Mtoto Akataa shule; Bora aende jela

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
9,642
2,000
Hilo nalo wazo maana elimu ya sasa matatizo tu
yuko sahihi, elimu siku hizi si ufunguo wa maisha na tena imegeuka na kuwa kufuli la maisha. mtu mwenye digrii hana ujuzi wowote wa kupambana na mazingira yake. zaidi zaidi elimu imemfungia afikirie kufanya vitu alivyosomea/kariri tu. sasa hapo si inakuwa kufuli la maisha?

dogo asisomeeee, achukue elimu ya kitaa.
 

Sisyphus

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
2,573
2,000
Sijazungumzia mtoto kutoenda shule kbs. Ninachozungumzia mtoto afike mpaka form 4, hii ndiyo daraja la elimu ambalo kila mtanzania anatakiwa afike iwe kwa viboko au ngumi.
Mm mwanangu akifika form 4 au 6 lazima aende VETA kwanza hiyo ni lazima na siyo ombi
Huko Veta anaenda kusomea nini ambacho kwenye mfumo wa elimu ya kawaida hakipo?
 

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
9,642
2,000
Dunia imebadilika Sana.Diamond angesoma asingemiliki rose royce.
Samatta angesoma asingemiliki ghorofa.
Bakresa angesoma asingekuwa milionea
Ila kumbuka na upande wa pili.
MO asingesoma asingemiliki simba kijanja.
Mello asingesoma asingeanzisha JF.
Japo dogo yupo sahihi binafsi nilichukua maamzi kama hayo
 

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,346
2,000
Wafrika tumejikuta kwenye duniani ya umasikini kwa kuamini haya mawazo. Vipaji vingi vinapotea shuleni kwa kuamini haya mawazo
Angalia elimu ya Messi, Diamond, Babu Tale, Zuchu
Niki wa pili pamoja na kuwa na Masters lkn anakula kupitia Muziki. Huyo mtoto anatakiwa akomaliwe asome mpk form 4 tu aende kwenye vyuo vya Ufundi.
Mm mwenyew pamoja na kuwa na elimu kubwa lkn nakula kupitia ujuzi nilionao ambao sijasomea chuo
Mess na Ronaldo wanalipwa na waliosoma ukumbuke. Wanacheza mpira kwenye viwanja vilivyojengwa na mainjinia wanalipwaa matangazo ya biashara ya kampuni zinazotumia wasomi kuzalisha bidhaa ata hayo matangazo yameandaliwa na wasomi.
 

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
9,642
2,000
Dogo kaamua akapige singeli inalipa kuliko shule.
Elimu sahihi ni form four kisha ingia mtaani upate elimu ya maisha.
Kusoma zaidi ni kujitakia umasikini
Kweli aisee elimu ya sasa ni kama unaweka odds
Kusoma 1.4 kutosoma 2.8
Kazi kwa mbetiji
 

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
9,642
2,000
Tuache kujidanganyaa humuu, basic education ambayo dogo anaikosa ni muhimu..
Advance na degree sawa hapo nakubali waweza utemane nako ila angalau basi form four,

Asaivi hata ukiishia st7 utapoteana, kwa nature ya maisha ya sasa ile tunaiita elimu ya msingi jina tuu ila 4m4 ndio ingekua ya msingi(basic), std 7 ingekua elimu ya awali...
Kinyume na hapo subiri kujiendeleza baadae au kubali kupigwa kwenye mambo mengi..
Ila hapo napo uko sawa ila labda wamemzingua shuleni ndo maana kaamua kukomaa asisome
 

Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
69,875
2,000
Hii inaitwa mind your own business...

saikolojia yake ndiyo ishagoma kuona umuhimu wa shule...
 

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
9,642
2,000
Mwishoni mwa miaka ya sabini nikiwa sekondari, mdogo wangu hakuchaguliwa kwenda sekondari. Kaka yetu mkubwa akampa alternatives mbili: ama achague kurudia darasa la saba mbali na nyumbani (ambayo wakati huo ilikuwa inafanyika na kaka alitaka jamaa huyu asikae karibu na starehe za nyumbani) au ampeleke shule ya sekondari ya kulipia, ambako atatakiwa kuwa makini na matumizi yake ya kujikikmu atakayokuwa anapata kutoka nyumbani kwani haitakuwa hela nyingi sana kwa sababu ya gharama za karo.

Bwana mdogo akakataa kwa mbwembwe sana kuwa yeye ana mipango yake; atasoma kwa posta na anataka kuanza kufanya biashara zake.

Ole wako ukutane naye leo, yaani bwana mdogo kachaakaa kweli kweli kuliko sisi wakubwa zake; yeye kuomba shilingi elfu mbili leo na kulaumu kuwa mbona tunamsahahu siyo jambo la ajabu kabisa kwake.

Nadhani video hii ni ya utani tu, ila kama ni kweli, huyu mtoto ataweza kujutia sana maishani mwake kuwa kwa nini alitumia utoto wake vibaya labda kama ana kipaji maalumu kama muziki, mpira na biashara za kununua na kuuza.
Kwenye hiyo video dogo yupo serious kabisa.
Ila swala la kukataa shule athari zake huja Kulingana na bahati ya mtu Kwa mfano mwingine anaweza kataa shule na akatoboa kimaisha ila mwingine anaweza kataa hivyo hivyo na maisha yanamkataa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom