Mtazamo wangu: Kero anazotatua Makonda zinamuhitaji azunguke nchi nzima miaka 60 ijayo

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,587
15,371
Mimi ni mtu wa imani, mpenzi wa Biblia na mqmbo chanya kwenye Quran. Kwa upeo wangu hafifu kisiasa nimeangalia malalamiko anayotatua Mh Makonda nimeona anahitaji kuzunguka nchi nzima miaka 60 ijayo angalau hadi 2084 Feb.

Kwanini?
1: Matatizo anayoletewa mtu kukatwa mapanga, kunyimwa malipo na halmashauri, etc yanayopelekea alie na wao waliao ni mengi karibu kila raia anayo. Na pia yanajirudiarudia.

2: Matatizo wanayoripotiwa na wananchi kwa mtazamo wangu hayatatuliwi field yanatatuliwa hukohuko afisini alikotoka. Naona alitakiwa kukaa kwa mamlaka tunayomuona nayo akae na mawaziri, wakurugenzi, na decision makers nchi nzima kisha atoe tamko moja ambalo atapita kama sasa kuhakiki utekelezwaji wa tamko lake.

3: Rais Magufuli alitembea nchi nzima ni muda mfupi tu uliopita. Watu walihama hadi mikoa kumvizia waeleze shida zao. Alienda mbali hadi kutembea na maburungutu ya fedha kutatua vinavyowezekana lakni hadi sasa inaonekana hakusaidia kitu maana malalamiko ni yaleyale.

Kwa hiki kinachofanyika ikiwa kina nia kificho zaidi ya hii tunayoiona ni sawa na kuzunguka duara, au kutafuta kipeuo cha moja huku ukitegemea majibu tofauti.

Ushauri
Malizia ziara zako za kisemaji, kisha mrudi mshauriane ofisini, ziara hizo uzifanye maofisini live. Wizarani, kwenye taasisi, na maofisi ya umma maana huko kwa wananchi hata wao wanasema lakini wanajua wanayemwambia anajua.

Ziara zijielekeze kwenye mfumo na wasimamizi wa mifumo suo huku kwa wananchi ambao hata sababu za matatizo yao zinarudishwa kwenye mifumo ambayo umeiruka.

Kama huu ndio ubunifu wa chama, basi utakuhitaji miaka 60 ili ufikie tatizo la kila mtu, na 60 za kutatua ikiwa Bwana Yesu atakuwa bado anahairisha kurudi kuangamiza dunia.

Wabheja sana.
 
  • Thanks
Reactions: ERT
Mbona ni siasa za wazi kabisa zile ila ajabu ni kua wabongo walivyo wapuuzi hawalioni hilo, wao wanaona anaupiga mwingi.

Kuna uongozi kila shina ajabu eti mtu toka juu ndo aje atatue kero ya maji kwa baba juma.
 
Back
Top Bottom