Binadamu walio acha athari kubwa ulimwenguni: dunia ikawa yao, kisha wao wakawa dunia mpaka leo

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
BINADAMU WALIO ACHA ATHARI KUBWA ULIMWENGUNI: DUNIA IKAWA YAO, KISHA WAO WAKAWA DUNIA MPAKA LEO.

Na. Comred Mbwana Allyamtu. (CMCA)
Saturday-03/12/2022
Marangu Kilimanjaro Tanzania

Hii list hapa chini ni ya viongozi ambao wameacha "Athari" Ulimwenguni, athari yao imebaki kama chachu hapa duniani.

Napo sema athari namanisha kuwa kupitia wao kuna jambo kubwa limezaliwa, wamebadilisha mtazamo wa dunia na wameanzisha Nadharia inayofuatwa mapaka sasa.

Wameacha alama ambayo inawafuasi wengi katika mitazamo, itikadi, falsafa, imani na msimamo kadhaa hapa ulimwenguni.

Lakini pia athari yao imepelekea wakumbukwe daima katika mataifa yao, mabara yao na duniani kwa ujumla.

George Washington...

Huyu alikuwa rais wa kwanza wa Marekani na ndiye aliyeongoza nchi hiyo kupata Uhuru kutoka kwa Waingereza mnamo mwaka 1776.

Washington ndie aliyetengeneza Marekani kuwa Taifa bora la kisiasa katika ulimwenguni wa demokrasia (United states is both a nation and an Idea).

Iko hivi...

July 4 1776 George Washington aliyaongoza makoloni 13 yaliyokuwa chini ya utawala wa ufalme wa Uingereza kujitangazia uhuru wake na baadaye kutengeneza serikali ya shirikisho iliyodumu kwa zaidi ya miaka 230 bila ya kuruhusu kiongozi wake yeyote kuweza kujitwalia mamlaka na kuwa dikteta.

Huu utaratibu wa kuifanya Marekani kuwa nchi ambayo kiongozi yoyote hawezi kujitwalia madaraka kiholela na kuwa dikteta umetengenezwa na Gorge Adam Washington, Washington ndiye aliyeifanya Marekani kuwa wazo la demokrasia ulimwenguni.

Haya tuendelee sasa, Marekani ilijitangazia uhuru wake hapo Philadelphia, Pennsylvania, mwezi July 4, 1776, Uhuru huu ulitokana na vita vya makoloni kumi na tatu ambavyo vilikuwa dhidi ya Ufalme wa Uingereza.

Draft ya uhuru ilipitishwa bila kupingwa mnamo Julai 2 (siku mbili kabla) ambapo nyaraka ya uhuru iliandaliwa na kamati ya watu watano wakiongozwa na John Adams ambaye alimpa assignment Thomas Jefferson ambaye aliandaa hatimaye ukapelekwa Bungeni na kufanyiwa marekebisho muhimu kisha ukapitishwa.

Hatimae 1789 Marekani ikawa Jamuhuri, kongamano la wachaguzi likapendekeza jina la Gorge Adam Washington kuwa raisi wa kwanza, alipitishwa na wajumbe bila kupingwa.

Uhuru wa Marekani umezaa wazo bora la "liberty and democracy" duniani ambao umekuwa msingi kazi wa demokrasia ulimwenguni kote, Mataifa yote duniani leo hujipima demokrasia kwa kuitazama Marekani.

Lakini pia Kanuni ya "liberty and democracy" ndio kanuni ya kupima ubora wa demokrasia na uhuru wa umma juu ya utawala bora, utaratibu huu ulianzishwa na Gorge Adam Washington na dunia nzima sasa hutumia Kanuni hii katika kutafuta ulimwenguni wa demokrasia "World of democracy"

Hii liberty and democracy yani "uhuru na demokrasia" imefanya Marekani kuwa Baba wa demokrasia ya aina yake ambayo leo imetengeneza kile kinachoitwa "Democracy regime systems" inayotawala dunia huku ikiacha athari ya ustaarabu mpya wa kila nchi kujitawala na kujiamulia mambo yake kwa uhuru.

Abraham Lincoln...

Huyu alikuwa raisi wa 16 wa Marekani, yeye ndie msingi wa upigwaji marufuku utumwa na biashara ya utumwa nchini Marekani, ikumbukwe kuwa miaka ya 1800 Marekani ndio ilikuwa soko kuu la utumwa duniani, hii ilitokana na kuwa kipindi hicho Marekani ndio ilikuwa eneo kubwa la uzalishaji duniani, 47% ya uzalishaji wote duniani ulikuwa Marekani.

Hii inamaana kuwa mali ghafi nyingi ilipatikana huko, migodi mingi ilikuwa huko viwanda vingi vilikuwa huko, hivyo nguvu kazi kubwa iliitajika ili kuhimili uzalishaji.

Abraham Lincoln akakatisha hili, ni sawa na kusema leo atokee kiongozi kuzuia ununuzi wa mafuta huko uarabuni ili kuzuia uchafuzi wa mazingira.

Ok iko hivi...

