Mtanzania Charles Mihayo jela maisha

Mtanzania Charles Mihayo jela maisha

Sio mzima huyu haiwezekani mtu mwenye akili timam akafanya kituko kama hiki . Nasita kusema kua ni ukatili wa hali ya juu kwani nahisi jamaa mgonjwa . Masikini mama yao sijui anajutaje kuwapeleka watoto kwa baba yao aaah haya mambo uyasome tu mitandaoini usiwe victim.

Lazima atakuwa na hitilafu kichwani ingawa hilo kwangu si udhuru wa yeye kutokuadhibiwa vikali.

Mtu mwenye akili timamu ni vigumu sana kufanya hivyo.
 
Siku zote akili za usiku huleta majuto tu. Afungwe tu, tumechoka.
Ova
 
Lazima atakuwa na hitilafu kichwani ingawa hilo kwangu si udhuru wa yeye kuadhibiwa vikali.

Mtu mwenye akili timamu ni vigumu sana kufanya hivyo.
Kweli si mzima kabisa haiwezekani kufanya unyama kiasi hicho hata kama ana bifu na mama watoto . Masikini vitoto vimekatiliwa uhai kikatili mno hii itasababisha watu waanze kua na mashaka na wataliki wao. Inauma mpaka unatamani kurudisha nyuma siku ili isiwe kweli watoto wabaki hai. Hivi mtu kama huyo haiwezekani akarudishwa hapa bongo ili afungwe jela za huku naona hastahili hata kuvuta hewa ya huko aliko aletwe jela zetu za bongo.
 
Hebu jamani tujaribu kuangalia upande mwengine wa sarafu hapa,huyu jamaa kunauwezekano kachizika na sabau ni hizi sheria zao za kupendelea upande mmoja kati ya wana ndoa wawili.Huenda mahakamani walimnyang'anya mke na kuchukua au kumpa custody rights zote za ulezi mwanamke peke yake,wakati mwingine huwa zinaweza zikawa very brutal na harsh na kama kichwa chako hakiko sawa utaishia kuwa criminal kama Mr Mihayo.
Hawa wazungu tuwaangaliye hivi hivi,cha kwanza wanachokipenda kutoka kwetu sisi weusi ni sehemu ya kustareheshwa na ikitokea kapata mimba hiyo inakuwa sio mbaya na atazaa na pindi akishazaa starehe na yeye huwa inapunguwa na kawaida yao hutafuta mtu mpya na akiisha mpata visa vinaanza mpaka utaachia manyanga wewe mwenyewe hata kabla ya mahakama kuingilia kati.Mimi namuona Mr Mihayo kama yeye ni victim hapa katenda tendo bila kujijua na kuujua ubaya wake na sasa anajionea mwenyewe na ninauhakika ameisha tia akili kichwani mwake hivi sasa.Yaani mwanaume mzima utawezaje kuua damu yako mwenyewe?huyu jamaa katudhalilisha sisi wabongo wote na watu wote wa Africa mashariki kwa ujumla,matusi makubwa sana hayo.M/Mpamba.
 
Ndio mimi ninawaogopa kuwaowa Wazungu kwa hayo matatizo hakawi kukuambia hakutaki unaweza kuchukuwa hautuwa mbaya zaidi ya huyu Shetani wa kibongo kuwauwa watoto wake Mkuu nyumba kubwa Mapenzi ya kizungu Sisi Watu weuesi hatuyawezi kabisa.

I totally disagree with you! Unaweza kuoa mwanamke kutoka nyumbani na akakukataa au akawa na tabia mbovu mno, Nina rafiki zangu 3 wameoa wazungu na maisha yanawaendea vizuri sana, Na wanawake wapo tayari hata kuishi bongo, it's all about choices & luck tuache stereotypes.
 
Last edited by a moderator:
Ndio mimi ninawaogopa kuwaowa Wazungu kwa hayo matatizo hakawi kukuambia hakutaki unaweza kuchukuwa hautuwa mbaya zaidi ya huyu Shetani wa kibongo kuwauwa watoto wake Mkuu nyumba kubwa Mapenzi ya kizungu Sisi Watu weuesi hatuyawezi kabisa.

Umeona eeehhh...
Inaelekea jamaa kadata sababu kaachwa siyo kuachana...kitu ambacho ni ngumu kutokea kibongo bongo...eti mkeo akwambie sikutaki...Refer kwa Frola Mbasha ...jamii haimuelewi binti mdogo anasema anataka talaka...maswali yanakuwa mengi na aaminiki hata atoe sababu gani...hili linafanya wanawake wengi wa stick na ndoa zao...sababu hawawezi kueleweka eti aseme sijisikii tena kuwa na mume wangu...na mimi naona inasaidia kwani with time wanandoa wana solve differences zao kuliko ukitukanwa kidogo unakimbilia mahakamani...

Sasa amezoea mfumo wetu kaona haiwezekani...

Nimekumbuka yule mwingine alojiua Russia sababu ya kuoa huko...bora yeye alijiua mwenyewe...huyu nae kama alikuwa na hasira angesaga tu vyupa awaache hao malaika...

Angekuwa nchi zinazonyonga angenyongwa...naona Australia hawana hiyo adhabu...
 
Dah!! Ugovi gani ikiwa mama anawapeleka watoto kwa baba yao? Sioni shida kama mama watoto wako anakutambua kama wewe ni baba wa watoto wake. Na watoto wakikua watajua kama wewe ndiyo baba yao. Ifike mida tukubali matokeo. Penzi halilazimishwi
 
Hebu jamani tujaribu kuangalia upande mwengine wa sarafu hapa,huyu jamaa kunauwezekano kachizika na sabau ni hizi sheria zao za kupendelea upande mmoja kati ya wana ndoa wawili.Huenda mahakamani walimnyang'anya mke na kuchukua au kumpa custody rights zote za ulezi mwanamke peke yake,wakati mwingine huwa zinaweza zikawa very brutal na harsh na kama kichwa chako hakiko sawa utaishia kuwa criminal kama Mr Mihayo.
Hawa wazungu tuwaangaliye hivi hivi,cha kwanza wanachokipenda kutoka kwetu sisi weusi ni sehemu ya kustareheshwa na ikitokea kapata mimba hiyo inakuwa sio mbaya na atazaa na pindi akishazaa starehe na yeye huwa inapunguwa na kawaida yao hutafuta mtu mpya na akiisha mpata visa vinaanza mpaka utaachia manyanga wewe mwenyewe hata kabla ya mahakama kuingilia kati.Mimi namuona Mr Mihayo kama yeye ni victim hapa katenda tendo bila kujijua na kuujua ubaya wake na sasa anajionea mwenyewe na ninauhakika ameisha tia akili kichwani mwake hivi sasa.Yaani mwanaume mzima utawezaje kuua damu yako mwenyewe?huyu jamaa katudhalilisha sisi wabongo wote na watu wote wa Africa mashariki kwa ujumla,matusi makubwa sana hayo.M/Mpamba.

Una hoja mkuu. Ndio maana Obama kawa Raia wa Marekani, akalelewa na baba wa kambo na baadaye bibi. Ila bado inabidi uwe na kichwa kibovu sana ili kuua watoto wako. Kwa kiasi fulani hii issue imefanya tuonekane ni watu wa ovyo sana kwa jamii.
Ova
 
Ni kweli wanawake wanaoolewa toka Tz na kupelekwa majuu wengi wana behave hovyo kuliko wazungu wenyewe...ni kama kumfungulia mbwa ...
Kinachofanya wafanye hivyo ni possibilities zinazotokana na sheria za huko za ku over protect wanawake... na ulimbukeni (wengi hata exposure hawana...wanameza kila wanachokiona mbele yao)

Nazijua kesi kadhaa za wabongo waliodatishwa na wabongo wenzao...ila wake zao kama wamesoma sana form four...na yenyewe ni shiiid...dada wa std 7 au form 4 akaishi Sweden sijui Denmark ...nchi ambayo mwanamke ni kila kitu unategemea nini??? Lazima utasongeshwa ugali aisee...na deki utapiga...zamu kwa zamu...

I totally disagree with you! Unaweza kuoa mwanamke kutoka nyumbani na akakukataa au akawa na tabia mbovu mno, Nina rafiki zangu 3 wameoa wazungu na maisha yanawaendea vizuri sana, Na wanawake wapo tayari hata kuishi bongo, it's all about choices & luck tuache stereotypes.
 
I totally disagree with you! Unaweza kuoa mwanamke kutoka nyumbani na akakukataa au akawa na tabia mbovu mno, Nina rafiki zangu 3 wameoa wazungu na maisha yanawaendea vizuri sana, Na wanawake wapo tayari hata kuishi bongo, it's all about choices & luck tuache stereotypes.

Right on!

Mambo ya stereotypes hayana nafasi katika dunia ya leo.

Nawajua couples kadhaa (waume Watanzania na wake Wamarekani wazungu, wazazi wa rafiki zangu) ambao wapo kwenye ndoa zaidi ya miaka 40 sasa na sijawahi kuwaona wala kusikia eti wamefanya mambo ya ajabu kisa wamekwaruzana tu na wenza wao.

Ukatili wa huyo jamaa usitumiwe kama chambo cha ku stereotype jamii nzima ya watu.

Hata Tanzania kuna ukatili wa ajabu sana hufanyika kati ya wanandoa kwa wanandoa na/ au wazazi kwa watoto lakini hiyo haina maana kwamba Watanzania wote au Waafrika wote ndo tuko hivyo.

Matatizo ya huyo jamaa na mkewe ni yao tu. Hayawakilishi matatizo ya jamii nzima.
 
Hebu jamani tujaribu kuangalia upande mwengine wa sarafu hapa,huyu jamaa kunauwezekano kachizika na sabau ni hizi sheria zao za kupendelea upande mmoja kati ya wana ndoa wawili.Huenda mahakamani walimnyang'anya mke na kuchukua au kumpa custody rights zote za ulezi mwanamke peke yake,wakati mwingine huwa zinaweza zikawa very brutal na harsh na kama kichwa chako hakiko sawa utaishia kuwa criminal kama Mr Mihayo.
Hawa wazungu tuwaangaliye hivi hivi,cha kwanza wanachokipenda kutoka kwetu sisi weusi ni sehemu ya kustareheshwa na ikitokea kapata mimba hiyo inakuwa sio mbaya na atazaa na pindi akishazaa starehe na yeye huwa inapunguwa na kawaida yao hutafuta mtu mpya na akiisha mpata visa vinaanza mpaka utaachia manyanga wewe mwenyewe hata kabla ya mahakama kuingilia kati.Mimi namuona Mr Mihayo kama yeye ni victim hapa katenda tendo bila kujijua na kuujua ubaya wake na sasa anajionea mwenyewe na ninauhakika ameisha tia akili kichwani mwake hivi sasa.Yaani mwanaume mzima utawezaje kuua damu yako mwenyewe?huyu jamaa katudhalilisha sisi wabongo wote na watu wote wa Africa mashariki kwa ujumla,matusi makubwa sana hayo.M/Mpamba.

Picha: Baba amfanyia ukatili mwanae! Kisa wivu wa mapenzi!!! Na hii ni huko Shinyanga, Tanzania na hakuna mzungu anayehusika.

DSC02925.JPG

Mkazi wa kitongoji cha Sango kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga Samson Bwire (54), ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa kumcharanga mapanga mtoto wake Devotha Gerald (4) kwa sababu za wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo limetokea leo jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana na mke wake Happiness (28) Elias huku akiwa amelewa pombe ambapo, mkewe alikimbia kitu kilichosababisha kumgeukia mtoto Devotha na kuanza kumkata mapanga kichwani.

Kwa mujibu wa majirani, kelele zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba walipoenda walimkuta Bwire akichoma nguo za mke wake, na alipowaona aliingia ndani na kuanza kumkata mapanga mtoto huyo huku akiwa amefunga mlango.

Imefafanuliwa kuwa, baada ya kusikia kelele za mtoto, majirani walianza kuvunja milango huku wakiomba msaada kituo cha Polisi na baada ya Polisi kufika walifanikiwa kumnusuru mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani.

Majirani kwa hasira walianza kumpiga Bwire ambaye ni askari polisi mstaafu wa cheo cha koplo kwa nia ya kumwua, hali ambayo imelipa jeshi la Polisi kazi ya ziada kumnusuru na kumpakia kwenye gari kwenda kituoni.

Hata hivyo Wakati gari la Poisi likiwa katika mwendo wa kasi eneo la soko la Mkulima, Bwire ameruka kutoka kwenye gari na kuangukia kwenye Lami kitendo kilichomsababishia majeraha makubwa sehemu za usoni.

Mtoto Devotha na baba yake Bwire wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu huku Bwire akiwa Chini ya Ulinzi mkali wa polisi.

Chanzo
 
Aisee ,ndugu Msarendo nini Segerea mambo yenyewe ni Keko huko watu wanalilia tigo ka ya kwao.Huyo Mihayo katutia aibu sana wabongo ingefaa serikali ya Tanzania imuombe akubali kurejeshwa huku na apalekwe lupango ya Keko kwanza kama mahabusu.
 
Kuliko watoto walelewe na Step father bora hicho alichofanya
 
Duh Nimesoma huku natetemeka kwa kuogopa, nimuue mwanangu Namkunda? Mungu niepushie mbali hilo pepo. Hata kama ni pombe, bangi au hasira zisinifikishe huku.

Urewedi wetu..
 
Huko hawana death penalty?!, that's what he deserves
 
Back
Top Bottom