Mtei alipotofautiana na Mwalimu Nyerere

Alitaka, kwa mfano, NMC irudi kwa akina Chande. Wao wamiliki 51% na serikali ibaki na 49%. Mzee Mtei alichokuwa anasisitiza ni serikali iache menejimenti ya mashirika haya. Na hili wala halikuwa wazo lake lilikuwa ni wazo la IMF na WB. Mkapa alikubali karibu kila kitu. Tumeishia wapi?

Mkapa alikubali wakati mashirika yanachechemea au yako hoi bin taaban, then what did you espect....! Tibu ugonjwa just unapojitokeza na hiyo ndio tiba na action sahihi, but ukichelewa..., tiba na action zake lazima zitakuwa tofauti na hivyo kupelekea hata matokeo ya tiba na hatua hizo zilizochukuliwa kuwa tofauti.

Ikumbukwe kwamba wakati huo, JKN na Mtei walikuwa right at the source of the current baddens. Hivyo chochote sahihi wakati ule kama kingefanyika hopeful tatizo lingetibika.
Soma signature yangu below to get the significance of this post/Discussion

Thank you
 
Mwanafalsafa,
Leo tuna vyama vingi lakini vyote ni upuuzi mtupu kwa sababu hakuna chama hata kimoja kinacho tangaza imani tofauti ya CCM -hakuna.. Vyama vyote vinatofautiana ktk sera zao (ibada) badala ya kimrengo (itikadi). Kama vile dini zetu kubwa zote zinatofautiana toka mwanzo, waislaam wana imani na nguzo zao tofauti na Wakristu, Mabudha, dini za jadi na kadhalika, hivyo inampa mwananchi Uhuru na haki ya kuchagua imani gani anayoikubali zaidi. Lakini kinachofanyika Tanzania hadi kesho, vyama vyote ni madhehebu ya dini moja. Vyama vyote vinalilia Udugu wetu, Uhuru wetu, Umoja wetu, Amani baina yetu na Haki za kijamii, hivi ni vitu ambavyo kwa tafsiri kubwa ndio Ujamaa na Kujitegemea.

Mkuu Mkandara
Usiangalie nchi zilizoendelea kama Marekani na Uingereza kisha ukachukua reference kwao with respect to Tanzania utakuwa hujatutendea haki. Kimsingi nchi hizo nilizozitaja kama mfano zipo katika tabia-hali ya Stable state, ndio maana unaona zime_specialize katika misingi miwili tofauti. Na hii ilitokea baada ya vyama vingi kujikuta vikiwa na lengo au msimamo mmoja hivyo kulazimika kuungana mpaka ikafika wakati ile intergration ikaishia kuzaliwa kwa pande mbili Repablican na Democracy. (Conservertives and Non Conservetives)

Pande zote zimeshikilia mfumo tofauti wa kiungozi kulinga na kipi kinapewa kipaumbele kuliko kingine katika muda husika. Ndio maana unaona vinaingi katika uongozi kwa kupokezana kulingana na ukweli kwamba nchi husika inahitaji kipaummbele fulani kwa wakati huo.


Hapa Tanzania, Bado sana kufika katika specilaization za namna hiyo kwa sababu bado tupo katika kuitafuta ile
Stable state ya nchi. Bado tunachangamoto nyingi sana, Kiuchumi, Kielimu, Kisiasa, Kidini na hata Kiutamaduni. Ni lazima tuzikabili hizi changamoto zote na kuzimudu hata kama sio kuzishinda kabisa, ndipo automatically tutajigundua kama nchi ni nini tunahitaji katika wakati husika.

Matatizo ya Tanzania kwa sasa ni katika kutumia rasilimali zake zote mbili vizuri, yaani
Rasilimali watu na Rasilimali Mali katika kutatua matatizo yake. Ndio maana vyama vyote, Taasisi mbalimbali, Jumuiya za kimataifa na n.k zote zina-focus katika hilo maana hilo ndio msingi wa kujitawala na kujikwamua katika nchi yoyote ile duniani, yaani kuwa na watu wenye Elimu na uwezo wa kuikabili nature, ili kuwa na Uchumi imara hasa unaotokana na misingi ya ndani ya nchi hasahasa kwa kuangalia resouces and talents zilizopo. Halafu mwisho unakabili extras as the means of enhancement.

Tatizo letu sio katika siasa, tatizo letu lipo katika Uongozi, unoweza kuleta uzalendo miongo mwa watu ilikuwa na nia sahihi ya maendeleo ya kitaifa na siyo maendeleo binafsi.


Thanks
 
Mkuu Mkandara
Usiangalie nchi zilizoendelea kama Marekani na Uingereza kisha ukachukua reference kwao with respect to Tanzania utakuwa hujatutendea haki. Kimsingi nchi hizo nilizozitaja kama mfano zipo katika tabia-hali ya Stable state, ndio maana unaona zime_specialize katika misingi miwili tofauti. Na hii ilitokea baada ya vyama vingi kujikuta vikiwa na lengo au msimamo mmoja hivyo kulazimika kuungana mpaka ikafika wakati ile intergration ikaishia kuzaliwa kwa pande mbili Repablican na Democracy. (Conservertives and Non Conservetives)

Pande zote zimeshikilia mfumo tofauti wa kiungozi kulinga na kipi kinapewa kipaumbele kuliko kingine katika muda husika. Ndio maana unaona vinaingi katika uongozi kwa kupokezana kulingana na ukweli kwamba nchi husika inahitaji kipaummbele fulani kwa wakati huo.

Hapa Tanzania, Bado sana kufika katika specilaization za namna hiyo kwa sababu bado tupo katika kuitafuta ile Stable state ya nchi. Bado tunachangamoto nyingi sana, Kiuchumi, Kielimu, Kisiasa, Kidini na hata Kiutamaduni. Ni lazima tuzikabili hizi changamoto zote na kuzimudu hata kama sio kuzishinda kabisa, ndipo automatically tutajigundua kama nchi ni nini tunahitaji katika wakati husika.

Matatizo ya Tanzania kwa sasa ni katika kutumia rasilimali zake zote mbili vizuri, yaani Rasilimali watu na Rasilimali Mali katika kutatua matatizo yake. Ndio maana vyama vyote, Taasisi mbalimbali, Jumuiya za kimataifa na n.k zote zina-focus katika hilo maana hilo ndio msingi wa kujitawala na kujikwamua katika nchi yoyote ile duniani, yaani kuwa na watu wenye Elimu na uwezo wa kuikabili nature, ili kuwa na Uchumi imara hasa unaotokana na misingi ya ndani ya nchi hasahasa kwa kuangalia resouces and talents zilizopo. Halafu mwisho unakabili extras as the means of enhancement.

Tatizo letu sio katika siasa, tatizo letu lipo katika Uongozi, unoweza kuleta uzalendo miongo mwa watu ilikuwa na nia sahihi ya maendeleo ya kitaifa na siyo maendeleo binafsi.

Thanks
Mkuu wangu kwanza kabisa hakuna mahala nimefananisha kati ya Marekani na Tanzania isipokuwa pale tu tunapozungumzia kitu kimoja. Kwa mfano tukisemea tuinataka Demokrasia, basi bila shaka tutatazama nini maana ya demokrasia na nchi gani imefanikiwa kupata hilo. Muhimu ni kwamba hatufuati dira waloitumia wao kufikia hapo isipokuwa utaratibu uhnaozungumzia demokrasia ni uleule.

Pia tunapozungumzia Uchumi na maendeleo ya nchi hatuwezi kukwepa ukweli kwamba Uchumi na maendeleo ya nchi una vipimo vyake ambavyo havijali nchi moja kuwa Marekani au Tanzania lakini kila nchi itakuwa na dira, mikakati na hata Utawala wake tofauti na nchi nyingine japokuwa sote tuna lengo moja. Hivyo kufananisha kwangu kunalenga tu yale ambayo yanatafsirika kwa maana moja.

Na kama umenisoma vizurin huko nyuma yote uloandika ndiyo niliyosema ingawa kwa maandishi tofauti. Nilichosema mimi ni kwamba sisi Tanzania tatizo letu tunaioga nchi hizo ktk kufuata misingi ya kibiashara hali sisi bado kabisa hatuna uwezo, nguvu na hata umri wa kushindana ila tunachotakiwa kujenga sasa hivi ni msingi bora wa maendeleo kabla ya kuyatafuta maendeleo.

Mkuu wangu nakuelewa sana, na hakika ndicho nachojaribu sana kukizungumzia hapa kwani stable state haiwezi kupatikana ikiwa vitu muhimu kama hivyo havipo ktk vipaumbele vya kitaifa. Tanzania leo tumepoteza kabisa Utamaduni wetu, kiswahili hapipendwi wala sii sifa ya kumpa mwananchi ajira. Atakuja Mkenya au MNigeria akizungumza kiingereza atapewa kazi pamoja na kwamba hafahamu kabisa kiswahili.. Na mtu huyo kazi na jukumu alokabidhiwa ni kuwahudumia Watanzania ambao asilimia 80 hawajui Kiingereza.

Hapo tayari umeshavunja nguvu ya rasilimali watu kwa sababu tu tunaamini ELIMU ni kiingereza. Na bahati mbaya sana hatuwezi kuzungumzia Uchumi bora ikiwa hata fedha yetu haitakiwi as means of exchange isipokuwa Dollar ndio legal tender kinamna.

Itafikia wakati hata Mkuilima atakuja dai dollar kuuza mazao yake hivyo Tsh itazidi kupoteza thamani yake hali wananchi wanaendelea kulipwa kwa Tsh..Hivyo rasilimali watu sii tu uwezoi wa wananchi kuzalisha isipokuwa malipo bora na kuthaminika kwao ndiko kunajenga vitu vyote tunavyovihitaji.

Na nikirudi kwa Mkapa, mkuu wangu Waswahili wanasema Mkeo akiwa tasa (asiyeweza kuzaa) kwanza jitazame wewe mwenyewe!..Nitaendelea kusema hivi vile viwanda na mashirika ambayo Mkapa aliyakuta yakichechemea yameshindwa kuzalisha sii viumbe vinavyofikiria kufanya hivyo ila ni sisi binadamu wananchi tulokuwa tukiendesha mashirika hayo..Kama kulikuwa na kasoro zosote nbasi kasoro hizo zilikuwa sisi waendeshaji wa mashirika na viwanada hivyo sii kosa la mashirika wala viwanda.

Hivyo alichotakiwa Mkapa kufanya ni kuhakikisha kwamba viwanda na mashirika yale yanapata uongozi bora zaidi kuyapa mwanzo mpya badala ya kuyauza kisha leo hii hatuna tena mashirika hayo isipokuwa tunaagiza kila kitu kutoka nje..Na kibaya zaidi tumeendelea kufanya hivyo ktk resourses zote kwa visingizio vya elimu ya wananchi wake hali all foreign investment nchini mwetu wafanyakazi wake kwa asilimia 99.9 ni Watanzania ukiondoa top management..Hivyo, basi tunajengewa woga - Fear, na imani ya kutojiamini zaidi ili tuendelee kuuza utu na Uhuru wetu kwa sababu hatujiamini.

