Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
Habari wakuu,
Mtindo huu wa bajaji kupakia abiria wawili mbele si mpya, naamini watu wengi mmekutana nayo hii hasa kwa wakazi wa Mbezi ya Kimara. Hili ni jambo hatari ambalo linaweza kusababisha majanga muda wowote, hasa ukizingatia madereva wengi wa bajaji walivyo rafu barabarani.
Kubwa zaidi wengine wakiona wamejaza hapo mbele, wanaongeza mtu mwingine hasa kama jamaa ni rafiki (mshkaji) yake, anatoka hapo mbele anakaa abiria mwingine huku yule aliyekuwa mbele anaenda kuning'inia nyuma ya bajaji!
Cha kushangaza ni kwamba inaonekana ni jambo la kawaida kabisa, kwani bajaji inapita mbele ya trafiki kwa kutamba kabisa wanaendelea na safari zao. Ama imekuwa moja ya sehemu ya kitega uchumi?
Na wewe abiria unayepanda bajaji kama hivi hujihurumii? Huthamini maisha yako kiasi cha kujihatarisha kama hivi?