Mambo yanazidi Kuwa Wazi, wengi waliamini Chadema ndio Chama cha kifamilia kwa sababu ya Mzee Mtei na Freeman kumbe ndio mfumo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,977
141,986
Zile kelele za Chadema Chama cha familia ya Mtei, oooh Chadema chama cha Wachagga mara ohooo Chadema ni Chama Cha Waluteli sasa hautazisikia tena kwa sababu Wana wa Wenye CCM wataanza kuendeshwa na magari yenye bendera kuanzia Chipukizi

Nikiwa Chipukizi ndipo nilipata bahati ya kushikana mikono na Rais Samora Machel wa Msumbiji akiwa na mwalimu Nyerere Uwanja wa Samora paluhengo

Chipukizi ni Taasisi kubwa sana wengi hawajui tu na ndio iliyowaibua hawa akina Makonda na Jokate

Ila sina hakika kama Chipukizi ile ya Kale na hii ya kidigitali zinafanana

Chadema hawana haja ya kuiga CCM wawe tu kama Wapentecoste Ubatizo ni wa Maji Mengi ukubwani unamkataa shetani ikiwa tayari unamjua

Ahsanteni!
 
Back
Top Bottom