Elimu haina mwisho. hata nchi tajiri kama Marekani bado inatafuta elimu na ipo ktk ushindani kiasi kwamba miaka 10 tu iliyopita ilikuwa ikiongoza duniani lakini leo wameshuka chini ya 10 bora, hivyo elimu sii swala la kukamilika kwani haliina mwisho. Tulipofikia tutaweza kwenda na uwezo wa elimu yetu na taratibu nchi itakuwa zaidi kwa nguvu tutakayoiweka ktk elimu na maendeleo kwa Ujumla. Hata hao walioendelea walianza na wasomi wachache sana lakini walikuwa makini sana ktk nguvu ya uzalishaji na soko (Demand and Supply), hivyo kupanua mahitaji ya elimu kwa kila hatua.

Mwisho, nitasema kwamba ktk makuzi ya Uchumi wa nchi yeyote ile hakuna formula na kibaya zaidi ni kwamba sisi Tanzania tunajaribu sana kupata maendeleo ktk hali mbaya, ni sawa na mgonjwa ambaye anatakiwa kupata ponya (dose) kwanza kabla ya kurudi kazini kuweza kuzalisha.
 
Mbona nchi za Asia kama China walifuata mfumo wa Ujamaa na hadi sasa wanao na taifa lao ndo limekuwa 2nd largest economy in the world from USA,?
JKN alichokikataa ni ule mfumo wa IMF/WB wa ku-dictate yaani ufanye kama wanavyotaka ,mnajikuta mna nchi kama jina tu huku ikiongozwa na kutoka Washington,hakutaka kutegemea misaada ya hao,alipenda sna tujitegemee wenyewe,ila sema tu tatizo la vita vya Iddi Amini pia vilichangia sana kuporomosha uchumi wa taifa na sarafu yetu kwa ujumla na kwa hilo kulikuwa hakuna mbadala zaidi ya vita.
Sasa leo tuna hao IMF/WB pamoja na kubinafisisha lakini taifa leo nusu ya bajeti yake inategemea wahisani,maana yake wahisani wakigoma wakati wowote serikali ina-collapse/default.J eni wapi tunakokwenda?ni wapi pazuri?
kweli kila mfumo una mazuri na mabaya yake,na kunapokuwa na matatizo kinachotakiwa ni kurekebisha na kuendelea na mazuri yake sio kuvunja mfumo mzima kama walivyofanya waliomfuatia JKN.Kuna mengi tu yaliyokuwa ni mazuri katika ujamaa ambayo huwezi kuyakuta katika nchi yeyote Africa hata hivyo pia kulikuwa na matatizo mengi ambayo hayawezi kupingika.
Mtoto wako akikunyeea je unakata mkono au unajisafisha?
Alitaka, kwa mfano, NMC irudi kwa akina Chande. Wao wamiliki 51% na serikali ibaki na 49%. Mzee Mtei alichokuwa anasisitiza ni serikali iache menejimenti ya mashirika haya. Na hili wala halikuwa wazo lake lilikuwa ni wazo la IMF na WB. Mkapa alikubali karibu kila kitu. Tumeishia wapi?
 
Mbona nchi za Asia kama China walifuata mfumo wa Ujamaa na hadi sasa wanao na taifa lao ndo limekuwa 2nd largest economy in the world from USA,?
JKN alichokikataa ni ule mfumo wa IMF/WB wa ku-dictate yaani ufanye kama wanavyotaka ,mnajikuta mna nchi kama jina tu huku ikiongozwa na kutoka Washington,hakutaka kutegemea misaada ya hao,alipenda sna tujitegemee wenyewe,ila sema tu tatizo la vita vya Iddi Amini pia vilichangia sana kuporomosha uchumi wa taifa na sarafu yetu kwa ujumla na kwa hilo kulikuwa hakuna mbadala zaidi ya vita.
Sasa leo tuna hao IMF/WB pamoja na kubinafisisha lakini taifa leo nusu ya bajeti yake inategemea wahisani,maana yake wahisani wakigoma wakati wowote serikali ina-collapse/default.J eni wapi tunakokwenda?ni wapi pazuri?
kweli kila mfumo una mazuri na mabaya yake,na kunapokuwa na matatizo kinachotakiwa ni kurekebisha na kuendelea na mazuri yake sio kuvunja mfumo mzima kama walivyofanya waliomfuatia JKN.Kuna mengi tu yaliyokuwa ni mazuri katika ujamaa ambayo huwezi kuyakuta katika nchi yeyote Africa hata hivyo pia kulikuwa na matatizo mengi ambayo hayawezi kupingika.
Mtoto wako akikunyeea je unakata mkono au unajisafisha?
 
Mkandara:

Samahani kwa kupunguza posti yako. Kwanza masuala ya ku-centralize na ku-decentralize tuliambiwa na watu haohao.

Nyerere alipokuwa anafanya centralization alipata baraka kutoka kwa mashirika na wahisani hayo-hayo ambao baadaya walitaka afanye decentralization.

Katika kipindi cha 1968-1980s, WB, IMF na wahisani waliamini kuwa umasikini wa nchi za kiAfrika utaondokana kwa kuiwezesha serikali kuendesha shughuli za maendeleo.

Hivyo wakati Nyerere anasaidia kuanzisha miradi ya maendeleo, Mobutu, Kenyatta, Banda na wengine walifaidika na misaada hiyo na wao walianzisha mashirika ya kiserikali.

Na matatizo ya kiuchumi yalioanza mwishoni mwa 79 and mwanzoni 80 yalitokea katika nchi zote za kiAfrika bila kungalia Itikadi ya nchi hizo.

Kwa mfano Félix Houphouët-Boigny, the father of African Capitalism, alijenga taifa imara kiuchumi na kijamii kwa kutumia misaada ya kifedha na kiutaalamu kutoka ufaransa. Matatizo ya dunia ya kiuchumi mwanzoni mwa 1980, yalisababisha migogoro ya kisiasa na kijamiii yanayoendelea mpaka sasa.


Kwa upande mwingine, Julius Nyerere, the father of African socialism, alijenga a welfare state kwa kutumia misaada kutoka nchi wahisani. Na matatizo ya kiuchumi ya 1980 yalisababisha uchumi na maendeleo ya Tanzania kuyumba mpaka leo.

Vilevile katika Afrika kulikuwepo na madikteta. Mfano mzuri ni Mobutu Seseseko. Naye kwa kutumia misaada kutoka nje aliweza kuleta maendeleo kwa kipindi fulani nchini Zaire. Mwaka 1970, Zaire chini ya Mobutu Seseseko ilikuwa na balanced bajeti.

Katika ziara yake Marekani, President Nixon alisema yafuatayo kuhusu Mobutu: "I find in studying your administration that you not only have a balanced budget but a favourable balance of trade and I would like to know your secret before meeting with the cabinet.'"

Ukichukua mfano hiyo hapo juu utaona kuwa misingi ya kiuchumi iliyotumika na serikali za kiAfrika ilikuwa FALSE.

Tulitumia favorable conditions zilizojitokeza wakati wa cold war kujenga uchumi. Ujamaa wa Tanzania usingekuwa ujamaa bila nchi za Scandinavia na zingine zenye liberal policies kumwaga misaada.

Vilevile Ufaransa ndio waliofanikisha Capitalism iliyokuwepo Ivory Coast na sio sera za Félix Houphouët-Boigny.

Na mwishoni bila misaada ya USA. Mobutu hazingeweza kukaa kubalance bajeti ya Zaire 1970.

Zakumi, hapa nichangie kidogo kuhusu IMF/WB kukubali Tanzania inazishe mashirika ya Umma. Kumbuka kwamba 1961 IMF/WB zilikuwa na miaka 20 tuu. Na hizi Organization zilitengenezwa kuwalinda wakubwa baada ya 1945, hasa kuijenga nchi za Ulaya ambazo zimeathirika na vita ya II ya dunia. Kwa hiyo 1960's hawa jamaa focus yao ilikuwa sana kwenye kujenga western hemisphere.

1970's mambo yakabadilika, sababu swala la DEVELOPING ECONOMY likawa new terms kwenye economics. Na hawa jamaa ndio wakashika hatamu. Kumbuka ya kwamba hawa mabwana Policies zao zinaendana kabisa na viongozi walio madarakani katika nchi ya USA and UK. 1976 Mafuta yalianza kupaa, Jimmy akaingia madarakani na policies zake za mlengo wa kushoto na zikashindwa. 1980's sasa ndio IMF/WB zika adopt agenda mpya ya Free trade, deregulation, privatization and small government. Hii ni conservative theory ambayo kwenye economics ni tricle down theory, which is more ideology kwa nchi za Africa.

Mwalimu aliukataa huu mfumo. Politics ndio ilikuwa inaongoza uchumi miaka 1980, na sio wachumi.
 
Mkuu:

Polls are pageantry contests and can't be used for validations of economic and financial theories. Besides, the Federal Reserves Bank of the USA is an independent organization which set its own policies.

Kwa mtaji huo, Ben Bernanke anapotoa sera zake, Obama na Democratics hawamwingilii. Na sera za Fed zimekuwa consistency bila kujali nani yupo madarakani.

Kuhusu theories za John Maynard Keynes hata Reagan na Bushes walizitumia. Katika vipindi vya hao republicans, matumizi ya jeshi yaliongezeka. Matumizi hayo yaliongeza kukua kwa military industrial complex ambazo zilitoa kazi kwa waMarekani. Misingi ya Internet unayotumia sasa ilijengwa na DoD.

Mzee Zakumi,

Hapo umegusa point ambayo nimekuwa nikilia nayo miaka nenda uje, means separation of power between Central Bank and Central Government. Hapa ndio kazi tunayo Tanzania, kwamba monetery policies zinakuwa crafted Ikulu and Fiscal Policies zinakuwa crafted Ikulu. You can't run a country kwa njia hiyo.

Serikali ingebaki kwenye swala la Fiscal Policies, kisha Gavana abaki kwenye monetary polices. Na bunge kuwa lina waangalia hawa wote wawili, na Bunge liwe lina Vote pendekezo la ugavana. Sio unampa mtu ugavana sababu mlikuwa mnacheza wote mduara Jolly's club, that is non sense.

Ndio maana nilisema Ndulu and Balali wote hawa qualify kuwa Magavana, period. Sababu hawa wote ni product ya World Bank and IMF ambapo ni makao makuu ya One Fits all policies, na hawa mabwana wanaimani kabisa na hawa watu.

Juzi nimesikia habari kutoka kwenye source yangu kwamba BOT iko kwenye trouble for sometime, na wanataka kutumia tools kama quantitave easing. Na hapo utaona kabisa walioshauri huo upuuzi ni wale wale IMF/WB.... Hawa jamaa ni washikaji zake JK, na ndio maana utaona mwaka juzi walikuja pale Kempisk kuleta wazimu wao, na JK akajitafuna tafuna pale.

Economist wetu inabidi wakae chini watoe recommendation za kumsaidia Mkulima kuyatoa. Nasio MKUKUTA, sometime unatamani hata kulia unapoangalia mababa mazima yanakaa chini na kukocopy upuuzi kama MKUKUTA, wazungu wanatucheka, walai wanacheka.
 
Huyo ndiyo MJAMAA Nyerere alivyofeli, lakini kuna la watu linaendelea kumshangilia Dictactor
 
Ushauri wa Mzee E Mtei kama ungekubaliwa na Mwl J K Nyerere wakati ule bila shaka mashirika yetu mengi ya umma yasingekufa na yangekuwa yanamilikiwa na watanzania [wazawa].

Ukaidi na ubishi wa Mwl J K Nyerere ulikuja kuliletea taifa hasara kubwa na bado tunaendelea kulipa gharama mpaka leo.

Mashirika ya umma yalikuja kuuzwa baadaye kwa wageni tena kwa bei ya kutupwa.Kwa kweli mpaka leo bado nakataa kabisa kumuenzi Mwl Nyerere kwasababu sera zake zimetufikisha kwenye lindi la umaskini mkubwa.
Nimeisoma hii na naona Magu anaelekea kule kule.....
 
Ushauri wa Mzee E Mtei kama ungekubaliwa na Mwl J K Nyerere wakati ule bila shaka mashirika yetu mengi ya umma yasingekufa na yangekuwa yanamilikiwa na watanzania [wazawa].

Ukaidi na ubishi wa Mwl J K Nyerere ulikuja kuliletea taifa hasara kubwa na bado tunaendelea kulipa gharama mpaka leo.

Mashirika ya umma yalikuja kuuzwa baadaye kwa wageni tena kwa bei ya kutupwa.Kwa kweli mpaka leo bado nakataa kabisa kumuenzi Mwl Nyerere kwasababu sera zake zimetufikisha kwenye lindi la umaskini mkubwa.
Sawa na ukaidi wa Jiwe sahivi.
 
Hapa chini ni post ya Mzee Edwin Mtei alipojiunga kujibu maswali mbalimbali ktk mada hii.



" Rafiki yangu amenipigia simu kushauri nifungue JF nione yanayosemwa juu yangu na hasa kutofautiana kwangu na Mwalimu Nyerere. Namshukuru. Nawashukuru pia wanaoonyesha interest katika simulizi hii ya maisha yangu iliyopo katika kitabu "From Goatherd to Governor"nilimojaribu kuweka experience na maoni yangu.


Pili katika comments hizi nimejifunza mengi na ningetaka kufuatilia hasa maandiko ya Godfrey Mwakikagile ambaye kama ikiwezekana ningemkaribisha nyumbani kwangu Arusha tuweze kujadili misimamo ya Mwalimu.. Hata Bwana "Shwari" pia ningeomba tukutane tubadilishane mawazo.


Tatu, nimesoma "Shwari" akisema na kukubaliana kwamba ili nchi kama yetu iendelee inahitaji "massive transfer of resources from developed countries". Naweza kusema ni mazingira yanayoweza ku-attract such resources nilijaribu kum-persuade Mwalimu akubali kuyaandaa Tanzania, lakini nikashindwa. Nimekiri katika kitabu changu kwamba the weakness I regret most in me is that I was not persuasive enough to make Mwalimu accept my approach to national economic issues.


Nne, kuna wanaJF wanaodhani ni mimi nilisababisha matatizo ya kiuchumi na fedha niliyotaka kuyatatua mwaka 1979/80. Nawashauri wasome hicho kitabu. Kwanza Vita vya Kagera au Idi Amin, by any stretch of the imagination, could not have been caused by or attributed to me. This was the immediate cause although I also highlightin my book the policies emanating from the Arusha Declaration and the mismanagement of the public corporations.


Tano, kuhusu lile tukio la mwisho la Mkutano kati ya Mwalimu, mimi na IMF Mission, nakumbuka ni Bo Karlstrom, IMF Delegation Laeader na mimi tu, tulizungumza. IMF staff aliyekuwepo alikuwa anaandika tu yale yaliyokuwa yanasemwa. Kama mtu huyo alijigamba baadae kwamba alizungumza pale, ni uzushi.


Mwisho, nakubaliana na wanaoshauri kwamba Press Secretary wa Mwalimu wakati huo, Paul Sozigwa aulizwe ili athibitishe kama aliagizwa atangaze "Edwin amejiuzulu" au la. Joseph Butiku aliyekuwa Msaidizi wa Mwalimu wakati huo anaweza pia kuulizwa. Wote JF wanawafahamu.


Ningetaka kurudia shukrani zangu kwa Watanzania wanaoonyesha interest katika mambo niliyaandika kuhusu maisha yangu na utumishi wangu kwa nchi yangu. " -- Edwin Mtei
 
Back
Top Bottom