It is too late!kama kweli author of this article ni mzalendo wa kweli kwa nini anatuletea makala hii wakati kama huu?ni baada ya kuona CHADEMA sasa inafanya vizuri!Watu wengi huwa na upofu inapofika hatua ya kujadili mambo yaliyofanywa na Nyerere!Mimi binafsi namheshimu sana Nyerere kwa mambo mazuri aliyoifanyia nchi hii,lakini naamini katika kuongoza nchi hii kuna mambo aliyoyafanya yalikuwa siyo mazuri pia.Kwa mfano nyerere alikataa swala la devaluation of our currency and restructuring of parastalstal organisations,hapa alifanya kosa kubwa,kwa kuwa ukishusha thamini ya fedha yako inafanya bidhaa zako unazoziuza nje ya nchi ziwe na bei ya chini na kuwezesha kuuza zaidi nje ya nchi,pia itaongeza nafasi za kazi ndani ya nchi,bila kusahau suala zima la ustawi wa jamii husika.Restructuring of parastastal organisations,hii pia lilikuwa wazo zuri kwa kuwa lingeyafanya mashirika yaweze kujiendesha yenyewe kwa faida,badala ya kutegemea ruzuku kutoka serikalini!Swali la msingi la kujiuliza ni kwamba,kama wazo la Nyerere lilikuwa zuri mbona mashirika ya umma yalikuja kufa yote?leo tuna mashirika mangapi ya umma?je shilingi ya Tanzania inapanda au inashuka ikilinganishwa na tharafu nyingine duniani?je tunatoka wapi na tunakwenda wapi?
Ukiendelea kusoma vizuri mada hii utagundua mwandishi anajaribu kuhuaianisha maisha binafsi ya Mtei na CHADEMA!hii mimi hainiingii akilini hata kidogo,kwa kuwa nachojua mimi ni kuwa CHADEMA ni chama chenye usajili halali,kina katiba, ambapo wanachama wake wana haki zao katika chama hicho!
Hapa ni lazima tutofautishe vitu viwili:Umakini na uongozi mzuri wa nyerere ni tofauti na ilivyo sasa kwa CCM.CCM ya leo ni chama goigoi kinacholinda ufisadi na kukumbatia matajili wachache.Udhaifu wa Mtei ni tofauti na umakini wa uongozi wa CHADEMA!
Msitake kutufanya wajinga kiasi hicho,makala hii ni ya kijinga kabisa, hakuna cha maana hapa!
Mbona jamaa kaweka wazi kwamba hii si ishu ya uchaguzi?Mjadala unaoendelea katika ukuta wake kule Facebook ni kwamba hii ni sehemu ya historia ya Chadema.