Paul Makonda amtaka waziri wa viwanda na biashara kuzunguka nchi nzima kutatua kero za wafanyabiashara

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara ,Jabali la siasa,mtetezi na Sauti ya wanyonge ametoa maagizo mazito ya chama ya kumtaka waziri wa viwanda na biashara kuzunguka nchi nzima kwa kusaidiana na naibu waziri wake,kwenda kusikiliza kwa kina na umakini kero za wafanyabiashara maeneo mbalimbali nchini.

Amesema katika ziara yake aliyoianza na anayoendelea nayo mikoani amekutana na kero na malalamiko mbalimbali yanayotoka kwa wafanyabishara.amesema kuwa viongozi wanapaswa kuwasikiliza wafanyabiashara na watu wengine na kuwapa majibu.

Pia alifikia hadi hatua ya kusema kuwa wafanyabiashara wakati mwingine wanalazimika kuichangia CCM pesa kwa kuogopa rungu la TAKUKURU na TRA,hivyo akataka viongozi kuwa karibu na kuwasikiliza kero zao wafanyabiashara na kuwasaidia ili hata kama wanaamua kukichangia chama basi wachangie kwa hiyari yao na siyo kwa hofu au uoga au vitisho vya aina yoyote ile.

Kwa hakika ndugu zangu Mheshimiwa Paul Makonda ni mtetezi na sauti ya wanyonge,ameinuliwa na Mungu mwenyewe kuja kumsaidia kazi Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan katika kuwafikia watanzania na kuwasikiliza kero zao. Kila mtanzania anafahamu uwezo mkubwa wa kiuongozi na ujasiri mkubwa alionao Mh Makonda .ni mtu jasiri kwelikweli, haogopi wala hatishwi wala kupigwa mkwala katika suala la kuwatetea na kuwasemea wananchi wanyonge.yupo tayari achukiwe na wengi lakini wanyonge wapate kupona na kupata tabasamu , matumaini na furaha katika mioyo yao.hiyo ndio furaha ya mh Makonda kutaka kuona watu wanyonge wanapata haki na kutendewa haki kwa haki.

Hataki kuona wananchi wanyonge wakionewa ,wakidhulumiwa haki zao,wakinyanyaswa na viongozi au watumishi wa umma au watendaji wa serikali,hataki kuona watu wakinyimwa haki kwa sababu ni maskini au kwa kuwa hawana ndugu wenye vyeo serikalini.

anataka watu wote watendewee haki waendapo popote pale kupata huduma au kutafuta msaada wa kero zao,anataka kila mtu asiklizwe na kupewa huduma bila ubaguzi kwa misingi ya aina yoyote ile.hiyo ndio kiu kubwa iliyo jaa katika kifua na moyo wa Mheshimiwa Makonda. Hiyo ndio kazi ya kitume iliyo ndani yake na hiyo ndio inayomfanya ,kumchochea na kumsukuma afanye kazi usiku na mchana na kuzunguka nchi nzima bila kuchoka kuwafikia watanzania na kuwasikiliza kila mtu kwa unyenyekevu na upole.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
IMG-20240208-WA0015.jpg
IMG-20240206-WA0027.jpg
IMG-20240208-WA0009.jpg
IMG-20240208-WA0006.jpg
IMG-20240205-WA0023.jpg
IMG-20240202-WA0010.jpg
IMG-20240208-WA0016.jpg
 
Hivi wewe mtu unajua kuwa watanzania hawana umeme wa uhakika?hivi unaijua kuwa maji yamekua bidhaa adimu sehemu nyingi? Unajua kuwa bie ya bidhaa karibia zote imepaa kupitq maelezo? Unaishi Tanzania ipi wewe?
 
Ukweli upi uliopo hapo.kazi yangu ni uhabarishaji na usema kweli wakati wote.
Nikuwekee Nyuzi zako mara Mama anakata kiu...mara Mama ni Nuru ya Mnyonge...?

Watu tumepinda hakuna umeme gharama za maisha ziko juu maji hayatoki mafuta yako juu nk.

Halafu wewe unakuja na POROJO humu.
 
Hivi wewe mtu unajua kuwa watanzania hawana umeme wa uhakika?hivi unaijua kuwa maji yamekua bidhaa adimu sehemu nyingi? Unajua kuwa bie ya bidhaa karibia zote imepaa kupitq maelezo? Unaishi Tanzania ipi wewe?
Bidhaa zipi hizo unazisema zote zimekaa?? Maana kama ni suakri tayari serikali imeshaingiza nchini tani za kutosha ambazo zinakwenda kuanza kusambazwa maeneo mbalimbali nchini na hivyo bei ya sasa itashuka haraka sana.

Kama ni bei za vyakula nazo zipo vizuri.mfano jaribu kuangalia bei ya kilo moja ya unga mwezi kama huu mwaka jana ilikuwa ni shilingi ngapi na Leo ni shilingi ngapi?

Kuhusu maji mimi niliko na hata mikoa jirani maji ni ya kutosha sana mpaka watu wanamwaga na kukinga mengine ya mvua na kuacha kabisa kutumia yale ya bombani ambayo nayo yapo ya kutosha tu.

Umeme nao hali inakwenda kutengemaa muda siyo mrefu kutokana na kuwashwa kwa mtambo wa kwanza katika bwawa la mwalimu Nyerere muda siyo mrefu ambapo litatupatia megawati 205 zitakazounganishwa katika grid ya Taifa.
 
Yaani 109 imegeuka kuwa mobile farm/garden, si mchezo 2024
Kuna tangazo moja la VODACOM nadhani ni Nipige Tafu lilikuwa na Jamaa na 109 yake imejaa mboga mboga halafu Zutu likakata😂🤣
 
Back
Top Bottom