Mtoto Akataa shule; Bora aende jela

Madukwa Peter

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
2,524
2,000
Mimi pia nakumbuka nilikataa kuanza darasa la kwanza (nilikataa shule)

nadhani ni utoto tu; ingawa nilikuwa na sababu zangu pia ambazo zilinifanya kukataa shule

ilitumika nguvu kubwa kuhakikisha naanza shule... mpaka nikakubali na hatimaye nikaanza kuipenda shule kuliko kawaida.
 
Kobello

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
7,699
2,000
Wala siyo kweli. Nina mifano hai
Mwenyewe najuta muda mwingi niliopoteza shuleni ni bora ningeishia Form 4 nikaenda VETA.
Dunia imebadilika sana kwa sasa. Tumekaririshwa ukisoma ndiyo utakuwa na maisha mazuri. Hii ni dhana potofu
Kuna watu wamemaliza chuo kikuu (wana degree zao) lkn maisha yao yanasikitisha. Maisha ya sasa ili ufanikiwa lazima uwe na ujuzi wowote km vile ufundi magari, nyumba, seremala, kuendesha gari n.k
Km umemaliza kwenye ualimu, uanasheria n.k utajikuta unasota mtaani utakapokosa kazi.
Mpelekee VETA akajifunze fani za maisha na siyo kukariri vitabu.
Shule ya msingi ni muhimu. Kwengine huko siyo lazima.
Huyo bado mdogo sana, apate elimu ya msingi. Inaonyesha kuna tatizo la kuonewa au kuchekwa na wenzake, waliangalie hilo kwa sababu hata anayemuhoji hayuko serious.
 
Mczigga

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
341
1,000
Wala siyo kweli. Nina mifano hai
Mwenyewe najuta muda mwingi niliopoteza shuleni ni bora ningeishia Form 4 nikaenda VETA.
Dunia imebadilika sana kwa sasa. Tumekaririshwa ukisoma ndiyo utakuwa na maisha mazuri. Hii ni dhana potofu
Kuna watu wamemaliza chuo kikuu (wana degree zao) lkn maisha yao yanasikitisha. Maisha ya sasa ili ufanikiwa lazima uwe na ujuzi wowote km vile ufundi magari, nyumba, seremala, kuendesha gari n.k
Km umemaliza kwenye ualimu, uanasheria n.k utajikuta unasota mtaani utakapokosa kazi.
Mpelekee VETA akajifunze fani za maisha na siyo kukariri vitabu.
Kwa maelezo yako ni sahihi kabisa ila kwa umri wa uyo dogo ni bado Sana kuacha shule tusije pata taifa la vilaza kwaihiyo ni Bora afike form 4 ni hatua nzuri tu ya kielimu after that apige mishe zake
 
Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
201,418
2,000
Sikuona umuhimu wa kuja kuringishia hausgeli kufundishwa na mwanao wa la tatu ni sawa na kusema huyo kijana asisome atakuja kufundishwa na mtoto wa boss wa darasa la tatu
Umeona sehemu nimeandika elimu haina umuhimu. Elewa mantiki.
 
MTOCHORO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
4,652
2,000
Wala siyo kweli. Nina mifano hai
Mwenyewe najuta muda mwingi niliopoteza shuleni ni bora ningeishia Form 4 nikaenda VETA.
Dunia imebadilika sana kwa sasa. Tumekaririshwa ukisoma ndiyo utakuwa na maisha mazuri. Hii ni dhana potofu
Kuna watu wamemaliza chuo kikuu (wana degree zao) lkn maisha yao yanasikitisha. Maisha ya sasa ili ufanikiwa lazima uwe na ujuzi wowote km vile ufundi magari, nyumba, seremala, kuendesha gari n.k
Km umemaliza kwenye ualimu, uanasheria n.k utajikuta unasota mtaani utakapokosa kazi.
Mpelekee VETA akajifunze fani za maisha na siyo kukariri vitabu.
Kama huna akili nyingi VETA panafaa kwasababu panakuandaaa kufanya vibarua
 
