Mtei alipotofautiana na Mwalimu Nyerere

Mtei alipotofautiana na Mwalimu Nyerere

hapa jf huwa tunaruhusu matusi tu!!
Wala hatutaki mashabiki wa vyama vingine isipokua chadema tu!!!

Peoplesssssssssssssssssssssssss poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer!!!!
Lmao!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nafikiri CCM wasiwe na wasiwasi, Tanzania ni yetu wote, hata wakikosa watapata muda wa kukaa pembeni na kuangalia walikosea wapi. Si lazima wao watawale kwa njia yoyote ile. Hawana haki kutoka mbinguni.

Tukubali demokrasia ichukue mkondo wake kwa amani, kama ni chadema sawa, na kama ni CCM nayo sawa ili mradi iwe demokrasia na si wizi na mizengwe.

Muda wa kutishana ulipita zamani
 
Zakumi, Mkandara na Kichuguu hizi ndio zilikuwa debate za awali kule Youngafrica mpaka Jambo then Jamii.

Kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1970 hali ya Tanzania ilianza kugeuka kuwa tete, Bei ya Mafuta ili panda mara mbili hili liliyeyusha ukuwaji wa uchumi wa miaka ya 1960. Azimio la Arusha likaawa ni hadithi za kale, na vita na nduli Idi Amin vikaongeza chumvi kwenye kidonda.

Baada ya kitabu hichi sasa naweza kuunganisha nukta, kwamba Dec 31, 1979 Mwalimu aliwaalika mabalozi ikulu wa ajili ya kusherekea mwaka mpya na akatoa speech ambayo iliwatusi IMF kwa asilimia 100%. Moja ya sehemu za speech hiyo mwalimu anasema hivi "Tanzania is not prepared to devalue its currency just because this is a traditional free market solution to everything and regardless of the merits of our position. It is not prepared to surrender its right to restrict imports by measures designed to ensure that we import quinine rather than cosmetics, or buses rather than cars for the elite"


Labda tujiulize jee kama tungekubaliana na suggestion za IMF (Washington Consensus) kwa small government, binafsisha, fungua bandari hakuna terriffs, ruhusu wawekezaji toka kila kona na n.k, jee nini kingetokea? Tukumbuke ya kwamba 70% ya Watanzania kipindi kile (bahati mbaya mpaka leo) walikuwa masikini wa kutupwa. Hawa watu walikuwa wanategemea subsidy za serikali kwenye Afya, Elimu na Kilimo (kwa asilimia fulani). Kukatisha hizo subsidy mara moja kusingekomesha matatizo kama IMF/WB walivyo suggest kwenye SAP.

Mwalim kugomea policy zinazo tengenezwa Washington ilikuwa ni sababu mmoja tuu, Policies hizo ni One Fits All. Maana strategy inatengenezwa kwa Africa nzima kisha kinacho badilishwa ni Heading. Mwalimu aliona umuhimu wa kutengeza strategy ambazo zinaendena na watu na uchumi wa Tanzania na sio Africa. Na hili ndio tatizo hadi leo tunalo, MGDs imetengezwa na Dr.Jeffrey D. Sachs's. Sachs's hajawai fika Lindi, Kibaoni, Kwamsisi wala Mwika, jee atawezaje kutengeza mfumo utakao waondolea hawa watu umasikini? Hii ndio argument ya Mwalimu, kwamba hawa watu walikuwa wanafly in na first class commercial plan, wanafikia Embassy au Kilimanjaro Hotel kwa siku mbili au tatu, kisha wanarudi kwao DC au London na kudevelop strategy ya kukomesha umasikini. Are you kidding me.


Si kweli kwamba Mwalim alikuwa hataki viwanda binafsi, lakini point yake ilikuwa mmoja kwamba Tanzania ilikuwa na masikini wengi sana kuwaachia asilimia ndogo ya Watanzania washikilie sector zote za uchumi kutaleta mgawanyo mkubwa kwa kanchi kadogo kama Tanzania. Baadhi wachumi wachache walilipinga hilo, wakiamini kabisa Capitalism is the medicine, lakini walisahau kwamba utaweka capitalism kwenye nchi ambayo majority hawana uwezo wa kulipia huduma za Afya, hawana uwezo wa kulipia ada za watoto wao, hawana uwezo kukimu maisha yao ya kila siku. Hawa ndio majority.

Huwezi kuweka capitalism wakati una benki mbili au tatu. Mwalimu alifahamu ya kwamba capitalism iliitaji mfumo dhabiti wa fedha, natazania wakati ule ilikuwa work in process.

Leo hii wataalamu wa IMF and WB ndio tumewajaza BOT na ndio wanatoa fatwa za uchumi. Hawa watu ni corrupted wa mind period. Botswana walishauliwa na IMF kumpatia kazi ya ugavana la Mbotswana mwenzao ambaye alikuwa IMF akifanya kazi hapo DC. Wakatuma team ije imfanyie mkubwa interview hapo hapo DC, walichokipata ni kwamba huyu mkubwa hakuwa na qualification za kuwa mchumi achilia mbali Gavana. Baada ya hapo IMF na WB wamekaa pembeni wazawa wanaendesha Botswana.

Zamani tulikuwa tunashauri vitabu vya kusoma hapa JF, leo nashauri hizi reading tatu. Kwanza soma The End of Poverty, Kisha soma The White Man Burden na Malizia na Globalization and its discontents. Hizi ni view tatu tofauti, utaona mawazo ya kina JK wape misaada, kisha utaona mawazo ya kina Mwalimu ya masikini watajikomboa wenyewe na cha tatu utaelewa kwa nini Nyerere aliachia ngazi. Na jee ni vipi Oil Crisis ya 1970s ilivyotengeneza utawala mpya.

Good thread, it worth reading.


Mtanganyika:

Kwa ridhaa tu ninapitia kazi fulani za Joseph Stalin. Japokuwa Stalin hakusoma sana lakini wakati ame-commission kuandika kitabu cha Political Economy ya USSR, alitoa points zenye maana sana.

Kwanza anasema kuzungumzia Economy, ni lazima uache rethorics na utumie scientific methods na utumie data kuonyesha maendeleo yako. Kwa Tanzania tumezidisha rethorics (siasa).

Pili anasema kuwa pamoja na kuwa Warusi walikuwa wanajenga Ujamaa lakini kwenye analysis ya ubepari ni lazima utaje na kukubali mazuri ya ubepari. Kwenye political rethoric, unaweza kuukandia ubepari unavyotaka. Lakini kwenye political economy ni lazima kutoa credits.

Kwa kutumia hii mifano miwili, naweza kusema kuwa tuli-base na mpaka sasa bado tume-base kwenye political rethorics. Kwa mfano miaka ya 70 uliweza kusema kuwa kiwanda cha viatu Morogoro kina faida kwa wananchi kwa sababu kilimilikiwa na serikali. Lakini ukitumia data na kuangalia mfumo mzima utaona kuwa kiwanda kizima kilikuwa kinawapa watu hasara.

Data zilizopo zinaonyesha kuwa WB, IMF na wahisani walishiriki kwa kiwango kikubwa kusaidia kuanzishwa kwa sekta ya umma kwa Tanzania na nchi zingine za kiAfrika. Kwa mfano kiwanda cha viatu Morogoro, zilikuwa ni pesa za kutoa WB. Mobutu Seseko alisaidia kiwanda cha kuyeyusha chuma cha zaidi ya dollar 300 million, na mitambo ya umeme ambayo mpaka sasa haijafanya kazi.

Swali linalokuja kwanini haohao watu waliotusaidia kufungua miradi ya thamani miaka ya 70, ilipofika miaka ya 80 wakawa wanasema vibinafsishwe?

Unaweza kusema kuwa Tanzania ilipata misukosuko ya kiuchumi. Lakini Zambia ilipopata uhuru ilikuwa na kipato cha kutosheleza huduma za jamii. Na kila dollar iliyopatikana kwa misaada iliyotoka WB, IMF au nchi wahisani, serikali ya Zambia ilitumbukiza kwenye investments. Kwa upande wa Tanzania kila dollar iliyopatikana ilikuwa inatumika kwenye investments na huduma za jamii. Cha kushangaza, kufikia mwanzoni mwa 80, Tanzania na Zambia wako kwenye kundi moja la umasikini.

Tanzania na Zambia ni nchi za amani, na viongozi wake wa mwanzo walikuwa visionary, lakini failures za kiuchumi za nchi hizi ni Phenomena ambayo sisi wenyewe inabidi kuifanyika kazi. Kuendelea kulaumu WB, IMF haitasidia.

Kuhusiana na wafanyakazi wa WB na IMF ambao wanapendekezwa kurudi nyumbani nakubaliana na wewe kimsingi. Wafanyakazi wengi wa taasisi hizi wanalipwa mishahara mikubwa kuliko hile ambayo wangeipata nyumbani. Hivyo wapo walioridhika na hawatumii muda wao kujifunza mapya hili wanaporudi nyumbani watoe expertise. Hata hapo nyumbani, watu wanataka kupata kazi BOT, TRA kupata mshiko mzuri.
 
Faida ya kuwa na thamani ndogo ya curreny ni kwamba production costs nchini kwako zinakuwa ni ndogo kuliko za nchi nyingine ukiziweka katika scale moja ya dola ya kimarekani. Kwa hivyo (assuming kuwa quality ya bidhaa zako ni nzuri kama za wenzako) ukiuza kwa profit margin sawa na washindani wako ambao curreny yao ina thamani kubwa, bidhaa zako zitakuwa na bei nafuu na zitavuta wateja sana. Hiyo ndiyo kubwa ya faida ya devaluation. Sasa kwa Tanzania tuliokuwa tunategemea kilimo ambapo bei za mazao ya kilimo (agricultural commodity prices) hazipangwi na muuzaji bali huendana na soko kama ilivyo kwenye stock market (tofauti na zile za viwandani), tusigeweza kufaidika kwa kwa vyovyote vile kwa kufanya devaluation kwani bei ya kahawa au pamba ingekuwa sawa kwa nchi zote za dunia. Ni tofauti na bei ya magari ambapo Toyota wanapanga bei zao wenyewe wanavyotaka na BMW pia wana bei zao wenyewe pia. Ni kutokana hali ya uchumi wa namna hiyo ndiyo maana devaluation isingesaidia sana uchumi wa Tanzania wakati huo.

Kiuchuguu:

Unayozungumza yana ukweli wake, lakini tutumie data kidogo. Uzalishaji wa mazao ya kilimo pekee yake katika kipindi unachozungumzia ulididimia kwa kiasi kikubwa kufikia 1979. Korosho na Mkonge tayari yalikuwa delisted. Wakulima wa pamba, kahawa na mazao mengine tayari walikatishwa tamaa na ukiritimba wa mamlaka za mazao.

Vilevile pamoja na kuwa kilimo kilikuwa ni uti wa mgongo, serikali ili-invest sana kwenye expansion ya viwanda ambavyo vingi vilikuwa ni hasara tu.

Hivyo faida unazoweka hapa za kuhusu mazao ya kilimo ni imaginary kwa sababu export ya mazao ya kilimo ilipungua sana. Hivyo kwanini unatoa sababu za agricultural commodity prices, wakati tulikuwa hatuna kitu cha kuuza?

Kitu kinapoitwa commodity ni lazima kiwe kimefuata the whole system of production and distribution. Nyerere alikuwa anaogopa devaluation wakati mamlaka zake za mazao zilikuwa hazina hela za kumlipa mkulima, kuprocess mazao na kuyasafirisha kwenda kwa mteja. Pamba ambayo mkulima kavuna lakini haina mnunuzi sio commodity.
 
Kiuchuguu:

Unayozungumza yana ukweli wake, lakini tutumie data kidogo. Uzalishaji wa mazao ya kilimo pekee yake katika kipindi unachozungumzia ulididimia kwa kiasi kikubwa kufikia 1979. Korosho na Mkonge tayari yalikuwa delisted. Wakulima wa pamba, kahawa na mazao mengine tayari walikatishwa tamaa na ukiritimba wa mamlaka za mazao.

Vilevile pamoja na kuwa kilimo kilikuwa ni uti wa mgongo, serikali ili-invest sana kwenye expansion ya viwanda ambavyo vingi vilikuwa ni hasara tu.

Hivyo faida unazoweka hapa za kuhusu mazao ya kilimo ni imaginary kwa sababu export ya mazao ya kilimo ilipungua sana. Hivyo kwanini unatoa sababu za agricultural commodity prices, wakati tulikuwa hatuna kitu cha kuuza?

Kitu kinapoitwa commodity ni lazima kiwe kimefuata the whole system of production and distribution. Nyerere alikuwa anaogopa devaluation wakati mamlaka zake za mazao zilikuwa hazina hela za kumlipa mkulima, kuprocess mazao na kuyasafirisha kwenda kwa mteja. Pamba ambayo mkulima kavuna lakini haina mnunuzi sio commodity.

