Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Na Mwalimu kama kiongozi wa nchi hawezi kukubali masharti ya IMF bila kutathmini athari yake kwa uchumi wa nchi na pia kwa hali ya maisha ya Wananchi wake. Na kuthibitisha kwamba Mwalimu alikuwa na haki ya kuyakataa masharti yale ya IMF masharti yale hayakufanikiwa katika nchi yoyote bali yaliongeza ugumu wa maisha kwa kasi kubwa sana.
BAK:
IMF haitoi masharti wala haisumbuani na nchi inayofanya vizuri kiuchumi. Na kama inafanya hivyo naomba mnipe mfano wa nchi moja. Kwa mtaji huu katika kipindi kile, kilichofanyika Tanzania kilikuwa na negative impacts kwa uchumi na wananchi wake.
Hivyo Mwalimu kukataa masharti kulikuwa na namna mbili. Stay the cource, kile alichokuwa anafanya kingeweza kufanikiwa. Au change the course, alikuwa na njia nyingine zaidi ya hile ya IMF na zaidi ya hile aliyokuwa anafuata.
Kutofanikiwa kwa masharti ya IMF kuna mambo mengi yanayochangia. Na unapoweza kuyatatua hayo mambo yenyewe tayari utaweza kujijengea knowledge base ya kukusaidia kutatua matatizo yako ya baadaye.
Lakini kukataa masharti kwa sababu ya ubishi na pride tu bila kuwa na alternative is one of the stupidest ideas.