Moses Jela maisha kwa kumbaka mtoto

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
MAHAKAMA ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, imemuhukumu Moses Method (23), mkulima na mkazi wa kijiji cha Kasuga kwenda jela maisha baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili mwenye umri wa miaka tisa.

Sambamba na hukukumu hiyo mahakama hiyo imemuamuru mshtakiwa kulipa fidia kwa muhanga kiasi cha shilingi milioni moja fedha taslimu.

Mwendesha Mashtaka Mkaguzi wa Polisi (INSP), Charles Mwakanyamale aliieleza mahakama kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 17, 2023 na alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 21, 2023.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kakonko, Ambilikile Kyamba amesema mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na hatimaye kumtia hatiani mshitakiwa kwa kosa hilo.

Source - Nipashe
 
Kila hakimu au jaji anasemaga hivyo hivyo kwamba wamejirishisha pasipo na shaka hata kama wamepigia simu kutoja juu in Rostam's voice
 
Back
Top Bottom