Zakumi, Mkandara na Kichuguu hizi ndio zilikuwa debate za awali kule Youngafrica mpaka Jambo then Jamii.
Kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1970 hali ya Tanzania ilianza kugeuka kuwa tete, Bei ya Mafuta ili panda mara mbili hili liliyeyusha ukuwaji wa uchumi wa miaka ya 1960. Azimio la Arusha likaawa ni hadithi za kale, na vita na nduli Idi Amin vikaongeza chumvi kwenye kidonda.
Baada ya kitabu hichi sasa naweza kuunganisha nukta, kwamba Dec 31, 1979 Mwalimu aliwaalika mabalozi ikulu wa ajili ya kusherekea mwaka mpya na akatoa speech ambayo iliwatusi IMF kwa asilimia 100%. Moja ya sehemu za speech hiyo mwalimu anasema hivi "Tanzania is not prepared to devalue its currency just because this is a traditional free market solution to everything and regardless of the merits of our position. It is not prepared to surrender its right to restrict imports by measures designed to ensure that we import quinine rather than cosmetics, or buses rather than cars for the elite"
Labda tujiulize jee kama tungekubaliana na suggestion za IMF (Washington Consensus) kwa small government, binafsisha, fungua bandari hakuna terriffs, ruhusu wawekezaji toka kila kona na n.k, jee nini kingetokea? Tukumbuke ya kwamba 70% ya Watanzania kipindi kile (bahati mbaya mpaka leo) walikuwa masikini wa kutupwa. Hawa watu walikuwa wanategemea subsidy za serikali kwenye Afya, Elimu na Kilimo (kwa asilimia fulani). Kukatisha hizo subsidy mara moja kusingekomesha matatizo kama IMF/WB walivyo suggest kwenye SAP.
Mwalim kugomea policy zinazo tengenezwa Washington ilikuwa ni sababu mmoja tuu, Policies hizo ni One Fits All. Maana strategy inatengenezwa kwa Africa nzima kisha kinacho badilishwa ni Heading. Mwalimu aliona umuhimu wa kutengeza strategy ambazo zinaendena na watu na uchumi wa Tanzania na sio Africa. Na hili ndio tatizo hadi leo tunalo, MGDs imetengezwa na Dr.Jeffrey D. Sachs's. Sachs's hajawai fika Lindi, Kibaoni, Kwamsisi wala Mwika, jee atawezaje kutengeza mfumo utakao waondolea hawa watu umasikini? Hii ndio argument ya Mwalimu, kwamba hawa watu walikuwa wanafly in na first class commercial plan, wanafikia Embassy au Kilimanjaro Hotel kwa siku mbili au tatu, kisha wanarudi kwao DC au London na kudevelop strategy ya kukomesha umasikini. Are you kidding me.
Si kweli kwamba Mwalim alikuwa hataki viwanda binafsi, lakini point yake ilikuwa mmoja kwamba Tanzania ilikuwa na masikini wengi sana kuwaachia asilimia ndogo ya Watanzania washikilie sector zote za uchumi kutaleta mgawanyo mkubwa kwa kanchi kadogo kama Tanzania. Baadhi wachumi wachache walilipinga hilo, wakiamini kabisa Capitalism is the medicine, lakini walisahau kwamba utaweka capitalism kwenye nchi ambayo majority hawana uwezo wa kulipia huduma za Afya, hawana uwezo wa kulipia ada za watoto wao, hawana uwezo kukimu maisha yao ya kila siku. Hawa ndio majority.
Huwezi kuweka capitalism wakati una benki mbili au tatu. Mwalimu alifahamu ya kwamba capitalism iliitaji mfumo dhabiti wa fedha, natazania wakati ule ilikuwa work in process.
Leo hii wataalamu wa IMF and WB ndio tumewajaza BOT na ndio wanatoa fatwa za uchumi. Hawa watu ni corrupted wa mind period. Botswana walishauliwa na IMF kumpatia kazi ya ugavana la Mbotswana mwenzao ambaye alikuwa IMF akifanya kazi hapo DC. Wakatuma team ije imfanyie mkubwa interview hapo hapo DC, walichokipata ni kwamba huyu mkubwa hakuwa na qualification za kuwa mchumi achilia mbali Gavana. Baada ya hapo IMF na WB wamekaa pembeni wazawa wanaendesha Botswana.
Zamani tulikuwa tunashauri vitabu vya kusoma hapa JF, leo nashauri hizi reading tatu. Kwanza soma The End of Poverty, Kisha soma The White Man Burden na Malizia na Globalization and its discontents. Hizi ni view tatu tofauti, utaona mawazo ya kina JK wape misaada, kisha utaona mawazo ya kina Mwalimu ya masikini watajikomboa wenyewe na cha tatu utaelewa kwa nini Nyerere aliachia ngazi. Na jee ni vipi Oil Crisis ya 1970s ilivyotengeneza utawala mpya.
Good thread, it worth reading.