Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 12,263
- 10,349
Well sasa unataka mjadala uwe wa dini maana naona tunapelekana ambako sintopenda zaidi kuingia. Kwanza kabisa nimeshasema kwamba swala la mahakama ya kadhi lipo kikatiba na kisheria maana tunafuata mfumo wa kisheria wa cultural law na ndio unaotambulika hata ktk ndoa za waislaam, mirathi na kadhalika kisheria. Sio kwamba hakuna kitu hiki kipo isipokuwa walicholalamika waislaam ni kwamba sheria hazifuatwi inavyopaswa kwa sababu baadhi ya hukumu zimefuata secular wakati ndoa ilikuwa ya kiislaam.
Zipo kesi za madai hata za wakristu ktk ndoa ama talaka ambazo zimeamuliwa ki secular wakati waliofunga ndoa ni wakatoliki ambao dini inawakataza kuachana isipokuwa kwa zinaa (kama sijakosea)..waumini wanaweza kulalamikia sheria na maamuzi ya korti zetu na ikaswihi, Hivyo hata Kanisa linaweza kabisa kuiomba serikali inapofikia maswala la kuvunja ndoa za waumini wake, mirathi au yaliyopo ktk cultural law wapelekwe mahakimu wanaoijua sheria ya dini yao. wakristu hawakatazwi kufanya hivyo ila maadam siku hizi tunapuyanga tu mambo mengi ya dini yamepuuzwa. Hakuna kosa kisheria na hakuna mahala waislaam wanakiuka katiba ila ndivyo ilivyotakiwa kuwa. Binafsi napingana na mahakama ya kadhi kwa sababu waislaam wenyewe wanafanya mengi kinyume cha imani ya dini leo utaka kuwahukumu baada yaa.
Mkuu wangu memorundum of Association ni kinyume cha sheria, na ndio maana ikaitwa makubaliano ya muafaka ambayo kisheria yanakosa nafasi. Hakuna mkataba baina ya serikali na serikali na ndio maana ikaitwa Muafaka kama ulivyofanywa wa CUF na CCM. Nionyehse mahala poppote ktk katiba kunaporuhusu vyama viwili kuandaa mbele ya uchaguzi jinsi ya kuongoza Zanzibar. Nionyeshe hata kipengele kimoja cha katiba yetu kinachoruhusu hivyo?. BTW nenda katazame tafsiri ya Muafaka (Memorundum of Association) halafu rudi tujadili hapa.
Unarudi kulekule. Hakuna mtu anayesema kuwa waislamu hawana haki ya kujiamulia mambo yao yenyewe. Tunachopinga ni kudai kuwa Mahakama hiyo iingizwe katika mfumo wa serikali. Ingawa wakatoliki hawatambui talaka lakini wahusika wanaweza kwenda serikalini na ndoa yao ikafanywa batili. Msimamo wa kidini hauingilii utendaji wa serikali. Ndivyo ilivyo. Na ndivyo inavyotakiwa kuwa. Hukumu kila siku inatakiwa kuwa secular katika nchi isiyo na dini bila kujali imani ya wahusika.
Wakatoliki wanakataa talaka, period. Umeoa au umeolewa basi utakuwa hivyo hadi kifo kitakapowakuta. Hawaangallii zinaa, ukatili au kitu kingine. Itakapofika Kanisa kuomba wao watoe hukumu katika masuala yanayowahusu wale waliobatizwa nao, nao tutawapinga. Katika nchi ambamo tumeoaniana, wengi kuwa wenye dini jina, na wengine wenye imani tofauti, hiyo tutaona ndio mwanzo wa kuigeuza nchi hii kuwa theocracy. Tutawapinga kama tunavyopinga Mahakama ya Kadhi ndani ya serikali.
Mkuu, mbona unachanganya Memorandum of Understanding (MoU) iliyopo baina ya mashirika ya kikristu na serikali na Memorandum of Association ambayo inaelekea iko kati ya CUF na CCM. Ni vitu viwili tofauti. MoU si mkataba bali ni makubaliano yasio na uzito wa kisheria. Hauwezi kumpeleka mtu Mahakamani kwa kutotekeleza yaliyopo kwenye MoU. MoA ni makubaliano ya ushirikiano ambayo ni ya kisheria. Ni mkataba wakati MoU si mkataba. Lakini hata hivyo sioni tatizo kwa vyama viwili kukubaliana kabla ya uchaguzi jinsi watakavyoshirikiana kama watashinda. Kama wananchi wanaona hivyo sivyo basi kwenye uchaguzi ujao watawaadhibu. Mbona Liberal Democrats wanashirikiana na wahasibu wao Conservatives huko Uingereza? na unaona jinsi wapiga kura wanavyowaadhibu?
Badala ya kulalamikia MoU ambayo inaipunguzia serikali mzigo wa kutoa huduma za kijamii basi na nyie mngeingia kwenye MoU yenu ili sote tufaidike. Kama vile mnavyowapeleka watoto wenu St. Joseph University nasi tunawapeleka watoto wetu Feza.
Amandla.....