Ndugu zanguni wana JF hoja siku zote hujibiwa na hoja. Wanaosema kwa nini Mzee Mtei kaandika kitabu leo, wanasahau kwamba kuandika kitabu ni haki yake ya msingi mzee Mtei. Prof.Babu aliandika kitabu chake wakati yupo jela, mpaka leo kuna baadhi ya Vyuo vinarecommend hicho kitabu.
Pili, ni vyema tusikilize pande zote mbili then tumia uwezo na upeo wako kujudge based on the facts presented. Na sio kusimama na kulalawa why now, why and why? Think kwanza then analyze.
Nikiwa kama mpenda uchumi, nimesoma vitabu vingi sana kuhusu IMF and World Bank na umafia wao. Kuna valid arguments ambazo tunaweza kujifunza kutoka kwa Mzee Mtei, jee walipo kubali kudevaluate the currency baada ya mwaka 1985 then what happened? Did we achieved what IMF recommended? Why IMF waliondoka kutoka kwenye SAP and introduce PRSP? Akiwa Washington DC jee ni kwa ukubwa gani policies IMF zilikuwa zina reflect policy za Ronald Reagan and Thatcher za free market, small government and no intervation? Jee kwa umasikini wa asilimia 70 ni kweli tungeweza kushindana katika soko huria na kushinda?
Kusema kweli argument za Sheka zimebase kwenye chuki kati ya Capitalism and Socialism ndio maana kwa asilimia kubwa naona hazijengi bali zinaboa. Sababu badala ya kutoa maono yake concern policy alizopresent Mzee Mtei kwa Mwalim ana present personal attack. Hii inaonyesha jinsi gani bwana Sheka alivyokuwa hana sera, bali ni chuki.
Kwa wale ambao hawajajikita sana kwenye uchumi, labda niseme kwamba Sera za IMF and WB ndio zinaongoza dunia ya tatu kwa kiasi kikubwa. Na ukweli ulio wazi IMF hawana nchi hata mmoja ambao wataweza kusema wale wamefuata recommendation zetu na wamefananikiwa. Nionyesheni moja kama kuna mtu anafahamu.
Upande mwingine, nimesoma na kuresearch policy za Mwalim kwa muda sasa. Nimeongea na good economist mbalimbali kuhusu what was inside mwalim brain. Kusema kweli out of honest Nyerere policy was based on idealogy and not scietific facts, however it can be defended. As one fellow at Wall Street magazine said "Dr. Nyerere may have been poor economist but he was skillful nation builder. He fused Tanzanian's 120 tribes into a cohesive state, preventing tribal conflicts plaguing so much of Africa"
Mtanganyika:
Paragraph yako ya mwisho ina ukweli fulani. Lakini bado inarudia mambo yaleyale ya ku-generalize Africans. Ukanda wa kwetu katika nchi za Tanzania, Malawi, Zambia hata Zimbabwe kuna amani fulani ambayo viongozi watu wanapata credits wakati hata wakati wa ukoloni tulikuwa tumetulia.
Ukichukua makabila ya Tanzania utaona hakuna kabila linaloweza ku-dominate wengine. Hivyo historia yake hipo unique. Wakati tunapata uhuru kulikuwa hakuna fault lines za kufanya makabila yapigane. Na vitu vilivyo sababisha kuelewana ni:-
1.) Hatukuwa na empire kubwa za kikabila kabla ya mkoloni. Na zile zilizokuwepo, zilikuwa tayari mixed na makabila mengine. Kwa mfano wasukuma na wanyamwezi tayari walikuwa wanafanya trades na watu wa pwani.
2.) Biashara ya utumwa, ngozi, madini, bunduki, nguo, pembe za ndovu ilisambaza lugha ya kiswahili na watu wa makabila tofauti kuoana.
3.) Makabila mengi ya Tanzania ni ya wakulima au wakulima-wafugaji. Hivyo sehemu kubwa watu walikuwa na vipande vyao vya ardhi ambao ni msingi mkubwa wa amani.
Mwingereza katawala Tanzania kwa amani. Tumepata uhuru kwa amani. Sasa ni sababu gani za sisi kufananishwa na nchi zingine za kiAfrica ambazo fault lines zipo.
Nyerere angekuwa rais wa Rwanda au Burundi, watu wangeangalia kabila lake na sio siasa zake. Angekuwa Nigeria au Sudani, angeangaliwa kwa kabila lake na dini yake.
Ukweli wa mambo uliopo ni kuwa kwa miaka inayokaribia 50 ya uhuru; viongozi wa Tanzania walikuwa wanajukumu la kutumia amani kujenga uchumi. Zoezi hilo wameshindwa (period).
Tukirudi kwenye mada halali, numbers don't lie. Nchi zote zinazoitwa emerging markets, zilipokea sehemu ndogo sana ya misaada kutoka nje na nchi zingine zilikataa.
Kuna watu hapa kila siku wanatoa mifano ya China kupiga maendeleo kwa kutumia Ujamaa. Mchina alikataa misaada. Kwa upande mwingine Tanzania ilikuwa inajenga Ujamaa kwa kutumia misaada na mikopo na hiyo ndio sababu ya Tanzania kutegemea IMF na WB.
Misaada inafumbaza viongozi wa kisiasa. Pamoja na mimi kukubali kuwa Mtei alikuwa sahihi, ukweli wa mambo mapendekezo yake yasingetufikisha popote kwa sababu ratio ya misaada ilikuwa bado kubwa sana ukilinganisha na juhudi zetu wenyewe.