UZUSHI Mtoto akianza kubeba vyuma vizito vya mazoezi anadumaa

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Wakuu kwema?

Niko na swali hili, nilisikia watu wakizungumza kuwa mtoto akianza kubeba vyuma vya mazoezi anadumaa, yaani anaacha kurefuka na kuishia kuwa na umbo lile lile la mtoto (anadumaa).

child-weights.jpg
Kuna ukweli wowote katika hili?
 
Tunachokijua
Mazoezi ya nguvu ni sehemu ya kawaida ya programu za michezo na utimamu wa mwili kwa watu, ingawa baadhi wanaweza kutumia mazoezi haya kama njia ya kuongeza ukubwa wa misuli ili kuboresha mwonekano.

Programu za mazoezi ya nguvu zinaweza pia kufanywa ili kujaribu kuboresha ufanisi wa utendaji kwenye michezo na kuzuia majeraha, kurekebisha majeraha, na/au kuongeza utimamu wa mwili kwa mwanamichezo husika.

Sawa na shughuli nyingine za kimwili, mazoezi ya nguvu yameonyeshwa kuwa na manufaa kwa afya ikiwemo kuboresha afya ya moyo na mishipa ya damu, kuongeza utimamu wa mwili, kuimarisha afya ya mfupa, kuweka sawa viwango vya mafuta mwilini Pamoja na kuboresha afya ya akili.

Tafiti za hivi karibuni zimeonesha pia manufaa manufaa ya kufanya mazoezi kwa Watoto wenye utindio wa ubongo.

Athari za Mazoezi kwenye ukuaji
Bila shaka umewahi kusikia kuwa kufanya mazoezi magumu ikiwemo kubeba vyuma hudumaza ukuaji wa watoto, na wazazi wengi hukataza watoto wao kujihusisha na mazoezi kwa kuhofia athari hizo.

JamiiForums imezungumza na madaktari, wataalamu wa mazoezi ya viungo pamoja na kurejea tafiti mbalimbali za afya na kubaini kuwa madai ya mazoezi ya kubeba vyuma hudumaza ukuaji wa watoto hayana ukweli.

Mathalani, kwa mujibu wa taasisi ya The American Pediatrics Association, mazoezi ya kubeba vyuma sio mabaya kwa watoto, isipokuwa taratibu sahihi zinapaswa kufuatwa ili kuondoa changamoto zote zinazoweza kujitokeza kwenye afya ya mtoto ikiwemo kumfanya adumae.

Hata hivyo, APA wanaonya juu ya matumizi ya madawa na kemikali za kusisimua misuli wakati wa mazoezi ambazo huwa sio salama kwa watoto. Kwa mujibu wao, watoto hawapaswi kutumia bidhaa hizo kwani ni hatari kwa afya.

Pia, inashauriwa kuwa umri sahihi wa kumuanzishia mazoezi mtoto ni walau kuanzia miaka 7 au 8 na kuendelea. Aidha, wanapaswa kushiriki mazoezi haya chini ya uangalizi wa mkufunzi mwenye ujuzi wa kutosha (Trainer)

Tovuti zingine za masuala ya Afya za Parents na Healthline zinakanusha pia uvumi huu, na zinafafanua kuwa watoto wanaweza kushiriki aina hiyo ya mazoezi kwa kufuata miongozo sahihi inayoshauriwa na wataalamu.

Athari za mazoezi
Yanapofanyika pasipo kufuata taratibu sahihi, mazoezi hususan ya kubeba vyuma vizito yanaweza kusababisha madhara makubwa kwenye afya ya binadamu.

Hapa kuna baadhi ya madhara yanayoweza kutokea:
  1. Majeraha ya misuli
  2. maumivu kwenye maungio ya mifupa
  3. Uchovu mkubwa
  4. Kuvunjika mifupa
  5. Kuongeza shinikizo la damu
  6. Kubeba uzito mwingi kunaweza kusababisha shinikizo kubwa kwenye mfumo wa mkojo na kusababisha matatizo kama vile kushindwa kwa kibofu cha mkojo
Ni muhimu kuchagua uzito unaofaa, kufuata mbinu sahihi za mazoezi, na kupumzika vya kutosha ili kuepuka madhara haya. Kuanza mazoezi ya kubeba vyuma vizito chini ya usimamizi wa mtaalamu au mkufunzi wa mazoezi kunaweza kusaidia kuzuia majeraha na kuhakikisha kuwa unafanya mazoezi kwa njia salama.
Ni kweli hata late Kawawa alibebeshwa vyuma ndio maana badala ya kurefuka kwanda juu yeye akawa anarefuka kwenda chini.
 
Chuma hakitaki ugali na dagaa au maharage hiyo ndio sababu.
Ila akizingatia protein hasa nyama Kwa wingi basi ni sababu ya kuongeza Afya kubwa.
 
Basi ayo maharage, dagaa na izo nyama kwa pamoja ndo protein unazipata umo kwa wingi, au ulikariri tu?
Kwanza hapo nimeongelea Kwa ujumla wake ukitaka niende deep zaidi naweka kukufanulia maana ya protein kama amino acids na aina zake ,mi ni trainer Kwa kusoma na pia Niko ktk hayo mambo ya fitness , sijui una maana gani kusema nimekariri?
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom