Ndugu wana JF,
Nimekumbana na habari hizi kwenye facebook kuna bwana mmoja anaitwa ERNESTO SHEKA nemeona nizirushe hapa ili watu waweze kuziona kwa sababu habari yenyewe ni ya uchochezi na upotoshaji mkubwa sasa wahusika wanaweza kuchukua hatua kabla ya damage hajifanyika: kwa sababu jungu limepikwa kweli kweli, CCM wana kazi mwaka huu
The Moment Of Truth:Kila Mtanzania Asome Hii.Sehemu ya Kwanza.
by
Ernesto Sheka on Wednesday, 20 October 2010 at 19:42
Tarehe 17 Oktoba nilieleza kijuujuu kwamba inawezekana mwaka 1979 Mwalimu Julius Nyerere alipomsimamisha kazi Edwin Mtei(gavana wa BoT wakati huo),kinyongo kiliendelea.Ulikuwepo msuguano mkubwa kati ya Mwalimu na Mtei kuhusu utekelezaji wa sera za IMF nchini Tanzania na katika moja ya mambo ambayo Mwalimi hakutaka hata kuyasikia lilikuwa suala la kushusha thamani shilingi yetu dhidi ya fedha za nchi za kigeni (devaluation) tulizokuwa tunafanya nazo biashara.Katika moja ya hotuba za Mwalimi alishaliongelea hili.1979 haukuwa mwaka mzuri kwa Edwin Mtei ila alipata kazi katika shirika la fedha IMF na kuhamia Marekani ambapo wanawe walipata elimu yao huku akiwepo Lilian Mtei ambaye baadaye alikuja kuolewa na Freeman Aikaeli Mbowe.
Historia haionyeshi kama Edwin Mtei,mtu aliyepata ugavana wa benki kuu akiwa na umri wa miaka 33 tu kwamba alimsamehe Mwalimu kwa fedheha hii.Najua wengi watasema kwamba haya yaliisha.Lakini tukumbuke kuwa maisha ya binadamu yanaathiriwa na matukio yanayoyazunguka.(Dacher Keltner,"The Compassionate Instinct: The Science of Human Goodness" uk.234-249).Kisasi hasa kwa mtu mwenye madaraka kushushiwa heshima yake kwa kile ambacho Edwin Mtei alikiamini ni sahihi ni jambo lisilopingika.Kwa hiyo toka mwaka 1979 Edwin Mtei tayari alishaanza kufikiri jinsi ya kupata sehemu yake,kurudisha heshima yake iliyopotea kama moja ya wasomi wa wakati huo lakini pia kumuonyesha Mwalimu kwamba alifanya kosa kumsimamisha kazi.Bahati haikuwa yake mapema na lilmpasa kusubiri kwa miaka takribani 13 hadi mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa huku mfumo wa kibepari ambao Mtei amekuwa moja ya makuwadi wake akiwa IMF ukishika mizizi na jamii nyingi za Kikomunisti za wakati huo zikirudi kwenye ubepari.Katika yote hayo ndoto yake ilikuwa inaendelea."Lazima niwaadabishe Nyerere na wote waliomsapoti".Tukumbuke kuwa ilikuwa ngumu hata kwa Lilian Mbowe ambaye alisoma chuo kikuu cha Maryland kupata kazi Tanzania wakati huo.Yote haya yalimzidishia Edwin Mtei uchungu huku akiamini kuwa familia yake ilikuwa na haki zaidi kuliko nyingine.Kwa hiyo mwaka 1992 ulipofika Chadema ikasajiliwa moja kwa moja.(Ndugu,jiulize utaratibu wote uliandaliwa lini,kwa nani na kwa faida ya nani?).Kushiriki siasa kwa Edwin Mtei huku Nyerere akiwa hai halikuwa jambo la busara sana,mzee huyu (ambaye kwa aina ya masterplan yake) naamini kwamba ni mwerevu sana akamuweka Bob Makani,huyu alipaswa kukipasha kiti moto kwa muda kabla Freeman Mbowe ambaye amemuoa Lilian Mtei (mtoto wa Mtei) kukabidhiwa mikoba ya kuendeleza plan yake.
Kuna maswali mnajiuliza:
Je,ni nani hasa Edwin Mtei?
Je,ilikuwaje Mbowe akashinda uenyekiti na si Zitto Kabwe?
Ni ipi hasa masterplan ya mzee huyu aliyechekeana kinafiki na Nyerere?
Imefanikiwa kiasi gani?
Je,anawatumia watu gani?Mimi naweza kuwa natumiwa bila kujua?
Vipi Wangwe?Melo?
Ni nani Deus Mallya na kina nani walimlipia mafunzo ya Kijajusi ughaibuni?(sasa ni mpiga picha wa Chadema)
Ni kweli Chadema walifuja dola milioni mbili kama msaada toka chama cha Conservative cha Uingereza?
Saed Kubenea,Jenerali Ulimwengu,Philemon Ndesamburo,Absolum Kibanda ni kina nani na wanahusika vipi na grand plan ya Mtei?
Nini maana ya "M.Z.M.S" katika Chadema na ilikuwaje Mtei akairushusu na ameiruhusu kufanya kazi katika mlolongo upi na nani yujo juu ya sheria ndani ya Chadema na kwa nini?
...Inaendelea.
Part II iko njiani na jiandae pia kwa video ya kuthibitisha baadhi ya mambo katika haya ninayoandika.
The Moment Of Truth:Hakikisha Kila Mtanzania Anasoma Haya.Tafakari:Sehemu ya Pili
by
Ernesto Sheka on Wednesday, 20 October 2010 at 23:37
Tarehe 17 June mwaka 1972 watu watano waliingia kwa siri katika makao makuu ya chama cha Democrats kwenye jengo la Watergate jijini Washington nchini Marekani.Mbali na kuchukua nyaraka za siri ambazo lengo kubwa lilikuwa kumlinda Richard Nixon pia waliharibu baadhi ya nyaraka.FBI walikuja kuugundua mchezo.Wakawakamata wahusika na Agosti 9, 1974,Richard Nixon alijiuzulu kama rais wa Marekani kutokana na kashfa hiyo huku ikibainishwa kuwa alikuwa na kifaa cha siri kilichorekodi sauti ndani ya ofisi hiyo na kila kitu kilichokuwa kinazungumziwa katika ofisi hiyo alikuwa akikifahamu.Nimeanza kwa mfano huu kujenga picha kwamba wanasiasa huwa wana malengo ambayo huwa nayo daima hadi kufa kwao.Edwin Mtei akiwa mmoja wapo kama nilivyosema katika sehemu iliyopita.
Swali kwa vijana wengi ni kwamba je Edwin Mtei ni nani limekuwa gumu wiki hii.Zaidi ya ugavana,uwaziri na ukulima wa kahawa hakuna wanaojua nini kipo nyuma ya pazia hili la Godfather.Mimi naanza kwa kuchambua huyu mtu ni nani na kila aya nasisitiza hatari yake kwa taifa letu na watu ambao ni ngazi zake muhimu.Hili ni jicho linalokutazama mtanzania kila hatua unayopiga na kuonyesha kwamba ni plan makini sana limefanyika kila linalowezekana kumuweka mbali na vyombo vya habari huku ukweli wa binti yake (ambaye ni mke wa Mbowe) kujihusisha na kuajiri mabinti wadogo na kisha kuwadhulumu katika Club yao ya usiku ya Bilicanas ukifichwa kwa kila nguvu na waandishi wa habari wanaolipwa na Edwin Mtei mwenyewe akiwamo mhariri wa gazeti la Tanzania Daima (mali ya Edwin Mtei kwa jina la Freeman Mbowe).Akiishi katika shamba lake Arusha,huku akijiita mkulima wa kahawa asiyependa makuu mzee huyu ni kama walowezi wa Zimbabwe.Kwa waliofika shambani kwake wanatambua naongea nini.(Inawezekana hili la kuwa setla alilianza mwaka1955 hadi 1959 alipokuwa Kenya akifanya kazi kampuni ua tumbaku ya Afrika Mashariki?Nitalichambua kwa hoja).
Ametoka wapi?Alizaliwa mwaka 1932 mkoani Kilimanjaro,mwaka 1946 alipata skolashipu toka Chagga Council (Waliompatia skolashipu hii wajukuu zao wengi wako katika kampuni zake kama wafanyakazi huku wengine wakishirikiana na vijana mbalimbali ambao hawajui lolote katika chadema kuifikia "ndoto").1953 alitoka Makerere na kuingia nchini Kenya katika kampuni ya tumbaku ya Afrika Mashariki.Itambulike kwamba wakati huu ulikuwa wakati wa vuguvugu la kudai haki ya mtu mweusi Tanzania na miaka minne baadaye TANU ilianzishwa.Huku mtu huyu akiwa Kenya,akifanya kazi katika serikali ya wazungu huku Mwalimu na wenzake wakiendesha baiskeli toka Pugu hadi Kariakoo na Upanga kutimiza ndoto ya watanzania.Mtei yeye alikuwa bize Kenya akiwa na girlfriend wake ambaye alimuoa miaka michache baadaye.Hapa tuanaona USALITI wa aina yake.Huku Mwalimu na wanaharakati wengine kama Bibi Titi,Mzee Mwinyimadi Tambaza,Sykes na wengineo wakichomwa jua Dar es salaam,Mtei na elimu yake ya Makerere alikuwa busy akifurahia maisha Nairobi hadi mwaka 1959 aliporudi Tanzania.Miaka 33 baadaye(1992) alitoa wapi kifua cha kujiita mwanamabadiliko???Tuendelee.
Tarehe 20 Januari 1959 alirudi nyumbani akaenda kwao Marangu na baadaye tarehe 9 Februari akafika Dar na akarudia kosa lile lile la kujitenga na wanaharakati wenzake.(Ukisoma katika kitabu chake ambako amejitahidi kwa nguvu zote kuupindisha ukweli utagundua kwamba hili alilipanga tangu akiwa Kenya).Akaenda kuomba kazi katika serikali ya kikoloni na kuajiriwa katika Central Secretariat of the Tanganyika Civil Service.Huu ni mwaka mmoja tu kabla ya uhuru!Kama gwiji wa mitandao ya kijamii (social networks),Mark Zuckerberg anavyosema,"this is a man who never believed and sipport other people's dreams." Hii ni sifa kubwa ya watu wabinafsi na waroho wa madaraka.(Ayn Rand,The Virtue Of Selfishness,uk 117 -129).(Kama kuna mtu anabisha hili mfuateni mkamuulize mtarudi na jibu kuwa alikuwa mbinafsi na msomi asiye mtu wa watu toka akiwa Makerere).HUYU NDIYE ANAYETAKA KUWA BABA WA TAIFA KWA GHARAMA YOYOTE ILE.Tuendelee.
Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na katika kusherehekea siku hiyo mzee huyu anajigamba akionyesha wazi hulka yake ya ubinafsi na kujali nafasi aliyo nayo akisema,"...and I remember celebrating that event very hard because I was newly married and in a newly created country,enjoying my job in a fairly senior position at the Secretariat."That's him pouring rubbish.
Mwaka 1963 akaajiriwa tena EACSO akarudi Nairobi.(Je,alishaanza kuota ndoto ya kuwa bepari?Tafakari).Alidumu kwa mwaka mmoja tu na Mwalimu (naamini 100% kwa kukosa wasomi wa kutosha) akamuita nyumbani aje kuwa katibu mkuu wa wizara ya fedha.Kutokana na ufinyu wa muda kuna mambo mazito ambayo nitawaeleza kwa kifupi sana na kuwaacha muone ni jinsi gani mtu huyu ambaye anajificha nyuma ya pazia pamoja na vibaraka wake kama mkwewe Mbowe na Slaa wanajaribu kuufanya umma wa watanzania vihiy😵ktoba mwaka 1965 kibaraka huyu wa faida binafsi akafanywa gavana mteule na Mwalimu Nyerere(narudia tena kwa jinsi hali inavyofuata huku mbele utaona kuwa alipewa nafasi hii kutokana na upungufu wa wataalamu na Mwalimu alim-doubt toka siku ya kwanza na daima alimuangalia hatua alizopiga).
Asubuhi ya Alhamis tarehe 6 Januari 1966 Edwin Mtei akiwa na umri wa miaka 34 alifanywa gavana rasmi wa benki kuu ya Tanzania na miezi michache baadaye (Tarehe 14 Juni 1966 ) shilingi ilianza kutumika rasmi.Hali haikuwa shwari kama ambavyo nimejaribu kueleza awali,mtu huyu hakuwa anaaminika na Mwalimu na ni sababu tosha kwa nini Mwalimu hakumpa nafasi ya kufanya maamuzi mengi.Utete wa hali hii ukazidi na Mwalimu kwa busara zake akampendekeza kuwa Katibu Mkuu wa EAC wakati huo.Hii ilikuwa mwezi Aprili mwaka 1974,kwa hiyo akatoka katika ugavana na kwenda EAC.Mwaka 1977 (miaka mitatu tu baada ya huyu Godfather kwenda pale),EAC ikavunjika.Kama mchumi hakuona dalili,akashindwa kutoa maono yake kwa usafi na nadiriki kusema anajua kwa nini watanzania wengi ambao leo ni wazee wa rika lake hawajalipwa na EAC.(anajua yeye ni sehemu ya tatizo hilo kwani watanzania wengi walibaki kama vibarua huku wengine wa Kenya wakipewa ajira na mkuu akiwa Edwin Mtei!!!!!!!!).Nitawaachia ninyi muamue.Baada ya hapo Mwalimu akamrudisha nyumbani tena,akamweka awe waziri wa Uchumi na Mipango mwaka 1977.Kauli zake kupokea nafasi hiyo zilikuwa za majivuno na kebehi na kuna mahali alijisahau na kusema,"although I held views critical of the general trend of things,I accepted to serve as Minister in 1977 in a spirit of constructive engagement, believing that I could play a part in improving matters whilst in rather than out."Nadhani alitamani Mwalimu afeli kabisa(rejea kujitenga kwake na wapigania uhuru na kujikomba kuomba kazi kwa wazungu) atimize ndoto yake.Nitaeleza kwa upana mbele.Tuendelee.
Hebu turudi nyuma kidogo.Jumapili tarehe 5 Februari 1967.Siku hii katika kikao Mwalimu alimruhusu afike kama observer tu!!!!Jiulize inaingiaje akili mtu mkubwa kama gavana wa benki kuu awe tu msikilizaji wa kawaida katika kikao kikubwa kama kile???(Muulizeni mkwe wake au yeye kama ana jibu.Believe me,hakuna mwenye kujua haya ninayoyaandika katika Chadema tunayoiona kama system yao ni kuokota ndege wanaokaribia kufa njiani na kuwafuga wakiwaita ndege bora.How does a political party that doesn't understand it's own history and motives behind it's founders move forward?It's a hoax.Political abracadabra.(Daniel Posner,Institutions and Ethnic Politics in Africa😛olitical Economy of Institutions and Decisions,uk.36-59).Mwenye macho haambiwi tazama.Naendelea.
Kitendo cha Mtei kuambiwa na Mwalimu akae kama msikilizaji tu kilimuuma sana,kumbuka huyu ni waziri na gavana wa kwanza wa benki kuu ya Tanzania.(connect the dots ujue Slaa huwa anapata wapi documents za BoT,na kwa nini anazipata leo na si jana,kuna mtu anakutazama).Mwenyewe anakubali katika baadhi ya maandiko yake kwa masikitiko kama pale alipopinga mambo makuu mawili.Villagisation mwaka 1971 hadi 1973 na kutishia kuhusu Capital flight kama Mwalimu angeamua kuingia katika Azimio la Arusha.Kuonyesha kwamba Mwalimu alishamuona si lolote tangu 1953 alipotoka Makerere na kuishi Nairobi miaka 6 huku wanaharakati wa kweli wakiwa Tanganyika,Mwalimu alimpuuza.(Iko wazi kwamba Mtei aliona hathaminiki na ndoto zake za ubepari zilikuwa wazi,tunaweza kusema kwa waziwazi wazo lake la kuasi serikali ya Mwalimu alikuwa nalo toka mwaka 1967,nitaeleza kwa nini).This is a man who believed in capitalism from day na Mwalimu alijua hivyo kwa hiyo hakumweka katika maamuzi makubwa in reality,alimwacha aelee na kumwangalia kwa karibu.
Hali ikazidi kuwa mbaya,1979 Mwalimu akamtimua huku yeye akisema aliachia ngazi mwenyewe (Jiulize kwa nini na ilikuwaje akatoa kitabu cha historia ya maisha yake baada ya kifo cha Mwalimu.So clear,it makes a click.).Naamini kama Mwalimu angekuwa na intelijensia bora,Mtei angekuwa wa kwanza kuihama Tanzania kabla ya marehemu Oscar Kambona.Katika moja ya maandishi yake anaeleza kwa kujificha sana kwamba alikuwa mtu safi huku akificha ukweli kwamba sera kama devaluation na reconstruction ya mashirika ya umma si sahihi kufuata tu oda za IMF bali pia kuangalia muda husika!Aibu sana.."..
The IMF therefore required us to devalue the Tsh and to review the management of our parastatals before they could give us balance-of-payments support. In the negotiations, I was able to get the IMF to scale down their demands on devaluation and make them accept that we would examine individual public corporations to see how they could be restructured to perform better.When I explained this approach to the President he was quite categorical that he would not accept any devaluation and that he would review the parastatals onlyat his own timing. He implied that he would not be dictated to from
Washington..." Anajaribu kusemaje?Mwalimu was stupid?How on earth do you restructure your parastatals when you don't have enough natives educated to take over and work with highly qualified foreigners?Ni simple economics.!Mtei alifumba macho na Mwalimu alipojiridhisha kwamba amembeba kiasi cha kutosha ila habebeki,akamtimua.Safari ya Marekani ikanukia na akaenda zake Washington.(The only reason he was never exiled ni kwa sababiu tayari alijua mengi sana kuhusu intelijensia ya nchi.Je,aliwafuata marafiki zake?).Tuendelee.
Novemba akarudi nyumbani.(Angalia timing!Just a year after Mwalimu has resigned!!)Huku nako mambo hayakuwa sawa,ujamaa ulishindikana.(si tu kwa sababu duniani haukufanikiwa lakini pia kwa sababu watu ambao Mwalimu alitegemea wangempa sapoti kama Mtei na Kambona walifanya majuha wakataka waishi ndoto zao ndani ya sekunde).Moja ya watu walipata masaibu ya Mwalimu ni Jenarali Ulimwengu ambaye alisimamishwa ubunge baada ya sakata la G55.Huyu akiamini kabisa kwamba yeye ni bora kuliko Jakaya Kikwete na Maalim Seif ambao walikuwa vijana wapenzi wa Mwalimu kipindi hicho akajikita katika habari huku naye akiwa na ndoto zake).
Ndoto na chuki zaja hadharani sasa baada ya miaka takribani 26,Julai 1992 mfumo wa vyama vingi ukaanza.The same year Mtei akaanzisha Chadema na mpaka ninapoandika hili,in practical terms yeye ni mwenyekiti wa Chadema,kwake yeye ile ni fimbo maalumu ya kumchapa Mwalimu Nyerere siku akifanikiwa japo kila mara anakosea mahesabu huku jamii ikizidi kuamka na kujua historia ya taifa na kuchambua mambo hatua kwa hatua.Uzee umekuwa wa mashaka na wasiwasi.Ni dhahiri kuwa masterplan ya kuanza kwa Chadema ilianza kuandikwa Nairobi na baadaye Washington huku ikiuwaza ubepari na Ikulu kabla hata ya usajili.Lilian Mbowe ni mtoto wa kike wa Edwin Mtei ambaye aliolewa na Mbowe.Ni daktari ambaye kama nilivyosema awali anajishughulisha na kuendesha club ya usiku katikati ya jiji la Dar es salaam mtaa wa Mkwepu.Nyumba zao hutumika kukusanya vijana na wengi wana upofu na historia ya Chadema,wanaogundua huondoka mara moja.(Mtafuteni David Kafulila atawahadithia sehemu hii).
Je,ilikuwaje Mbowe akashinda uenyekiti na si Zitto Kabwe?
Edwin Mtei namnukuu akisema,"we can't give this position to a man from nowhere" akimaanisha Zitto Kabwe,Zitto alitaka kuondoka ila alibaki kwa sababu zake.Tafakari hiyo kauli ya Mtei.Who's a man from nowhere and who's a man from somewhere??Ni ipi hasa masterplan ya mzee huyu aliyechekeana kinafiki na Nyerere?To revenge and take back his dignity and self interests.Ni ndoto yake ya ujanani na anaomba Watz tumsaidie.
Imefanikiwa kiasi gani?
Hali ni ngumu,ukabila bado umekuwa tatizo.Kifo cha Wangwe,maneno kuhusu viti maalumu,uwepo wa Deus Mallya aliyevuruga mpango wa kufunika sakata la kula pound za waingereza kama ruzuku kwa chama na baadaye kufoji risiti .(John Mnyika alikuwa kinara wa shughuli hii ya kuchakachua risiti).Wangwe's head had a price tag but Deus Mallya made a noise and Chadema let him went down and come up alone(sifa kubwa ya majasusi unapoharibu mpango wa kazi na ukapata tatizo).Ninapoandika hili,Deus Mallya ni mpiga picha na designer rasmi wa Chadema huku mifupa na damu ya Chacha Zakayo Wangwe ikilala udongoni kule Tarime.
Je,anawatumia watu gani?Mimi naweza kuwa natumiwa bila kujua?
Anawatumia watu ambao mkwewe,Freeman Mbowe humpelekea.Hakuna details zozote kuonyesha kama Slaa,zitto na Mtei walikuwa na uhusiano wa karibu miaka saba nyuma!Wachezaji waliokaa pamoja siku mbili wanataka kuomba mechi.Sick jokes.Jenerali Ulimwengu,Saed Kubenea,Maxence Melo,Mike Mushi (huyu baadaye alikimbia).Kuchafua nchi mtandaoni kwa kutumia mtandao wa Maxence Melo ambao una mahusiano ya karibu na baadhi ya watu waliko Houston,Texas.Absalom Kibanda (ni mwandishi na mhariri wa Tanzania Daima ambaye anatembea juu ya ukanjanja wa kutupwa).Unaweza kutumika bila kujua kama hutasikiliza na kutafakari na kuhoji.Sote tunakubaliana huwezi kuacha kutumia gari lako zima ukaamua kuazima gari la jirani yako ambalo lina taa mbovu,tairi mbili mbovu na mafuta hakuna.
Nini maana ya "M.Z.M.S" katika Chadema na ilikuwaje Mtei akairushusu na ameiruhusu kufanya kazi katika mlolongo upi na nani yujo juu ya sheria ndani ya Chadema na kwa nini?M.Z.M.S ni ufupisho wa watu wenye veto power ndani ya Chadema japo zinatofautiona uzito.(Mama Shida Salum,mama mzazi wa Zitto anajua hili).Mbowe,Zitto,Mnyika na Slaa.Uzito wa kura uko kama nilivyoorodhesha majina toka juu kwenda chini.Kama mtu sijamtaja hapo ujue hata Mtei hataka kujus undani wako.
Hitimisho:
Nashukuru kwa kuisoma,je utamsaidia Mtei kumchapa Mwalimu Nyerere bakora kisha alete ilani yake?Si ile inayonadiwa.Je,unajua undani kwa nini moja ya sera za Chadema ni kuigawa nchi katika zones?(majimbo)?Ni nani wanakusudia wawe magavana,majimbo hayo ni yapi na kwa nini?
Muda umeniishia ila tafakari na amua mwenyewe.
Mungu Ibariki Tanzania.
Ernesto Sheka.
Oktoba 20,2010
Butiama,Musoma, Tanzania.
NB:I'll release a video few days to come kuelezea baadhi ya mambo katika note hizi mbili.