Abaraham Lincoln, kupitia hotuba yake ya Gettysburg (Gettysburg Address) ambayo hadi leo ni moja ya hotuba nzuri kabisa katika historia ya Taifa la Marekani, iliyopaza sauti juu ya masuala ya Usawa (principles of Human equality), hotuba hiyo ilifungua mabadiriko makubwa ya usawa Marekani ambayo baadae mabadiriko hayo yalisambaa duniani kote.

Hotuba hiyo ilipeleka kutolewa kwa tangazo la Ukombozi (Emancipation Declaration) mnamo tarehe 1 Januari 1863, tamko ambalo lilipelekea Bunge la Seneti kuifanyia mabadiliko (marekebisho) ya 13, Katiba ya Marekani, kuharamisha na kuzuia (abolished) mambo ya utumwa na biashara ya utumwa katika Taifa hilo.

Kwasababu Marekani ndio ilikuwa soko kubwa la utumwa duniani, kufa kwa biashara ya utumwa duniani (world slave trade) kukapelekea biashara ya utumwa kudorora, kukosa mashiko na hatimae kufa kabisa ulimwenguni.

Kwaiyo "Principles of Human equality" iliyo anzishwa na Abraham Lincoln ikamaliza biashara ya utumwa duniani ambayo ilikuwa na Zaidi ya miaka 2000, yani ndio kusema kuwa Lincoln ndio mwasisi wa uhuru wa mwanadamu dhidi ya kutumikishwa na mwanadamu mwingine.

Bila Lincoln utumwa ungekuwepo mpaka sasa, ikumbukwe kuwa utumwa ni moja ya njia kuu ya uchumi duniani iliyodumu kwa zaidi ya miaka 3000, tiba ya utumwa ilipatiwa na dawa na Lincoln.

"Principles of Human equality" ndio iliyokuja kuboresha demokrasia yenye ubora iliyokuwepo, demokrasia iliyokuwepo awali ilikuwa na mgawanyo wa majority na minority, yani vizazi bora na vizazi duni, Lincoln akaja na mbinu linganifu ya demokrasia, inayoitwa "Democracy is the government of the people, by the people, for the people."

Toka hapo, demokrasia iliyo asisiwa Ugiriki ikaboreshwa na kubeba dhana ya "Lincoln democracy thought" ambayo ilitaka wote bila kujali tabaka anatakiwa kuwa na haki sawa katika sauti ya maamuzi, kwakua "Vox pupul vox Deus" (Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu).

Kwaiyo haki sawa ndani ya wanadamu msingi wake ni Abraham Lincoln, leo ulimwenguni wote wanaufuata utaratibu huu katika tawala zote, na Binadamu hupambana kutafuta msingi huu ulimwenguni.

Otto Von Edward Bismarck...

Huyu ndiye msingi wa Ujerumani tuijuayo Leo, Ndiye kiongozi aliyeiuanganisha Germany mwaka 1870's, kabla ya mwaka 1871 hakukuwa na taifa moja liloitwa Ujerumani, kulikuwa na makabila ya kijerumani yaliyokuwa na nguvu na migogoro kila kukicha.

Kila walipojaribu kuunganisha makabila yao kuwa taifa moja ilishindikana, swali la kuungana lilikuwa gumu kupata jibu lake, Falme ya Austria ilipendekeza iundwe ‘'Greater Germany’' (Großdeutsche Lösung) ambapo Jamii zote zinazozungumza kijerumani ziunganishwe pamoja chini ya Austria, ‘'Ujerumani Kubwa'’ hii ingejumuisha majimbo yote ya Falme ya Austria yaliyokaliwa na Wajerumani na hata yale yenye watu wengine kama waSlovak, waUkraine, waItalia, waCzech n.k Wazo hili liliungwa mkono na Wakatoliki wengi, lakini lilishindikana.

Wazo hili lilipingwa na Falme ya Prussia, ambayo ilipendekeza iundwe ‘'Little Germany’' (Leindeutsche Lösung) ama '‘Ujerumani ndogo'’ ambapo yangeunganishwa maeneo ya kaskazini tu huku Austria na majimbo yote ambayo hayakaliwi na Wajerumani yakiachwa nje.

Walitaka Ujerumani ‘'pure’' ya Wajerumani tu, na hoja hii iliungwa mkono na wajerumani waProtenstant.

Juhudi zilifanywa kuiunda Ujerumani moja, moja ya juhudi hizo ni Wanasiasa toka jamii mbalimbali za Wajerumani walikuja pamoja na kukubaliana kuunda Bunge kulijadili suala hili kwa mapana, katika makubaliano waliona yafaa kuunda ‘'Ujerumani ndogo'’ ambayo itahusisha jamii za Wajerumani wote ukiacha wale walio chini ya Falme ya Austria.

Mpango huu ulikamilika na wanasiasa hao walimteua Mfalme Frederick William IV wa Falme ya Prussia kuwa kiongozi wao, lakini alikataa.

Alikataa sababu ya kujua ukweli kuwa Falme ya Prussia haikuwa na uwezo kijeshi kutawala maeneo yote yale na haikuwa na uwezo kupambana na Falme ya Austria ambayo ilipambana kwa hali na mali kuona wazo la kuunda ‘'Ujerumani ndogo'’ katu haifanikiwi,

Kupitia sakata hili, Otto von Bismarck alitumia fursa kujipatia imani ya Mfalme Frederick ambaye binafsi yake hakutaka vita na Austria.

