Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,050
- 144,458
Kwa mtazamo wangu,inawezekana kabisa baadhi ya wale waliounga mkono juhudi na kisha kupewa vyeo,baadhi yao walipandikizwa huku wakiwa wamepewa kazi maalumu na moja ya kazi wanayofanya ni hayo yanayoendelea huko twitter ambapo tunaona nyaraka zinavujishwa kila kukicha.
Pia,inawezekana wako waliounga mkono juhudi kutafuta maisha tu lakini katika nafsi zao hawako kabisa upande wa wenye mamlaka na sehemu ya hao huenda ndio wanatumia vitengo walivyokabidhiwa kuvujisha nyaraka hizi tunazozisoma huko twitter kila kukicha.
Vile vile inawezeka mababeru nao wanavujisha baadhi ya document zilizopaswa kuwa siri na kama ni hivyo,basi hata mabeberu nao watakuwa hawako upande wao na kwa maana hiyo watakuwa wanapigwa humu nchini na pia wanapigwa kutoka nje ya nchi na kwa hali hii sijui kama watasalimika.
Kuhusu wahamaiaji waliopewa vyeo na mamlaka,tutambue watu hawa bado wana vina-saba na huko walikotoka ambapo ndugu na jamaa zao wanateswa na wengine kudhalilishwa, hivyo kibinadamu, ni rahisi kutumika kulipa kisasi kwa kufanya hujuma kwa kutumia vitengo au idara walizokabidhiwa.
Huko twitter kwa yule jamaa hivi sasa ni bandika,bandua mpaka unajiuliza huyu mtu ni mtu mmoja au ni taasisi kwa maana ya kikundi cha watu chenye malengo fulani?
Hivyo,inawezekana Baba Mwenye Nyumba ameanza kuvuna alichopanda kwa takribani miaka mitano sasa na bila shaka mavuno yakachanganya sana msimu huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Wacha tusubiri.