Mtei alipotofautiana na Mwalimu Nyerere

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,883
31,049
SI mara nyingi viongozi walioshika nyadhifa za juu katika Tanzania huamua kuandika vitabu vinavyoelezea maisha yao binafsi na ya utumishi wa umma wakati wanapostaafu.

Kwa sababu ya kasoro hiyo, baadhi ya mambo ya kihistoria waliyoyatenda wakati wa utumishi wao, hayafahamika kwa vijana wengi wa leo.

Pengine ni kwa sababu hiyo, mmoja wa viongozi hao wa zamani ambaye alipata kuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu Tanzania na Waziri wa Fedha na Mipango, Edwin Mtei, aliona busara ya kuandika kitabu kinachoelezea maisha yake.

Kitabu hicho, kinachoitwa From Goatherd to Governor, kilizinduliwa Jumanne ya wiki iliyopita mjini Dare es Salaam katika sherehe fupi iliyohudhuriwa pia na watu kadhaa maarufu nchini.

Mmoja wa wazungumzaji katika hafla hiyo alikuwa mwandishi na mchapishaji wa vitabu nchini, Walter Bbgoya wa kampuni ya uchapishaji ya Mkuki na Nyota. Yeye hakutaka kuwa mnafiki mbele ya Mtei.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kitabu hicho From Goatherd to Governor’ (kutoka kuwa mchunga mbuzi hadi kuwa gavana) kwenye ukumbi wa British Council, Dar es Salaam, Bbgoya alisema kwamba alikuwa mmoja wa watu waliokuwa upande wa Mwalimu Nyerere alipotofautiana naye kuhusu sera za uchumi.

Bbgoya, ambaye sasa ni mmoja wa wanafamilia ya Mtei (kutokana na watoto wao kuoana), alisema wakati huo aliungana na msimamo wa Mwalimu na kukubaliana naye kwamba mashirika ya fedha ya kimataifa yalikuwa yanataka kuiburuza Tanzania.

Hata hivyo, alimsifu kwa kuwa na ujasiri usiokuwa wa kawaida wa kukisimamia kile alichokuwa akikiamini licha ya kupingwa na Mwalimu hivyo kuwasilisha yeye binafsi barua ya kujiuzulu kwa kiongozi huyo wa nchi.

Hata Mwenyekiti wa Bodi ya Uhariri ya gazeti hili, Jenerali Ulimwengu alipopewa nafasi ya kuzungumza, pamoja na mambo mengine, alimsifu Mtei kwa kulieza kwa ufasaha mkubwa tukio la kujiuzulu kwake uwaziri baada ya kutofautiana na Mwalimu mapema Desemba, 1979.

Aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ibrahim Kaduma, ambaye alifanya kazi na Mtei katika Wizara ya Fedha, alimsifu Mtei kwa uzalendo aliokuwa nao wakati wote alipokuwa mtumishi wa umma.

Alisema kwamba mambo mengi leo yanakwenda ovyo kwa sababu watu hawaweki uzalendo mbele kama walivyokuwa wanafanya watu wa aina ya Mtei walipokuwa serikalini.

Alitoa mfano wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mjini Dar es Salaam.

Alisema kwamba Mtei hakutaka jengo hilo lijengwe na kampuni ya ujenzi ya nje ya nchi hivyo akasisitiza ujenzi huo ufanywe na kampuni ya kizalendo ya Mwananchi Engeneering and Contracting Company (MECCO) iliyokuwa chini ya chama cha TANU ikapewa kazi hiyo baada ya kushinda zabuni.

Kwa hakika, ukisoma kitabu cha From Goatherd to Governor, sakata zima la kujiuzulu kwake uwaziri litakushangaza kama wengi walivyoshangazwa hata na Mtei mwenyewe kwamba hakupata kujikuta katika msukosuko mkubwa au kulazimika kuikimbia Tanzania.

Ndiyo, tukio kama hilo wakati wa enzi hizo za chama kimoja katika nchi nyingi za Afrika lilikuwa sababu tosha ya kuonekana au kuchukuliwa kuwa mhaini, hivyo lolote lingeweza kumpata.

Lakini Mtei, si tu hakupata msukosuko wa aina yoyote, lakini miaka mitatu baadaye Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa IMF akiwakilisha nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza isipokuwa Afrika Kusini enzi hizo za ubaguzi wa rangi nchini humo.

Hivyo akaenda kwenye makao yake makuu mjini Washington, Marekani ambako alifanya kazi hiyo kwa miaka minne akizunguka dunia katika kuifanya kazi hiyo kwani alikuwa anahitajika kusafiri sana.

Lakini ni nini hasa walichokuwa wamekosana na Mwalimu hata akalazimika kujiuzulu uwaziri wa fedha? Ni hadithi ndefu, lakini kimsingi ni kwamba Mwalimu alikataa kukubaliana na mpango wa IMF wa kurekebisha uchumi wa Tanzania wakati huo kama yeye alivyokuwa amekubaliana na ujumbe wa IMF ulioongzwa na Bo Karlstrom, raia wa Sweden.

Kulikuwa na mambo mawili ambayo Mwalimu hakukubaliana nayo na mambo hayo ni kupunguza thamani ya shilingi na kufanya marekebisho ya menejimenti ya mashirika ya umma ambayo mengi yalikuwa yakiendeshwa kwa hasara.

Kuhusu mashirika hayo yaliyokuwa yakiendeshwa kwa ruzuku ya serikali yalivyokuwa yakiendeshwa kwa hasara, Mtei anaeleza katika kitabu hicho jinsi alivyompatia mtaalamu mmoja wa Denmark kazi ya kuchunguza shughuuli za lililokuwa Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC).

Ripoti ya mtaalamu huyo ilionyesha matumizi mabaya ya magari ya shirika hilo yaliyokuwa yakifanywa na viongozi wasio waaminifu na madereva.

Kutokana na ripoti hiyo, Mtei anasema aliona kwamba dawa ya kuyanusuru mashirika hayo ni kuwa na mameneja na wasimamizi ambao pia ni wadau katika uendeshaji wa makampuni hayo.

Mtei anasema wazo lake lilionekana kuwa na chembechembe za ubebari, kitu ambacho kilikuwa sumu wakati huo. “Lakini ilikuwa muhimu kuwa muwazi kwa Rais, kwani sikuwa na ufumbuzi mwingine,” anasema Mtei.

Kwa kuwa na wazo hilo, Mtei anasema alikuwa amefikiria kuwakaribisha watu au makampuni yanayomilikiwa na Chande Industries kurejeshewa sehemu ya hisa ili kuwepo na menejimenti nzuri na mali za shirika zipate kulindwa.

Kwa mujibu wa Mtei, mpango huo ungefanikiwa kwa kuwa Andy Chande mwenyewe aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa NMC na chini yake shirika hilo liliendedshwa kwa mafanikio makubwa.

Ujumbe wa IMF ulitoa wazo ambalo alikubaliana nalo kwamba kama taifa litapunguza matumizi ya ulinzi na kufanya marekebisho ya menejimenti za mashirika ya umma ili ziondokane na ruzuku kubwa inayotoka serikalini, thamani ya shilingi ingepunguzwa na kuanzia hapo mambo taratibu yangekwenda vizuri.

Kwa mujibu wa Mtei, suala la kuingilia menejimenti za mashirika ya umma na kupunguza thamni ya shilingi, ni mambo ambayo Mwalimu alikuwa hataki kuyasikia.

Baada ya kumweleza Karlstrom msimamo wa Mwalimu, Ofisa huyo wa IMF aliomba ujumbe wake ukutane naye Mwalimu. Ofisa huyo alikuwa na matumini kwamba angeweza kumfanya Mwalimu alegeze msimamo wake.

Mtei alifanya mpango wa kukutana na Mwalimu na akafanikiwa kuwakutanisha nyumbani kwa Mwalimu (Msasani), Novemba 29, 1979. Kilichotokea siku hiyo ndicho kilichomfanya Mtei ajiuzulu uwaziri.

Kwa mujibu wa Mtei, Mwalimu alishikilia msimamo ule ule na si tu hakuyumba; bali aliuupuza katikati ya mazungumzo kwa kuondoka ghafla kwenda kupunga upepo eneo la baharini nyuma ya nyumba yake ya Msasani.

Baada ya kuwaacha solemba kwenye veranda, Mtei alimfuata Mwalimu ili angalau amwambie kwamba wanaondoka. Alipomwendea, Mwalimu akamwambia kwamba wageni waliokuja walikuwa wajeuri na yeye hawezi kuiacha nchi yake iongozwe kutoka Washington (Marekani).

Alimwambia kwamba awaambie warudi Washington; kwani yeye hatathubutu kuishusha thamani ya Shilingi ya Tanzania.

Mtei anasema katika kitabu hicho kwamba hakulala usingizi siku hiyo aliporudi nyumbani. Akakata shauri ajiuzulu uwaziri. Siku inayofuata ilikuwa ya mapumziko lakini pamoja na hivyo akaenda ofisini asubuhi kuandika barua hiyo ya kujiuzulu.

Aliandika barua hiyo ya kujiuzulu kwa mkono wake ili baadaye ipigwe chapa. Baada ya kumaliza kuiandika barua hiyo akapokea simu kutoka kwa John Malecela aliyekuwa Waziri wa Kilimo kwamba wanatakiwa nyumbani kwa Mwalimu Msasani.

Mwalimu alikuwa amewaita kuzungumza nao suala la Serikali kununua kiwanda cha Tanganyika Planting Company kilichokuwa kinamilikiwa na Denmark.

Baada ya kufika ofisini kwake alidhamiria kuiwasilisha barua ile ya kujiuzulu aliyoiandika kwa mkono; hivyo alipotoka ofisini kwa safari ya Msasani, nje ya ofisi hiyo akakutana na msaidizi wa Mwalimu ambaye alimpatia barua.

Akaitupa barua hiyo kwenye kiti cha gari yake bila ya kuisoma. Akakaa kwenye kiti cha dereva tayari kwa safari ya kurudi tena Msasani kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu.

Baada ya kuisoma barua yake, Mwalimu alimwuliza iwapo msaidizi wake alikuwa amempatia barua aliyomtuma ampe. Mtei akamweleza kwamba alikuwa amekutana naye nje ya ofisi na kumkabidhi barua hiyo ambayo hajaisoma kwani iko kwenye gari.

Mwalimu alionekana kufikiria kidogo na kumwambia kwamba anamshukuru kwa barua yake. Akamwita msaidizi wake kumwambia kwamba akatangaze kwenye vyombo vya habari kwamba Waziri wa Fedha amejiuzulu na kwamba yeye amekubali.

Kumbe barua ambayo Mtei alikuwa bado hajaisoma ilikuwa inatoka kwa Mwalimu ikimweleza kwamba ametengua uteuzi wake wa uwaziri wa fedha!

Katika barua hiyo fupi, Mwalimu alimweleza kwamba ameamua kutengua uwaziri wake wa Fedha na Mipango na kuongeza kwamba asingeruhusu serikali kuongozwa na Washington.

Katika aya nyingine ya barua hiyo, Mwalimu alisema kwamba alikuwa amemuelekeza awafukuze nchini watu hao wa IMF; lakini yeye (Mtei) hakufuata maelekezo yake.

Mtei anasema katika kitabu hicho kuwa asingeweza kuijibu barua hiyo au kumwandikia barua Rais kwa ufafanuzi kwa sababu aliamini kwamba kwa kupokea barua yake ya kujiuzulu na kuikubali, ile ya kwake ya kutengua uwaziri wake ilikuwa imefutwa.

Hata hivyo, alisikitika kwamba Mwalimu bado alikuwa ameshikilia msimamo wake kwamba juhudi walizokuwa wakizifanya zilikuwa zinatokana na maelekezo kutoka Washington.

Pia Mtei anasema alishindwa kutafisri maneno ya Mwalimu alipomwambia kwamba watu hao warudi Washington kuwa ni sawa na kwamba “wafukuzwe nchini”.

Mtei anashangaa katika kitabu hicho kwa kutupiwa kazi ya kuwafukuza maofisa hao wa IMF nchini wakati yeye hakuwa waziri anayehusika na kuwafukuza nchini wahamiaji haramu.

Mtei, ambaye sasa ni mkulima wa kahawa mkoani Arusha, ni mwanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Hicho ni chama pekee ambacho Mwalimu aliwahi kukisifu kwamba kina sera nzuri miongoni mwa vyama upinzani nchini


Source: Raia Mwema
 
Ushauri wa Mzee E Mtei kama ungekubaliwa na Mwl J K Nyerere wakati ule bila shaka mashirika yetu mengi ya umma yasingekufa na yangekuwa yanamilikiwa na watanzania [wazawa].

Ukaidi na ubishi wa Mwl J K Nyerere ulikuja kuliletea taifa hasara kubwa na bado tunaendelea kulipa gharama mpaka leo.

Mashirika ya umma yalikuja kuuzwa baadaye kwa wageni tena kwa bei ya kutupwa.Kwa kweli mpaka leo bado nakataa kabisa kumuenzi Mwl Nyerere kwasababu sera zake zimetufikisha kwenye lindi la umaskini mkubwa.
 
Halafu mnatulazimisha tumfanye mtakatifu.Mwalimu katutia umaskini mkubwa watanzania bahati mbaya mpaka leo bado kuna watu wanatakuamisha eti alikuwa sahihi kutuingiza watanzania katika siasa za ujamaa.
 
Halafu mnatulazimisha tumfanye mtakatifu.Mwalimu katutia umaskini mkubwa watanzania bahati mbaya mpaka leo bado kuna watu wanatakuamisha eti alikuwa sahihi kutuingiza watanzania katika siasa za ujamaa.
nani tena huyo mkuu anayekulazimisha bila ridhaa yako? Kwa bahati mbaya waliofuata baada ya Nyerere sio tu walitufanya tubakie pale tulipokuwa, bali turudi nyuma hatua nyingi na kuwa Taifa lisilo na mwelekeo.
 
<font size="3">Ushauri wa Mzee E Mtei kama ungekubaliwa na Mwl J K Nyerere wakati ule bila shaka mashirika size="3">Ukaidi na ubishi wa Mwl J K Nyerere ulikuja kuliletea taifa hasara kubwa na bado tunaendelea kulipa gharama mpaka leo.

Mashirika ya umma yalikuja kuuzwa baadaye kwa wageni tena kwa bei ya kutupwa.Kwa kweli mpaka leo bado nakataa kabisa kumuenzi Mwl Nyerere kwasababu sera zake zimetufikisha kwenye lindi la umaskini mkubwa.

Katika nchi mpya zilizoendelea huko Asia hawakufuata ushauri mbovu wa IMF. Ni ujinga kuongozwa toka W/DC. Kwa sasa tunafuata huo msahafu wao na mambo ndo kama vile yanarudi nyuma. Wao kila ugonjwa dawa ni panadol. Kansa yetu ni ya kizazi ambapo kupona kwake mpaka kiondolewe.
 
Ushauri wa Mzee E Mtei kama ungekubaliwa na Mwl J K Nyerere wakati ule bila shaka mashirika yetu mengi ya umma yasingekufa na yangekuwa yanamilikiwa na watanzania [wazawa].
Ukaidi na ubishi wa Mwl J K Nyerere ulikuja kuliletea taifa hasara kubwa na bado tunaendelea kulipa gharama mpaka leo.

Mashirika ya umma yalikuja kuuzwa baadaye kwa wageni tena kwa bei ya kutupwa.Kwa kweli mpaka leo bado nakataa kabisa kumuenzi Mwl Nyerere kwasababu sera zake zimetufikisha kwenye lindi la umaskini mkubwa.
Kinunue kile kitabu cha Mtei ukisome kwanza. Watanzania tumeyaua wenyewe mashirika ya UMMA. Alichokuwa anapendekeza Mtei ni kuwaondoa WAZAWA kwenye MANAGEMENT za mashirika haya kama Mkapa alivyofanya kwa TANESCO akaleta NetGroup yake, akaondoa DAWASA akaleta City Water, juzi hapa JK naye akajaribu kwa TRC na yenyewe inaelekea itashindikana.

Sheria kali kama zile za CHINA ndizo zitakazoiokoa NCHI yetu. Nani ataziandaa na zitapita katika BUNGE lipi?
 
uchumi na siasa ni vitu vinavyokinzana, mwalimu alikuwa mwanasiasa na mtei mchumi,

mandela aliacha ofisi ya sheria ambayo ilikuwa ya kwanza kwa waafrica kwa wakati huo ili atumikie wananchi ambao hata hawajamchagua.....

everyone moved by the spirit to archieve, especially on field he/she desired regardless the money, shame, fame, failure, status, family etc.

nadhani mwalimu na mtei walikuwa na different ideology and ambition, so ikawa rahisi kufall apart, anyway nice to know!
 
mi sioni kwanini mnamlaumu huyu mzee marehemu,.kwani ujamaa ilikuwa ni political ideology kama zilivyo nyingine, ,youcreate an idea then you try to put the same into realit, ikifaulu safi, ikishindikana unatafuta nyingine..someni JURISPRUDENce. ndio maana when he realised kwamba idea yake imekuwa futile, akaamua kuachia nchi na wengine wajaribu, but alileta ujamaa kati yetu, we love each other sio kama kenya uganda somalia etc. hayo ni baadhi ya mafanikio ya ujamaa.. No one who is perfect.
 
...Ngongo nina imani Mtei kwenye kitabu chake atakuwa amedadavua masuala mengi ya msingi kuhusu maendeleo ya nchi yetu wakati ule pamoja na upinzani aliokuwa anaupata...Sijui kama hiki kizazi cha sasa cha viongozi wetu wamejifunza kitu kwa maandiko ya Mtei...Mi naona kama vile nchi imevamiwa na majambawazi....Ufisadi mawio mpaka machweo!!! Wapi naweza kupata hiki kitabu mkuu??
 
Kinunue kile kitabu cha Mtei ukisome kwanza. Watanzania tumeyaua wenyewe mashirika ya UMMA. Alichokuwa anapendekeza Mtei ni kuwaondoa WAZAWA kwenye MANAGEMENT za mashirika haya kama Mkapa alivyofanya kwa TANESCO akaleta NetGroup yake, akaondoa DAWASA akaleta City Water, juzi hapa JK naye akajaribu kwa TRC na yenyewe inaelekea itashindikana.
Sheria kali kama zile za CHINA ndizo zitakazoiokoa NCHI yetu. Nani ataziandaa na zitapita katika BUNGE lipi?

Mkuu mapendekezo ya Mtei hayakuwa kwenye kuleta management za wageni, yalikuwa ni kuweka watu wenye uwezo kwenye management, sasa kama wakati ule tafsiri ilikuwa ni wageni, that is different matter.

Na mapendekezo yake hayakuwa kwenye jambo moja tu, yalikuwa mengi na comprehensive. Mtu yoyote responsible aliyekuwa kwenye wadhifa wake wakati ule angesema kama alivyosema. Kuna baadhi ya wanafiki walikuwa wanasema ndio mzee hata kama wanajua kabisa sio.

Kuna wengine walikuwa wanafiki na kujipendekeza kwa Nyerere, huku mioyoni mwao walikuwa tofauti sana.

Kama tungetekeleza SAPs miaka ile, na kama privatization ingetekelezwa wakati ule, na kama mapendekezo ya Mtei yangetekelezwa basi sasa tusingekuwa tunalia na tuliyofanyiwa na Mkapa, tungekuwa tumepata akili ya kudeal nayo na tungekuwa better than we are now. Still naona kuwa Mzee Mtei alikuwa sahihi.

I wonder JKN alikuwa anaongea nini na Mtei baada ya Mwinyi kuanza kutekeleza ambayo Nyerere aliona hayafai.
 
Mkuu mapendekezo ya Mtei hayakuwa kwenye kuleta management za wageni, yalikuwa ni kuweka watu wenye uwezo kwenye management, sasa kama wakati ule tafsiri ilikuwa ni wageni, that is different matter.

Na mapendekezo yake hayakuwa kwenye jambo moja tu, yalikuwa mengi na comprehensive. Mtu yoyote responsible aliyekuwa kwenye wadhifa wake wakati ule angesema kama alivyosema. Kuna baadhi ya wanafiki walikuwa wanasema ndio mzee hata kama wanajua kabisa sio.

Kuna wengine walikuwa wanafiki na kujipendekeza kwa Nyerere, huku mioyoni mwao walikuwa tofauti sana.

Kama tungetekeleza SAPs miaka ile, na kama privatization ingetekelezwa wakati ule, na kama mapendekezo ya Mtei yangetekelezwa basi sasa tusingekuwa tunalia na tuliyofanyiwa na Mkapa, tungekuwa tumepata akili ya kudeal nayo na tungekuwa better than we are now. Still naona kuwa Mzee Mtei alikuwa sahihi.

I wonder JKN alikuwa anaongea nini na Mtei baada ya Mwinyi kuanza kutekeleza ambayo Nyerere aliona hayafai.
Alitaka, kwa mfano, NMC irudi kwa akina Chande. Wao wamiliki 51% na serikali ibaki na 49%. Mzee Mtei alichokuwa anasisitiza ni serikali iache menejimenti ya mashirika haya. Na hili wala halikuwa wazo lake lilikuwa ni wazo la IMF na WB. Mkapa alikubali karibu kila kitu. Tumeishia wapi?
 
Mwalimu alikuwa sahihi na kama angekubali ushauri mbovu wa Mtei leo tungekuwa na hali mbaya zaidi.

Show me one country iliyoendelea kutokana na sera za world bank na IMF na mimi nitakuonyesha nchi zilizoendelea kwa kukataa ushauri wao mbaya

Kwa bahati mbaya sana mawazo ya Mtei yameshafanyiwa kazi na awamu zilizofuata na matokeo yake ndio hapa tulipo sasa tunalifikiria azimio la Atown.

Mtei kwanza hasemi ukweli, yeye hajajiuzulu bali alilazimishwa/alifukuzwa na Mwalimu. Ndio maana anadai eti barua ya kutengua uwaziri wake hakuwahi kuisoma anakijikuta anawahi kuwasilisha barua ya kujiuzulu! what a coincidence! Kasubiri Mwalimu kafa ndio anatoa uongo wake huu.

Huyu mzee anatakiwa awe mtu wa mwisho kutu hubiria haya kufuatia vituko alivyofanya kwenye uchaguzi wa Chadema hivi karibuni.
 
kanda2 said:
Mwalimu alikuwa sahihi na kama angekubali ushauri mbovu wa Mtei leo tungekuwa na hali mbaya zaidi.

Show me one country iliyoendelea kutokana na sera za world bank na IMF na mimi nitakuonyesha nchi zilizoendelea kwa kukataa ushauri wao mbaya

Kwa bahati mbaya sana mawazo ya Mtei yameshafanyiwa kazi na awamu zilizofuata na matokeo yake ndio hapa tulipo sasa tunalifikiria azimio la Atown.

Mtei kwanza hasemi ukweli, yeye hajajiuzulu bali alilazimishwa/alifukuzwa na Mwalimu. Ndio maana anadai eti barua ya kutengua uwaziri wake hakuwahi kuisoma anakijikuta anawahi kuwasilisha barua ya kujiuzulu! what a coincidence! Kasubiri Mwalimu kafa ndio anatoa uongo wake huu.

Huyu mzee anatakiwa awe mtu wa mwisho kutu hubiria haya kufuatia vituko alivyofanya kwenye uchaguzi wa Chadema hivi karibuni.

kanda2,

..Mtei anadai Paul Sozigwa alipewa agizo na Mwalimu kutangaza kwamba amejiuzulu nafasi ya Uwaziri wa Fedha.

..kama Mtei amemsingizia Mwalimu, basi Paulo Sozigwa yupo, anaweza kusema ukweli wa tukio hili.

..pia nadhani rekodi za RTD zipo na zitaeleza kama taarifa kwa wananchi ilikuwa Mtei amefukuzwa kazi, au amejiuzulu.

..Mzee Butiku na Mzee Apiyo pia walikuwepo na wanaweza kutueleza wananchi nini kilitokea kati ya Mwalimu na Mtei.

..Mtei hakuwa amekubaliana na kila kitu ambacho IMF ilipendekeza. tena kuna baadhi ya mapendekezo kama yaliyohusu exchange rate ambayo Mtei alipendekeza yatekelezwe in two phases ili kuweza kuona kama yanafanya kazi kama IMF/WB wanavyodai. Mtei alikuwa anafanya yote hayo ili ku-accomodate mawazo ya Mwalimu Nyerere.

..bahati nzuri nimeshuhudia awamu za Maraisi wote hapa Tanzania. miaka ya mwisho ya utawala wa Mwalimu ilikuwa migumu sana kiuchumi. hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya na ahueni ilikuwa haionekani ktk kila alichojaribu kufanya Mwalimu Nyerere.


..vilevile ni vizuri tukaelewa kwamba hata wakati wa Mwalimu Nyerere, Tanzania ilipata misaada kibao toka WB na IMF. sijui kama mnakumbuka uswahiba wa Mwalimu Nyerere na Raisi wa WB ambaye alipata kuwa Waziri wa Ulinzi wa US Robert Mac Namara. Tanzania tulichukua uanachama wa IMF wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

..kwa mtizamo wangu tulipaswa kuchukua ushauri wa Mtei kabla hali ya uchumi haijaharibika kabisa. tungechukua hatua zile mapema basi tungekuwa na leverage zaidi ktk ku-neogotiate na IMF/WB.
 
Kama nakumbuka vizuri, Mwalimu alitoa hata hotuba kuhusiana na tofauti zake na Mtei. Nadhani tofauti yao kubwa ilikuwa ni kwenye kushusha thamani ya shilingi ili kuweza kupata mkopo mkubwa toka IMF. Mwalimu katika hotuba yake hiyo alidai kwamba kushusha thamani ya shilingi hakuongezi tija yoyote kwa Watanzania bali gharama ya maisha na akatoa mfano kwamba kama tulikuwa tunanunua trekta moja kwa magunia 10 ya kahawa baada ya kushusha thamani ya shilingi yetu trekta lile lile tungelinunua kwa magunia 15 ya kahawa. Waliokuja baada yake walishusha thamani ya shilingi yetu na hadi hii leo sioni mafanikio yake kwa nchi yetu.

Nakumbuka hotuba hiyo Mwalimu aliitoa usiku (8.00pm EAT au baada ya Taarifa ya habari ya saa mbili) na madhumuni yake ilikuwa ni kuonyesha wapi walihitilafiana na Waziri Mtei mpaka kusababisha ajiuzulu. Mwalimu alitumia muda mrefu sana katika hotuba hiyo kuelezea athari za kushusha kwa thamani ya shilingi na kama mtakavyokumbuka Mwalimu hakuwa mnafiki siku zote alisema ukweli kama ulivyokuwa.
 
This is what JFK called "A Profile in Courage"

History has vindicated Mtei.Hata kama hatua alizopendekeza zisingezaa matunda, zilikuwa inevitable na kuzichelewesha kumesababisha hali kuwa mbaya zaidi tu.

Halafu mnaona Nyerere alivyokuwa anawadiss watu wa administration yake mwenyewe? Yaani mtu mnaongea mwanamme na mwanamme mwenzako halafu mtu anasusa na kwenda kupunga upepo baharini? Anakuacha solemba? Ustaarabu gani huu?

Halafu tukisema Nyerere haambiliki tunaonekana waongo.
 
Bubu Ataka Kusema,

..naomba usome kitabu cha Mzee Mtei ili ujue nini kilitokea kuhusu kushusha thamani ya shilingi.

..vilevile mapendekezo ya Mtei na timu yake hayakuhusu kushusha thamani ya shilingi ya Tanzania peke yake, yalihusu masuala mengi ya jinsi ya kujikwamua na matatizo ya uchumi wakati ule.

..binafsi nadhani Mwalimu angekuwa mkweli ktk kutufafanulia Watanzania kwamba kwa kiasi kikubwa tunahusika na kuporomoka kwa uchumi wetu, leo hii tusingekuwa tunabishana kiasi hiki.

..pia lazima tuelewe kwamba IMF na WB walianza kutuingilia ktk kufanya maamuzi baada ya kuchukua mikopo toka kwao na kushindwa kuonyesha tumefanyia nini mikopo hiyo.

NB:

..kuna mtu amegusia kuhusu Mtei kupendekeza NMC irudishwe kwa familia ya kina Chande.

..katika hili itakuwa vizuri kama tutaelewa kwamba familia ya kina Chande walikuwa wamiliki wa NMC kabla haijataifishwa. vilevile Mwalimu alimteua Chande kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya NMC hata baada ya kuitafisha.

..kuna wataalamu toka Sweden walioletwa kufanya uchunguzi kuhusu biashara na uendeshaji wa NMC. timu hiyo ya wataalamu iligundua matatizo makubwa ikiwemo HUJUMA NA UZEMBE WA WATUMISHI WAZALENDO. moja ya mapendekezo yao ilikuwa ni muundo wa shirika la NMC pamoja na umiliki wake.
 
Bluray said:
Halafu mnaona Nyerere alivyokuwa anawadiss watu wa administration yake mwenyewe? Yaani mtu mnaongea mwanamme na mwanamme mwenzako halafu mtu anasusa na kwenda kupunga upepo baharini? Anakuacha solemba? Ustaarabu gani huu?

Halafu tukisema Nyerere haambiliki tunaonekana waongo.

Bluray,

..unajua hata mimi nilishangaa kusikia kwamba Mwalimu alim-treat Waziri wake wa Fedha, pamoja na ujumbe/ugeni wa IMF/WB.

..personally nadhani Mtanzania yeyote yule ange-serve wakati wa matatizo yale ya miaka ya 80, angekuja na mapendekezo yaleyale aliyoyatoa Mzee Mtei.

..najua umekisoma kitabu hiki, mimi kisa kilichonishangaza ni kile cha kuwapeleka watumishi/wataalamu wa serikali kwenda kuchimba mitaro Dodoma. what a wastage of time, money, and resources!!?
 
Bluray,

..unajua hata mimi nilishangaa kusikia kwamba Mwalimu alim-treat Waziri wake wa Fedha, pamoja na ujumbe/ugeni wa IMF/WB.

..personally nadhani Mtanzania yeyote yule ange-serve wakati wa matatizo yale ya miaka ya 80, angekuja na mapendekezo yaleyale aliyoyatoa Mzee Mtei.

..najua umekisoma kitabu hiki, mimi kisa kilichonishangaza ni kile cha kuwapeleka watumishi/wataalamu wa serikali kwenda kuchimba mitaro Dodoma. what a wastage of time, money, and resources!!?

Nimesoma posti zako tatu. Na itabidi nikipitie kitabu cha Mtei. Kwa sources ambazo nimezipitia zinaonyesha kuwa kulikuwa na mambo mengi wakati ule.

Kwanza kulikuwa na matatizo ya kiuchumi wa kidunia uliosababisha na mambo mengi. Pili vita vilikuwa vimemalizika na gharama za vita zilikuwa kubwa. Hivyo kitaalamu yale aliyopendekeza Mtei yalitakiwa yafanyike.

Kuna sababu ambazo zilichangia Nyerere kutokubaliana na Mtei:

Kwanza kulikuwa na imani kuwa matatizo yaliyoikumba Afrika katika mwisho mwa 70 na mwanzoni mwa 80 yalikuwa ya muda na nchi zinaweza kujitoa. Lakini miaka ilivyokwenda ndio ilionekana kuwa iliyokuwepo ni Phenomena mpya na hakuna nchi itakayoweza kujitoa.

Pili, kulikuwa na imani kuwa miongozi iliyokuwa ikiwepo hile ya Azimio la Arusha ilikuwa safi na njia pekee ya kujenga taifa. Vilevile iliaminika kuwa miongozi hii na chini ya uongozi bora tungefika tu.

Tatu, viongozi waliogopa kuwa mipango ya WB na IMF ingesababisha vurugu kwa miji kwa sababu maisha yangekuwa mazito sana. Tukumbuke kuwa kipindi kile serikali ilifanya expansion kubwa ya ajira na huduma za jamii.
 
Namheshimu sana mzee Mtei kwa uamuzi na mawazo yake, lakini hata yeye alikuwa na makosa mengi sana..kwanza kabisa inasikitisha sana kuona Mtei alijiuzuru sii kwa sababu ya utendaji wake kazi, ila kwa sababu mwalimu aliwamfukuza huyo mjumbe wa IMF...was mwalimu right? aliposema hawezi kuiacha nchi yake iongozwe kutoka Washington!.... Hilo mtajaza wenyewe...ila yangu ni haya.

1. a). Ushauri aliopewa ulitoka IMF ambao hadi leo hii hawana mfano wa NCHI hata MOJA iliyofanikiwa kutokana na mikakati yeke..HAKUNA nchi hata moja jamani mweee! toka hiyo mwaka 1979 hadi leo na nchi kibao zilifuata masharti yao wakapunguza thamani ya fedha zao na kadhalika - Hawajafanikiwa.

b) Kabla ya mwalimu kuondoka July 1984, mwalimu alikubali na kuinua mikono, mawazo ya MTEI yalifuatwa kwa mara ya kwanza.. Tanzania tulifungua milango yetu tukaishusha thamani ya shilingi, mashirika ya Umma si tu yaliuza hisa, ila yaliuzwa kabisa ili serikali isiwe na mkono ndani yake.. Results..NOTHING! ndio kwanza matatizo yamezidi, mpango huo umeibua Mafisadi na matumizi yamekuwa makubwa zaidi kwani hakuna Ofisa wa serikali asiyeendesha gari kubwa, la mama na watoto yote ni chaguo lake. Leo hii serikali inapoteza fedha zaidi ya wakati wowote kwani fedha hii hutoka ktk kodi ya wananchi, hutoka ktk mikataba feki, hutoka katika vikwazo kwa wawekeshaji kwa kuzingatia mkono mtupu haulambwi.

c) Of all people Mtei alitaka kumweka CHANDE kuwa mbia wa serikali...by the way hivi leo huyu Chande anamiliki mashirika mangapi ikiwa toka mwaka 1979 alikuwa bingwa kama sio mafioso! where is he hiding! maanake wawekezaji wakubwa nchini wanajulikana vizuri na wananchi wote.

d) Kupunguza matumizi ya Ulinzi pia siwezi kusema ni wazo zuri ama baya kwani ndio kwanza tulitoka ktk vita na Uganda.. Kenya na Malawi walikuwa na beef na Tanzania kiasi kwamba wakati ule Ubabe wa silaha na jeshi ndio ulitengeneza jina la NCHI..Enzi ya Cold war, hata sisi vijana wa mjini Ubabe ndio ilikuwa deal, huendi club kama huna Ubavu na homeboyz behind you..Hivyo sijui kama Tanzania isingekuwa imara ktk Ulinzi tungeweza kupita kipindi kile pasipo majaribio toka nchi za jirani.

Kifupi, nashindwa kuelewa haswa hiki kitabu cha Mtei kimekuja na lengo gani zaidi ya kuonyesha mwalimu was wrong, and HIM mtei was right.. lakini sijui kama Mtei mwenyewe anaweza kutuonyesha ni jinsi gani Tanzania ingeweza kufanikiwa zaidi ya hadithi ya kufikirika..No one knows kabisa kwa sababu mafanikio ya UCHUMI wa nchi hayapo ktk kitabu ila kuna utaratibu unaolenga mafanikio kwa kuzingatia WATU na MAZINGIRA.

Watanzania wanaitwa WADANGANYIKA sii kwa kufumaniza, ila sisi ni wadanganyika including yeye mwenyewe Mtei..Na asili ya Mdanganyia ni mtu ambaye sii kwamba siku zote huukubali ukweli laa hasha ila yupo karibu sana na kukubali Utapeli na kuuwekea kifua kwmaa ndio ukweli..Ni hali ambayo tunaionma hata katika maisha yetu.. watu wapo radhi kuwekea dhamana wanapodanganywa kuliko kusikia ukweli kwa ni siku zote Utapeli huja kwa lugha moja tu - GOOD NEWS!, na ukweli huja kwa sura mbiili ambazo ndio reality ya maisha ya mwanadamu..Tunadanganywa na matapeli toka kila kona siku hizi...imefikia hata kina Riostam kuwa mipapa, watu ambao tulikuwa tukifukuzana mjinii kusaka misheni town..

Ni Wadanganyika hawa hawa walikuwepo enzi ya mwalimu na ndio hawa wanaoendesha Uchumi wetu leo tukimwondoa yeye mwenyewe Mtei.. meaning kukosekana kwa Mtei hakuwezi kuwa sababu ya kushindwa kwetu kufanikiwa. I hope analo la kusema leo wakati shilingi yetu imetoka Tsh 17 kwa dola hadi Tsh 1200 tena kwa bei ya sokoni na tunashindwa kupiga hatua hata moja mbele.

Wakuu zangu -Almost, every single suggestion Mtei aloiweka wakati ule imejaribiwa ktk kipindi cha miaka 25 iliyopita... na bado tunaendelea kujifunza toka IMF, lakini hakuna positive results kwa sababu alichoshindwa kuelewa Mtei na IMF ni kwamba WATU na MAZINGIRA ndio chanzo cha Bluepirnt ya Ujenzi wa UCHUMI..Pili, walishindwa na wanaendelea kushindwa kutofautisha kati ya TATIZO na MAHITAJI kiasi kwamba ktk maradhi yote haya sisi hupewa pill na dose moja..
 
Kuna element moja ambayo ninyi hamuifahamu. Walikuja junior officers wa World Bank pale DSM na Mtei akawapeleka kumwona Mwalimu Msasani. Wale vijana ( one of them was a Ugandan I knew, and very arrogant) wakaanza kum "lecture" Mwalimu on what he needs to do. Mwalimu aliona kuwa wamekiuka protocal akawafukuza na kumwambia Mtei wala asiwasindikize. Baadaye, the same evening, Mwalimu akampigia simu Mtei wakutane wao wawili and he was told Mtei was hosting a party for those officers. Mwalimu hit the roof and what followed is history.
 
Back
Top Bottom