Bismarck alifahamika Kuwa miongoni mwa watu waliotaka kuona Prussia inawachapa Austria vitani, lakini siku moja alisimama Bungeni na kupinga vikali hoja za waliotaka vita dhidi ya Austria, Mfalme alimpenda akampandisha cheo.

Otto von Bismarck, kama mwanasiasa nguli alivuta muda na kukuza jeshi la Prussia mpaka kuwa lenye nguvu, hapo akatafuta chokochoko na Falme ya Austria, Mwaka 1866 Jeshi la Falme ya Prussia liliingia vitani dhidi ya lile la Falme ya Austria ambapo jeshi la Prussia lilishinda na kuitia aibu Austria.

Baadae ilatokea vita dhidi ya Ufaransa, Prussia wakashinda kirahisi, Ushindi wao huo ulizithibitishia falme nyingine za Ujerumani kuwa inawezekana na watakuwa salama chini ya Prussia.

Prussia ikafanikiwa kuziunganisha jamii za Wajerumani na kuunda '‘Ujerumani ndogo’' (leindeutsche Lösung).

Hivyo ikapelekea kuwepo kwa taifa la Ujerumani leo hii, Ujerumani ambayo ndio Taifa kubwa Ulaya, taifa lenye ushawishi ulimwenguni kwa kila kitu, nchi ya nne kwa uchumi mkubwa duniani.

Sasa kwanini nasema Otto von Bismarck kaacha athari ulimwenguni?

Ok ni hivi....

Otto Von Bismarck ndie mwasisi na Kiongoz shupavu aliejenga Dola-Kuu ambayo baadae lilitamalaki balani ulaya na kutawala Dola nyingine nyingi balani ulaya.

Kiongozi huyo ndio anayetajwa kama kiongozi aliyoionganisha taifa la Ujerumani tunaloliona likiishi leo, ambalo ndio Taifa kubwa Ulaya kiuchumi, ndio taifa linalo ogopeka zaidi Ulaya.

Misingi ya Otto Von Bismarck ndio imeifanya Ujerumani kuwa (Dola-himaya Na Miliki Kuu Ya Sita Ya Dunia) "Popular-super power" (The 6th World Super-supremacy Empire) Katika Ulimwengu Wa Kibeberu Na Kifashisti 1800s - 1945 (World Of Imperialism And Fascism "The policy of extend power in World of Captalism").

Katika historia ya dunia ni mataifa 10 pekee yaliyo pata hadhi ya kuwa Dola-himaya Na Miliki Kuu Ya Dunia yani "Popular-super power" (The World Super-supremacy Empire), Ujerumani ilishika nafasi ya sita(6), Marekani ndio inashika nafasi hii kwa sasa ambayo ni taifa la 10 toka ulimwengu wa mataifa viranja ulipo anza.

Msigi wa kuifikisha hapo Ujerumani na kupata heshima hii ni alama ya Otto von Bismarck.

Hii ndio sababu nchi nyingi za Ulaya hadi sasa hazimkubali sana Mjerumani kwa sababu zinamuogopa, Kwa kifupi Ujerumani hajawahi kupendwa na watu waoga, kwasababu Ujerumani ni mbabe, jeuri, mbishi, asiyeshindwa kirahisi, mpambanaji, mkorofi lakini mzalendo. Yupo tayari kufanya lolote kwa ajili ya taifa lake, yani patriotism.

Mwasisi wa dhana ya "Nationality and patriotism" ni Otto von Bismarck, yeye ndio tafsiri halisi na sahihi ya utaifa na uzalendo.

Duniani kote mpaka sasa utumia dhana ya "Nationality and patriotism" katika kuonesha uzalendo na kuilinda nchi.

Mao Tse Tung...

Huyu ndie raisi wa kwanza wa jamuhuri ya watu wa China (people's republic of China), wao humuita mwenyekiti, wengine wamemfanya kuwa Mungu wa dini ya Mao.

Huyu diye kiongozi aliyeacha alama isiyofutika mpaka sasa kwa kuanzisha Ukomunisti wa kichina (Chinese characteristics of Communism) huu ni mfumo wa kijamaa unaofuata Mapinduzi ya asili ya Kichina, mfumo huu aliubolesha kutoka kwa ujamaa kutoka kwa Kar Max na Lenin.

Mao alianzisha Mfumo huu mwaka 1949, na kuanzisha nchi itakayofuata mfumo huo, mpaka sasa mfumo wake unaongoza watu billion 1.5 duniani, ndio mfumo pekee ambao umeweza kukabiliana na mfumo wa dunia wa ubepari na umesalia salama.

Vladimir Lenin...

Huyu jamaa ana maelezo marefu sana, ila ntaeleza kwa uchache, Huyu ndie mwasisi na mwaanzilishi wa mfumo wa Ujamaa katika Dola (Founder of the theory of Socialism) katika dhana ya ujamaa wa ulimwengu (Doctrine of World Socialism).

Ikumbukwe kuwa ulimwenguni umepitia mifumo mitano mpaka sasa katika njia kuu za uchumi ambazo ni World of Communalism, World of Slavery, World of Feudalism, World of Capitalism na World of Socialism.

Sasa hii World of Socialism kuitoa katika dhana ya makaratasi iliyoasisiwa na Karl Max na kuiweka katika matendo na kuigeuza kuwa mfumo wa utawala ni Vladimir Lenin.

Huyu Vladimir Lenin ndie aliyebadilisha nadharia ya Karl Marx ambae ndie mwasisi wa nadharia ya ujamaa na mwandishi wa kitabu maarufu cha wajamaa kinachoitwa "Das Kapital"(the Capital), Friedrich Engels mwananadharia wa ujamaa na mpinga ubepari na kisha kuufanya ujamaa kuwa mfumo katika siasa na dolo.

Vladimir Lenin ndio mwanadamu wa kwanza kuanzisha dola la kijamaa la Soviet Union, dola kubwa na tishio duniani (Soviet Union and world of socialism), nchi karibu 70 duniani zilifuata mfumo huo kutia ndani, Cuba, Yugoslavia, Poland, Ujerumani mshariki, China, Vietnam, Angola, Venezuela, Korea ya kaskazini na nyingine nyingi.

Mwanzilishi wa mfumo huu na wazo hilo ni Vladimir Lenin, ambae athari yake imeenea ulimwenguni pote mapaka sasa.

Mahatma Gandhi...

Huyu ni Baba wa uhuru wa India, huko India kapewa heshima ya kuwa Baba wa taifa la India.

Kwanini yupo kwenye kundi la viongozi walio acha athari duniani?

Ni Kwamba...

Mahatma Gandhi au Mohandas Karamchand Gandhi, ndiye kiongozi aliye anzisha nadharia ya "Non violence".

Nadharia hii ni njia ya kutafuta maridhiano, amani au haki pasina kumwaga damu, Gandhi alitumia njia hii katika mapambano yake ya kuitafutia uhuru Taifa la India dhidi ya Mkoloni Mwingereza mnamo mwaka 1947.

Staili yake, Ghandi ya kutotumia njia za vita na fujo, hasa hasa kwa kutumia migomo isiyohusisha machafuko, iliweza kuwa chachu ya kuibuka kwa wapigania uhuru na haki wa mkondo kama huo wa Ghandi, sehemu mbalimbali duniani.

Hadi leo mfumo huo huitwa "Non violence mechanism au Gandhi peace thought" imekuwa sehemu ya mitaala mingi ulimwenguni, nchi kadhaa ikiwemo Tanganyika, Ghana, Malawi Ireland na nyingine nyingi zilitumia njia hizo kujipatia uhuru.

Ghandi anapewa heshima kubwa sana duniani kiasi kwamba tarehe yake ya kuzaliwa kila mwaka ya tarehe 2 Oktoba huadhimishwa kama ni siku ya Kimataifa ya kusherehekewa siku ya Kimataifa ya Amani (International Day of Non violence).

Mtume Muhammad (PBH)...

Muhammad, alizaliwa mwaka 570 BK, katika Mji wa Makka ulioko katika Peninsula ya Kiarabu.

Alizaliwa katika ukoo ujulikanao kama Banu Hashimu, tawi la ukoo ulioheshimika sana na maarufu kutoka kabila la Wakureshi (Quraysh).

Baba yake Muhammad, Abd al-Muttalib, alifariki dunia na kumuacha mke wake aliyeitwa Amina binti Wahb akiwa na ujauzito (mimba ya Muhammad), Mzee Abd al-Muttalib alifia karibu na Madina akiwa safarini kibiashara kutokea katika nchi ya Palestina na Al-sham (leo ikiitwa Siria).

Inahadithiwa kwamba hata mama yake Muhammad alikuja kuaga dunia wakati Muhammad akiwa na umri wa miaka sita na hivi kutoa nafasi kwa Muhammad kulelewa na Baba yake mdogo, Baadaye Muhammad katika makuzi yake Muhammad alifanikiwa kuwa mfanya biashara jambo lililotoa nafasi kwake kuwa na heshima na sauti katika jamii yake ya Kikureshi.

Wakati ambao Muhammad alikuwa “amenawiri” kibiashara na kihadhi ni wakati ambao pia jamii yake ilikuwa katika matatizo na migogoro mikubwa ya hali ya njaa kali tokana na miundombinu ya chakula kuharibiwa na vita, watu kukosa kazi za kuwawezesha kumudu mahitaji ya kila siku, hali ya vuruguvurugu, hali ya kubaguana (hususani wanawake), mapigano baina ya makabila na uongozi mbaya wa viongozi wa kikabila, mmomonyoko wa maadili wa hata watu wake, hasa toka kabila lake.

Mambo yote haya, inasemekana yalimfanya Muhammad awe anahitaji kukaa peke yake kutafakari, Basi, ni katika mkondo huo, inasemekana alijikuta akiwa amejenga utamaduni wa kuhudhuria kwenye pango la Hira, lililoko Jabal an-Nour, karibu na Makka, umbali wa maili tatu hivi kusini mwa Makka ili kuwa anafanya taamali(meditation), Kufanya taamali ilikuwa ni desturi ya watu wa jamii ya Muhammad.

Ni kutokana na mazoea hayo ya kuwa anaenda huko pangoni, inasemekana siku moja usiku akiwa hapo pangoni, nyota zikiwaka kwa namna ambayo miale yake ilikuwa inapenya macho yake na anga zikiwa linawaka utafikiria ni mchana,mara alimuona Malaika Gabrieli mbele yake na kisha Malaika kumuamrisha hivi: “Soma”.Naye akamjibu malaika, “Sijui kusoma”.

Malaika akiisha kujibiwa hivyo na Muhammad, akamshika na kumkaba kwa nguvu. Inasemekana Malaika alifanya hivyo mara mbili na kisha akamuamuru Muhammad kukariri tena au kurudia maneno (aya) yafuatayo baada ya kuwa yametamkwa na malaika:

“Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba; amemuumba binadamu kwa tone la damu. Soma! Na Mola wako Mlezi ni mkarimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui.” (surat Iqra)

Baada ya majaribio manne yote ya kumtaka Muhammad kukariri ujumbe ambao malaika Gabrieli alikuwa ametoka nao kwa Mungu, inasemekena kwamba malaika aliondoka, na kumuacha Muhammad akiwa katika hali ya mfadhaiko na hivi akaamua kuondoka kurudi nyumbani kwake ambapo alipofika huko alimusimulia mke wake Khadija yaliyomkuta huko pangoni.

Mkewe Muhammad, Mama Khadija baada ya kuwa amepewa mkanda mzima wa mkasa huo huko pangoni, akampa moyo Muhammad na akamshauri wakamuone binamu yake aliyeitwa Waraqah bin Nawafal (ambaye alikuwa ni mtawa/kasisi wa Wa-nestorian) ili kupata mausia yake juu ya jambo hilo.Wanestorian walikuwa ni kundi (wazushi) ambao walikuwa wametengwa na Kanisa Katoliki kutokana na kiongozi wao aliyeitwa Mar Nestorius kutengwa na Kanisa kufuatia Mtaguso wa Efeso(Ephesius) uliofanyika mwaka 431BK.

Nestorius, alikuwa ni Mtawa na Askofu wa Constantinople(leo ikiitwa Instabul), Nestorius alitengwa kutokana na fundisho lake lililojulikana kama Theotokos (Mother of God), Kimsingi kupitia fundisho hilo, ni kwamba Nestorius hakuwa akiamini kwamba Yesu alikuwa Mungu kweli.

Kwa hiyo, kwa wadhifa ule bila shaka kasisi Waraqah alikuwa na ufahamu wa kiasi fulani juu ya maandiko ya kiyahudi na Kikristu na hivi Khadija na Muhammad walichukulia kwamba kwa nafasi yake angaliweza kueleza ni nini hasa hicho kilichokuwa kimemtokea Muhammad.

Kwa hiyo, baada ya kumuona Kasisi Waraqah, inasemekana, Waraqah alimthibitishia Muhammad kuwa hicho kilichokuwa kimemtokea pangoni ulikuwa ni unabii,

Kasisi Waraqah alienda mbali katika kisa cha kule pangoni ulikuwa ni ufunuo kutoka kwa Mungu. Nanukuu: “Oh,binamu! Unasema, uliona nini?”

Basi, Muhammad akarudia kumueleza kilichomtokea,Waraqah akiishakusikia hivyo akahitimisha kwa kumwambia Muhammad hivi:

“Huyo alikuwa ni Namus (akimaanisha Gabriel) ambaye Mungu alimtuma pia kwa Musa, Natamani ningalikuwa nina umri mdogo niishi muda mrefu nione jinsi ambavyo watu wangalikufurusha”. ( “I wish I could live up to the time when your people would turn you out.”), (Tafsiri ni yangu).

Basi, Muhammad, akishakusikia hivyo, akumuuliza Waraqah: “Ni kweli watu watanipinga?”(“Will they drive me out?”). (Tafsiri niyangu).Bila kusita, Waraqah akamwambia: ”Mtu yeyote aliyepata kuja mbele ya jamii na jambo kama hili lako, aliashia kuwa adui mkubwa; na laiti kama ningalikuwa na siku nyingi za kuishi hadi nyakati hizo basi, ningalipambana upande wako.

Muhammad alivyoridhishwa na Tafsiri ya Kasisi Waraqah na kuanza utume

Toka hapo mapaka sasa Muhammad amekuwa na wafuasi wapatao billion 2 duniani kote wanaofuata mafundisho yake ya uislam.

Uislam ndio dini ya pili yenye wafuasi wengi ulimwenguni kwa kuwa na waumin billion 2 nyuma ya ukristo wenye wafuasi billion 2.38.

Issa Bin Mariam (Yesu Christ)...

Huyu ISSA bin Mariam au Noel au Yesu ndio kupitia yeye ilianzishwa dini ya ukristo.

Wakati wa uhai wake hakuanzisha ukristo lakini wafuasi wake waliamzisha dini kwa jina lake.

Majina niliyoyatamka hapo juu yanafanana, Lugha ya Kiarabu inafanana na lugha ya Kiarau lugha hii ni lugha dada ya Kiarabu hivyo, zinafanana Issa hutamkwa na Waarabu na Isai hutamkwa na Bani Israil (wana wa Israil) ambao hutumia lugha ya Aramic.

Bwana Yesu alikuwa anaitwa Yehoshua lakini Wayunani walishindwa kuita Yehoshua wakaita Yesu, Kwa hiyo waliacha "Ho" na "shua" wakakata Yesu.

Yesu alizaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huko Bethlehemu ya Uyahudi, Maisha yake yalikuwa ya pekee kwa kuwa alifahamu vitu vingi kwa mfano, sheria hata kuwazidi walimu wa sheria japokuwa hakusomea sheria, Alifanya pia maajabu mengi ya kimiujiza, alikuwa na falsafa kubwa kuliko hata wanafalsafa wa kipindi hicho.

Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kuanzia ujio wake.

Waumini wake ndio wanaunda Kanisa la Kikristo ambalo linapatikana leo katika madhehebu mengi duniani, Karibu wote wanamwamini kuwa Mungu aliyechukua umbile la mwanadamu au, kwa lugha nyingine, kuwa Mwana wa Mungu.

Hapa duniani Yesu alizaliwa na Bikira Maria kama malaika alivyomuambia: “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo, hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu” (Lk 1:35).

Hata hivyo Wakristo wachache wanaamini kuwa yeye ni mtume wa pekee wa Mungu ila si Mungu.

Katika dini ya Uislamu, Yesu anajulikana kama Nabii Isa, Waislamu wanaamini kuwa yeye alikuwa nabii wa Mungu ila hakuwa mwana wa Mungu wala Mungu.

Hata hivyo ukristo umekuwa na wafuasi wengi ulimwenguni karibu watu billion 2.38 ni wafuasi wa imani ya ukristo.

Queen Elizabeth....

Huyu alikuwa ni malikia wa Uingereza, chini ya uongozi wake na utawala wake ndipo nchi nyingi zilizokuwa chini ya utawala wa Uingereza zilipewa Uhuru wao kwa amani bila mtutu, alikuwa mfuasi wa peaceful decolonization.

Alama ya kupenda Diplomacy and International Relations with peaceful decolonization imefanya athari yake iwe kubwa mpaka sasa, athari yake inayoishi sasa ni jumuaia ya madola (Commonwealth).

Commonwealth ni zalio la Diplomacy and International Relations with peaceful decolonization hii ndio athari ya Malikia Elizabeth ll ambae karibu watu milioni 750 wanaishi ndani yake.

Siddharta Gautama Buddha...

Huyu ndio muasisi wa dini ya Buddha, Buddha ni mfumo wa kidini uliotokana na mafundisho ya Siddharta Gautama.

Mafundisho ya Buddha yalianzishwa na Siddhartha Gautama aliyezaliwa mnamo mwaka 563 KK, alizaliwa huko Lumbini, (leo ni nchi ya Nepal) au huko Kapilavastu, Piprahwa, Uttar Pradesh, India au tena Kapileswara, Orissa, India, bado ni utata mahali halisi alipo zaliwa.

Anaitwa pia "Buddha wa kihistoria" au "Buddha Shakyamuni" kwa sababu katika imani yao kuna mabuddha mbalimbali.

Neno "Buddha" si jina bali ni cheo cha heshima chenye maana ya "aliyeamka", Humo mna kiini cha imani ya Ubuddha kuwa binadamu huishi kwa kawaida bila ya kutambua hali yake mwenyewe, lakini akielewa mafundisho anakuja kuamka na kuona hali yake pamoja na njia inayopaswa kufuatwa.

Katika haya yote Wabuddha hufuata mfano wa Buddha Shakyamuni wakitegemea kufika kwenye hali ya kuamka.

Kati ya Wabuddha kuna mielekeo mbalimbali kama madhehebu, madhehebu ya budha yenye wafuasi wengi ni pamoja na

1-Mahayana, hasa katika nchi kama China, Uthai, Burma, Kambodia.

2-Hinayana au Theravada
3-Vajrayana au Ubuddha wa Tibeti
4-Zen (ubudha wa nchini Japani)

Mpaka sasa dini ya Buddha ina waumini milioni 573 duniani kote, ndio dini ya Nne (4) kwa waumin wengi nyuma ya Hindu, Islam na ukristo.

Sanātana Dharma...

Hii ni nadharia iliyoanzishwa katika kuzaliwa dini ya Hindu, aijulikani hasa nani mwanzilishi wake, lakini inatajwa kuwa ndio nadharia ya kidini ya kale zaidi ulimwenguni.

Dini ya Uhindu, au Hindū Dharma, ni dini kubwa yenye asili katika Bara Hindi, sehemu kubwa ya wafuasi wake wapo India, ndio dini rasmi huko Nchini India, Ikiwa na wafuasi milioni 900 duniani kote, ni dini ya tatu baada ya Ukristo na Uislamu kwa wingi wa waumini.

Cerdic the Worf of Gewissae...

Huyu Cerdic ndio chimbuko la ufalme wa Uingereza, huyu ndio Babu wa ufalme na taifa la Uingereza, kwa kilatini huitwa Cerdicus.

Huyu anaelezwa kuwa ndio chimbuko la nasaba za uzao wa Anglo-Saxon, na ndio kiongozi wa mwanzo wa Anglo-Saxon (as a leader of the Anglo-Saxon settlement of Britain), pia ndio mwasisi wa nchi ya Uingereza na ndio mwanzilishi wa mwanzo wa ufalme wa Uingereza tunao uona sasa (the founder and first king of Saxon Wessex),

Utawala wake uliza kuanzia mwaka 519 hadi mwaka 534 AD, yeye ndio chimbuko la Uingereza na ufalme wa Uingereza yenyewe.

Athari yake ulimwenguni ni kwamba ufalme wa Uingereza ndio ufalme wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni kuliko falme zote.

Pharaoh Menes, Memphis, Mena....

Huyu ndio mfalme na Farao wa kwanza wa Egypt au Misri, huko zamani iliitwa Kemet.

Huyu Menes ndio mwasisi wa mafarao wote huko Misri ndio mtawala wa kwanza wa Egypt
(The first ruler of Kemet) inatajwa kuwa alikuweo mika ya 3000 iliyopita japo wengine husema utawala wake uliishi miaka ya 5660 BC.

Yote ya yote ameishi miaka 5000 au 7000 iliyopita, utawala wake ndio uliojenga Kemet kuwa Dola-himaya ya Pili Dunia, yani baada ya Mesopotamia dola ya pili ulimwenguni kumiliki dunia ni Kemet.

Yeye ndio mwanzilishi wa chimbuko la ustaarabu duniani, ustaarabu wote unaouona duniani asilimia 60 ni kutoka kwake.

Sargon of Akkad...

Huyu Sargon, au Sargon of Akkad, anatajwa kuishi Karne 23rd zilizopita kabla ya kristo, huyu ndie mwasisi wa dola ya Mesopotamia, dola ya kwanza kuanzishwa Duniani.

Yeye ndie mtu wa Kwanza kubuni kuwa na mfumo wa dola na serikali, yeye ndio mtu au mwanadamu wa kwanza kuunda dola (who was one of the earliest of the world’s great empire builders), aliijenga Mesopotamia kuanzia Syria, Anatolia na Elam (western Iran).

Yeye ndio aliyeanzisha wa nasaba ya kwanza ya Semitic dynasty ambayo inadhaniwa kuwa ndio nasaba anzilishi wa kikosi cha jeshi la Mesopotamia ambalo ndio jeshi la kwanza kuanzishwa Duniani (considered the founder of the Mesopotamian military tradition)

Kwaiyo madola yote na Jeshi zote duniani ni athari yake huyu mwamba.

Julius Caesar....

Katika historia ya dola 10 kubwa duniani zilizowahi kuitawala dunia yani "World Hegemony" (World Super-Supremacy power), huyu jemedari Gaius Julius Caesar, hushika namba moja kwa umaarufu na ushawishi duniani na pia namba 1 kwa viongozi waliowahi kuwa na nguvu ulimwenguni.

Caesar ni kutoka katika ukoo wa kikabaila (feudalism clan) wa babu yao aliyeitwa Sextus Julius Caesar ambaye ndie babu yake Julius Caesar, Gaius Julius Caesar ni mtoto wa Aurelia, na Kabaila Gaius Celius Caesar, moja ya familia maarufu Rome na senator wa Roman Senatus.

Gaius Julius Caesar katika maisha yake rasmi alikuwa na mtoto mmoja aliyeitwa Julia, mwingine ni Caesarion aliyezaa na Kleopatra japo huyu akutambulika sana.

Mtoto mwingine ni mpwa wake aliye muasili (adoptive) aliyeitwa Augustus, huyu Augustus ndio hufahamika kama "The Roman Principate" au pia hufahamika kama "Pax Romana".

Huyo Augustus ndio Oktaviano yani Augustus of Prima Porta, mtawala (emperor) wa kwanza wa Roma aliyetawazwa na kutawala kuanzia
16 January 27 BC mpaka tarehe 19 August AD 14.

Caesar ndio alama ya watawala wenye ushawishi na nguvu ulimwenguni, jina lake limeacha kumbukumbu kubwa duniani, utakapowataja Alexander the great, Menes, Charlemagne (Kololo Mkuu), Æthelstan the great, Louis the German, Cecrops, Rurik of Ladoga. Ghensi Khan, Jimmu, Qin Shi Huang the great, Sargon of Akkad, Cyrus the Great na Osman Ghazi, huwezi kuliacha jina la Caesar ambalo litachorwa kwa wino mwekundu.

Caesar alikuwa mtu na nusu, jemedari mkuu na mpambanaji asiosaulika duniani.

Gaius Julius Celius Sextus Caesar, mwasisi wa Dola-Himaya ya Rumi (Rome Empire), huyu Gaius Julius Caesar au Kaisari kwa wengi wanavyomjua alikuwa jemedari aliyeacha alama kubwa ulimwenguni mpaka sasa.