Unaloongea sasa ndilo hilo la upande wa pili wa bembea niliozungumza katika post yangu ya kwanza. Thamani ya shillingi ilikuwa siyo silver bullet, tatizo lilikuwa kwenye undeshaji, na ndiyo maana nikasema kuwa Nyerere alifanya makosa kuendelea kuwabana wafanya biashara binafsi. Gharama za kuendesha yale mashirika ya umma ilikuwa ni kubwa sana kuliko faida iliyoletwa na mashirika hayo. Kufa kwa kilimo kulisababishwa na mashirika hayo kushindwa kununua mazao yale kwa sababu matumizi ya kuendesha mashirika yalikuwa yamemaliza capital yote ya kununulia mazao. Wakulima hawakuwa na motisha wa kuendelea kulima kwa vile walikuwa hawawezi kuuza, soko lao lilikiwa ni kwenye hizo mamlaka za mazao. Devaluation isingesababisha mashirika yale yaweze kununua mazao na kuyauza nje kwa faida bila kuwaonea wakulima hasa ukizingatia kuwa import-export ratio ya nchi yetu ilikuwa na bado inaendelea kuwa ni kubwa sana.
 
"Ernesto Cheka ni alias inayotumiwa na yule mtoto wa JK aliyeshindwa kusoma kokote duniani na sasa anajiita mtaalamu wa Teknohama".No more comments
 
Mtanganyika:

Kwa ridhaa tu ninapitia kazi fulani za Joseph Stalin. Japokuwa Stalin hakusoma sana lakini wakati ame-commission kuandika kitabu cha Political Economy ya USSR, alitoa points zenye maana sana.

Kwanza anasema kuzungumzia Economy, ni lazima uache rethorics na utumie scientific methods na utumie data kuonyesha maendeleo yako. Kwa Tanzania tumezidisha rethorics (siasa).

Pili anasema kuwa pamoja na kuwa Warusi walikuwa wanajenga Ujamaa lakini kwenye analysis ya ubepari ni lazima utaje na kukubali mazuri ya ubepari. Kwenye political rethoric, unaweza kuukandia ubepari unavyotaka. Lakini kwenye political economy ni lazima kutoa credits.

Kwa kutumia hii mifano miwili, naweza kusema kuwa tuli-base na mpaka sasa bado tume-base kwenye political rethorics. Kwa mfano miaka ya 70 uliweza kusema kuwa kiwanda cha viatu Morogoro kina faida kwa wananchi kwa sababu kilimilikiwa na serikali. Lakini ukitumia data na kuangalia mfumo mzima utaona kuwa kiwanda kizima kilikuwa kinawapa watu hasara.

Data zilizopo zinaonyesha kuwa WB, IMF na wahisani walishiriki kwa kiwango kikubwa kusaidia kuanzishwa kwa sekta ya umma kwa Tanzania na nchi zingine za kiAfrika. Kwa mfano kiwanda cha viatu Morogoro, zilikuwa ni pesa za kutoa WB. Mobutu Seseko alisaidia kiwanda cha kuyeyusha chuma cha zaidi ya dollar 300 million, na mitambo ya umeme ambayo mpaka sasa haijafanya kazi.

Swali linalokuja kwanini haohao watu waliotusaidia kufungua miradi ya thamani miaka ya 70, ilipofika miaka ya 80 wakawa wanasema vibinafsishwe?

Unaweza kusema kuwa Tanzania ilipata misukosuko ya kiuchumi. Lakini Zambia ilipopata uhuru ilikuwa na kipato cha kutosheleza huduma za jamii. Na kila dollar iliyopatikana kwa misaada iliyotoka WB, IMF au nchi wahisani, serikali ya Zambia ilitumbukiza kwenye investments. Kwa upande wa Tanzania kila dollar iliyopatikana ilikuwa inatumika kwenye investments na huduma za jamii. Cha kushangaza, kufikia mwanzoni mwa 80, Tanzania na Zambia wako kwenye kundi moja la umasikini.

Tanzania na Zambia ni nchi za amani, na viongozi wake wa mwanzo walikuwa visionary, lakini failures za kiuchumi za nchi hizi ni Phenomena ambayo sisi wenyewe inabidi kuifanyika kazi. Kuendelea kulaumu WB, IMF haitasidia.

Kuhusiana na wafanyakazi wa WB na IMF ambao wanapendekezwa kurudi nyumbani nakubaliana na wewe kimsingi. Wafanyakazi wengi wa taasisi hizi wanalipwa mishahara mikubwa kuliko hile ambayo wangeipata nyumbani. Hivyo wapo walioridhika na hawatumii muda wao kujifunza mapya hili wanaporudi nyumbani watoe expertise. Hata hapo nyumbani, watu wanataka kupata kazi BOT, TRA kupata mshiko mzuri.

Zakumi,

Siasi na Uchumi ni vitu viwili vizivyo shabiina, lakini wanasiasa wengi wana influance kubwa kwenye uchumi. Tulichokosea Tanzania ni kwamba tuliweka Benki Kuu na Wizara ya Fedha kama mihimili miwili ya serikali. Badala ya kuacha Benki Kuu ikatengeneza fiscal Policy na Wizara ya Fedha na serikali ikaongoza Monetery Policy.

Kuanzia BOT ya mzee Mtei mpaka ya Ndulu zote hazijawi kuwa chombo huru. Madhara yake ni kwamba Politician wamekuwa wakifanya maamuzi ambayo yana influance ya short term ili wao wapete credit kwa wapiga kura. Most of the time politician wanaangalia popularity kwenye policy badala nini kifanyike kwa maendeleo ya nchi.

IMF and WB wameusika tangu mwanzoni mwa Tanzania mpaka leo hii. Nilikuwa nataka kusikia kutoka kwa mzee Mtei jee anadhani ni madhara gani Tanzania imepata kutokana policies za IMF and WB? Na jee kama wakiingia Chadema madarakani ni vipi watareverse hizo policies? Sababu moja ya makubaliano ya kusamehewa madeni ni kukubaliana na policies za hawa jamaa.
 
naona watu wengi mnachanganya devaluation na depreciation.
devaluation ni pale BOT inapoamua kushusha shilingi kwa maksudi against the reference currency ya tz ambayo ni us dollars. hii inaweza ikawa kusaidia export. au BOT inapoamua kuprint hela kwa maksudi ili ku cover budget deficit

lakini kuongezeka kwa bei sukari kutoka 600 hadi 1000, au kushuka kwa thamani ya shilingi kwa dola kutoka 5 hadi 1500 over the years hii ni depreciation.

Semilog:

Ngoja tuchukue definitions zako za devaluation na depreciation na tuziweke katika scenario za uchumi wa Tanzania. Kama nitakosea naomba mnisahihishe. Hapa naiweka hypothetical scenario.

Kwa mfano serikali ya Tanzania iwe inategemea misaada kutoka nje hili kulipa mishahara ya wafanyakazi. Imefika mei mosi, vyama vya wafanyakazi vinaomba ongezeko la mishahara. Kwa sababu serikali ya Tanzania ni ya chama cha wakulima na wafanyakazi inahamua kupandisha mishahara. Lakini kinachofanyika ni kufanya devaluation ya shilingi. Hivyo kwa dola moja yanapatikana madafu mengi yanayolipa ongezeko la mshahara. Lakini kwa sababu nchi inategemea import ya bidhaa. Bei ya vitu inapanda (inflation).

Mwaka unaofuatia kwenye mei mosi wafanyakazi wanaandamana tena. Serikali inaongeza tena mishahara kwa kutumia kiini macho cha devaluation ya dola ya wahisani. Bei ya vitu inaongezekana (inflation).

Zoezi la wafanyakazi kuandamana na kuongezewa biashara linaendelea kila mwaka kwa kipindi cha miaka kumi. Hivyo kutokana na definitions ulizotoa devaluation itakuwa imesababisha depreciation.
 
Unaloongea sasa ndilo hilo la upande wa pili wa bembea niliozungumza katika post yangu ya kwanza. Thamani ya shillingi ilikuwa siyo silver bullet, tatizo lilikuwa kwenye undeshaji, na ndiyo maana nikasema kuwa Nyerere alifanya makosa kuendelea kuwabana wafanya biashara binafsi. Gharama za kuendesha yale mashirika ya umma ilikuwa ni kubwa sana kuliko faida iliyoletwa na mashirika hayo. Kufa kwa kilimo kulisababishwa na mashirika hayo kushindwa kununua mazao yale kwa sababu matumizi ya kuendesha mashirika yalikuwa yamemaliza capital yote ya kununulia mazao. Wakulima hawakuwa na motisha wa kuendelea kulima kwa vile walikuwa hawawezi kuuza, soko lao lilikiwa ni kwenye hizo mamlaka za mazao. Devaluation isingesababisha mashirika yale yaweze kununua mazao na kuyauza nje kwa faida bila kuwaonea wakulima hasa ukizingatia kuwa import-export ratio ya nchi yetu ilikuwa na bado inaendelea kuwa ni kubwa sana.


Kichuguu:

Kwa msingi wa kwamba devaluation sio silver bullet nakubaliana na wewe. Na vilevile nakubaliana na posti yako ya mwanzo. Sasa turudi katika kipindi kile ulipokuwa UDSM.

Kwa sasa hivi inaonyesha history has exonerated Mtei. Lakini kipindi kile mko UDSM inaonyesha Nyerere ali-win the debate. Je kwenye community yenu ya UDSM kuna walioona kuwa Mtei alikuwa na ukweli fulani?
 
View attachment 15566

Ndugu wana JF,

Nimekumbana na habari hizi kwenye facebook kuna bwana mmoja anaitwa ERNESTO SHEKA nemeona nizirushe hapa ili watu waweze kuziona kwa sababu habari yenyewe ni ya uchochezi na upotoshaji mkubwa sasa wahusika wanaweza kuchukua hatua kabla ya damage hajifanyika: kwa sababu jungu limepikwa kweli kweli, CCM wana kazi mwaka huu

The Moment Of Truth:Kila Mtanzania Asome Hii.Sehemu ya Kwanza.


by Ernesto Sheka on Wednesday, 20 October 2010 at 19:42



Tarehe 17 Oktoba nilieleza kijuujuu kwamba inawezekana mwaka 1979 Mwalimu Julius Nyerere alipomsimamisha kazi Edwin Mtei(gavana wa BoT wakati huo),kinyongo kiliendelea.Ulikuwepo msuguano mkubwa kati ya Mwalimu na Mtei kuhusu utekelezaji wa sera za IMF nchini Tanzania na katika moja ya mambo ambayo Mwalimi hakutaka hata kuyasikia lilikuwa suala la kushusha thamani shilingi yetu dhidi ya fedha za nchi za kigeni (devaluation) tulizokuwa tunafanya nazo biashara.Katika moja ya hotuba za Mwalimi alishaliongelea hili.1979 haukuwa mwaka mzuri kwa Edwin Mtei ila alipata kazi katika shirika la fedha IMF na kuhamia Marekani ambapo wanawe walipata elimu yao huku akiwepo Lilian Mtei ambaye baadaye alikuja kuolewa na Freeman Aikaeli Mbowe.

Historia haionyeshi kama Edwin Mtei,mtu aliyepata ugavana wa benki kuu akiwa na umri wa miaka 33 tu kwamba alimsamehe Mwalimu kwa fedheha hii.Najua wengi watasema kwamba haya yaliisha.Lakini tukumbuke kuwa maisha ya binadamu yanaathiriwa na matukio yanayoyazunguka.(Dacher Keltner,"The Compassionate Instinct: The Science of Human Goodness" uk.234-249).Kisasi hasa kwa mtu mwenye madaraka kushushiwa heshima yake kwa kile ambacho Edwin Mtei alikiamini ni sahihi ni jambo lisilopingika.Kwa hiyo toka mwaka 1979 Edwin Mtei tayari alishaanza kufikiri jinsi ya kupata sehemu yake,kurudisha heshima yake iliyopotea kama moja ya wasomi wa wakati huo lakini pia kumuonyesha Mwalimu kwamba alifanya kosa kumsimamisha kazi.Bahati haikuwa yake mapema na lilmpasa kusubiri kwa miaka takribani 13 hadi mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa huku mfumo wa kibepari ambao Mtei amekuwa moja ya makuwadi wake akiwa IMF ukishika mizizi na jamii nyingi za Kikomunisti za wakati huo zikirudi kwenye ubepari.Katika yote hayo ndoto yake ilikuwa inaendelea."Lazima niwaadabishe Nyerere na wote waliomsapoti".Tukumbuke kuwa ilikuwa ngumu hata kwa Lilian Mbowe ambaye alisoma chuo kikuu cha Maryland kupata kazi Tanzania wakati huo.Yote haya yalimzidishia Edwin Mtei uchungu huku akiamini kuwa familia yake ilikuwa na haki zaidi kuliko nyingine.Kwa hiyo mwaka 1992 ulipofika Chadema ikasajiliwa moja kwa moja.(Ndugu,jiulize utaratibu wote uliandaliwa lini,kwa nani na kwa faida ya nani?).Kushiriki siasa kwa Edwin Mtei huku Nyerere akiwa hai halikuwa jambo la busara sana,mzee huyu (ambaye kwa aina ya masterplan yake) naamini kwamba ni mwerevu sana akamuweka Bob Makani,huyu alipaswa kukipasha kiti moto kwa muda kabla Freeman Mbowe ambaye amemuoa Lilian Mtei (mtoto wa Mtei) kukabidhiwa mikoba ya kuendeleza plan yake.

Kuna maswali mnajiuliza:
Je,ni nani hasa Edwin Mtei?
Je,ilikuwaje Mbowe akashinda uenyekiti na si Zitto Kabwe?
Ni ipi hasa masterplan ya mzee huyu aliyechekeana kinafiki na Nyerere?
Imefanikiwa kiasi gani?
Je,anawatumia watu gani?Mimi naweza kuwa natumiwa bila kujua?
Vipi Wangwe?Melo?
Ni nani Deus Mallya na kina nani walimlipia mafunzo ya Kijajusi ughaibuni?(sasa ni mpiga picha wa Chadema)
Ni kweli Chadema walifuja dola milioni mbili kama msaada toka chama cha Conservative cha Uingereza?
Saed Kubenea,Jenerali Ulimwengu,Philemon Ndesamburo,Absolum Kibanda ni kina nani na wanahusika vipi na grand plan ya Mtei?
Nini maana ya "M.Z.M.S" katika Chadema na ilikuwaje Mtei akairushusu na ameiruhusu kufanya kazi katika mlolongo upi na nani yujo juu ya sheria ndani ya Chadema na kwa nini?
...Inaendelea.

Part II iko njiani na jiandae pia kwa video ya kuthibitisha baadhi ya mambo katika haya ninayoandika.


The Moment Of Truth:Hakikisha Kila Mtanzania Anasoma Haya.Tafakari:Sehemu ya Pili


by Ernesto Sheka on Wednesday, 20 October 2010 at 23:37



Tarehe 17 June mwaka 1972 watu watano waliingia kwa siri katika makao makuu ya chama cha Democrats kwenye jengo la Watergate jijini Washington nchini Marekani.Mbali na kuchukua nyaraka za siri ambazo lengo kubwa lilikuwa kumlinda Richard Nixon pia waliharibu baadhi ya nyaraka.FBI walikuja kuugundua mchezo.Wakawakamata wahusika na Agosti 9, 1974,Richard Nixon alijiuzulu kama rais wa Marekani kutokana na kashfa hiyo huku ikibainishwa kuwa alikuwa na kifaa cha siri kilichorekodi sauti ndani ya ofisi hiyo na kila kitu kilichokuwa kinazungumziwa katika ofisi hiyo alikuwa akikifahamu.Nimeanza kwa mfano huu kujenga picha kwamba wanasiasa huwa wana malengo ambayo huwa nayo daima hadi kufa kwao.Edwin Mtei akiwa mmoja wapo kama nilivyosema katika sehemu iliyopita.

Swali kwa vijana wengi ni kwamba je Edwin Mtei ni nani limekuwa gumu wiki hii.Zaidi ya ugavana,uwaziri na ukulima wa kahawa hakuna wanaojua nini kipo nyuma ya pazia hili la Godfather.Mimi naanza kwa kuchambua huyu mtu ni nani na kila aya nasisitiza hatari yake kwa taifa letu na watu ambao ni ngazi zake muhimu.Hili ni jicho linalokutazama mtanzania kila hatua unayopiga na kuonyesha kwamba ni plan makini sana limefanyika kila linalowezekana kumuweka mbali na vyombo vya habari huku ukweli wa binti yake (ambaye ni mke wa Mbowe) kujihusisha na kuajiri mabinti wadogo na kisha kuwadhulumu katika Club yao ya usiku ya Bilicanas ukifichwa kwa kila nguvu na waandishi wa habari wanaolipwa na Edwin Mtei mwenyewe akiwamo mhariri wa gazeti la Tanzania Daima (mali ya Edwin Mtei kwa jina la Freeman Mbowe).Akiishi katika shamba lake Arusha,huku akijiita mkulima wa kahawa asiyependa makuu mzee huyu ni kama walowezi wa Zimbabwe.Kwa waliofika shambani kwake wanatambua naongea nini.(Inawezekana hili la kuwa setla alilianza mwaka1955 hadi 1959 alipokuwa Kenya akifanya kazi kampuni ua tumbaku ya Afrika Mashariki?Nitalichambua kwa hoja).

Ametoka wapi?Alizaliwa mwaka 1932 mkoani Kilimanjaro,mwaka 1946 alipata skolashipu toka Chagga Council (Waliompatia skolashipu hii wajukuu zao wengi wako katika kampuni zake kama wafanyakazi huku wengine wakishirikiana na vijana mbalimbali ambao hawajui lolote katika chadema kuifikia "ndoto").1953 alitoka Makerere na kuingia nchini Kenya katika kampuni ya tumbaku ya Afrika Mashariki.Itambulike kwamba wakati huu ulikuwa wakati wa vuguvugu la kudai haki ya mtu mweusi Tanzania na miaka minne baadaye TANU ilianzishwa.Huku mtu huyu akiwa Kenya,akifanya kazi katika serikali ya wazungu huku Mwalimu na wenzake wakiendesha baiskeli toka Pugu hadi Kariakoo na Upanga kutimiza ndoto ya watanzania.Mtei yeye alikuwa bize Kenya akiwa na girlfriend wake ambaye alimuoa miaka michache baadaye.Hapa tuanaona USALITI wa aina yake.Huku Mwalimu na wanaharakati wengine kama Bibi Titi,Mzee Mwinyimadi Tambaza,Sykes na wengineo wakichomwa jua Dar es salaam,Mtei na elimu yake ya Makerere alikuwa busy akifurahia maisha Nairobi hadi mwaka 1959 aliporudi Tanzania.Miaka 33 baadaye(1992) alitoa wapi kifua cha kujiita mwanamabadiliko???Tuendelee.

Tarehe 20 Januari 1959 alirudi nyumbani akaenda kwao Marangu na baadaye tarehe 9 Februari akafika Dar na akarudia kosa lile lile la kujitenga na wanaharakati wenzake.(Ukisoma katika kitabu chake ambako amejitahidi kwa nguvu zote kuupindisha ukweli utagundua kwamba hili alilipanga tangu akiwa Kenya).Akaenda kuomba kazi katika serikali ya kikoloni na kuajiriwa katika Central Secretariat of the Tanganyika Civil Service.Huu ni mwaka mmoja tu kabla ya uhuru!Kama gwiji wa mitandao ya kijamii (social networks),Mark Zuckerberg anavyosema,"this is a man who never believed and sipport other people's dreams." Hii ni sifa kubwa ya watu wabinafsi na waroho wa madaraka.(Ayn Rand,The Virtue Of Selfishness,uk 117 -129).(Kama kuna mtu anabisha hili mfuateni mkamuulize mtarudi na jibu kuwa alikuwa mbinafsi na msomi asiye mtu wa watu toka akiwa Makerere).HUYU NDIYE ANAYETAKA KUWA BABA WA TAIFA KWA GHARAMA YOYOTE ILE.Tuendelee.

Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na katika kusherehekea siku hiyo mzee huyu anajigamba akionyesha wazi hulka yake ya ubinafsi na kujali nafasi aliyo nayo akisema,"...and I remember celebrating that event very hard because I was newly married and in a newly created country,enjoying my job in a fairly senior position at the Secretariat."That's him pouring rubbish.

Mwaka 1963 akaajiriwa tena EACSO akarudi Nairobi.(Je,alishaanza kuota ndoto ya kuwa bepari?Tafakari).Alidumu kwa mwaka mmoja tu na Mwalimu (naamini 100% kwa kukosa wasomi wa kutosha) akamuita nyumbani aje kuwa katibu mkuu wa wizara ya fedha.Kutokana na ufinyu wa muda kuna mambo mazito ambayo nitawaeleza kwa kifupi sana na kuwaacha muone ni jinsi gani mtu huyu ambaye anajificha nyuma ya pazia pamoja na vibaraka wake kama mkwewe Mbowe na Slaa wanajaribu kuufanya umma wa watanzania vihiy😵ktoba mwaka 1965 kibaraka huyu wa faida binafsi akafanywa gavana mteule na Mwalimu Nyerere(narudia tena kwa jinsi hali inavyofuata huku mbele utaona kuwa alipewa nafasi hii kutokana na upungufu wa wataalamu na Mwalimu alim-doubt toka siku ya kwanza na daima alimuangalia hatua alizopiga).

Asubuhi ya Alhamis tarehe 6 Januari 1966 Edwin Mtei akiwa na umri wa miaka 34 alifanywa gavana rasmi wa benki kuu ya Tanzania na miezi michache baadaye (Tarehe 14 Juni 1966 ) shilingi ilianza kutumika rasmi.Hali haikuwa shwari kama ambavyo nimejaribu kueleza awali,mtu huyu hakuwa anaaminika na Mwalimu na ni sababu tosha kwa nini Mwalimu hakumpa nafasi ya kufanya maamuzi mengi.Utete wa hali hii ukazidi na Mwalimu kwa busara zake akampendekeza kuwa Katibu Mkuu wa EAC wakati huo.Hii ilikuwa mwezi Aprili mwaka 1974,kwa hiyo akatoka katika ugavana na kwenda EAC.Mwaka 1977 (miaka mitatu tu baada ya huyu Godfather kwenda pale),EAC ikavunjika.Kama mchumi hakuona dalili,akashindwa kutoa maono yake kwa usafi na nadiriki kusema anajua kwa nini watanzania wengi ambao leo ni wazee wa rika lake hawajalipwa na EAC.(anajua yeye ni sehemu ya tatizo hilo kwani watanzania wengi walibaki kama vibarua huku wengine wa Kenya wakipewa ajira na mkuu akiwa Edwin Mtei!!!!!!!!).Nitawaachia ninyi muamue.Baada ya hapo Mwalimu akamrudisha nyumbani tena,akamweka awe waziri wa Uchumi na Mipango mwaka 1977.Kauli zake kupokea nafasi hiyo zilikuwa za majivuno na kebehi na kuna mahali alijisahau na kusema,"although I held views critical of the general trend of things,I accepted to serve as Minister in 1977 in a spirit of constructive engagement, believing that I could play a part in improving matters whilst in rather than out."Nadhani alitamani Mwalimu afeli kabisa(rejea kujitenga kwake na wapigania uhuru na kujikomba kuomba kazi kwa wazungu) atimize ndoto yake.Nitaeleza kwa upana mbele.Tuendelee.

Hebu turudi nyuma kidogo.Jumapili tarehe 5 Februari 1967.Siku hii katika kikao Mwalimu alimruhusu afike kama observer tu!!!!Jiulize inaingiaje akili mtu mkubwa kama gavana wa benki kuu awe tu msikilizaji wa kawaida katika kikao kikubwa kama kile???(Muulizeni mkwe wake au yeye kama ana jibu.Believe me,hakuna mwenye kujua haya ninayoyaandika katika Chadema tunayoiona kama system yao ni kuokota ndege wanaokaribia kufa njiani na kuwafuga wakiwaita ndege bora.How does a political party that doesn't understand it's own history and motives behind it's founders move forward?It's a hoax.Political abracadabra.(Daniel Posner,Institutions and Ethnic Politics in Africa😛olitical Economy of Institutions and Decisions,uk.36-59).Mwenye macho haambiwi tazama.Naendelea.

Kitendo cha Mtei kuambiwa na Mwalimu akae kama msikilizaji tu kilimuuma sana,kumbuka huyu ni waziri na gavana wa kwanza wa benki kuu ya Tanzania.(connect the dots ujue Slaa huwa anapata wapi documents za BoT,na kwa nini anazipata leo na si jana,kuna mtu anakutazama).Mwenyewe anakubali katika baadhi ya maandiko yake kwa masikitiko kama pale alipopinga mambo makuu mawili.Villagisation mwaka 1971 hadi 1973 na kutishia kuhusu Capital flight kama Mwalimu angeamua kuingia katika Azimio la Arusha.Kuonyesha kwamba Mwalimu alishamuona si lolote tangu 1953 alipotoka Makerere na kuishi Nairobi miaka 6 huku wanaharakati wa kweli wakiwa Tanganyika,Mwalimu alimpuuza.(Iko wazi kwamba Mtei aliona hathaminiki na ndoto zake za ubepari zilikuwa wazi,tunaweza kusema kwa waziwazi wazo lake la kuasi serikali ya Mwalimu alikuwa nalo toka mwaka 1967,nitaeleza kwa nini).This is a man who believed in capitalism from day na Mwalimu alijua hivyo kwa hiyo hakumweka katika maamuzi makubwa in reality,alimwacha aelee na kumwangalia kwa karibu.

Hali ikazidi kuwa mbaya,1979 Mwalimu akamtimua huku yeye akisema aliachia ngazi mwenyewe (Jiulize kwa nini na ilikuwaje akatoa kitabu cha historia ya maisha yake baada ya kifo cha Mwalimu.So clear,it makes a click.).Naamini kama Mwalimu angekuwa na intelijensia bora,Mtei angekuwa wa kwanza kuihama Tanzania kabla ya marehemu Oscar Kambona.Katika moja ya maandishi yake anaeleza kwa kujificha sana kwamba alikuwa mtu safi huku akificha ukweli kwamba sera kama devaluation na reconstruction ya mashirika ya umma si sahihi kufuata tu oda za IMF bali pia kuangalia muda husika!Aibu sana.."..
The IMF therefore required us to devalue the Tsh and to review the management of our parastatals before they could give us balance-of-payments support. In the negotiations, I was able to get the IMF to scale down their demands on devaluation and make them accept that we would examine individual public corporations to see how they could be restructured to perform better.When I explained this approach to the President he was quite categorical that he would not accept any devaluation and that he would review the parastatals onlyat his own timing. He implied that he would not be dictated to from
Washington..." Anajaribu kusemaje?Mwalimu was stupid?How on earth do you restructure your parastatals when you don't have enough natives educated to take over and work with highly qualified foreigners?Ni simple economics.!Mtei alifumba macho na Mwalimu alipojiridhisha kwamba amembeba kiasi cha kutosha ila habebeki,akamtimua.Safari ya Marekani ikanukia na akaenda zake Washington.(The only reason he was never exiled ni kwa sababiu tayari alijua mengi sana kuhusu intelijensia ya nchi.Je,aliwafuata marafiki zake?).Tuendelee.

Novemba akarudi nyumbani.(Angalia timing!Just a year after Mwalimu has resigned!!)Huku nako mambo hayakuwa sawa,ujamaa ulishindikana.(si tu kwa sababu duniani haukufanikiwa lakini pia kwa sababu watu ambao Mwalimu alitegemea wangempa sapoti kama Mtei na Kambona walifanya majuha wakataka waishi ndoto zao ndani ya sekunde).Moja ya watu walipata masaibu ya Mwalimu ni Jenarali Ulimwengu ambaye alisimamishwa ubunge baada ya sakata la G55.Huyu akiamini kabisa kwamba yeye ni bora kuliko Jakaya Kikwete na Maalim Seif ambao walikuwa vijana wapenzi wa Mwalimu kipindi hicho akajikita katika habari huku naye akiwa na ndoto zake).

Ndoto na chuki zaja hadharani sasa baada ya miaka takribani 26,Julai 1992 mfumo wa vyama vingi ukaanza.The same year Mtei akaanzisha Chadema na mpaka ninapoandika hili,in practical terms yeye ni mwenyekiti wa Chadema,kwake yeye ile ni fimbo maalumu ya kumchapa Mwalimu Nyerere siku akifanikiwa japo kila mara anakosea mahesabu huku jamii ikizidi kuamka na kujua historia ya taifa na kuchambua mambo hatua kwa hatua.Uzee umekuwa wa mashaka na wasiwasi.Ni dhahiri kuwa masterplan ya kuanza kwa Chadema ilianza kuandikwa Nairobi na baadaye Washington huku ikiuwaza ubepari na Ikulu kabla hata ya usajili.Lilian Mbowe ni mtoto wa kike wa Edwin Mtei ambaye aliolewa na Mbowe.Ni daktari ambaye kama nilivyosema awali anajishughulisha na kuendesha club ya usiku katikati ya jiji la Dar es salaam mtaa wa Mkwepu.Nyumba zao hutumika kukusanya vijana na wengi wana upofu na historia ya Chadema,wanaogundua huondoka mara moja.(Mtafuteni David Kafulila atawahadithia sehemu hii).

Je,ilikuwaje Mbowe akashinda uenyekiti na si Zitto Kabwe?
Edwin Mtei namnukuu akisema,"we can't give this position to a man from nowhere" akimaanisha Zitto Kabwe,Zitto alitaka kuondoka ila alibaki kwa sababu zake.Tafakari hiyo kauli ya Mtei.Who's a man from nowhere and who's a man from somewhere??Ni ipi hasa masterplan ya mzee huyu aliyechekeana kinafiki na Nyerere?To revenge and take back his dignity and self interests.Ni ndoto yake ya ujanani na anaomba Watz tumsaidie.

Imefanikiwa kiasi gani?
Hali ni ngumu,ukabila bado umekuwa tatizo.Kifo cha Wangwe,maneno kuhusu viti maalumu,uwepo wa Deus Mallya aliyevuruga mpango wa kufunika sakata la kula pound za waingereza kama ruzuku kwa chama na baadaye kufoji risiti .(John Mnyika alikuwa kinara wa shughuli hii ya kuchakachua risiti).Wangwe's head had a price tag but Deus Mallya made a noise and Chadema let him went down and come up alone(sifa kubwa ya majasusi unapoharibu mpango wa kazi na ukapata tatizo).Ninapoandika hili,Deus Mallya ni mpiga picha na designer rasmi wa Chadema huku mifupa na damu ya Chacha Zakayo Wangwe ikilala udongoni kule Tarime.

Je,anawatumia watu gani?Mimi naweza kuwa natumiwa bila kujua?
Anawatumia watu ambao mkwewe,Freeman Mbowe humpelekea.Hakuna details zozote kuonyesha kama Slaa,zitto na Mtei walikuwa na uhusiano wa karibu miaka saba nyuma!Wachezaji waliokaa pamoja siku mbili wanataka kuomba mechi.Sick jokes.Jenerali Ulimwengu,Saed Kubenea,Maxence Melo,Mike Mushi (huyu baadaye alikimbia).Kuchafua nchi mtandaoni kwa kutumia mtandao wa Maxence Melo ambao una mahusiano ya karibu na baadhi ya watu waliko Houston,Texas.Absalom Kibanda (ni mwandishi na mhariri wa Tanzania Daima ambaye anatembea juu ya ukanjanja wa kutupwa).Unaweza kutumika bila kujua kama hutasikiliza na kutafakari na kuhoji.Sote tunakubaliana huwezi kuacha kutumia gari lako zima ukaamua kuazima gari la jirani yako ambalo lina taa mbovu,tairi mbili mbovu na mafuta hakuna.

Nini maana ya "M.Z.M.S" katika Chadema na ilikuwaje Mtei akairushusu na ameiruhusu kufanya kazi katika mlolongo upi na nani yujo juu ya sheria ndani ya Chadema na kwa nini?M.Z.M.S ni ufupisho wa watu wenye veto power ndani ya Chadema japo zinatofautiona uzito.(Mama Shida Salum,mama mzazi wa Zitto anajua hili).Mbowe,Zitto,Mnyika na Slaa.Uzito wa kura uko kama nilivyoorodhesha majina toka juu kwenda chini.Kama mtu sijamtaja hapo ujue hata Mtei hataka kujus undani wako.

Hitimisho:
Nashukuru kwa kuisoma,je utamsaidia Mtei kumchapa Mwalimu Nyerere bakora kisha alete ilani yake?Si ile inayonadiwa.Je,unajua undani kwa nini moja ya sera za Chadema ni kuigawa nchi katika zones?(majimbo)?Ni nani wanakusudia wawe magavana,majimbo hayo ni yapi na kwa nini?

Muda umeniishia ila tafakari na amua mwenyewe.
Mungu Ibariki Tanzania.
Ernesto Sheka.
Oktoba 20,2010
Butiama,Musoma, Tanzania.

NB:I'll release a video few days to come kuelezea baadhi ya mambo katika note hizi mbili.

KAZI MNAYO.MPINGENI KWA HOJA SASA TUONE U-GREAT THINKER WENU.AMEKOPI HADI KAULI ZA MTEI.KAZI IPO.:A S thumbs_up:
 
Wala asiwaumize kichwa huyu Ernesto Sheka. Hii habari ingeletwa na independent member ningeumiza kichwa; lakini baada ya kufuatilia kidogo tu naona wale wale, - maji taka; ==== pants on fire!!


"Kwa wote mnaoandika maombi ya scholarship hapa hapa kwenye.. of B. COM(ACCOUNT) at the university of Dodoma(UDOM),I'm seeking. Ernesto Sheka (JAKAYA MRISHO KIKWETE FOR 2010) UDOM project overview is on air at. Hapa mtakuta habari mbalimbali za kampeni na taarifa zinazohusiana na. Edward Muhoza kaija we ujui kitu nyamaza tuu unatia aibu nani asiye jua ccm.
Lenght of string "Links on "JAKAYA MRISHO KIKWETE FOR 2010" | Facebook": 62 chars"
Ernesto Sheka · JAKAYA MRISHO KIKWETE FOR 2010 ... UhuruOne If you could kindly drop us a private message or email on network-support@uhuruone.com
 
Mnasubiri nini? tarehe 31 tuna kwenda kukamilisha kazi..

67545_155702807802411_128458070526885_237584_1174256_n.jpg
 
Da nimefurahi sana. Kumbe Mzee Mtei ni msomi hivyo? Halafu aliukwaa ugavana at 33 years old? Huyu ndiyo angetufaa kuwa Rais wa Tanzania. Halafu eti Nyerere alikataa devaluation, sasa tuliposhinikizwa kwenye financial sector reform kuacha shillingi ijirekebishe kimasoko sasa tuko wapi? Tulikataa tulichokikubali!!

Hapa ni jungu tu na watanzania hawadanganyiki ng'ooooo. Tena ngoja niwagongee MODs waipeleke hii thread kunako. Uchafu huu. Mbona vibaraka wanatafuta kila mbinu kuchafua hali ya hewa? Kama kweli vibaraka na chama chenu ni kidume kwa nini mnaogopa hivyo. Acheni wananchi watenge wenyewe pumba na mchele. Acha demokrasia ichukue mkondo wake.
 
Da nimefurahi sana. Kumbe Mzee Mtei ni msomi hivyo? Halafu aliukwaa ugavana at 33 years old? Huyu ndiyo angetufaa kuwa Rais wa Tanzania. Halafu eti Nyerere alikataa devaluation, sasa tuliposhinikizwa kwenye financial sector reform kuacha shillingi ijirekebishe kimasoko sasa tuko wapi? Tulikataa tulichokikubali!!

Hapa ni jungu tu na watanzania hawadanganyiki ng'ooooo. Tena ngoja niwagongee MODs waipeleke hii thread kunako. Uchafu huu. Mbona vibaraka wanatafuta kila mbinu kuchafua hali ya hewa? Kama kweli vibaraka na chama chenu ni kidume kwa nini mnaogopa hivyo. Acheni wananchi watenge wenyewe pumba na mchele. Acha demokrasia ichukue mkondo wake.

Nimesoma comments nyingi sana hapa na Facebook hakuna mtu aliyejibu kwa hoja.Kwa ufupi inaamanisha Sheka kasema ukweli na ndio maana critics wa upinzani hasa Chadema wanaikimbia hii habari.Na sitashangaa ikifutwa hapa JF.
 
KAZI MNAYO.MPINGENI KWA HOJA SASA TUONE U-GREAT THINKER WENU.AMEKOPI HADI KAULI ZA MTEI.KAZI IPO.:A S thumbs_up:

Haya ni yale yale ya CUF na Mahita ya 2005. Mfa maji haachi kutapatapa.

Kila chama kina historia yake na namna kinavyoendesha mambo yake.

Hoja ya Mtei na Ubepari haipo tena kwani CCM walishautupa Ujamaa Zanziba wakati Mwalimu yoko hai bila hata kumualika kwenye kikao cha kuvunja Azimio la Arusha. Wakatengeneza ubepari wa wizi wa mali za umma (Sio wa kufanya kazi ili kupata mali) mchana kutwa, Wakajimilikisha maeneo ya uwindaji, Wakajimilikisha bandari, Makampuni ya simu (Vodacom, et al - Kumbuka Msekwa alivyo wekwa kuwa mkurugenzi wakati akiwa spika na bado wakamtetea -eti ni wivu wa kike wa watanzania!!!!!!!)

Hoja ya chama kuendeshwa na familia, hii usiseme, kama, CCM wamecopy, ndio mwisho wamechukua mpaka nukta. At least hatumuoni Lilian majukwaani!! Makamba naye - Wanajitengenezea vijikoo vya kifalme!!

Tuombe moja, Huyu bwana Sheka akimaliza, tutashusha historia ya Mtandao na vyote walivyofanya kwenye nchi hii. Watu watajua, Nani Mkumbwa Ally, Salva Rweyemamu, RA, EL, etc.

We are opening the pandora's box. Stay tuned.
 
hivi hao ccm sio mabepari?????mbonma kila siku mkuu wao yuko ulaya kwa hao mabepari akibembeleza ulaji??????crap crap crap...na mbona wao wameshusha thamani ya shilingi??????nia yao hasa ilikuwa ni nini??????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom