Mtei alipotofautiana na Mwalimu Nyerere

Una maana tupate approval ya WB/IMF au tuachane nao na kujiundia mfumo wetu?

Strangely, Wachumi wetu wengi wanafikiri kuandika majarida n akufanya kazi WB/IMF, ADB na UN ndio njia pekee ya kuinua uchumi wetu.

Nimesema wakati fulani kuwa ningekuwa Mkuu wa Kitivo cha Uchumi UDASA, ningeweka kama sharti kwenye mitaala kuwa kila Mwanafunzi ili afaulu na kupata Shahada ya Uchumi, ni lazima awasilishe project ambayo itakuwa ni 50% ya maksi zake za kufaulu kwa kuonyesha mradi wa maendeleo unaofanya kazi ambao ameukuza kwa kushirikiana na wananchi iwe wa Mtaa, Kata, Kijiji, SACCOS au kikundi chochote cha Ushirika na tuone wakiimarika katika miaka hiyo minne waliyokuwa na "Mchumi" huyu!

No mkuu simaanishi tupate approval ya WB/IMF. Mimi naamanisha kuangalia mfumo huo tulio kuwa nao kabla ya ukoloni na tuufanye wa kisasa na kitaalamu zaidi.

Na kuhusu hiyo sehemu nyekundu hapo nimeipenda sana kwa sababu moja kuu. Ume point out tatizo moja ambalo nime liona lina tusumbua sana. Sisi Tanzania tuna watu ambao tuwaite "book worms"ambao kusoma kitu kutoka kwenye kitabu na kufaulu siyo tatizo. Lakini tatizo linakuja kuapply mtu kuapply elimu aliyo ipata. Sasa watu hawa wakifika makazini ambapo hamna vitabu vya kusoma wana chemsha.Mfumo wetu umebase sana kwenye mitihani tu na real work experience inakua haipo. Ndiyo maana napenda mfumo wa elimu wa Marekani kwa sababu una create watu ambao wanaweza kuapply elimu wanayo jifunza practically. We have smart people but when it comes to these guys applying their knowledge and skills in the real world it is like taking them out of their element completely.
 
"Na dhana hii Ujamaa na kujitegemea ilipigwa vita kwa sababu zamani huwezi kuwa Mkomunist kisha ukasema wewe ni kati au nusu Bepari, U have to choose a side na ndipo mwalimu alipopotea maboya. mambo mengi ktk Azimio hilo yalikuwa ya Ukomunist zaidi ya jamii ya kiafrika kama Azimio lenyewe linavyoagiza. Sasa sielewi kama ilikuwa ni uroho wa madaraka au alitaka kukamilisha kwanza dhana ya kwanza kujenga Ujamaa pasipo kupata ushindani. Hilo siwezi kiumhukumu isipokuwa ni one of his failure ilotokana na mfumo mzima wa kisiasa enzi zile (cold war) Do I blame him, nooo kwani hata wale waliofuata upande wa pili pia hawakufika mahala popote hadi Utandawazi na soko huria ulipoingia."

Mkuu kutokana na maelezo yako hapa inaonyesha ni lazima tukubali kwamba hata tukiwa ni mfumo wetu wenyewe unao lingana na mazingira yetu bado inabidi tuiadjust ikubaliane na hali halisi ya mfumo wa dunia. Hapa kama ulivyo sema ilikuwa hauwezi kuwa vugu vugu ilikua aidha uwe mkomunisti au mbepari. Kwa hiyo there was little Nyerere could do. Sasa je hata sasa hivi tukiamua tuwe wajamaa hatuta kuwa under pressure kuadjust mfumo wetu kulingana na hali halisi ya dunia? If we had to compromise the Arusha Declaration then to fit the cold war, will we be free from external pressures now to adopt our own system? Na mambo ya utandawazi nahisi kama tutaishia kufanya tu kama Nyerere alivyo fanya which is to give in to reality.
 
Mwanafalsafa1,

..Mzee Mtei hana makosa kwa kutoa kitabu chake wakati Mwalimu ameshafariki.

..kitabu hiki kinahusu masuala mengi kuhusu maisha na utumishi wa Mzee Mtei kwa nchi yake.

..matatizo ya Mtei na Mwalimu yame-cover chapter moja au mbili tu.

..kwa muda mrefu sana Mzee Mtei alifanya kazi vizuri na bosi wake Mwalimu Nyerere.

..kitabu cha Mtei ni changamoto kwa wengine nao waandike vitabu kuhusu maisha na mchango wao kwa taifa letu.

..Watanzania tungekuwa na utamaduni wa kufanya research na kuandika vitabu, madai ya Mtei kuhusu mzozo wake na Mwalimu yangeweza kuhakikiwa kwa kulinganisha na habari zilizotolewa na waandishi[labda Butiku,Apiyo,..] wengine.

..tatizo siyo Mtei kuandika kitabu baada ya Mwalimu kufariki. tatizo ni uchache wa waandishi wa vitabu Tanzania.

Rev.Kishoka, Mkandara,

..hatupaswi kuwa RIGID ktk kushughulikia matatizo ya uchumi wa Taifa letu.

..WB na IMF walitufadhili hata wakati wa utawala wa Mwalimu kabla ya kutumbukia ktk matatizo ya uchumi.

..ni kwasababu mambo yalikuwa hayaendi vizuri ndiyo wakafikia "kutuingilia" ktk kufanya maamuzi.

..vilevile WB/IMF hakuwakujialika wenyewe Tanzania, ni sisi ndiyo tuliwafuata kuwataka ushauri na kuwaomba msaada.

..kauli mbiu ya Mkandara, "watu na mazingira" inapaswa kuongezewa kubwagizo cha "paka asiyekamata panya hana maana."

..nyinyi ni watu wazima na mlikuwepo wakati wa matatizo ya uchumi ya miaka ya 80. naamini kabisa kwa hali ile, staying the course was not a wise thing to do. we needed to institute changes on how we run our economy.

..nchi ilikuwa na hali mbaya kiuchumi kiasi cha wananchi kuanza kuhoji uhalali wa serikali iliyokuwepo. naamini kabisa matatizo yale ya uchumi yangeendelea usalama wa nchi yetu ungekuwa hatarini. mkumbuke kwamba hoja ya kina Mc Ghee na Uncle Tom ilikuwa serikali kushindwa kuendesha uchumi.

..hatua alizopendekeza Mzee Mtei zilikuwa na lengo la kutukwamua ktk matatizo ya kiuchumi tuliyokuwa nayo. siamini kama zile zilikuwa hatua za kudumu zilizopaswa kufuatwa wakati wote-- milele na milele.

..kusema kwamba Mtei was wrong, ni sawa na kudai hakukuwa na tofauti, au ahueni yoyote ya kiuchumi, kati ya miaka ya mwisho ya utawala wa Mwalimu, na miaka ya mwanzo ya utawala wa Mzee Mwinyi.

..wakati wowote ule tunapobaini kwamba sera fulani za uchumi hazina faida basi tunapaswa kuzirekebisha. inawezekana yale aliyopendekeza Mtei yalikuwa yanafaa wakati ule, lakini sasa hivi hayafai. kwa msingi huo tunapaswa kuachana nayo.

NB:

..Wamarekani hawaoni dhambi ku-adopt sera za kijamaa-jamaa ili kujikwamua ktk matatizo yao ya kiuchumi.

..Watanzania na sisi hatuna haja ya kujisikia kama vile tumekula nyama ya mtu kwa kuchukua baadhi ya sera za kibepari ili tupate ahueni ya kiuchumi.

..Mzee Cleopa Msuya aliwahi kuulizwa kuhusu suala la ubinafsishaji akasema hakuna aliyetushikia bunduki kichwani kuzuia serikali yetu isimiliki baadhi ya mashirika.
 
Mwanafalsafa,
yafuatayo ni mawazo yangu na yasichukuliwe ndio maamuzi ya maana sana.
Kwanza umenielewa vizuri sana na maswali ayko yamejipanga vizuri kiasi kwamba imenirahishia kufikiri zaidi.

Azimio la Arusha kama dira ya Kitafa haikuwa na makosa na wala haina makosa, tena basi sasa hivi ndio inatakiwa kufanya kazi kuliko wakati wowote ule..Mkuu Ujenzi wa UJAMAA na KUJITEGEMEA kwa sababu unaendana sambamba na mila na desturi zetu pamoja na hata imani zetu za kidini iwe hata za aslimia. tatizo la Azimio lenyewe, kama ulivyosema lilijaa mikakati au niseme sera za Kikomunist, ilani na sera ambazo zilipingana na imani yenyewe, nikatolea mfano wa enzi zile kutokuwa uhuru wa vyama vingi.

Na dhana hii Ujamaa na kujitegemea ilipigwa vita kwa sababu zamani huwezi kuwa Mkomunist kisha ukasema wewe ni kati au nusu Bepari, U have to choose a side na ndipo mwalimu alipopotea maboya. mambo mengi ktk Azimio hilo yalikuwa ya Ukomunist zaidi ya jamii ya kiafrika kama Azimio lenyewe linavyoagiza. Sasa sielewi kama ilikuwa ni uroho wa madaraka au alitaka kukamilisha kwanza dhana ya kwanza kujenga Ujamaa pasipo kupata ushindani. Hilo siwezi kiumhukumu isipokuwa ni one of his failure ilotokana na mfumo mzima wa kisiasa enzi zile (cold war) Do I blame him, nooo kwani hata wale waliofuata upande wa pili pia hawakufika mahala popote hadi Utandawazi na soko huria ulipoingia.

Swali la pili umeniuliza kama rasilimali zilizopo zigawanywe mkoa hadi mkoa na umeshauri mfumo wa Federal Government. I dont think so!..
Hakika mkuu wangu tutakuwa tunafanya makosa makubwa kama tutaendelea kutumia Federal Government kwa sababu matatizo yetu yanaanzia hapo. Kila mkoa unaweza jitosheleza kwa resources zake na ujenzi wa sehemu hizo utawezeshwa tu ikiwa wananchi wake wataweza kujizatiti kuzalisha kile walichokuwa nacho kulingana na vipaji vyao, hivyo elimu zaidi itawasaidia kuongeza mavuno ama kuboresha mazingira hayo.

Tatizo letu halipo ktk kugawana mavuno lipo ktk usimamizi mzima wa maendeleo ya Uchumi wetu na ndio maana unaona viongozi wetu wakileta wakulima waarabu wachimba mafuta kuja kulima Mpunga wakamwacha Mrufiji na Mwana Kyela akifanya umachinga. Hivyo kama utamwezesha Mwana Kyela kupanda juu, bila shaka huyu ndiye atakaye watupia kamaba watazania wengine, hivyo maendeleo ya wananchi yatatokana na WATU na sio serikali ambayo kazi yake ni kuweka policies tu kulinda huo mgannyo kwa njia ya kodi.

Hivyo kama tunaamini Ujamaa, basi panga la mshirika linavyokuwa kubwa ndivyo atakavyochangia zaidi kuwavuta wa chini ambao nao watakuwa na mamlaka ya kuwavuta wengine toka chini. Vita ya kupambana na umaskini ni swala letu sote, lakini mkono wa serikali ndani ya maliasili hizi ndio unatupeleka kusiko. Utandawazi unajieleza wazi kabisa kwamba Tanzania tunaweza fanya biashara na nchi yoyote ile hivyo hata kwa mtu binafsi inatakiwa iwe hivyo hivyo..tunabadilishana mavuno kama utajiri wa mali zetu na ndivyo mataifa au jamii zinaendelea.

Na mwsiho nitasema pia ule mpango wa majimbo pia haufai kwani tunayo tayari Mikoa na wilaya zake. Kinachotakiwa ni kuwawezesha wananchi wa mikoa na wilaya hizo kuzalisha kile walichonacho kuwapandisha ngazi na wao ndio watakao tupa sisi kamba..kazi kubwa ya serikali kuu ni kuhakikisha kamba hiyo inawafikia wa chini ili jamaa alokwisha fika ju asije ingia mitini..

Mkandara:

Ni makosa kuita Azimio la Arusha kuwa ni dira ya taifa. Watanzania tuache unafiki. Hile ilikuwa ni mipango ya Nyerere na kwa nidhamu ya woga watu wakalifuata bila kijadili au kuelewa maana yake.
 
Kuna element moja ambayo ninyi hamuifahamu. Walikuja junior officers wa World Bank pale DSM na Mtei akawapeleka kumwona Mwalimu Msasani. Wale vijana ( one of them was a Ugandan I knew, and very arrogant) wakaanza kum "lecture" Mwalimu on what he needs to do. Mwalimu aliona kuwa wamekiuka protocal akawafukuza na kumwambia Mtei wala asiwasindikize. Baadaye, the same evening, Mwalimu akampigia simu Mtei wakutane wao wawili and he was told Mtei was hosting a party for those officers. Mwalimu hit the roof and what followed is history.

Jasusi:

We una mambo mengi lakini mpaka tukuchokoze ndio unaleta data. Anyway, nimeikopi kwenye kitabu changu cheusi.
 
napinga kipengele cha 1a) angalia nchi za South East Asia kama Singapore na nyinginezo hata Dubai wote hawa wanafuata mapendekezo ya IMF ndo maana wako mbali na nchi yao inakuwa kiuchumi namna hiyo hata China pia pamoja na kuwadanganya ati Wajamaa ukiangalia vizuri ni changa la macho wanafuata karibu mapendekezo yote ya IMF! Tatizo la China ni kwenye democracy basi ila kiuchumi wanafuata IMF! Tuache kudanganyana humu ndani hata nchi kama Zimbabwe na Kenya zilifutat IMF ndo maana zikawa food basket at time kabla ya huu uhuni wa sasa unaochanganyika na rushwa iliyokithiri!
 
Kwendeni zenu Tanzania haikuwa uwanja wa mazoezi kujaribia azimio ambalo ni impractible hadi leo na linasababisha mpk leo watu kuendelea kuiweka CCM madarakani! Azimio la Arusha lilikuwa juju la kutupumbaza na mpaka leo ni mzimu wetu
 
Mkuu mapendekezo ya Mtei hayakuwa kwenye kuleta management za wageni, yalikuwa ni kuweka watu wenye uwezo kwenye management, sasa kama wakati ule tafsiri ilikuwa ni wageni, that is different matter.

Na mapendekezo yake hayakuwa kwenye jambo moja tu, yalikuwa mengi na comprehensive. Mtu yoyote responsible aliyekuwa kwenye wadhifa wake wakati ule angesema kama alivyosema. Kuna baadhi ya wanafiki walikuwa wanasema ndio mzee hata kama wanajua kabisa sio.

Kuna wengine walikuwa wanafiki na kujipendekeza kwa Nyerere, huku mioyoni mwao walikuwa tofauti sana.

Kama tungetekeleza SAPs miaka ile, na kama privatization ingetekelezwa wakati ule, na kama mapendekezo ya Mtei yangetekelezwa basi sasa tusingekuwa tunalia na tuliyofanyiwa na Mkapa, tungekuwa tumepata akili ya kudeal nayo na tungekuwa better than we are now. Still naona kuwa Mzee Mtei alikuwa sahihi.

I wonder JKN alikuwa anaongea nini na Mtei baada ya Mwinyi kuanza kutekeleza ambayo Nyerere aliona hayafai.

Baada ya Mwinyi kuanza kutekeleza ambayo Nyerere aliona hayafai tumeambulia ama kufaidika vipi? Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe na TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO! Nchi za Asia zimepiga hatua kubwa haraka haraka bila hata ya kufuata mambo ya IMF. Mwalimu was very right! Lini Waafrika tutajifunza kujiamulia mambo yetu wenyewe bila kuwaita IMF etc waje watu-convince?

Mwalimu alikuwa ana msimamo - TUUTUMIE UHURU WETU KIKAMILIFU KWA KUJITEGEMEA WENYEWE hata katika masuala ya kufikiri ni kipi bora kwa nchi yetu - kwetu sisi wenyewe na si kukubali kufikiriwa na wengine!
 
Yeap:

Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe. Lakini Mipango ya Azimio la Arusha na maendeleo yote wakati wa kipindi cha Mwalimu ilitegemea misaada na mikopo kutoka nje?

Tuwe wa kweli. Nchi za Asia zilikuwa the least kuhitaji misaada kutoka nje kuleta maendeleo yao. Hivyo positions za nchi hizo ziliwezesha kuendelea bila kuhitaji misaada.
 
Jasusi said:
Kuna element moja ambayo ninyi hamuifahamu. Walikuja junior officers wa World Bank pale DSM na Mtei akawapeleka kumwona Mwalimu Msasani. Wale vijana ( one of them was a Ugandan I knew, and very arrogant) wakaanza kum "lecture" Mwalimu on what he needs to do. Mwalimu aliona kuwa wamekiuka protocal akawafukuza na kumwambia Mtei wala asiwasindikize. Baadaye, the same evening, Mwalimu akampigia simu Mtei wakutane wao wawili and he was told Mtei was hosting a party for those officers. Mwalimu hit the roof and what followed is history.

Jasusi,

..maelezo ya Mtei ni kwamba walikwenda Msasani kumuona Mwalimu saa kumi jioni.

..ujumbe wa IMF uliomba kukutana na Mwalimu kwa mategemeo kwamba wataweza kumshawishi akubaliane na hatua wanazopendekeza. Mtei alishaongea na Mwalimu lakini akashindwa kum-convince.

..apart frm Mwalimu, waliokuwepo ktk kikao hicho ni kiongozi wa ujumbe wa IMF akiitwa Bo Karlstrom ambaye ni raia wa Sweden na msaidizi wake, Mtei, na Ernest Mulokozi PS was Hazina.

..maelezo ya Mtei ni kwamba aliyetoa briefing ni Bo Karlstrom.

..I dont want to give all the details hapa inabidi usome kitabu.

..lakini Mtei anadai kwamba aliwaeleza[kwenye kikao cha chai nyumbani kwa Mtei] jamaa wa IMF kwamba the negotiations had broken down.

..sasa kama Nyerere aliona Mtei amekaidi maagizo yake ya kuwafukuza jamaa wa IMF, ni nini kilichomzuia Nyerere kwenda kuwakamata kwenye kikao chao cha chai na kuwatoa kwenye ardhi ya Tanzania?

..kwa mtizamo wangu Mwalimu just had a bad day. Mwalimu tunayemkumbuka kwa kuwa-dress down miamba kama, Margareth Thatcher, na Ronald Reagan, ashindwe kumdhibiti kwa hoja afisa mdogo wa IMF toka Uganda?

NB:

..nategemea Mzee Mtei atakuja kutolea maelezo zaidi yaliyojiri ktk hicho kikao cha Msasani.

..anahitaji kutoa maelezo kama kweli kulikuwa na kijana wa Kiganda aliyemtibua Mwalimu.

..vilevile anapaswa kueleza iwapo alipigiwa simu na Mwalimu waonane lakini yeye akaamua kuendelea kunywa chai na ujumbe wa IMF.

..
 
Mwalimu tunayemkumbuka kwa kuwa-dress down miamba kama, Margareth Thatcher, na Ronald Reagan, ashindwe kumdhibiti kwa hoja afisa mdogo wa IMF toka Uganda?

Hmmm..really? Unaweza kutoa ushahidi? Maana Ronaldus Magnuss alikuwa kiboko....

Halafu sidhani kama Nyerere alikuwa mkali wa hoja. Kilichomfanya aonekane mkali wa hoja ni nidhamu ya uoga. Enzi hizo ilikuwa almost kufuru kumpinga.

Sasa hivi sijui ange-fare vipi maana watu hatukopeshi tena. Ukichemsha watu watachambua hata accent yako.

Halafu Thatcher na Reagan wewe umewaona miamba kwa vile walikuwa ni viongozi wa mataifa makubwa? So basically kila waziri mkuu wa Uingereza na raisi wa Marekani ni mwamba?
 
Jasusi,

..maelezo ya Mtei ni kwamba walikwenda Msasani kumuona Mwalimu saa kumi jioni.

..ujumbe wa IMF uliomba kukutana na Mwalimu kwa mategemeo kwamba wataweza kumshawishi akubaliane na hatua wanazopendekeza. Mtei alishaongea na Mwalimu lakini akashindwa kum-convince.

..apart frm Mwalimu, waliokuwepo ktk kikao hicho ni kiongozi wa ujumbe wa IMF akiitwa Bo Karlstrom ambaye ni raia wa Sweden na msaidizi wake, Mtei, na Ernest Mulokozi PS was Hazina.

..maelezo ya Mtei ni kwamba aliyetoa briefing ni Bo Karlstrom.

..I dont want to give all the details hapa inabidi usome kitabu.

..lakini Mtei anadai kwamba aliwaeleza[kwenye kikao cha chai nyumbani kwa Mtei] jamaa wa IMF kwamba the negotiations had broken down.

..sasa kama Nyerere aliona Mtei amekaidi maagizo yake ya kuwafukuza jamaa wa IMF, ni nini kilichomzuia Nyerere kwenda kuwakamata kwenye kikao chao cha chai na kuwatoa kwenye ardhi ya Tanzania?

..kwa mtizamo wangu Mwalimu just had a bad day. Mwalimu tunayemkumbuka kwa kuwa-dress down miamba kama, Margareth Thatcher, na Ronald Reagan, ashindwe kumdhibiti kwa hoja afisa mdogo wa IMF toka Uganda?

NB:

..nategemea Mzee Mtei atakuja kutolea maelezo zaidi yaliyojiri ktk hicho kikao cha Msasani.

..anahitaji kutoa maelezo kama kweli kulikuwa na kijana wa Kiganda aliyemtibua Mwalimu.

..vilevile anapaswa kueleza iwapo alipigiwa simu na Mwalimu waonane lakini yeye akaamua kuendelea kunywa chai na ujumbe wa IMF.

..

Jokakuu:

Mwalimu alikuwa hapendi kupigwa lecture.
 
Hmmm..really? Unaweza kutoa ushahidi? Maana Ronaldus Magnuss alikuwa kiboko....

Halafu sidhani kama Nyerere alikuwa mkali wa hoja. Kilichomfanya aonekane mkali wa hoja ni nidhamu ya uoga. Enzi hizo ilikuwa almost kufuru kumpinga.

Sasa hivi sijui ange-fare vipi maana watu hatukopeshi tena. Ukichemsha watu watachambua hata accent yako.

Halafu Thatcher na Reagan wewe umewaona miamba kwa vile walikuwa ni viongozi wa mataifa makubwa? So basically kila waziri mkuu wa Uingereza na raisi wa Marekani ni mwamba?

Watanzania kwa Nyerere na WaGhana kwa Kwame. Yaani huwezi kuwaletea ubishi.
 
Watanzania kwa Nyerere na WaGhana kwa Kwame. Yaani huwezi kuwaletea ubishi.

Yeah...wanawaona kama Miungu vile. Nyerere kutofautiana na Thatcher au Reagan siyo big deal...ni suala la kimtizamo tu. Tatizo letu sisi Miafrika hatuna au tulikuwa hatuna utamaduni wa kutoa mawazo kwa uhuru hivyo kufanya fikra za Nyerere zionekane ni sahihi. Na sahihi my ass....

Nchi gani yenye watu sophisticated watakaokumbatia indoctrination kama 'zidumu fikra sahihi za mwenyeketi'....ebo!! Ujinga mtupu
 
Julius,

..kwani hujui kwamba Ronald Reagan alikuwa mtupu na mbaguzi?

..of the script Reagan alikuwa hamna kitu pale.

..hebu angalia hapa:

" I would have voted against the Civil Rights Act of 1964."
--Ronald Reagan, Los Angeles Times, June 17, 1966
 
Watanzania kwa Nyerere na WaGhana kwa Kwame. Yaani huwezi kuwaletea ubishi.

Nah,

I beg to differ.Watanzania wanamuona Nyerere kama demi-god.

Waghana walimuondoa Kwame kwa mtutu.

Simply no comparison.
 
Yeah...wanawaona kama Miungu vile. Nyerere kutofautiana na Thatcher au Reagan siyo big deal...ni suala la kimtizamo tu. Tatizo letu sisi Miafrika hatuna au tulikuwa hatuna utamaduni wa kutoa mawazo kwa uhuru hivyo kufanya fikra za Nyerere zionekane ni sahihi. Na sahihi my ass....

Nchi gani yenye watu sophisticated watakaokumbatia indoctrination kama 'zidumu fikra sahihi za mwenyeketi'....ebo!! Ujinga mtupu

Afu kuna mijitu mipumbavu ilikuwa inaiga mpaka sauti yake na kuvaa.
 
Jokakuu:

Mwalimu alikuwa hapendi kupigwa lecture.

In short, haambiliki.

Mi nakwambia ndiyo mana viongozi wengi hawataki kuandika biographies zao.Kuna mambo yako so embarassing.Kama hilo la kwenda kupunga upepo lina tofauti gani na udikteta sasa?

Halafu tukisem Nyerere alikuwa haambiliki watu wanakataa.Nyerere alikuwa akishindwa debate anachukua rungu la dola.
 
Julius,

..kwani hujui kwamba Ronald Reagan alikuwa mtupu na mbaguzi?

..of the script Reagan alikuwa hamna kitu pale.

..hebu angalia hapa:

" I would have voted against the Civil Rights Act of 1964."
--Ronald Reagan, Los Angeles Times, June 17, 1966

Kuhusu ubaguzi hilo sijui. So I can't say much.

Ila utupu? Hell no! Huyu mtupu unayemsema wewe ndiye yule aliye debate na Nuclear Scientist Jimmy Carter na kuja kumshinda vibaya sana kwenye uchaguzi mkuu? Ndiye huyu mtupu unayemzungumzia? Mtupu unayemzungumzia wewe ndiye yule isingekuwa kwa kura 3,000 kule Minnesota angesweep majimbo yote kwenye uchaguzi mkuu wa 1984? Mtupu anshinda majimbo 49/50 kwenye uchaguzi wa Marekani? Hebu cheki hii nukuu kutoka Wiki: "He was a gifted student from an early age who always had a fondness for reading"

Eti mtupu? Nadhani mtupu tunaye sisi. Reagan hakuwa mtupu hata kiduchu. Hizo zilikuwa ni propaganda za Democraps waliposhindwa hoja na kuanza mashambulizi ya nafsi yake. Mtupu hawezi kusweep uchaguzi wa Marekani aisee.
 
Nah,

I beg to differ.Watanzania wanamuona Nyerere kama demi-god.

Waghana walimuondoa Kwame kwa mtutu.

Simply no comparison.

Waliomuondoa waliboronga zaidi na kupandisha chart ya Dear Leader, the prophet Kwame.
 
Back
Top Bottom