Kwanza kabisa yeye ndio Mwanadamu wa kwanza sura yake kuwekwa kwenye pesa, kabla ya hapo hakuna sura ya kiongozi yoyote yule aliyewahi kuwekwa kwenye sarafu ya pesa.

Pili, yeye ndio Mwanadamu wa kwanza kabisa baada ya kifo chake aligeuzwa kama mungu wa dola, baada ya yeye kufariki huko Rome Empire, walianza kumuabudu kama Mungu, Binadamu mwingine aliyepewa hadhi hiyo ni Mfalme wa kwanza wa Japan aliyeitwa Jimmu.

Tatu, Gaius Julius Caesar ndio Mwanadamu wa kwanza duniani jina lake kutumika kama cheo rasmi cha ukuu wa Dola, neno "Kaiser" lilitumika ulaya yote kurejelea cheo cha mfalme.

Nne, Gaius Julius Caesar ndio Mwanadamu wa tatu duniani kutembea umbali mrefu kwa faransi akiwa nyuma ya mfalme Timul (Ghensi Khan) na Simón Bolívar.

Tano, Caesar ndio Mwanadamu wa pili kupigana vita vingi duniani.

Pamoja na mengine mengi Gaius Julius Caesar aliacha alama kubwa kwenye historia ya ulimwengu ambayo inaishi na kutumiwa moaka Sasa.

Wengine walio acha alama duniani ni Pamoja na...

Mfalme wa kwanza wa Ufaransa, Charlemagne (Kololo Mkuu)...

Huyu ndiye aliye anzisha dola ya Ufaransa (Galia) na kamanda aliye eneza ukristo na kuulinda Ulaya, bila yeye ukristo ungefutika Ulaya, hivyo uhai wa ukristo Ulaya ni uwepo wake.

Mfalme wa kwanza wa makabila ya Ujerumani (Germanic tribes) Louis the German...

Huyu ndio babu wa Makabila yote yanayounda jamii ya Ujerumani yani Dutch, wote wanao zungumza kidachi chimbuko lao ni kwa huyo Babu yao.

Mfalme wa kwanza wa Ugiriki Cecrops pamoja na Alexander the Great...

Hawa ndio waasisi wa himaya ya Ugiriki iliyo zalisha elimu duniani, Ugiriki ndio chimbuko la Elimu ya kisasa na utawala wa sheria duniani.

Waanzilishi ni Mfalme Cecrops pamoja na Alexander the Great.

Mfalme wa kwanza wa Russia Rurik of Ladoga...

Huyu Rurik of Ladoga ndie babu wa Russia, Ukraine na Slav wote Ulaya, uhodari na ubabe wa warusi na waslav wote umetoka kwa huyu bwana.

Wengine walio acha alama duniani ni Pamoja na.....

Mfalme Ghensi Khan, mwasisi wa Dola ya Mongoli.

Mfalme Jimmu, mwasisi wa Japan.

Mfalme Qin Shi Huang the great, mwasisi wa China ya kale.

Mfalme Cyrus the Great, mwasisi wa Dola ya Umedi na Uajemi.

Mfalme Osman Ghazi Pamoja na Ertugrul Ghazi, waanzilishi wa Dola ya Ottoman.

Hawa ndio Binadamu ambao wameacha Athari Ulimwenguni, athari zao ndio maisha ya Dunia Mpaka sasa.

Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526 uungwe group la Maktaba Kuu kwa gharama ya Tsh 3000/=.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057.
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.
___________________________
View attachment 2434560
A14VAyvYsTL.jpg
View attachment 2434561View attachment 2434562View attachment 2434564View attachment 2434563View attachment 2434566View attachment 2434567View attachment 2434565
 
View attachment 2434560View attachment 2434568View attachment 2434561View attachment 2434562View attachment 2434564View attachment 2434563View attachment 2434566View attachment 2434567View attachment 2434565
Yesu siyo Issa.
 
Asante sana, nikuombe utupangie dola/ mataifa yaliyowahi kuwa mataifa makubwa na kuitawala Dunia. Nadhani mtiririko ni kama hivi:
1.Mesopotamia
2.Kemet
3.Uajemi (Kama sijakisea)
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.USA

Niombe ujaze hayo magepu.

Sent from my Infinix X693 using JamiiForums mobile app
 
Kemet empire, babylon empire, roman empire, persian empire, ottoman empire, mongolian empire, colonians empire based on Africa, then capitalism empire organized by western nations and ruled by USA then will fall downside to African empire, after the long circle of Satanism rulers
 
Umekosea kumlinganisha Yesu Mungu...na wanadamu.

Alikua hai, akazaliwa kama Mwanadam, Akafufua wafu , naye akafa ma siku ya Tatu akafufuka nayuko hai hata Leo akiwa ameketi mkono wakiume wa baba yake, akituombea dhambi zetu kusamehewa nakutupa nafasi ya kurithi uzima wa milele.

Acha kumuweka kwenye kundi la vitu vya kijinga
 
Kemet empire, babylon empire, roman empire, persian empire, ottoman empire, mongolian empire, colonians empire based on Africa, then capitalism empire organized by western nations and ruled by USA then will fall downside to African empire, after the long circle of Satanism rulers
Barikiwa sana

Sent from my Infinix X693 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom