Mkuu wangu hapa sijui umezungumza kipi maanake kama utasema tatizo letu sio demokrasia ni system ya Uchumi lakini unarudi nyuma sana kwenye Ujamaa badala ya kuzungumzia system gani mbaya wakati huu..Hivi sisi hatufuati freemarket economy leo hii au unahesabu sisi wakati wa Nyerere lakini China hutaki kuhesabu wakati wa Mao Tse Tung ila wakati huu au toka Deng.Tatizo letu Tanzania siyo Demokrasia, bali ni system ya Uchumi. Ujamaa umeturudisha nyuma kimaendeleo kwa sababu tulikuwa tunategemea kila kitu kifanywe na serikali. China haina Demokrasia lakini uchumi wao mzuri kwa sababu wanafuata free market. Saudi Arabia hawana Demokrasia, lakini uchumi wao mzuri kwa sababu wanafuata free market.
Mpaka leo Tanzania, bado tunaamini kwamba serikali ndiyo Solution, kwa sababu ya Ujamaa. Hili ndilo tatizo linalorudisha nyuma Tanzania kimaendeleo.
Mkuu kama umenisoma vizuri nimetumia Demokrasia kama mfano unaoweza kuonyesha madhara ya kuiga vitu pasipo kuwa na malengo kulingana na watu na mazingira yenu..Nimetenganisha Utawala bora unaotegemeana demokrasia ili kuondoa Udikteta (malengo) na kuweka mamlaka hayo mikononi mwa wananchi wake, jambo ambalo halikutokea kwetu lakini limetokea nchi nyinginezo.. mfano huu nimeuweka ili mradi kufananisha hali hiyo na mfumo wa kiuchumi unaotumia free market kwa lengo la kukuza Uchumi lakini pia sisi tumeshindwa kufanikiwa ndani ya freemarket.
Mwisho, Mkuu wangu China hakuna freemarket economy na ndio maana wanapanga thamani ya fedha yao, nani anaruhusiwa kuingia nchini mwao, miradi gani ya wananchi na ipi ya mashirika ya nje na kwa masharti gani... Kisha, Saudi Arabia pia hawafuati free market economy huwezi kwenda huko na kuwekeza kama unavyoweza kufanya nchi za magharibi.. Utajiri na mali yao ni hazina ya Sultani na nasaba yake hao wengine wote wanakula zaka na sadaka tu ya mfalme...
Udikteta wa Saudia ni wa Ki monarchy na ule wa China ni sawa na CCM isipokuwa mazingira yetu na China ndio tofauti pia wao wameendelea kuwa Wajamaa hadi leo kwani still uchumi wao uko controlled na serikali kwa kupitia majimbo. Hawakubinafsisha kila kitu hivyo huwezi kusema ni freemarket economy na wala sii Ukomunist ingawaje bado chama tawala kina nguvu na mamlaka sawa na wakati wa Mao Tse Tung..