Mimba Kutoka: Hivi ndivyo utakavyofanya Kupata mtoto Salama

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
MIMBA KUTOKA; HIVI NDIVYO UTAKAVYOFANYA KUPATA MTOTO SALAMA.

Anaandika Robert Heriel
Yule Shahidi

Binti yangu endapo utakutwa na mkosi wa Aina Hii, naamn ndio Tatizo la mimba kutoka basi Mimi Baba yako sikukusahau katika hili. Tena Kijana wangu ikiwa Mkeo utakayemuoa, unayempenda, atakuwa na tatizo hili basi nawe sijakusahau. Wala usimuache, tena usimnyanyase wala kumuangalia Kwa jicho la lawama, na chuki, na kumbeza. Bali mpende Kwa sababu wewe ndiye kimbilio na tumaini lake. Ilinde ahadi uliyompatia kuwa utampenda Daima na kuilinda furaha yake.

Haya nisikuchoshe Kwa sababu Sisi Watibeli ni Watu wenye maneno mengi.

Mara nyingi mimba hutoka mara Kwa mara zaidi Kwa Binti aliyetoa mimba. Nimesema Mara nyingi Ila sio mara zote. Ikiwa Binti alifanya hayo basi itampasa kufanya toba ili kuondoa kaburi katika tumbo lake.

Ni sharti amuambie mwenza wake ikiwa hajui chanzo cha Hilo tatizo ni nini. Ikiwa ataona hatia na kuona Aibu kueleza Historia hiyo Mbaya ya kutisha, basi itampasa kutubu yeye mwenyewe kulingana na Yule Mungu anayemuamini Kwa maana Ipo miungu mingi.

Matatizo ya homoni na mifumo ya Uzazi kama maumivu Makali Wakati WA hedhi, kukosa hedhi Kwa muda au Kupata hedhi kulikopitiliza mfano siku kumi au zaidi, au Kupata siku moja, kupata maumivu upande kushoto au wakulia wa Ovari, ni moja ya Red alert kuwa Uzazi wako unaweza ukasumbua. Ni vizuri ukapata mtoto Mapema ili kujihakikishia kabisa. Ninaposema mapema ninamaanisha umri wa miaka 17- 25 uwe ushapata mtoto walau mmoja.

Ukiwa na tatizo la mimba kutoka, ni vizuri ufanye haya:

1. Mimba isiingie kwa bahati mbaya, bali upange kabisa
Mimba Ikiingia Kwa bahati Mbaya hutojua na hautochukua hatua yoyote kuilinda. Kikawaida MTU hujua anamimba Baada ya wiki mbili mpaka mwezi. Na ikiwa una tatizo la mimba kutoka unaweza kujikuta hizo wiki ambazo haujui unamimba ndio kipindi hicho kiumbe "kijusi" kinakuwa dhaifu na ni rahisi Kutoka.

Hapo ndio utapata tishio la mimba kutoka kama maumivu kwenye Mji WA mimba au kiuno, na Wakati mwingine Damu Kutoka ambayo ni hatari ya mwisho kabisa.

Ni vizuri Kupanga kabisa mwezi Fulani napata ujauzito ili ujihami na kujilinda tangia siku ya Fertilization (urutubishaji wa Yai) kuanzia day one mpaka siku ya mwisho ya kujifungua.

2. Mimba ikiwa changa au kabla haijaingia zingatia vyakula vyenye madini ya chuma, protein na maji mengi
Vyakula vyenye madini ya chuma hasa mbogamboga za mjani kama mchicha Pori, Spinach, ni vizuri katika kutawala Homoni za mwili wako. Lakini pia Vinaboresha maumbile ambayo ni makazi ya Mtoto ambayo ni Mji wa Uzazi na kuta zake ambazo mtoto ataji-attach.

3. Usifanye kazi Kabisa, wala kufanya movement zinazotumia nguvu
RATIBA yako iwe Kulala, kukaa, Kula, kwenda kuoga, Kulala tena hasa kwenye miezi MITATU ya mwanzo"First Trimester". Ikiwa Mkeo ni mjamzito na mshajua anatatizo la mimba kutoka, ni Bora umpe likizo ya miezi Tisa bila kufanya kazi yoyote Ile wala kutembea tembea Kwa muda mrefu hasa miezi MITATU ya mimba. Wewe kama mume fanya kazi zote, kama unaenda kazini ajiri Msaidizi wa ndani iwe ni HK (Housekeeping wa kwenda kurudi) au HM(Housemaid wa kulala hapohapo) kama hauna pesa ya kuajiri basi unaweza muita ndugu au Mama yako au yake aje akusaidie. Na inatakiwa iwe miezi tisa.

Nasisitiza asifanye kazi yoyote Ile, Kutokana na sababu zifuatazo:

i) Mimba changa inakuwa bado Ipo chini ya mji wa mimba kwenye miezi MITATU ya mwanzo, bado haijapanda juu kujiattach kwenye kuta za Uzazi. Hivyo Kasi yoyote ngumu inaweza kuifanya itoke.

Mwezi wa nne WA mimba Second Trimester kijusi hupanda juu hivyo sio rahisi Kutoka na hata MTU akitaka kuitoa mimba ya miezi minne kuendelea ni lazima atolewe Kwa kuingiziwa vyuma.

ii) Placenta cord bado haijamuunganisha mtoto na Mama. Lile kondo linalomuunganisha Mama na mtoto bado halitatokeza, lile licha ya kusaidia kumlisha virutubisho mtoto vinavyotoka Kwa Mama lakini pia linasaidia kumshika mtoto.

4. Kula vyakula vinavyomeng'enywa Kwa urahisi hasa katika miezi MITATU ya mwanzo
Wakati WA mimba changa ni Wakati homoni zinakuwa juu Hali inayofanya mfumo wa chakula usifanye kazi vizuri, pia kichefuchefu cha mara Kwa mara ni uhakika. Vyakula vinavyomeng'enywa Kwa wepesi ni kama ugali, wali wa bokoboko, mchicha, maziwa, mayai.

Kudhibiti kichefuchefu ni muhimu ili kuzuia kutapika kwani Wakati mwingine unapotapita unatumia nguvu nyingi na kusababisha maumivu kwenye Mzunguko wa kiuno na eno la mji wa Uzazi. Usisahau Kula mbogamboga yaani hiyo iwe ni chakula cha lazima miezi yote Tisa ikiwa unatatizo la mimba kutoka.

Ikiwa unatapika chakula unachokula Hali inayopelekea kukosa nguvu ña mwili kukosa virutubisho ulivyodhamiria uvipate utafanya hivi:

a) Epuka sehemu yenye harufu au hewa nzito
b) Kaa sehemu yenye ubaridi, tumia AC au Feni au kaa kwenye vivuli vya miti kwenye hewa Safi.
c) Kula kidogokidogo mara Kwa mara hakikisha tumbo lisiwe tupu. Ikiwezekana nunua Biscuits, Karanga, korosho, Mkate n.k. Kila lisaa limoja ule. Kidogo.
d) Piga Mswaki kila mara unapokula chakula au kitu chochote. Au Baada ya kuhifadhi mate muda mrefu mdomoni.

Zingatia, sio muda wote homoni zinakuwa juu hivyo sio muda wote urahisi kichefuchefu na kutapika, kuna wiki urahisi kichefuchefu Asubuhi, kuna wiki Mchana kuna wiki Usiku. Kuna wiki Mchana wote. N.k.

5. Jipe/mpe timetable ili usiwe/asiwe Bored
Kukaa bila kufanya kazi, kulala na kuamka ni moja ya Programu ambayo inachosha. Ili Mkeo au ili usichoke ni vizuri kuweka timetable ambayo itaku-keep busy.

Mfano
1. Kuamka saa 01:00 - 2:00 Asubuhi.
2. Usafi, kuoga, kupiga Mswaki 2:00-3:00 Asubuhi
3. Kunywa chai 03;00-03:30
4. Kupumzika. 03:30 - 04:00 Asubuhi
5. Kuchora au kuimba au kusoma 4:00-5:30: Asubuhi
6. Kula matunda au Karanga au korosho, Saa 5:30-6:00
7. Kuperuzi mtandaoni Saa 6;00 -7:30
8. Chakula cha mchana Saa 7:30- 8:00 Mchana
9. Kulala Saa 8:00- 10:00 jioni
10. Usafi WA mwili 10:00- 10-30 jioni
11. Kunywa juisi au Baiti 10:30- 11:00 jioni
12. Piga Stori au chat au peruzi 11:00 - 12:00 jioni
13: fanya matembezi kidogo 12:00-12:30
14: Fanya Usafi WA mwili 12:30- 1:00 Usiku
15. Kula chakula cha jioni 1:00 -1:40 Usiku
16. Refresh Kwa kuangalia TV 1:40- 2:40 Usiku
17. Fanya ibada ya maombi na familia 2:40-03:30 Usiku
18. Kalale 3:30-4:00 Usiku uwe umelala

Huo ni mfano tu?

Kama ni Mwanamke muajiriwa na mimba zako zinatoka toka hapo ni Bora ukaongea na Muajiri akupe likizo usiende kazini. Sasa itakupasa uchague Kazi au mtoto endapo Muajiri akikataa. Hata hivyo unaweza omba likizo kwenye miezi MITATU ya mwanzo ya mimba. Zingatia Watu wenye mimba kutoka hawatakiwi hata Kupata mitikisiko ya Bajaji au Pikipiki kwenye bumps.

Endapo mimba ya Kwanza itatoka ni vizuri kuonana na wataalamu WA afya wakuambie chanzo cha mimba kutoka ni nini na nini ufanye kutibu hilo tatizo. Ni vizuri upumzike walau miezi MITATU mpaka sita ndipo ubebe mimba nyingine lakini ukiwa umepanga ili kuilinda.

Ni vizuri Baada ya kupokea Majibu ya Ultrasound kuwa mimba imetoka, ni Bora ukachukue vipimo katika Kituo kingine cha afya ili kuthibitisha kama majibu yanalingana. Kwani wapo baadhi ya madaktari hushindwa kusoma Ultrasound.

Mambo mengine yanayopelekea mimba kutoka ni:
I) Kupata maambukizi ya Malaria
ii) Kijusi au mtoto kuugua na Kufa tumboni.
iii) Kiwango cha sukari na madini ya chuma mwilini

Epuka kunywa madawa yoyote Yale Wakati Unamimba bila maelekezo ya Daktari.

Taikon Acha nipumzike. Kwa leo tuishie hapo. Mwenye swali anaweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Taikoni hivi inakuaje mama mjamzito anakosa hamu ya Kula kabisa mimba inaweek kama 3 aina tatizo Kwa mtoto atakaye zaliwa?

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app

Kukosa Hamu ya Kula inatokana na mabadiliko ya homoni katika mwili wake..
Apewe chakula ambacho anahamu nacho(anachojisikia Kula), pili, ale vyakula rahisi kumeng'enywa.

Madhara Kwa mtoto itategemea na Hali hiyo itamchukua muda gani lakini kwake itamfanya awe na afya dhoofu.
Ni lazima ajikaze Kula..Kula ni Dawa na Dawa ni lazima sio hiyari
 
Kukosa Hamu ya Kula inatokana na mabadiliko ya homoni katika mwili wake..
Apewe chakula ambacho anahamu nacho(anachojisikia Kula), pili, ale vyakula rahisi kumeng'enywa.

Madhara Kwa mtoto itategemea na Hali hiyo itamchukua muda gani lakini kwake itamfanya awe na afya dhoofu.
Ni lazima ajikaze Kula..Kula ni Dawa na Dawa ni lazima sio hiyari
Sawa afu Taikoni kuhesabu mimba unahesabu kuanzia siku ilioingia au ln?

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom