Mti wa Chuma
JF-Expert Member
- Jul 2, 2015
- 331
- 99
Bunge la 11liliingia siku yake ya nne (4) Ijumaa ambapo ilikuwa siku maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuhutubia bunge na kufungua rasmi. Kabla ya Mh. Magufuli hajaingia wabunge wa upinzani wanaounda UKAWA walianza kupiga makelele wakimtaja Maalim Seif wa Zanzibar. Hali hiyo ilimlazimu spika wa bunge Job Ndugai kuamuru watoke nje baada ya kuwataka watulie lakini hawakufanya hivyo.
Cha kujiuliza; Walichaguliwa na wananchi kwenda bungeni kufanya vitu vya ajabu?
UKAWA sioni wanachodai hadi kupiga makelele ndani ya ukumbi tukufu la bunge. Katika kufuatilia kwangu kwa undani zaidi kuna mtu nyuma ya wabunge wa UKAWA, na si wote wanapenda kufanya fujo (kupiga kelele).
Kwa mtazamo wangu UKAWA inakoelekea watapoteza mwelekeo pia watakosa matumaini kwa wananchi, uchochezi huu huchangiwa na viongozi wakubwa wa vyama vinavyounda UKAWA. Cha kushangaza hata sheria inayozungumzia ukomo wa kipindi cha Rais Zanzibar wanapindisha.
Kwa mtazamo wangu UKAWA muda si mrefu watatengana.