Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,875
Fact-Check ,Fact-Check Kuhusu Migogoro Ardhi.
Kwenda kwa Muenezi wa Matamko Bwana Ndug.Paul Makonda.
Bwana Muenezi Mtoa Matamko umetoa tamko Kwaniaba ya chama kumpa Waziri Mkuu miezi 6 kushughulikia suala la migogoro ya ardhi nchini. Miaka 60 ya uhuru ,CCM mmetawala mmeshindwa kutatua changamoto ya migogoro ya ardhi nchini mtawezaje leo kwa kutoa "matamko " na kutoa miezi 6 huku miaka 60 mmeshindwa bwana Muenezi Mtoa Matamko?.
Migogoro mingi ya ardhi chanzo chake ni kushindwa kwa utekelezaji wa sera na mipango na ubunifu ,CCM mmeshindwa kutatua changamoto ya Ardhi nchini , mmeshindwa hata kutekeleza ilani yenu,sasa mmeamua kujificha kwenye mgongo wa matamko ya Bwana Muenezi.
Bwana Muenezi Mtoa Matamko, punguza kutoa matamko,matamko hayatasaidia kitu.Soma katiba yenu ya CCM ibara ya 107(2) a -e , inaelezea majukumu yako kama Muenezi . Jukumu lako la kwanza ni kushughulikia masuala ya itikadi na sera za CCM . Sera ni pamoja na "Ilani". kama unataka kuleta uwajibikaji basi vyema iwe kupitia ilani yenu sababu Wananchi watawapima kupitia ilani yenu,tujue kwanini mliyoahidi kuhusu Ardhi hamjatekeleza hadi sasa?. Na huu unapaswa kuwa uthibitisho wa kwamba CCM na serikali yake wameshindwa kutatua changamoto ya Ardhi nchini.
Mfano, ilani yenu CCM ya 2020,kurasa ya 116 kuanzia kifungu cha 72 mliahidi "Upangaji,Upimaji na umilikishaji wa Ardhi " hii ina maana mliahidi Ardhi zote nchini kupimwa . Bwana Muenezi Mtoa Matamko nikupe taarifa kutoka kwa Mtoa taarifa ya kwamba hadi sasa naongea na wewe Upangaji ,Upimaji na urasimishaji wa Ardhi nchini umefikia asilimia 25% ya vijiji vyote,Tume ya Mipango bora ya Ardhi mnaipa bajeti ndogo kwasababu sio kipaumbele chenu kutatua migogoro ya ardhi nchini kupitia kupima Ardhi yote.
Kwa tafsiri hiyo CCM mmeshindwa tangu awali kusimamia serikali yenu kuhakikisha mipango ya serikali ya muda mfupi, muda wa kati na mrefu inashabihiana na ahadi zenu na sera zenu mlizoahidi kwenye ilani ya 2020 . Ni wazi kwa tafsiri hii CCM na serikali yake mmeshindwa kazi ya kutatua changamoto za wananchi.Mwaka mmoja na nusu sasa kuelekea 2025 mmeshindwa kutekeleza ahadi yenu katika ilani yenu ya Upangaji, Upimaji na urasimishaji wa ardhi nchini (Ilani ya CCM kurasa 116. ).
ACT wazalendo katika ilani yetu 2020 kurasa wa 37, tulisema tutafuta gharama za Upimaji wa viwanja na Ardhi nchi nzima sababu tunaamini kupanga miji ni wajibu wa serikali sio Wananchi. CCM mmeshindwa kuipima nchi hii sababu sio kipaumbele kwenu ,mnawezaje kujipa kazi ya kukata matawi sasa badala ya shina ?.
Bwana Muenezi wa matamko,sasa mmemgeuza Waziri wa Ardhi kuwa mtatua migogoro ya ardhi hadi ngazi ya vijijini. Mmeshindwa kutekeleza Mikakati imara na ya muda mrefu kama tulivyoahidi ACT Wazalendo kwenye ilani yetu kurasa wa 37,kujengea uwezo stahiki Halmshauri za vijiji ,Kamati za Ardhi za vijiji,mabaraza ya ardhi ya vijiji katika usuluhishi (Mediation) na utatuzi wa migogoro ya ardhi huko huko chini, na pia kuwezesha rasilimali fedha mabaraza ya Wilaya na Mahakama ya ardhi katika kushughulikia migogoro ya ardhi. Badala yake mmegeuza wizara kuwa wasuluhishi wa Migogoro ya ardhi nchini badala ya kuweka mifumo imara nchini.
Bwana muenezi wa matamko,umempa miezi 6 Waziri Mkuu Majaliwa aratibu wizara 3, Wizara ya Tamisemi,Wizara ya Ardhi na Wizara ya Maliasili kushughulikia migogoro ya ardhi nchini. Bwana Muenezi wa matamko nikupe taarifa kutoka kwa Mtoa taarifa ya kwamba Serikali ya CCM 2019 iliagiza mawaziri 5 kwenda Kigoma -Kasulu kushughulikia mgogoro wa Ardhi Msitu wa Makere Kusini(Kagerankanda) walikwenda na hakuna mgogoro uliotatuliwa hadi sasa mgogoro bado upo.
Pia tar 16,Feb 2019 serikali ya CCM iligiza mawaziri 8 kwenda Mbarali-Mbeya kutatua mgogoro wa Ardhi wa GN.28 ya 2008 ila walienda zidisha mgogoro , hadi sasa mgogoro upo na umezidi mara dufu. Bwana Muenezi mlishindwa kutatua migogoro hii miwili ya ardhi Kigoma (Makere) na Mbarali (GN 28) ,mtaweza kutatua migogoro ya ardhi nchi nzima kwa miezi 6 uliyotoa Bwana Muenezi Mtoa Matamko ?.
Ahsante.
Abdul Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa.