Tuna Bunge kibogoyo, tuwaadhibu wabunge waliopitisha mkataba wa DP World

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Umofia kwenu.

Dibaji inasomeka.
Bunge na wabunge ambao kimsingi ni wawakilishi na sauti za wananchi wameonesha wazi kutowatetea tena wananchi na limeungana na serikali kuu kuitafuna nchi.

Kupitia Mkataba wa DPW tumeona wazi namna Bunge letu linavyojipendekeza kwa watawala badala ya kuisimamia na kuishauri serikali. Spika wa Bunge amegeuka mpigadebe wa serikali Bungeni. Amekuwa msimamizi mkuu wa shughuli za serikali Bungeni.

Nawashauri Watanzania wenye umri wa kupiga Kura, kutowarejesha wabunge hawa Bungeni katika uchaguzi wa 2025. Tusiwapigie kura wagombea wowote kutoka CCM kwa sababu tumeshaelewa dhumuni lao halisi ni kuiuza Tanzania kidogo kidogo kama walivyofanya Loliondo na kwingineko.

Nanyi wanasiasa wenye uwezo, jitokezeni kuwania nafasi mbalimbali ktk uchaguzi wa 2024/2025. Kuwaachia CCM kuendelea kutawala ni kumsusia fisi bucha
 
Back
Top Bottom