MTOCHORO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
4,652
2,000
Mm mwenyewe nina degree lkn nakula kupitia ujuzi mwingine ambao sijasomea darasani ambapo ningeanza muda kbla sijaenda form 5 ningekuwa mbali sana.
Niwe na chuki na wenye degree wakati wapo mtaani wanafanya kazi mpaka za watu waliomaliza darasa la 7. Wapo wana wengi tu ninaowafahamu wanalia njaa na degree zao
Shida ni Degree uliyoipata kwa mkumbo, kisa umepangiwa na TCU na wewe ukaingia kichwa kichwa, wenzio waliosoma Vitu vya maaana wanakula maisha wanakazi ya kusign tu wewe fundi mchundo
 
Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
2,200
2,000
Wala siyo kweli. Nina mifano hai
Mwenyewe najuta muda mwingi niliopoteza shuleni ni bora ningeishia Form 4 nikaenda VETA.
Dunia imebadilika sana kwa sasa. Tumekaririshwa ukisoma ndiyo utakuwa na maisha mazuri. Hii ni dhana potofu
Kuna watu wamemaliza chuo kikuu (wana degree zao) lkn maisha yao yanasikitisha. Maisha ya sasa ili ufanikiwa lazima uwe na ujuzi wowote km vile ufundi magari, nyumba, seremala, kuendesha gari n.k
Km umemaliza kwenye ualimu, uanasheria n.k utajikuta unasota mtaani utakapokosa kazi.
Mpelekee VETA akajifunze fani za maisha na siyo kukariri vitabu.
Mshakalili kua kusoma ni kufika chuo kikuu, huko veta unaenda kufanya nini kama sio kusoma pia, iyo form four ni nini kama sio kusoma huko.

Kwa umri wa uyo dogo unamshauri aache shule kwa umri huo na si ajabu hajui kusoma wala kuandika hapo. Mkuu em acheni kudanganya watu kua elimu haina umuhimu ilhali wewe unaitumia hiyo elimu kuvuna maarifa na taarifa humu jf.

Mwache asome mpaka form four hapo ndo unaweza kusema mwache aamue mwenyewe sasa lakini kwa huyo dogo akili yake bado saana, na atajuta tu kama asiposoma.
 
Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
201,418
2,000
Wengi wanaoilalamikia degree ni wale waliomaliza form six wakakurupukia kusaka form za vyuo au kufata mkumbo wa kujiunga TCU iwapangie vyuo bila wao kufanya utafiti wa kina wa masomo wanayoyamudu na fani zinazowafaa. Ile bendera upepo wa ili mradi nami nipo chuo matokeo yake ndo haya majuto ya kutosha
Shida ni Degree uliyoipata kwa mkumbo, kisa umepangiwa na TCU na wewe ukaingia kichwa kichwa, wenzio waliosoma Vitu vya maaana wanakula maisha wanakazi ya kusign tu wewe fundi mchundo
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
12,201
2,000

Mwishoni mwa miaka ya sabini nikiwa sekondari, mdogo wangu hakuchaguliwa kwenda sekondari. Kaka yetu mkubwa akampa alternatives mbili: ama achague kurudia darasa la saba mbali na nyumbani (ambayo wakati huo ilikuwa inafanyika na kaka alitaka jamaa huyu asikae karibu na starehe za nyumbani) au ampeleke shule ya sekondari ya kulipia, ambako atatakiwa kuwa makini na matumizi yake ya kujikikmu atakayokuwa anapata kutoka nyumbani kwani haitakuwa hela nyingi sana kwa sababu ya gharama za karo.

Bwana mdogo akakataa kwa mbwembwe sana kuwa yeye ana mipango yake; atasoma kwa posta na anataka kuanza kufanya biashara zake.

Ole wako ukutane naye leo, yaani bwana mdogo kachaakaa kweli kweli kuliko sisi wakubwa zake; yeye kuomba shilingi elfu mbili leo na kulaumu kuwa mbona tunamsahahu siyo jambo la ajabu kabisa kwake.

Nadhani video hii ni ya utani tu, ila kama ni kweli, huyu mtoto ataweza kujutia sana maishani mwake kuwa kwa nini alitumia utoto wake vibaya labda kama ana kipaji maalumu kama muziki, mpira na biashara za kununua na kuuza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom