusoma, chanzo nimekupa toka kwa Wa Israel wenyewe. Msikiti unahusika vipi hapa?
 
Kumbe wewe huijui Israel! Israel ina maajenti wake ndani ya Hamas,Hezibollar,al queda,karibu kila nchi.
Kwa hiyo inachofanya ni kuisambaratisha Hamas kwa kuigawa katika katika makundi.
Wewe ndio hujui. Kwa taarifa yako hata Hamas iliundwa na Mosad kwa nia ya kuisambaratisha Fatah ya Yaser Arafat. Kilichotokea mwenyewe umekiona.
 
Hizo taarifa ni za uongo kabisa na hazina ushahidi wowote. Acheni kuleta habari za kuchuuza kutoka kwenye majengo yenu ya ibada maarufu kama "masjid" na kuzisambaza humu kwa lengo la upotoshaji.
Wenzako wameingia katika CHANZO na kukuta taarifa za ukweli, ndio maana wanajadili HOJA. Amka!!!!! Acha uvivu wa kusoma.
 
Gharama ya kutafuta uhuru ni kubwa. Wangoni laki 3 waliuawa wakipigana na Wajerumani mwaka 1905. Population ya Wangani wakati huo haikufika hata milioni 2.

Leo wewe unakaa, uko huru na kuandika bila kujua kuwa safari ya kusaka uhuru ilianzia huko. Afghanistani zaidi ya miaka 30 wakipigana na kuusaka uhuru, bila kujali idadi ya watu waliokufa katika vita. Niishie hapo bila kutaja Vietnam, na wahindi wekundu waliomalizwa huko Marekani.

Safari ya Gaza ni kupata nchi inayoitwa Palestina, hawana uchaguzi mwingine.
Achana na madogo wa humu utachoka bure
 
Kitu kimoja umeshindwa kutofautisha ni huo uhuru wa hizo nchi na Israel. Kule Israel hata kabla hawajaja wayahud hao wakimbiz wa ulaya walikuwepo wayahud wa asili wakiishi na waarabu so pale myahud anapigana vita ya jihad ni either afe afutike au abaki kama taifa. So njia nzur sio waliotumia Hamas ambao viongoz wao wanakula bata huko dunian ila kukubaliana namna ya kuishi vinginevyo kila siku kichapo tu mpaka akili ziwakae. Hata hapo South Africa walikubali kukaa maisha yakatokea sio kila unachohtaji huku dunian utakipata chief. Red Indian na hata aboriginal kule Australia na America walikubali maisha wanaendelea. Unapambana na mtu ambae amezaliwa hapo na aliyempigania ni babu yake unataka aende wapi? Hawa jamaa wanasukumwa zaid nawaislam kwaajili ya al Aqsa nothing more.
 
Wahuni sio watu!! Hamas washaanza kulia Lia kwamba Kuna njama za kuunda serikali mpya bila wao kushirikishwa.
 
Gharama ya kutafuta uhuru ni kubwa. Wangoni laki 3 waliuawa wakipigana na Wajerumani mwaka 1905. Population ya Wangani wakati huo haikufika hata milioni 2.

Leo wewe unakaa, uko huru na kuandika bila kujua kuwa safari ya kusaka uhuru ilianzia huko. Afghanistani zaidi ya miaka 30 wakipigana na kuusaka uhuru, bila kujali idadi ya watu waliokufa katika vita. Niishie hapo bila kutaja Vietnam, na wahindi wekundu waliomalizwa huko Marekani.

Safari ya Gaza ni kupata nchi inayoitwa Palestina, hawana uchaguzi mwingine.
na uhuru ukapata mwaka 1905 ? mifano iwe na uhalisia , ww unatoa mifano ya ajabu ilihali ww usingeweza mudu hali maisha ya Gaza ya sasa

KUWENI NA HURUMA JAMANI
 
Back
Top Bottom