Mtei alipotofautiana na Mwalimu Nyerere

Haya ya Mtei Vs Nyerere tumeyasikia...kuna anayefahamu zengwe la Kambona Vs Nyerere atupashe?
 
Nafikiri tungepata mtawala wa jinsi ya Mwl. tungekuwa mbali kwa sasa, yeye aliyoyafanya wakati wake yanatosha na kuzidi ebu imagine, wakati ule watu hawajajua umuhimu wa elimu alafu wangeambiwa waanze kuripia elimu kwa watoto woa, kwa mujibu wa sera za IMF hali ingekuwaje leo hii?? wazazi wakalipe gharama za matibabu wakati ule je mimi nawe tungekuwa hapa tulipo?? Kana kwamba hayo hayatoshi leo hii bado tuna waarabu/ waajemi wakishirikiana na wazawa wanataka kuinyonya tanzania kama wanavyotaka na kutuibia,na la kusitikisha zaidi wanataka ata kutuwekea viongozi madarakani ambao wawe vibaraka wao. Kinachoiua Tanzania leo hii ni uongozi mbovu na wizi uliopindukia unaofanywa na watawala wetu na wala si sera za mwalimu za wakati huo, hizo sera zikifuatwa barabara na watawala wetu hakika Tanzania itakuwa nchi ya neema!!!
 
Nyerere was by no means perfect. So it is very surprising when people jump on to every mistake Nyerere did as if the man was expected to make no mistakes. I admire Mwl Nyerere very much and I appreciate him for all the good that he has done for our country. I for one am not a fan of Azimio la Arusha and consider it one of his biggest mistakes. abut despite his mistakes when leading the country what matters most is his motives for what he did. If he did what he thought was best for the country then he can be forgiven in my book. Those others things about his personality like him being arrogant, stubborn or whatever.......well.......no one has a perfect personality.

I think the best way to remember Mwl Nyerere is not to pretend that he had no fault neither is it to try to blame him for every single problem this country is facing. History is already written down. If we can not follow him by his examples we can at least learn from his mistakes. People, Nyerere wasn't perfect, but looking at other leaders in Africa around his time I say we should be thankful Tanzania didn't end up with the likes of Mengistu, Mobutu, Iddi Amin and other such characters.

Rest in peace Nyerere.
 
Bubu Ataka Kusema,

..naomba usome kitabu cha Mzee Mtei ili ujue nini kilitokea kuhusu kushusha thamani ya shilingi.

..vilevile mapendekezo ya Mtei na timu yake hayakuhusu kushusha thamani ya shilingi ya Tanzania peke yake, yalihusu masuala mengi ya jinsi ya kujikwamua na matatizo ya uchumi wakati ule.

..binafsi nadhani Mwalimu angekuwa mkweli ktk kutufafanulia Watanzania kwamba kwa kiasi kikubwa tunahusika na kuporomoka kwa uchumi wetu, leo hii tusingekuwa tunabishana kiasi hiki.

..pia lazima tuelewe kwamba IMF na WB walianza kutuingilia ktk kufanya maamuzi baada ya kuchukua mikopo toka kwao na kushindwa kuonyesha tumefanyia nini mikopo hiyo.

NB:

..kuna mtu amegusia kuhusu Mtei kupendekeza NMC irudishwe kwa familia ya kina Chande.

..katika hili itakuwa vizuri kama tutaelewa kwamba familia ya kina Chande walikuwa wamiliki wa NMC kabla haijataifishwa. vilevile Mwalimu alimteua Chande kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya NMC hata baada ya kuitafisha.

..kuna wataalamu toka Sweden walioletwa kufanya uchunguzi kuhusu biashara na uendeshaji wa NMC. timu hiyo ya wataalamu iligundua matatizo makubwa ikiwemo HUJUMA NA UZEMBE WA WATUMISHI WAZALENDO. moja ya mapendekezo yao ilikuwa ni muundo wa shirika la NMC pamoja na umiliki wake.

Sera za kushusha thamani ya currency ambazo zimepigiwa debe sana na IMF na WB hazijaleta mafanikio yoyote katika nchi nyingi za dunia ya tatu.

Inawezekana kabisa kuhitilafiana kati ya Mwalimu na Mtei hakukusababishwa na kushusha thamani ya shilingi pekee lakini labda hili la kushusha thamani ya shilingi ndilo Mwalimu aliliona lina athari kubwa sana kwa uchumi wa Tanzania na gharama za maisha kutokana na bidhaa mbali mbali ambazo tulikuwa tunaagiza nchi za nje kuongezeka bei kwa kasi sana kufuatia kushushwa huko kwa thamani ya pesa zetu.

Kujiuzulu kwa Waziri wa Fedha kutokana na hitilafu kati yake na kiongozi wa nchi ni huleta mtikisiko katika nchi yoyote ile duniani na ndiyo maana Mwalimu kaamua kuwahutubia Watanzania ili kuwafahamisha sababu zilizosababisha kujiuzulu kwa Mtei kama kulikuwepo na hitilafu nyingine kati yao basi labda Mwalimu hakuzipa uzito mkubwa kama ya kushusha thamani ya shilingi yetu.

Na hadi hii leo katika nchi nyingi za dunia ya tatu ikiwemo Tanzania sera (Economic Reforms Policies) mbali mbali za IMF na WB zimeleta hali ngumu zaidi kwa wananchi wa nchi hizo badala ya kuzikwamua kiuchumi kama ilivyodaiwa na IMF na WB ambao walikuwa wanazishinikiza nchi za dunia ya tatu zikubali masharti yao mbali mbali ili zijikwamue kiuchumi.
 
Nyerere was by no means perfect. So it is very surprising when people jump on to every mistake Nyerere did as if the man was expected to make no mistakes. I admire Mwl Nyerere very much and I appreciate him for all the good that he has done for our country. I for one am not a fan of Azimio la Arusha and consider it one of his biggest mistakes. abut despite his mistakes when leading the country what matters most is his motives for what he did. If he did what he thought was best for the country then he can be forgiven in my book. Those others things about his personality like him being arrogant, stubborn or whatever.......well.......no one has a perfect personality.

I think the best way to remember Mwl Nyerere is not to pretend that he had no fault neither is it to try to blame him for every single problem this country is facing. History is already written down. If he can not follow him by his examples we can at least learn from his mistakes. People, Nyerere wasn't perfect, but looking at other leaders in Africa around his time I say we should be thankful Tanzania didn't end up with the likes of Mengistu, Mobutu, Iddi Amin and other such characters.

Rest in peace Nyerere.
Mwanafalsafa,
Mkuu wasomi wengi sana wamekuja baada ya Mwl. kushindwa kiuchumi na kumkebehi sana Uongozi wake. Lakini the fact relains hakuna nchi yoyote duniani haikuteteleka ktk kipindi hicho..Marekani wenyewe walikuwa chali hadi Reagan alipokuja na sera tofauti za kiuchumi mwaka 1984 na kuweza kubadilisha kabisa sura nzima ya Uchumi duniani. Kinyume cha pale kama asingefanikiwa leo tungekuwa tukizungumza hadithi nyingine kabisa.

And I'm touched when wasomi mnalipopinga Azimio la Arusha pasipo kuelezea haswa kinagaubaga ni lina makosa gani as AZIMIO la kujenga jamii ya watu walio sawa na huru kwa kupitia Ujamaa na Kujitegemea..Ningependa sana Pundit, Bluray, Jokakuu na Zakumi wasomi huu wasifu wangu kwani ni muhimu sana wanielewe.

Mimi sii msomi, tena basi hapa JF na elimu yangu ya madrasa ndio kabisaaaa! mkuu wangu, Azimio la Arusha lilizaa - Ujamaa na kujitegemea ambayo ilikuwa DIRA ya Kitaifa, hivyo vitu vyote vilipangwa tukifuata dira hiyo hivyo ikiwa palikuwepo na makosa ni muhimu sana tuyaweke wazi iwe ni ktk utekelezaji wake au dhana nzima ya itikadi hii..

Binafsi nimeisha sema sana kuhusiana na Ujamaa kwani hakuna baina yetu anayepinga Udugu wetu (Ujamaa) kuwa ndio njia pekee ya kutuweka huru na amani hasa baada ya kutawaliwa..UMOJA wetu ulikuwa muhimu sana wakati ule na bado utaendelea kuwa muhimu kwa watu maskini..Maslahi binafsi hayawezi jenga taifa maskini hata siku moja isipokuwa tutagawana Umaskini na mwenye nguvu atachukua kila kitu.itikadi hii inaweza tu kufanya kazi ktk Taifa tajiri na lenye resources tofauti nasi..tunarudi pale pale ktk watu na Mazingira.

Mwalimu aliposhindwa na pengine niseme makosa makubwa ya Azimio hilo ktk ujenzi wa jamii ni pale mwl. alipochukua sera nyingi za Kikomunist na kuziingiza katika itikadi isiyofanana.. Huwezi kujenga haki ya jamii kwa kuwalazimisha wananchi wote wafuate imani yako. mambo mengi sana ndani ya Azimio la Arusha yalikuwa kama dini ya dhehebu moja wakati nchi yetu haikuwa ktk mfumo huo. Ni sawa na kusema nchi haina dini ila watu wake ndio wenye dini, kisha ukaweka sheria za dini moja kwa watu wote. Hapo ndipo mwalimu au Azimio la Arusha lilipopwaya kwani kuna sheria nyingi za kuwafunga wananchi..kwa mfano, Kujitegemea ni pamoja na kuwepo vyama vingi yaani unawaacha wananchi huru kuchagua itikadi waitakayo kisiasa, lakini mwalimu/Azimio hakutupa haki hiyo..Kama tungekuwa na vyama vingi toka mwanzo, tukaelewa tofauti ya itikadi moja hadi nyingine na vyama vikaundwa kuwakilisha imani tofauti za kisiasa na kiuchumi basi sidhani kama haya ya kina Mtei na wengine yangetokea isipokuwa kwa makosa ya sera.

Leo tuna vyama vingi lakini vyote ni upuuzi mtupu kwa sababu hakuna chama hata kimoja kinacho tangaza imani tofauti ya CCM -hakuna.. Vyama vyote vinatofautiana ktk sera zao (ibada) badala ya kimrengo (itikadi). Kama vile dini zetu kubwa zote zinatofautiana toka mwanzo, waislaam wana imani na nguzo zao tofauti na Wakristu, Mabudha, dini za jadi na kadhalika, hivyo inampa mwananchi Uhuru na haki ya kuchagua imani gani anayoikubali zaidi. Lakini kinachofanyika Tanzania hadi kesho, vyama vyote ni madhehebu ya dini moja. Vyama vyote vinalilia Udugu wetu, Uhuru wetu, Umoja wetu, Amani baina yetu na Haki za kijamii, hivi ni vitu ambavyo kwa tafsiri kubwa ndio Ujamaa na Kujitegemea.
 
Mkuu Mkandara asante sana kwa hoja yako. Japo sikuwepo wakati wa Azimio la Arusha najua kutokana na kusoma na kusikia kutoka watu walioona mambo first hand. Mimi nita sema sababu yangu kuu ya kupinga Azimio la Arusha na in fact umenisaidia kwa kutoa jibu mwenyewe. Naomba nikunukuu mheshimiwa.

'Mwalimu aliposhindwa na pengine niseme makosa makubwa ya Azimio hilo ktk ujenzi wa jamii ni pale mwl. alipochukua sera nyingi za Kikomunist na kuziingiza katika itikadi isiyofanana.. Huwezi kujenga haki ya jamii kwa kuwalazimisha wananchi wote wafuate imani yako."

Mkuu kuna watu walikua wana nyanganywa mali zao walizo chuma kwa jasho lao all in the name ya "kugawana umasikini" na mimi hili ndilo kubwa ninalo pingana nalo. Mkuu hata iweje hauwezi kufanya wananchi wote sawa na walingane kimaisha haiwezekani. Katika kila jamii kuna kua na wenye nazo na walio na chache zaidi. Na sioni tatizo la hili mkuu kwa sababu kila mtu katika jamii ana muhitaji mwenzake. maskini ana muhitaji tajiri na vice versa. Leo hii wote tukiwa sawa nani atamfanyia kazi mwenzake? Kweli ina wezekana kujenga jamii ambayo kila mtu ana uwezo sawa? Kila mmoja wetu kazaliwa na vipaji tofauti na jinsi tunavyo kua tuna pata ujuzi tofauti. Kwenye jamii utakua na wavivu, je ni haki mchapa kazi agawane umasikini na mvivu? Kuna walio tumia muda mwingi kusoma, je nae huyu aishi sawa na yule ambae hakuona umuhimu wa elimu? Hiyo siyo haki hata kidogo.

Tatizo langu la pili ni kwamba ujamaa ulijenga unafiki mkubwa sana. Kuna baadhi ya viongozi waliji limbikizia mali huku waki hubiri kugawana umasikini nakutegemea kila mtu aishi sawa. Kuna wale ambao ujamaa uli sababisha unafiki bila kupenda na kuji tambua. nitoe mfano. Kwenye Azimio watu walitakiwa wakae kwenye vijiji vya ujama. Seti mkuu? Watu walitakiwa waishi sawa seti mkuu? Je Nyerere aliye kua akiishi kwenye kasri kwa jina la Ikulu na kutembea na msululu wa magari na vingora alikua anaishi kama alivyo taka wananchi wake waishi? Hapo si unaona mzee wetu alitaka watu waishi maisha fulani ambayo yeye mwenyewe alikua haishi?

Kama nilivyo sema mkuu Nyerere was a great man and a great leader despite his short comings. In summary of what I've said this is why I am against Azimio la Arusha.

a)It expected every one to be equal. Meaning some will reap even what they have not worked for and some will lose what they have worked hard for. Ni sawa sawa na mimi nichangie shilingi 20 wewe uchangie shilingi 80 lakini faida tugawane 50-50. Je hiyo ni haki?

b)Ujamaa ulikua unafiki kwa sababu kuna watu wengi sana walikua hawaishi sawa na wengine. There wasn't equality as they wanted it to be. Siwezi amini kiongozi kama Nyerere aliyekua ana hudumiwa na serikali alikua na hali sawa na masikini waliokua wakiishi kijijini.

These are my two main arguments against Azimio la Arusha and Ujamaa. Ujamaa did have it's benefits like you mentioned on your post but these two side affects alone are enough for me to advocate against Azimio.
 
Mwenyezi Mungu, shukrani tunaongelea jambo la msingi an si upuuzi wa Mafisadi wa Tanzania! Amen!

Nikirudi kwenye hoja, ingawa naweza kumvulia kofia Mtei kwa ujasiri wa kuongea kilichotokea, bado natatizwa na mambo kadhaa yaliyoya kawaida ambayo tunayo mpaka leo.

Kwanza nikimuongelea Mtei, sidhani kama kitabu hiki nia yake ni kujionyesha kuwa yeye alikuwa na busara zaidi kuliko Mwalimu Nyerere au kuwa yeye ni bingwa zaidi. Sijakisoma kitabu bali kwa kusoma yaliyosemwa, na ninavyomfahamu Mtei, nitashangaa sana nikisikia kuwa alitunga hiki kitabu kujigamba.

Kuna mambo kadhaa yaliyojitokeza katika majadiliano yenu humu nduani kuhusu nafasi na amri zinazotoka WB/IMF.

Ukweli ni kuwa hakuna sera hata moja ya WB/IMF iliyowahi kufanya kazi na kuwa bora na mahiri na kuinua ustawi wa jamii au nchi kwa muda mrefu au kwa kudumu.

Kila sera na pendekezo la WB/IMF pamoja na kuwa wanakuja kwa nia ya kutusaidia kwa kutupa misaada na mikopo ambayo ukiangalia kwa undani ni kukomaza utumwa kwetu, haijawahi kufanya kazi mahali popote kwa mafanikio ya muda mrefu.

Kinachovunwa na misaada/mikobo na ushauri wa WB/IMF ni sawa na ile starehe ya asili aliyopewa Mwanadamu anapomaliza tendo la kujamiiana!

WB/IMF hawana nia ya kuona nchi kama Tanzania ikipiga hatua za kimaendeleo na kuwa nchi inayojitegemea na kujitosheleza. Siku Tanzania ikifika hatua hiyo, jua kwamba hakutakuwa na Taifa Kubwa duniani na hakuna atakayekuwa akitegemea cha mtu.

Fikiria katika Ukoo na Familia, pale kila mtu anapojitutumua na kujitegemea, yule ambaye siku zote alijiona Masihi na anazo za kuwakoga wenzake na kuwadhalilisha, nguvu na majigambo hayo huisha pale nduguze wanapoacha kwenda kumuomba misaada au kumtegemea. Mtu huyu sasa hugeuka kuwa Mwenzetu!

Hivyo ndivyo ncho ambazo ni Matajiri duniani, hsa matajiri kutokana na unyonyaji, ndivyo wanavyoogopa kuona nchi nyingine zina kuwa na nafasi na nguvu sawa si za kiuchumi, tuu, bali mpaka kisiasa, kijamii na kuwa na sauti kubwa.

Angalia jinsi nchi kama Marekani inavyoipiga vita China au hata Urusi na hata kufanya mbinu juu chini kuhujumu kuimarika kwa nchi kama China na India kiuchumi.

Ubabe wa Nyerere, ulistahili kutokana na ukweli kuwa WB/IMF hawakuwa wakitutakia heri, walikuwa wanatupa lile bwii la mara moja mtu akipiga jani au kukausha balasi la chibuku na kujisikia yuko freshi na baada ya muda kupita, mtu huyu hurudi pale pale alipokuwa.

Thamani ya fedha ya nchi ni Usalama wa Taifa. Hivyo kwa WB/IMF kusema Tanzania ipunguze bajeti ya Ulinzi ili ijitutumue lakini ni sawa kwa Marekani na Urusi kuongeza bajeti zao za Kijeshi badala ya kufanya mambo ya maana kusaidia Mwanadamu wa kawaida ni UJUHA mtupu! Haiwezekani Tanzania mpunguze jeshi, lakini Marekani aongeze jeshi, kwa minajjili gani?

Mtei alikuwa na mawazo mazuri, lakini kama Wachumi wengine wa Tanzania hata wa leo walioko BOT kama Marehemu Balali au Ndulu, wanasahau somo moja nalo ni WATU na MAZINGIRA!

Nchi haiwezi kujengwa kwa uchumu wa kukariri insha za kwenye vitabu au madaftarini, nchi itajengeka kwa kuangalia mazingira halisi, kuwaelewa watu wake na kutumia nyenzo zinazoeleweka kwa jamii hiyo.

Mfano, huwezi kuhubiri kulima kutumia Combine Harvester au Planter la kuvunja na shikam ikiwa kulima kwa jembe la mkono na kupalilia magugu ni kitu kigeni kwa mtu ambaye miaka 100 iliyopita, vizazi vyake vilikuwa vikijinyofolea mizizi na kujishibisha!

Uchumi IMARA kwa nchi kama Tanzania utajengwa kwa njia nyepesi sana na wala si nadharia za ajabu (complex theories and mechanism) ajabu ambazo ni za vitabu vya jamii ambazo zilipita hapa tulipo miaka 400 - 700 iliyopita.

Si dhana yangu kutetea kuwa sisi ni wachanga hivyo hatuwezi au tusubiri miaka yetu 800 kukukua kimaendeleo, bali ni kubadilisha mtazamo wetu na kujiuliza tutamjengeaje Mtanzania misingi imara ya kujizalishia mali si kwa matumizi ya kila siku tuu, bali ni ziada na kuanza kujitegemea?

Ukiangalia kichwa kichwa, mapendekezo ya Mtei yanafaa hata leo hii, lakini tatizo si kukosekana kwa mapendekezo, bali ni utaahira wetu (mentality) ambao unaathiri kufanikiwa kwa mambo mengi na ndipo utaelewa anachosema Bob Mkandara kuhusu WATU na MAZINGIRA.

NIkirudi kwenye Azimio la Arusha, Azimio ukilisoma, halina mahali popote paliposema watu wanyang'anywe mali au washurutishwe kuishi kimasikini au kwa dhiki au kulazimishwa kuhama makazi.

Programu za kufanikisha Azimio na siasa za Ujamaa na mtazamo wa kujenga jamii zilizoshikamana iwe kwa dhamiri za kuleta maendeleo na kujenga umoja na kujenga Taifa au woga wa kushindwa kudhibiti jamii ndio kulifikia kufanya utekeleaji wa programu kama Vijiji vya Ujamaa, Maduka ya Ushirika na mengine kufeli.

Aidha, UNAFIKI na UZANDIKI wa watendaji wa Serikali ambao walihubiri Ujamaa, hukuwao wenyewe wakiwa ni MAFISADI na WAHUJUMU wakuu wa sera walizokuwa wakituaminisha Watanzania, kuliongezea chachu ya kuzorota kwa kukua kwa ufanisi na juhudi katika uzalishaji mali.

La mwisho, nitarudi kumlaumu Mwalimu Nyerere, pamoja na mapenzi yangu ya dhati kwake.

Kama vile Mwalimu alivyoweza kutushawishi kulienzi na kulipenda Azimio la Arusha na hata kuishi katika mfumo wa Ujamaa na siasa za Ujamaa na Kujitegemea, Mwalimu alipaswa kutushawishi kujirekebisha pale ilipoonekana kuna ulazima wa kubadilisha mfumo ili tuanze kuleta mafanikio.

Nafikiri ni kiburi na jeuri ya kutokutaka kuonekana kuwa yeye Mwalimu alikuwa anakula Matapishi yake ndiko kulimfanya atuongoze mwishini mwa Urais wake kwa Mafumbo na Misamiati migumu, badala ya kutuambia ukweli na kututaka tujiunge naye katika vita mpya kuushinda Ujinga, Maradhi na Umasikini.

Lakini, pamoja na hayo, bado nauliza, ikiwa Nyerere ni miaka 10 tangu atutoke dunia hii, ni mzimu au mzuka gani ambao unawafanya Wachumi na Wanasiasa wa Tanzania washindwa kutuundia mfumo wetu wenyewe wa kiuchumi unaofanya kazi kwa matakwa yetu wenyewe na si kwa kile tunacholazimishwa au kutishiwa na WB/IMF na hata Paris Club?

Mkirudi kulisoma Azimio la Arusha, kuna sehemu naambatanisha hapa chini ambapo kunazungumzi amadhara ya kutegemea fedha za kutoka kwa Wahisani, japo najiuliza kwa nini Nyerere mwenyewe alikubali misaada jinsi alivyoipokea au ilikuwa ni njia yake ya kudai marejesho (reparations due to colonialism)?

Labda kwa kuwa Azimio la Arusha lilikuwa gumu kulielewa kama vile ilivyo vigumu kwa Mkristo kuielewa Biblia, ndio maana bado tunaamini Azimio lilikuwa baya. Mithili pale Azimio linaposema

Nchi yenye Ujamaa kamili ni nchi ya wafanyakazi: haina
ubepari wala ukabaila. Haina tabaka mbili za watu: tabaka ya
chini ya watu wanaoishi kwa kufanya kazi, na tabaka ya juu ya
watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi. Katika nchi ya Ujamaa
kamili mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi
hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi
aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali
hayapitani mno.
Katika nchi ya Ujamaa kamili watu peke yao ambao huishi
kwa jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao
ni watoto wadogo, wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao,
kwa muda, Jumuiya imeshindwa kuwapatia kazi yo yote ya
kujipatia riziki kwa nguvu zao wenyewe.
Nchi yetu ni nchi ya Wakulima na Wafanya kazi, lakini si nchi ya
Ujamaa kamili. Ina misingi ya ubepari na ukabaila na
vishawishi vyake. Misingi hii ya ubepari na ukabaila yaweza
ikapanuka na kuenea.
, je watu tulilielewa vipi na wale waliokuwa viongozi walielewa vipi kauli kama hizi?

Nashukuru kuwa Mzee Mtei, kaongea bila kumumunya, kayaweka wazi yaliyotokea na kadri tutakavyomsoma, tutakuja baini kuwa laiti kama Wachumi wasomi wetu wangegeuka na kujenga Uchumi wa Tanzania kwa kuangalia WATU na MAZINGIRA, Tanzania tungekuwa mbali mno.

Labda walichosahau kina Mtei, Balali, Ndulu na Mkulo ni kung'ang'ania kujua mambo ya M1, M2 na M3 na zile chati/grafu za demand na supply badala ya kumchunguza Mluguru anazalisha mali vipi na anaelewa vipi maana ya kujitegemea na kuwa tajiri!

Ndio maana kwenye ile mada yangu inayosuasua ya Creation of Wealth or Creating Richness, watu bado tunaangalia nani mchawi na sasa hivi mchawi si Ujamaa tena au kukosekana kwa tija, ubunifu na ufani si kati yetu bali mchawi n Mafisadi!
 
Mwnafalsafa,
Kwanza nashuhuru kwa kukiri kwako kuwa hukuwepo wakati wa Azimio hilo ila umesoma na kusikia kutoka kwa watu waliooana..first hand - ulivyoisherehesha!
Hakika pasipo unafiki zaidi ya kukufahamisha kwamba hayo yote uliyosikia ni kweli isipokuwa UONGOI unakuja pale walipokwambia madhumuni ya kufanya hivyo.

Sii kweli kabisa kwamba watu walinyang'anywa mali zao ili kugawana Umaskini, kwanza hadhithi hii haiwezi leya maana ikiwa kilichochukuliwa ni MALI... hivyo utajiri ghfla hauwezi kuitwa umaskini. Dhumuni la kuchukua mali za watu ilikuwa ni mfumo mzima wa kiuchumi (Kikomunist) ambalo lengo lake ni serikali kuendesha Uchumi wa nchi, hivyo hakuna mgawanyo wowote ulofanyika kama ule wa Idd Amin alipopora mali za wahindi.

Pili, Ni tafsiri mbaya ya usawa wa binadamu wote uloitu,ia..wakati wote walikuwepo matajiri na watu hawakuchukuliwa mali zao kwa sababu ni matajiri ili kuleta usawa ktk kipato..huo ni uongo mwingine...The logic behind Usawa wetu na unakubaliwa na sote pamoja na kwamba unafiki upo..ni ni ktk kutafuta HAKI. Yaani tunaamini binadamu wote sawa mbele ya sheria ili tupewe nafasi sawa za kujiendeleza...Kama sii imani hii watu kama Mwinyi, Mkapa au JK wasingeweza fika walipofika tungetawaliwa na kina Fundikira, Marealle, Mkwawa na wengineo ambao walikuwa na resources zaidi ya kila mmoja wetu na pengine Andy Chande ndiye angekuwa rais wetu wa kwanza.. Kwa hiyo imani hii inatupa sote nafasi sawa za kutuwezesha kufika tunakokusudia iwe ktk Ubepari au Ujamaa isipokuwa ni ktk matumizi mabaya ya viongozi wetu imani hii ilijengwa na imnai hiyo..Lakini ukweli ni kwamba hali ya kugawana mali ni mfumo wa kiuchumi wa kanisa la Kisoshalist. Hawa wanaamini hakuna sababu ya mtu mmoja kutajirika akimwacha mwenzie maskini wa kutupa na wanaamini kabisa dhana ya mpanda ngazi ambaye siku zote huwa na watu walioishika hiyo ngazi na ukisha fika juu basi wape kamba wa chini nao wakufuate.
Ni imani ambayo sote Watanzania tunaikubali, ni moja ya mila na desturi zetu (as maskini) kwamba mmoja wetu akipanda juu bila shaka atamrusha mwenziwe pia. Na ndio maana nasisitiza sana kutenganisha Watu na Mazingira ya nchi mbili. Labda ipo siku nitapata muda wa kuelezea vizuri zaidi kuhusu WATU na MAZINGIRA isipokuwa nitakwambia kwamba hakuna nchi hata moja au hata States mbili za USA zinafanana ama kuigana isipokuwa kila states inajitazama..mfano, Wisconsin wazuri kwa Ufugaji hivyo wamejizatiti ktk mifugo na uzalishaji wake wakati Michigan wao ktk viwanda vya magari. wao na kamari wakati jirani yao Texas wana mafuta...Tofauti hizi utazikuta kila nchi. Muingereza na viwanda vya Magari na kadhalika wakati WaHollanzi wazuri kwa Maua hawakukimbilia kuunda magari pia. Kila nchi ina resources na vipaji vhake kulingana na watu na mazingira yao hivyo Elimu na Uchumi wa nchi unajengwa kwa misingi hiyo..

Sio sisi tunaotaka kuibadilisha mkoa wa Mwanza uwe kama California..kila siku tunatolea mifano nchi nyingine kwa rasilimali tusokuwa nazo..na hatuwezi kuepuka kabisa Usoshalist kwa sababu sisi bado ni maskini na tunaweza tu kugawana umaskini wetu, kinyume cha hapo tutakuwa tunajidanganya kwa sababu hatuna matajiri na hatuwezi kuunda matajiri ikiwa utajirisho hautakuwa na mfumo bora unaolenga kuwainua maskini walioko chini.. Trust me mkuu wangu kwa mwendo huu wa sasa basi tegemea sana kitu kama French Revolution kwani alama zote sasa hivi zinajitokeza.
 
Viambatanisho vyangu nilivyotaja hapo awali kuhusu Azimio la Arusha.


Mnyonge hapigani kwa Fedha:
Lakini ni dhahiri kwamba tumefanya makosa katika kuchagua
silaha; kwani silaha tuliyochagua ni fedha. Tunataka kuondoa
unyonge wetu kwa kutumia silaha ya wenye nguvu, silaha ambayo
sisi wenyewe hatuna. Katika mazungumzo yetu, mawazo yetu, na
vitendo vyetu ni kama tumekata shauri kwamba bila fedha mapinduzi
yetu hayawezekani. Ni kama tumesema, “Fedha ndiyo msingi wa
maendeleo. Bila fedha hakuna maendeleo”!
Hii ndiyo imani yetu ya sasa. Viongozi wa TANU mawazo yao ni
kwenye fedha. Viongozi wa Serikali, wanasiasa na watumishi,
mawazo yao na matumaini yao ni kwenye fedha. Viongozi wa
wananchi na wananchi wenyewe katika TANU, NUTA, Bunge, UWT.,
Vyama vya Ushirika, TAPA na makundi mengine ya wananchi,
mawazo yao na maombi yao na matumaini yao ni FEDHA. Ni kama
wote tumekubaliana na tunasema kwa sauti moja, “Tukipata fedha
tutaendelea, bila fedha hatutaendea”!


Na kusema kuwa Serikali haina fedha maana yake ni nini?
Maana yake ni kuwa Wananchi wa Tanzania hawana fedha. Kiasi
walichonacho hutozwa kodi, na kodi hiyo ndiyo inayoendesha
shughuli za Serikali hivi sasa na maendeleo mengine ya nchi.
Tunapotaka Serikali ifanye shughuli zaidi za maendeleo kwa fedha
tunataka Serikali itumie fedha zaidi. Na kama Serikali haina fedha
zaidi tunataka izipate, yaani iongeze kodi.
Ukidai Serikali itumie fedha zaidi unataka izipate; na njia ya
kuzipata ni kodi. Kudai Serikali itumie fedha nyingi bila kukubali kodi
zaidi ni kudai Serikali ifanye miujiza; ni sawa na kudai maziwa zaidi
bila kutaka Ng’ombe akamuliwe tena. Lakini kukataa huku kukiri
kwamba tunapodai Serikali itumie fedha zaidi nia yetu ni kutaka
Serikali iongeze kodi kunaonyesha kuwa tunatambua ugumu wa
kuongeza kodi. Tunatambua kuwa ng’ombe hana maziwa zaidi;
kwamba hata ng’ombe mwenyewe angependa ayanywe maziwa hayo
au yanywewe na ndama wake au yauzwe yamfae yeye na jamaa
yake; utashi huo hauwezi kuondoa ukweli kwamba hana maziwa
zaidi.

Fedha kutoka nje ya Tanzania, Je?
Njia moja tunayotumia kujaribu kuepukana na lazima hii ya kukiri
kodi zaidi ikiwa twataka fedha zaidi ni kutilia sana mkazo fedha za
kutoka nje ya Tanzania. Fedha hizi za kutoka nje ni za aina tatu:-
(a)
Zawadi: Yaani Serikali ya nje iipe Serikali yetu fedha za bure
tu kama sadaka kwa ajili ya mpango fulani wa maendeleo.
Wakati mwingine shirika lo lote la nje liipe Serikali yetu au
Shirika jingine katika nchi yetu msaada fulani kwa ajili ya
maendeleo.
(b)
Mkopo: Sehemu kubwa ya fedha tunazotazamia kupata
kutoka nchi za kigeni si zawadi au sadaka, bali ni mkopo.

Serikali ya nje au Shirika la nje, kama vile Benki, hukopesha
Serikali yetu fedha fulani kwa ajili ya kazi zetu za
maendeleo. Mkopo huu huwa una masharti yake ya kulipa,
kama vile muda wa kulipa, na kima cha faida.
(c)
Raslimali ya Kibiashara: Aina ya tatu ambayo pia ni kubwa
kuliko ya kwanza, ni ile ya fedha za watu au makampuni
yanayotaka kuja katika nchi yetu kuanzisha shughuli mbali
mbali za uchumi kwa manufaa yao wenyewe. Na sharti
kubwa walitakalo jamaa hawa wenye fedha zao ni kwamba
shughuli yenyewe iwe ni ya faida – kwao – na pia kwamba
Serikali iwaruhusu kuondoa faida hiyo Tanzania na kuipeleka
kwao. Hupenda pia kwa jumla Serikali iwe na siasa
wanayokubaliana nayo au ambayo haihatarishi uchumi wao.
Hizo ndizo njia tatu kubwa za kupata fedha kutoka nje ya
nchi yetu. Kuna mazungumzo mengi ajabu juu ya jambo hili
la kupata fedha kutoka nchi za kigeni. Serikali yetu na
viongozi wetu wa makundi mbalimbali hawaachi kufikiria njia
za kupata fedha kutoka nje. Na tukizipata au japo tukipata
ahadi tu ya kuzipata mara magazeti yetu, au radio zetu na
viongozi wetu hutangaza jambo hilo ili kila mtu ajue kuwa
neema imekuja au iko njiani inakuja. Tukipata msaada
hutangaza; tukipata mkopo hutangaza; tukipata kiwanda
kipya hutangaza; tukiahidiwa msaada, mkopo au kiwanda

kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au
shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda, mara
hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo
hayo. Na kisa? Ni kuwajulisha wananchi kwamba, tunaanza
mazungumzo ya neema!


 
Natamani Mwalimu angekuwa bado yuko hai ili naye atueleze ni kipi hasa kilichojiri hadi kuhitilafiana na Mtei. Kila jambo lina pande mbili, labda wale waliokuwa karibu na Mwalimu miaka hiyo ilipotokea hitilafu kati ya Mwalimu na Mtei labda watajitokeza na wao kuzungumza ufahamu wao wa nini hasa kililichotokea hadi kusababisha Mtei kujiuzulu. Mwalimu tulimuita majina mengi sana kama Mzee haambiliki, mchonga meno, Mussa n.k. lakini kwa mano yangu pamoja na kuwa hakuwa perfect kama kiongozi alifanikiwa katika mambo mengi kama Kiongozi wa Tanzania ukilinganisha na mafanikio yaliyopatikana kwa ujumla wakati wa Mwinyi, Mkapa na Kikwete.
 
Namalizia kunukuu kwa hili:


TUSITEGEMEE FEDHA KULETA MAENDELEO
Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu
kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini.
Ni ujinga vile vile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza
kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka
nje badala ya fedha zetu wenyewe. Ni ujinga kwa sababu mbili.
Kwanza, hatuwezi kuzipata. Ni kweli kwamba zipo nchi ambazo
zaweza na zapenda kutusaidia. Lakini hakuna nchi moja duniani
ambayo iko tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga
viwanda katika nchi yetu kutimiza shabaha zake zote za maendeleo.
Nchi zenye dhiki ni nyingi sana duniani. Na hata kama nchi zote
zenye neema zingekubali kuzisaidia nchi zenye dhiki, bado ingekuwa
msaada huo hautoshi. Lakini nchi zenye neema hazitakubali. Hata
katika nchi ile ile, matajiri huwa hawatoi fedha zao kwa hiari ili
zisaidie Serikali kuondoa dhiki.
Njia ya kuzipata fedha za matajiri ili zisaidie umma ni kuwatoza
kodi wakipenda wasipende. Hata hivyo huwa hazitoshi. Ndiyo
maana japo tungewakamua vipi wnanachi na wakazi wa Tanzania,
matajiri na maskini, hatuwezi kupata fedha za kutosha kutimiza
mipango yetu ya maendeleo. Wala duniani hakuna Serikali ambayo
yaweza kuyatoza kodi mataifa yenye neema, yakipenda yasipende, ili
kusaidia mataifa yenye dhiki. Hata hizo zisingelitosha. Hakuna
Serikali ya Dunia nzima. Fedha ambazo nchi zenye neema hutoa
huwa kwa wema wao, au hiari yao au kwa manufaa yao wenyewe.
Haiwezekani basi, tupate fedha za ktuosha kwa njia hiyo.


MISAADA NA MIKOPO
VITAHATARISHA UHURU WETU
Pili, japo kama tungeweza kuzipata; hivyo ndivyo tunavyotaka
kweli? Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli
hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo ya
Taifa jingine kwa maendeleo yake. Hata kama pangetokea Taifa au
mataifa ambayo yako tayari kutupa fedha zote tunazohitaji
kuendesha mipango yetu ya maendeleo isingekuwa sawa kwa nchi
yetu kuipokea misaada hiyo bila kujiuliza matokeo yake yatakuwa nini
kwa Uhuru wetu na uzima wetu.
Msaada ambao ni kama chombo cha kuongeza juhudi, au
nyenzo ya juhudi, ni msaada ambao una manufaa. Lakini msaada
unaoweza ukawa sumu ya juhudi si msaada wa kupokea bila kujiuliza
maswali.
Kadhalika mikopo. Kweli mkopo ni bora kuliko misaada ya
“bure”. Mkopo nia yake ni kuongeza jitihada au kuifanya jitihada
itoe matunda mengi zaidi. Sharti moja la mkopo huwa ni kuonyesha
jinsi utavyoweza kuulipa. Maana yake ni kwamba sharti uonyeshe
kuwa unakusudia kuufanyia kazi itakayoleta manufaa ya
kukuwezesha kuulipa.
Lakini hata mikopo ina kikomo. Sharti upime uwezo wa kulipa.
Tunapokopa fedha kutoka nje mlipaji ni Mtanzania. Na kama
tulivyokwisha sema Watanzania ni watu maskini. Kuwabebesha watu
maskini mikopo ambayo inawazidi kimo si kuwasaidia bali ni
kuwaumiza. Na hasa inapokuwa, mikopo hiyo ambayo wanatakiwa
walipe haikuwafaidia wao, bali ilifaidia watu wachache tu.
Na Viwanda vya wenye raslimali zao je?
Ni kweli tunavitaka.
Hata tumepitisha katika Bunge sheria ya kulinda raslimali ya wageni
wanaoanzisha mipango mbali mbali ya uchumi katika nchi yetu. Nia
yetu na matumaini yetu ni kuwafanya waone kuwa Tanzania ni nchi
inayofaa kuingiza raslimali zao. Kwani raslimali yao itakuwa salama
italeta faida. Na faida hiyo wenyewe wataweza kuiondoa bila
vipangimizi. Tunayo matumaini ya kupata fedha za maendeleo mbali

mbali kwa njia hii. Lakini hatuwezi kupata za kutosha. Lakini hata
kama tungeweza kuwaridhika kabisa Wageni hao na Makampuni
hayo mpaka yakubali kuanzisha mipango yote ya uchumi tunayohitaji
katika nchi yetu, hivyo ndivyo tunavyotaka kweli?
Kama tungeweza kushawishi wenye raslimai wa kutosha kutoka
Amerika, na Ulaya kuja kwetu na kuanzisha Viwanda vyote, na
mipango mingine yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi hii, hivi
kweli tungekubali bila kujiuliza maswali? Tungekubali kweli kuacha
uchumi wetu wote uwe mikononi mwa wageni kwa ajili ya kupata
faida na kuipeleka katika nchi zao? Hata kama wasingedai
kuhamisha faida na kupeleka makwao, bali faida yote watakayopata
wataitumia hapa hapa Tanzania kwa maendeleo zaidi. Hivi kweli
tungekubali jambo hili bila kujiuliza hasara zake kwa Taifa letu? Huu
Ujamaa tunaosema kuwa ndiyo shabaha yetu tungeujengaje?
Twawezaje kutegemea nchi za nje na Kampuni za nje kwa
misaada na mikopo na raslimali kwa maendeleo yetu bila kuhatarisha
uhuru wetu? Waingereza wana methali isimayo “Amlipaye mwimbaji
ndiye huchagua wimbo”. Tutawezaje kutegemea nchi za kigeni na
Makampuni ya kigeni kwa sehemu kubwa ya maendeleo yetu bila
kuzipa nchi hizo na makampuni hayo sehemu kubwa ya uhuru wetu
wa kutenda tupendavyo. Ukweli wenyewe ni kwamba hatuwezi.
Tukariri basi. Tumefanya makosa kuchagua fedha, kitu
ambacho hatuna, kiwe ndicho chombo kikubwa cha mipango yetu ya
maendeleo. Tunafanya makosa kudhani kuwa tutapata fedha kutoka
nchi za kigeni. Kwanza, kwa sababu kwa kweli hatuwezi kupata
fedha za kutosha kwa maendeleo yetu. Na pili, hata kama
tungeweza, huko kutegemea wengine kungehatarisha uhuru wetu na
siasa nyingine za nchi yetu.
 
Asante mkuu Mkandara kwa kufafanua baadhi ya myth za Ujamaa na Azimio la Arusha. Kama nilivyo sema awali sikuwepo wakati huo kwa hiyo kila kitu ninacho jua kuhusiana na swala hilo ni kujifunza mwenyewe na kusikia kwa watu.

Mkuu you raise a very interesting topic unaposema "WATU na MAZINGIRA". Ni kweli kwamba kila nchi ina resources zake na hata ndani ya nchi kila eneo lina resources zake.

Sasa je mkuu unadhani Ujamaa ulitufaa sisi na mazingira yetu. Kwa maana je Azimio la Arusha liliweka policies tailor made for us au zilikua ni policies zilizo azimwa? Maana I'm under the impression kwamba hata hilo Azimio la Arusha ni policies za sehemu zingine na watu wengine ambalo lilipewa tu jina la kiswahili. Kwa sababu mimi nadhani kama kweli Azimio la Arusha liliaddress sisi kama sisi na matatizo yet unique basi linge fanikiwa. Sasa je tatizo lilikua policies zilizo azimwa au kwenye implementation ya hizo sera?

Swala la pili. Tanzania tume jaliwa rasilimali nyingi. Kila mkoa tuseme una rasilimali zake. Je hizi rasilimali za kila mkoa zitumike kwa manufaa ya nchi nzima au tuendeleze mkoa mmoja mmoja kutokana na rasilimali zake? Mimi nafikiri kwa mazingira yetu federal system ingetufaa sana. Kwa maana kila mkoa uendelezwe kutokana na rasilimali zake badala ya tunavyo fanya sasa ambapo rasilimali za kila mkoa zina tumika kama mali ya taifa zima ila hatuoni hiyo mikoa wala taifa lenyewe liki nufaika na rasilimali hizo.
 
Mkandara,

Watanzania watastaajabu kusikia kuwa Ukristo, Uislamu na Uzayuni vyote ni mashujaa na mashabiki wa mfumo wa kijamaa.

Katika mafundisho ya Uislamu, kuna kitu kinachozungumziwa kinachoitwa Baytul- Maal. Kwenye Ukristo, Yesu Kristo mwenyewe alizungumzia ugumu wa Matajiri na hata kumtetea mtu aliye masikini. Juzi Jumapili tumesoma tena kutoka Injili ya Marko kuhusu yule mwanamke mjane aliyetua senti tano, huku matajiri wakileta masanduku ya fedha kama Sadaka.

Hivyo hata mafundisho yetu ya kiimani tunayakaidi, kwa tamaa za kujitajirisha!

Sasa tunapogeuza pesa kuwa ndio njia pekee, na kushindwa kujua Jumuiya yetu na historia yetu na hata utamaduni wetu katika kujenga mfumo bora wa kiuchumi, hapo ndipo ninaposhangaa.

Wasukuma, enzi za enzi, kabla ya Mkoloni, walishirikiana katika kuwinda na kutafuta chakula. Walimpa Mtemi kile cha Mtemi na kingine waligawana na hata kuuza kwa Wahaya, Wakurya, Wanyamwezi, Wanyiramba na Waha!

Je tulishindwa nini kuangalila mfumo wa Wasukuma na kuujenga uimarike na kuufanya ubadilike na wakati badala ya kumwambia Msukuma mfumo wako ni butu, batili na ni wa Kishenzi chukua huu wa Kizungu?
 
Natamani Mwalimu angekuwa bado yuko hai ili naye atueleze ni kipi hasa kilichojiri hadi kuhitilafiana na Mtei. Kila jambo lina pande mbili, labda wale waliokuwa karibu na Mwalimu miaka hiyo ilipotokea hitilafu kati ya Mwalimu na Mtei labda watajitokeza na wao kuzungumza ufahamu wao wa nini hasa kililichotokea hadi kusababisha Mtei kujiuzulu. Mwalimu tulimuita majina mengi sana kama Mzee haambiliki, mchonga meno, Mussa n.k. lakini kwa mano yangu pamoja na kuwa hakuwa perfect kama kiongozi alifanikiwa katika mambo mengi kama Kiongozi wa Tanzania ukilinganisha na mafanikio yaliyopatikana kwa ujumla wakati wa Mwinyi, Mkapa na Kikwete.

Well said mkuu. With all of Mwl's imperfections he was an exceptional leader. Kila mtu ana mapungufu yake. Mimi ndiyo maana nadhani hawa viongozi wangekua wanaandika vitabu mapema baada ya kuondoka kwenye uongozi. Mzee Mtei anakuja kuandika kuhusu matokeo ya mwaka 1979 leo wakati mhusika hayupo hai kujitetea. Chukulia mfano wenzetu wa nje. Watu right after tokeo wanaandika vitabu. Kama Obama's campaign manager David Plouffe juzi kamaliza kuandika kitabu kinacho itwa "The Audacity to Win". Hapo ina maana kama kuna mzozo wowote wahusika wanaweza kujitetea straight away kuliko kama angeandika miaka 20 au 30 ijayo. Sasa hapa tuta sikia upande mmoja tu nao ni wa bwana Mtei.
 
Asante mkuu Mkandara kwa kufafanua baadhi ya myth za Ujamaa na Azimio la Arusha. Kama nilivyo sema awali sikuwepo wakati huo kwa hiyo kila kitu ninacho jua kuhusiana na swala hilo ni kujifunza mwenyewe na kusikia kwa watu.

Mkuu you raise a very interesting topic unaposema "WATU na MAZINGIRA". Ni kweli kwamba kila nchi ina resources zake na hata ndani ya nchi kila eneo lina resources zake.

Sasa je mkuu unadhani Ujamaa ulitufaa sisi na mazingira yetu. Kwa maana je Azimio la Arusha liliweka policies tailor made for us au zilikua ni policies zilizo azimwa? Maana I'm under the impression kwamba hata hilo Azimio la Arusha ni policies za sehemu zingine na watu wengine ambalo lilipewa tu jina la kiswahili. Kwa sababu mimi nadhani kama kweli Azimio la Arusha liliaddress sisi kama sisi na matatizo yet unique basi linge fanikiwa. Sasa je tatizo lilikua policies zilizo azimwa au kwenye implementation ya hizo sera?

Swala la pili. Tanzania tume jaliwa rasilimali nyingi. Kila mkoa tuseme una rasilimali zake. Je hizi rasilimali za kila mkoa zitumike kwa manufaa ya nchi nzima au tuendeleze mkoa mmoja mmoja kutokana na rasilimali zake? Mimi nafikiri kwa mazingira yetu federal system ingetufaa sana. Kwa maana kila mkoa uendelezwe kutokana na rasilimali zake badala ya tunavyo fanya sasa ambapo rasilimali za kila mkoa zina tumika kama mali ya taifa zima ila hatuoni hiyo mikoa wala taifa lenyewe liki nufaika na rasilimali hizo.

Socrates,

Msukuma alikuwa ni mwindaji, mfugaji na akijilimia vitu vichache. Katika mfumo wake wa Kijima ambao Mzungu alisema ni wa KIS HE NZI, Msukuma aliweza kujitosheleza yeye na familia yake, alifanya kazi kwa kushirikiana na wenzake, walitoa Zaka kwa Mungu wao Manumbu na walimpa Mtemi wao yale mazao yaliyo bora.

Masalio waligawanyana katika nyumba na koo, na kisha wakaenda Ukuriani, Unyirambani na kubadilishana bidhaa na Wahaya, Wanyamwezi na Waha.

Huu mfumo ulikuwa na tatizo gani kuendelezwa na kuboresha na badala yake tukasokomezewa mfumo mpya kabisa wa Kizungu huku tukidharauliwa na kuambiwa Historia na Utamaduni wetu ni wa kijinga?

Hata kama leo Dhahabu ziko Mwanza, Uranium iko Singida, Alizeti iko Kilimanjaro, je kwa nini tuachane na jadi letu la kushirikiana na kubadilishana bidhaa kisa eti mikoa ijitosheleze ka Ubinafsi?

Kwa nini leo Mkandara ambaye ni Mkerewe, atakwenda Usukumani kwa Nyani Julius na kumsaidia kuzika pamoja na kuwa wanaitana Watani?
 
Socrates,

Msukuma alikuwa ni mwindaji, mfugaji na akijilimia vitu vichache. Katika mfumo wake wa Kijima ambao Mzungu alisema ni wa KIS HE NZI, Msukuma aliweza kujitosheleza yeye na familia yake, alifanya kazi kwa kushirikiana na wenzake, walitoa Zaka kwa Mungu wao Manumbu na walimpa Mtemi wao yale mazao yaliyo bora.

Masalio waligawanyana katika nyumba na koo, na kisha wakaenda Ukuriani, Unyirambani na kubadilishana bidhaa na Wahaya, Wanyamwezi na Waha.

Huu mfumo ulikuwa na tatizo gani kuendelezwa na kuboresha na badala yake tukasokomezewa mfumo mpya kabisa wa Kizungu huku tukidharauliwa na kuambiwa Historia na Utamaduni wetu ni wa kijinga?

Hata kama leo Dhahabu ziko Mwanza, Uranium iko Singida, Alizeti iko Kilimanjaro, je kwa nini tuachane na jadi letu la kushirikiana na kubadilishana bidhaa kisa eti mikoa ijitosheleze ka Ubinafsi?

Kwa nini leo Mkandara ambaye ni Mkerewe, atakwenda Usukumani kwa Nyani Julius na kumsaidia kuzika pamoja na kuwa wanaitana Watani?

So basically mkuu the system I was proposing ilikuwepo kabla ya ukoloni. Kwamba kila eneo ilitumia rasilimali zake kuji tosheleza. That's what I'm advocating. Kwa nini sasa tusi boreshe huo mfumo tulio kuwa nao na kuufanya ulingane na hali halisi ya leo?(kwa maana leo hii kumuambia mtu arudi kwao akawinde itakua ngumu). Maana siku hizi karibia kila mtu anaona kukimbilia Dar Es Salaam ndipo paku patia mafanikio. Let's promote the different industries which are allowed by our resources the excess of which will flow to other parts of the country.

Ukiweka mfumo mzuri hata ubinafsi unaweza kunufaisha taifa zima. Kwa mfano kwamba hata tajiri akiwa na tamaa ya kutajirika zaidi ni lazima kodi yake itaongezeka kwa jinsi anavyo tajirika na hapo ata nufaisha taifa zima.
 
Mwanafalsafa,
yafuatayo ni mawazo yangu na yasichukuliwe ndio maamuzi ya maana sana.
Kwanza umenielewa vizuri sana na maswali ayko yamejipanga vizuri kiasi kwamba imenirahishia kufikiri zaidi.

Azimio la Arusha kama dira ya Kitafa haikuwa na makosa na wala haina makosa, tena basi sasa hivi ndio inatakiwa kufanya kazi kuliko wakati wowote ule..Mkuu Ujenzi wa UJAMAA na KUJITEGEMEA kwa sababu unaendana sambamba na mila na desturi zetu pamoja na hata imani zetu za kidini iwe hata za aslimia. tatizo la Azimio lenyewe, kama ulivyosema lilijaa mikakati au niseme sera za Kikomunist, ilani na sera ambazo zilipingana na imani yenyewe, nikatolea mfano wa enzi zile kutokuwa uhuru wa vyama vingi.

Na dhana hii Ujamaa na kujitegemea ilipigwa vita kwa sababu zamani huwezi kuwa Mkomunist kisha ukasema wewe ni kati au nusu Bepari, U have to choose a side na ndipo mwalimu alipopotea maboya. mambo mengi ktk Azimio hilo yalikuwa ya Ukomunist zaidi ya jamii ya kiafrika kama Azimio lenyewe linavyoagiza. Sasa sielewi kama ilikuwa ni uroho wa madaraka au alitaka kukamilisha kwanza dhana ya kwanza kujenga Ujamaa pasipo kupata ushindani. Hilo siwezi kiumhukumu isipokuwa ni one of his failure ilotokana na mfumo mzima wa kisiasa enzi zile (cold war) Do I blame him, nooo kwani hata wale waliofuata upande wa pili pia hawakufika mahala popote hadi Utandawazi na soko huria ulipoingia.

Swali la pili umeniuliza kama rasilimali zilizopo zigawanywe mkoa hadi mkoa na umeshauri mfumo wa Federal Government. I dont think so!..
Hakika mkuu wangu tutakuwa tunafanya makosa makubwa kama tutaendelea kutumia Federal Government kwa sababu matatizo yetu yanaanzia hapo. Kila mkoa unaweza jitosheleza kwa resources zake na ujenzi wa sehemu hizo utawezeshwa tu ikiwa wananchi wake wataweza kujizatiti kuzalisha kile walichokuwa nacho kulingana na vipaji vyao, hivyo elimu zaidi itawasaidia kuongeza mavuno ama kuboresha mazingira hayo.

Tatizo letu halipo ktk kugawana mavuno lipo ktk usimamizi mzima wa maendeleo ya Uchumi wetu na ndio maana unaona viongozi wetu wakileta wakulima waarabu wachimba mafuta kuja kulima Mpunga wakamwacha Mrufiji na Mwana Kyela akifanya umachinga. Hivyo kama utamwezesha Mwana Kyela kupanda juu, bila shaka huyu ndiye atakaye watupia kamaba watazania wengine, hivyo maendeleo ya wananchi yatatokana na WATU na sio serikali ambayo kazi yake ni kuweka policies tu kulinda huo mgannyo kwa njia ya kodi.

Hivyo kama tunaamini Ujamaa, basi panga la mshirika linavyokuwa kubwa ndivyo atakavyochangia zaidi kuwavuta wa chini ambao nao watakuwa na mamlaka ya kuwavuta wengine toka chini. Vita ya kupambana na umaskini ni swala letu sote, lakini mkono wa serikali ndani ya maliasili hizi ndio unatupeleka kusiko. Utandawazi unajieleza wazi kabisa kwamba Tanzania tunaweza fanya biashara na nchi yoyote ile hivyo hata kwa mtu binafsi inatakiwa iwe hivyo hivyo..tunabadilishana mavuno kama utajiri wa mali zetu na ndivyo mataifa au jamii zinaendelea.

Na mwsiho nitasema pia ule mpango wa majimbo pia haufai kwani tunayo tayari Mikoa na wilaya zake. Kinachotakiwa ni kuwawezesha wananchi wa mikoa na wilaya hizo kuzalisha kile walichonacho kuwapandisha ngazi na wao ndio watakao tupa sisi kamba..kazi kubwa ya serikali kuu ni kuhakikisha kamba hiyo inawafikia wa chini ili jamaa alokwisha fika ju asije ingia mitini..
 
So basically mkuu the system I was proposing ilikuwepo kabla ya ukoloni. Kwamba kila eneo ilitumia rasilimali zake kuji tosheleza. That's what I'm advocating. Kwa nini sasa tusi boreshe huo mfumo tulio kuwa nao na kuufanya ulingane na hali halisi ya leo?(kwa maana leo hii kumuambia mtu arudi kwao akawinde itakua ngumu). Maana siku hizi karibia kila mtu anaona kukimbilia Dar Es Salaam ndipo paku patia mafanikio. Let's promote the different industries which are allowed by our resources the excess of which will flow to other parts of the country.

Ukiweka mfumo mzuri hata ubinafsi unaweza kunufaisha taifa zima. Kwa mfano kwamba hata tajiri akiwa na tamaa ya kutajirika zaidi ni lazima kodi yake itaongezeka kwa jinsi anavyo tajirika na hapo ata nufaisha taifa zima.
Haya ndio maswali ya kuwauliza hao wanao tuongoza!
 
So basically mkuu the system I was proposing ilikuwepo kabla ya ukoloni. Kwamba kila eneo ilitumia rasilimali zake kuji tosheleza. That's what I'm advocating. Kwa nini sasa tusi boreshe huo mfumo tulio kuwa nao na kuufanya ulingane na hali halisi ya leo? (kwa maana leo hii kumuambia mtu arudi kwao akawinde itakua ngumu). Maana siku hizi karibia kila mtu anaona kukimbilia Dar Es Salaam ndipo paku patia mafanikio. Let's promote the different industries which are allowed by our resources the excess of which will flow to other parts of the country.

Ukiweka mfumo mzuri hata ubinafsi unaweza kunufaisha taifa zima. Kwa mfano kwamba hata tajiri akiwa na tamaa ya kutajirika zaidi ni lazima kodi yake itaongezeka kwa jinsi anavyo tajirika na hapo ata nufaisha taifa zima.

Una maana tupate approval ya WB/IMF au tuachane nao na kujiundia mfumo wetu?

Strangely, Wachumi wetu wengi wanafikiri kuandika majarida n akufanya kazi WB/IMF, ADB na UN ndio njia pekee ya kuinua uchumi wetu.

Nimesema wakati fulani kuwa ningekuwa Mkuu wa Kitivo cha Uchumi UDASA, ningeweka kama sharti kwenye mitaala kuwa kila Mwanafunzi ili afaulu na kupata Shahada ya Uchumi, ni lazima awasilishe project ambayo itakuwa ni 50% ya maksi zake za kufaulu kwa kuonyesha mradi wa maendeleo unaofanya kazi ambao ameukuza kwa kushirikiana na wananchi iwe wa Mtaa, Kata, Kijiji, SACCOS au kikundi chochote cha Ushirika na tuone wakiimarika katika miaka hiyo minne waliyokuwa na "Mchumi" huyu!
 
Back
Top Bottom