Mtazamo: Waliounga mkono juhudi na kisha kuaminiwa na kupewa vitengo, huenda baadhi walitumwa na sasa ndio wanahusika na yanayoendeleea huko Twitter

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Kwa mtazamo wangu,inawezekana kabisa baadhi ya wale waliounga mkono juhudi na kisha kupewa vyeo,baadhi yao walipandikizwa huku wakiwa wamepewa kazi maalumu na moja ya kazi wanayofanya ni hayo yanayoendelea huko twitter ambapo tunaona nyaraka zinavujishwa kila kukicha.

Pia,inawezekana wako waliounga mkono juhudi kutafuta maisha tu lakini katika nafsi zao hawako kabisa upande wa wenye mamlaka na sehemu ya hao huenda ndio wanatumia vitengo walivyokabidhiwa kuvujisha nyaraka hizi tunazozisoma huko twitter kila kukicha.

Vile vile inawezeka mababeru nao wanavujisha baadhi ya document zilizopaswa kuwa siri na kama ni hivyo,basi hata mabeberu nao watakuwa hawako upande wao na kwa maana hiyo watakuwa wanapigwa humu nchini na pia wanapigwa kutoka nje ya nchi na kwa hali hii sijui kama watasalimika.

Kuhusu wahamaiaji waliopewa vyeo na mamlaka,tutambue watu hawa bado wana vina-saba na huko walikotoka ambapo ndugu na jamaa zao wanateswa na wengine kudhalilishwa, hivyo kibinadamu, ni rahisi kutumika kulipa kisasi kwa kufanya hujuma kwa kutumia vitengo au idara walizokabidhiwa.

Huko twitter kwa yule jamaa hivi sasa ni bandika,bandua mpaka unajiuliza huyu mtu ni mtu mmoja au ni taasisi kwa maana ya kikundi cha watu chenye malengo fulani?

Hivyo,inawezekana Baba Mwenye Nyumba ameanza kuvuna alichopanda kwa takribani miaka mitano sasa na bila shaka mavuno yakachanganya sana msimu huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Wacha tusubiri.
 
Kweli kabisa huwezi kuattach hizo docs za twitter ili hata tusiojua kinachoendelea tujue?
 
Kigogo🇰🇪 (@kigogo2014) · Twitter

👉Kuna wakati Dr Mpango unatia huruma sana yaani! 😂😂😂 👉Haya ndiyo madhara ya kuwa kwenye serikali isiyokuwa na mipango mnakimbia kimbia tu mpaka WB wana suspend kuwapa hela 👉Halafu muwe mnawaambia matarumbeta yenu hii hela ya Ubungo interchange ni mkopo wa WB @TZMsemajiMkuu

Twitter · saa 1 iliyopita

👉Doto na Mpango WB walisimamisha kuwapa hela maana kazi ilikuwa haiendi hela mnafanyia mambo mengine! Sasa next time maichezee hela za watu 👉MATAGA-niliwaambia sitaki kujibizana na nyie maana hamjui kitu. Si mlisema hela ni ya Ndani haya someni barua hii huku mtajua mwenye mbwa

Twitter · saa 2 zilizopita

👉Waziri Mpango unasuasua sana kuamia haya mambo! Hii NICOL ni majangiri watupu wamejaa humu! 👉Why are you not acting? Hivi nyie watu mbona wavivu sana kufanya kazi kwa speed? Mmekula maharage ya wapi nyie?

1591518129230.jpeg


1591518129629.jpeg


1591518129427.jpeg


1591518129833.jpeg


1591518130043.jpeg
 
Back
Top Bottom