Uchaguzi ni mchakato sio kupiga kura. Je, tupunguze idadi ya wabunge bungeni?

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Tunapoongelea katiba tuangalie pia marekebisho kwenye taratibu za vyama vya siasa. Tuna wabunge wengi ambao ndani ya miaka mitano ya ubunge kuna wabunge hawajawahi kuongea chochote bungeni iwe kwa mdomo au maandishi(Wabunge mabubu).

Vyama vya siasa havitaki viguswe na katiba vinaona vipo sahihi mpaka sasa katika misingi yao, Wanasiasa hawataki kujadili misingi ya vyama vyao na uwajibikaji mbele za wananchi hasa idadi yao bungeni kuwa ni kubwa kuliko pato la Taifa.

Mchakato wa uchaguzi ni hatua inayojumuisha kuwatambua kwa kina wanaopenda kugombea katika eneo husika uaminufu wao,uwezo wao na tabia zao.

Yasipofanyika hayo ndio matokeo ya kuwa na wabunge aina ya Gekul Pauline,Wananchi wa eneo husika huko babati baada ya tukio ndio sasa wanaelezea maisha yake, tabia yake na uaminufu wake kuwa ulikuwa wa hovyo na hafai kwenye jamii na hafai kuwaongoza ni kama walilazimishwa tu.

Michakato ya kwenye vyama vya siasa ya kutuamulia mgombea ambaye hafahamiki mbele ya wananchi tabia zake,uwezo wake na uaminufu wake ni tatizo kubwa sana

Hatuna haja ya kuwa na wabunge zaidi ya miatatu bungeni.

Tuna mikoa ishirini na sita tu,Tunahitaji kila mkoa kuwa na Gavana mmoja tu au muwakilishi mmoja tu bungeni.

Nini kifanyike kwenye michakato ya uchaguzi na idadi ya wabunge kikatiba

Mosi,Watu wajitokeze ndani ya mkoa husika iwe kupitia vyama au binafsi washindane kwa hoja kwenye mikutano ya hadhara waulizwe maswali ,Waambiwe mambo yao na taarifa zao kama za ukwepaji kodi,Unyanyasaji wa kijinsia,ubadhirifu wao na mwenendo mzima wa tabia zao.

Pili,Kuwe na kamati maalumu ya vetting ndani ya mkoa husika na itakayosimamia michakato ya uchaguzi hadi kuhesabu kura ,kamati ambayo wananchi wenyewe ndio waamue nani aingie kwenye kamati kwa kupiga kura, kamati hiyo itaacha kufanya kazi pale uchaguzi unapomalizika ingawa itakuwa hai kwa kipindi cha miaka mitano .

Tatu.Wagombea wote waambiwe kwa uwazi mbele ya wananchi kwanini majina yao hayafai kugombea mbele ya jamii na wapewe nafasi ya kujitetea au kujibu hoja kwa ushahidi.

Nne,Waliopita ndio wapigiwe kura na mkoa husika kupata muwakilishi mmoja kama mbunge au Gavana wa mkoa husika atakae wakilisha mkoa husika bungeni.

Mwisho,Huyo muwakilishi atawajibika kwa mkoa husika na atatakiwa atoe taarifa kwa wananchi katika kila mwenendo wa maendeleo na wananchi wasiporidhika wawe na uwezo wa kumuwajibisha kupitia kamati yao inayosimamia vetting.

Nafasi ya kisiasa ya mkuu wa mkoa iondolewe kabisa tubakiwe na watendaji wa serikali katika mkoa,Kwa sasa nafasi ya utendaji ipo chini ya RAS (Regional administrative secretary) Ndani ya mkoa mtendaji wa upande wa serikali awe RAS tu na sio tuwe na pambo la mkuu wa mkoa.

Kwenye bunge kubwa la bajeti tunaweza waruhusu pia wawakilishi wa serikali yaani Ma RAs pamoja na wabunge wao wakaingia bungeni hivyo kufanya jumla ya watu hamsini na mbili tu bungeni yaani ishirini na sita wa serikali na ishirini na sita wa kisiasa.

Jumla =wabunge 26+Ma Ras 26=52

Hatuna haja ya kuwa na wabunge miatatu bungeni ambao uwezo wao ni mdogo na hawana maarifa ya kulitoa Taifa hapa tulipo,Tuna idadi ya wawakilishi wa kusifia tu badala ya kuweka hoja mezani.

Mfano,Mabadiliko ya mfumo wa elimu yameongelewa juu juu tu kwa kuwakutanishi wadau baadhi ,Ukisoma mapendekezo unagundua bado tatizo letu la elimu liko pale pale tumepunguza tu iwe miaka sita ya kusoma na hii inatokana na kukosa wawakilishi sahihi ambao walitakiwa kupata taarifa toka kwa wananchi kupitia muwakilishi wao.

Sijasikia muwakilishi yeyote akitoa taarifa mbele za wananchi kuhusu mwenendo wa Taifa, Tupo wapi, Tumekwama wapi na nini kinakwamisha na tunafanya nini kusonga mbele.
 
Tunapoongelea katiba tuangalie pia marekebisho kwenye taratibu za vyama vya siasa.Tuna wabunge wengi ambao ndani ya miaka mitano ya ubunge kuna wabunge hawajawahi kuongea chochote bungeni iwe kwa mdomo au maandishi(Wabunge mabubu)

Hatuna haja ya kuwa na wabunge miatatu bungeni ambao uwezo wao ni mdogo na hawana maarifa ya kulitoa Taifa hapa tulipo,Tuna idadi ya wawakilishi wa kusifia tu badala ya kuweka hoja mezani
Naunga mkono hoja
P
 
Tunapoongelea katiba tuangalie pia marekebisho kwenye taratibu za vyama vya siasa.Tuna wabunge wengi ambao ndani ya miaka mitano ya ubunge kuna wabunge hawajawahi kuongea chochote bungeni iwe kwa mdomo au maandishi(Wabunge mabubu)

Vyama vya siasa havitaki viguswe na katiba vinaona vipo sahihi mpaka sasa katika misingi yao,Wanasiasa hawataki kujadili misingi ya vyama vyao na uwajibikaji mbele za wananchi hasa idadi yao bungeni kuwa ni kubwa kuliko pato la Taifa
Asante Kwa kuleta hoja ambayo itajadiliwa na watu wachache lakini Wenye akili. Kuwa na Idadi kubwa ya watumishi wasio na tija ni kukaribisha anguko la Taasisi. Nchi kama Taasisi hatuna haja ya kuwa na rundo la watumishi wasio na tija huku wakiendelea kulipwa mamilioni ya fedha ambazo tungeweza kuzitumia Kwa shughuli nyingine za maendeleo.

Mapendekezo ya kuwa na Mbunge mmoja Kwa Kila mkoa ni mazuri, lakini Mimi nashauri Kila mkoa uwe na Wabunge wawili tu bila kujali ukubwa wa mkoa husika. Mmoja mwanaume na mmoja mwanamke. Kisha hao MaRAS wanaweza kuongezeka na jumla watakuwa 78.
 
Asante Kwa kuleta hoja ambayo itajadiliwa na watu wachache lakini Wenye akili.
Kuwa na Idadi kubwa ya watumishi wasio na tija ni kukaribisha anguko la Taasisi. Nchi kama Taasisi hatuna haja ya kuwa na rundo la watumishi wasio na tija huku wakiendelea kulipwa mamilioni ya fedha ambazo tungeweza kuzitumia Kwa shughuli nyingine za maendeleo.
Mapendekezo ya kuwa na Mbunge mmoja Kwa Kila mkoa ni mazuri, lakini Mimi nashauri Kila mkoa uwe na Wabunge wawili tu bila kujali ukubwa wa mkoa husika. Mmoja mwanaume na mmoja mwanamke. Kisha hao MaRAS wanaweza kuongezeka na jumla watakuwa 78.
Naunga mkono hoja, na hili hata wanaopigania katiba sasa hasa wanasiasa hawalipendi kabisa

Kuwa wachache bungeni wanaona watakosa madaraka
 
Kila wananchi laki 2 wawakilishwe na mbunge mmoja,
Viti maalum vifutwe,
Ubunge wa kuteuliwa ufutwe,
Wagombea binafsi waruhusiwe,
Mbunge akihama chama, akijiuzulu, akifariki au akiondolewa kwa namna yoyote nafasi yake ijazwe na chama alichohama
Wabunge waliofukuzwa chamani mwao wasiruhusiwe kuendelea kukaa bungeni.
 
Yasipofanyika hayo ndio matokeo ya kuwa na wabunge aina ya Gekul Pauline,Wananchi wa eneo husika huko babati baada ya tukio ndio sasa wanaelezea maisha yake, tabia yake na uaminufu wake kuwa ulikuwa wa hovyo na hafai kwenye jamii na hafai kuwaongoza ni kama walilazimishwa tu.
Aliyelazimisha wao kuongozwa na Gekul ni nani ?
 
Back
Top Bottom