Uchaguzi 2020 Mtanzania amka: Wasanii kazi yao ni usanii, Kampeni za Uchaguzi Mkuu si usanii, hatuhitaji maigizo wala kukatiwa mauno!

Chama cha wahuni hicho na waongo hawajui wanataka nini Mkuu.



Msikilizeni huyu kijana.

Baadhi ya wasanii walikuwa wakifanya mambo machafu.

Mambo yasiyoendana na maadili ya Watanzania.

CCM iwe makini katika kuchagua wasanii wa kufanya kampeni.

 
tafuteni kura sio kasoro chama kipi malaika nipisheni mie
Halafu nyie CCM mnajifanya kukemea mambo ya 'kishoga' kumbe huko kwenu ndio mna kiwanda Cha kufyatua hao machoko' na stripers!

Ona huyu mchicha mwiba mwanaccm, duuh laana hii!
Screenshot_20200913-215354_1600023440278.jpg
 
Vijana wajitathmini kura zao watampa nani. Nchi ni yao. Maamuzi ni yao.

Hizi kukuru kakara zote za ccm, target ni wao. Hivyo kazi kwao.
 
CCM ndio zao hizo,hawana Sera za kuwaambia watu,kazi yako kuambatana na wafanya vituko
 
Halafu nyie CCM mnajifanya kukemea mambo ya 'kishoga' kumbe huko kwenu ndio mna kiwanda Cha kufyatua hao machoko' na stripers!

Ona huyu mchicha mwiba mwanaccm, duuh laana hii!View attachment 1569057
Hivi kumbe vyama vingine hamjawahi tumia wasanii au kwa vile mmewakosa safari hi,i maneno yamekuwa mengi endeleeni na sera za wasanii wenzenu wanapeta hahaaaaaa uzuri namba mlishaisoma
 
Nimemsikiliza huyu kiongozi kijana wa huko Mwanza ndani ya Chadema hakika nimejua Chadema ina hazina ya vijana wenye akili sana ila hatujawapa fursa ya kutosha.
Ameelezea dharau itumikayo na Magufuli na CCM yake ambapo badala ya kutumia mikutano hii ya kampeni kuwaeleza wananchi mbinu watakazo kuja nazo kuondoa umasikini, elimu duni, ajira, pension za wastaafu nk wao wanawaletea Mauno na wasanii. Hii ni dharau kubwa. Msikilize

 
Msikilizeni huyu kijana.

Baadhi ya wasanii walikuwa wakifanya mambo machafu.

Mambo yasiyoendana na maadili ya Watanzania.

CCM iwe makini katika kuchagua wasanii wa kufanya kampeni.



=======

Kila baada ya miaka mitano ukichagua hovyohovyo itakugharimu wewe, mke wako, mdogo wako, mama yako mpaka jiranii yako.

Kuna watu wanataka kuwakaririsha kuwa uchaguzi ni shabiki za Simba na Yanga nilikaa masaa kadhaa mwenyewe katika mda wa upweke nikatafakari inawezekana vipi katika nchi masikini vijana wasomi hawana ajira dada zetu wanadanga angali wana elimu vijana wenzuetu wanaitwa Marioo kwa kutembea na mama zetu ili waishi Magufuli,Mabula na Madiwani wanatuletea wasanii!

Nisikilizeni chukua hii kwa mujibu wa katiba ni jukwaa linalozungumza hatma ya maisha ya watanzania, sisi watoto masikini elimu ni msaada wetu, elimu inatafsiriwa jukwaani hapa afya za mama zetu mama wajawazito inatafsiriwa kwenye jukwaa hili wafanyabiashara hawa wadogowadogo ambao wanaishi maisha ya shida wanapigwa jua asubuhi mpaka jioni hatma yao na majibu magumu yanatakiwa yatokee hapa.

Magufuli na wenzake wanamleta Diamond anakata viuno halafu, halafu sikia sasa wanasema leta mauno, mauno leta mauno nisikilize mama yangu ni mstaafu aliniaga akaniambia mwanangu nataka nikamsikilize Magufuli pengine pensheni yangu atatoa mstakabali wa pensheni yangu, aliporudi nyumbani nikamuuliza mama Magufuli kakuahidi chochote juu ya pensheni yangu? Akasema mwanangu nimekuta mauno.

Nisikilize hivi hivi sisi watu masikini tunahitaji mauno ya Diamond? Tunahitaji mauno ya Zuchu? Nisikilize nilipitapita huko kwenye biblia nikasoma Mithali 31 inasema hivi
Mpe kilevi yule aliye karibu na kupotea mpe mvinyo masikini asahau shida zake.

Nikagundua Magufuli hakuwa na sera ya kuwaambia watanzania alitaka atuleweshe mziki ili tusimuulize maswali, walala atusahaulishe kuwa kuna watanzania masikini anatafuta namna ya kuwawekea mziki ili nyinyi msahau shida zenu.

Nisikilizeni Bob Marley anasema hivi sakafu ya baridi jana usiku kilikuwa ni kitanda changu kipande cha tofarikiliwa ni ni mto wangu jana usiku sikupata chakula wala tumaini la chakula ila niliamini ipo siku nitapata ukombozi nenda kasikilize wimbo wa Duppy Conqueror wa Bob Marley.

Maana yake ni nini kuna watanzania ambao usiku ukiingia anachukua boksi analala nje ya duka la muhindi hajui atakula nini anateseka ana matanio ya kuwa na familia pengine kamuacha dada yake yupo amekaa delux anasubiria wa kumnunua sababu amemaliza chuo kikuu hakuna msaada.

Huyu ambae ametoka Sengerema analala kwenye balaza la wahindi mwanae akienda shule anakaa chini kama mlivyokaa chini makamanda anaandika ili siku moja awe daktari kwenye shule za Magufuli anakuja anatuletea zama za mauno kwa watanzania masikini hawa ni dharau.

Mwalimu Nyerere anasema mtu mzima akikudanganya na anajua anakudanganya amekuon mjinga. Niweke msimamo wa mwisho nyakati kama hizi mwambie Mabula kwenye masumbwi kuna watu wenye uzani uzito na uzani mwepesi lakini nyakati hizi wenye uzani mwepesi wanalenga shabaha akamuulize Goliati Daudi alifanya nini. Kama anawapima wagombea wetu kwa fedha itakula kwake.
Mkuu JokaKuu hata kama una chuki na utawala ulioko madarakani, kwa sababu zozote, hoja zako ni vioja mwanzo mwisho.

Natamani kukulaumu kwa jinsi ulivyowananga na kuwadharilisha wasanii, lakini nyuma ya yote jilaumu mwenyewe

Mnadai Uhuru na Haki, iweje wasanii watengwe? Mbona mnajichanganya? Huo siyo unafiki?
 
Mkuu JokaKuu hata kama una chuki na utawala ulioko madarakani, kwa sababu zozote, hoja zako ni vioja mwanzo mwisho.

Natamani kukulaumu kwa jinsi ulivyowananga na kuwadharilisha wasanii, lakini nyuma ya yote jilaumu mwenyewe

Mnadai Uhuru na Haki, iweje wasanii watengwe? Mbona mnajichanganya? Huo siyo unafiki?

..nyimbo na mashairi ya ccm yanapaswa kuwachoma MABEBERU.

..CCM imeacha asili yake imekuwa chama cha wahuni wasiofuata maadili.
 
Back
Top Bottom