Mbeleni atajutia maamuzi yake
Kwahiyo bangi ndio hua inafanya watu wasipende Shule?Sio bangi kweli !?, That's abnormal
Wala siyo kweli. Nina mifano hai
Mwenyewe najuta muda mwingi niliopoteza shuleni ni bora ningeishia Form 4 nikaenda VETA.
Dunia imebadilika sana kwa sasa. Tumekaririshwa ukisoma ndiyo utakuwa na maisha mazuri. Hii ni dhana potofu
Kuna watu wamemaliza chuo kikuu (wana degree zao) lkn maisha yao yanasikitisha. Maisha ya sasa ili ufanikiwa lazima uwe na ujuzi wowote km vile ufundi magari, nyumba, seremala, kuendesha gari n.k
Km umemaliza kwenye ualimu, uanasheria n.k utajikuta unasota mtaani utakapokosa kazi.
Mpelekee VETA akajifunze fani za maisha na siyo kukariri vitabu.
Kweli kabisa siku akipiga kitabu akawa majaliwa ndio atakumbuka kauli yake.
Hapana mkuu. Faida ya elimu kwanza ni kujua kusoma na kuandika. Unaweza ukawa hujasoma ila ukabahatika kupata pesa za kutosha lakini hutazifaidi kwa dunia ya leo hata sms ya muamala ikiingia itabidi ukaombe msaada wa kusomewa ujue kilichomo. Hela zako zoote ila bank hutaweza shika kalamu kuandika cheki etc
Faida ya pili inakupa ka uelewa ka mambo na ujanja katika hizo harakati za kukariri
Sasa kwa kesi ya huyu mtoto hataki shule hapo huwezi jua kama anajua kusoma na kuandika huko veta si atawapa shida waalimu kuanza kumfundisha a e i o u
Elimu sio mpaka degree ila punguza chuki kwa wenye degree. Leo hii wanaobeza elimu na wakapata bahati ya kushika pesa nyingi wanawakazania watoto wao kusoma mpaka degree
Hapo ubongo wa nyuma unafanya kazi.
Hasira ni zaidi ya bangi

Kuna haja ya kuchunguza shule alokuwa anasoma ili kujua tatizo lipo wapiKwa hiyo tuwe na kauli moja kua aachwe