Uchaguzi 2020 Mtanzania amka: Wasanii kazi yao ni usanii, Kampeni za Uchaguzi Mkuu si usanii, hatuhitaji maigizo wala kukatiwa mauno!

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,269
54,664
Msikilizeni huyu kijana.

Baadhi ya wasanii walikuwa wakifanya mambo machafu.

Mambo yasiyoendana na maadili ya Watanzania.

CCM iwe makini katika kuchagua wasanii wa kufanya kampeni.



=======

Kila baada ya miaka mitano ukichagua hovyohovyo itakugharimu wewe, mke wako, mdogo wako, mama yako mpaka jiranii yako.

Kuna watu wanataka kuwakaririsha kuwa uchaguzi ni shabiki za Simba na Yanga nilikaa masaa kadhaa mwenyewe katika mda wa upweke nikatafakari inawezekana vipi katika nchi masikini vijana wasomi hawana ajira dada zetu wanadanga angali wana elimu vijana wenzuetu wanaitwa Marioo kwa kutembea na mama zetu ili waishi Magufuli,Mabula na Madiwani wanatuletea wasanii!

Nisikilizeni chukua hii kwa mujibu wa katiba ni jukwaa linalozungumza hatma ya maisha ya watanzania, sisi watoto masikini elimu ni msaada wetu, elimu inatafsiriwa jukwaani hapa afya za mama zetu mama wajawazito inatafsiriwa kwenye jukwaa hili wafanyabiashara hawa wadogowadogo ambao wanaishi maisha ya shida wanapigwa jua asubuhi mpaka jioni hatma yao na majibu magumu yanatakiwa yatokee hapa.

Magufuli na wenzake wanamleta Diamond anakata viuno halafu, halafu sikia sasa wanasema leta mauno, mauno leta mauno nisikilize mama yangu ni mstaafu aliniaga akaniambia mwanangu nataka nikamsikilize Magufuli pengine pensheni yangu atatoa mstakabali wa pensheni yangu, aliporudi nyumbani nikamuuliza mama Magufuli kakuahidi chochote juu ya pensheni yangu? Akasema mwanangu nimekuta mauno.

Nisikilize hivi hivi sisi watu masikini tunahitaji mauno ya Diamond? Tunahitaji mauno ya Zuchu? Nisikilize nilipitapita huko kwenye biblia nikasoma Mithali 31 inasema hivi
Mpe kilevi yule aliye karibu na kupotea mpe mvinyo masikini asahau shida zake.

Nikagundua Magufuli hakuwa na sera ya kuwaambia watanzania alitaka atuleweshe mziki ili tusimuulize maswali, walala atusahaulishe kuwa kuna watanzania masikini anatafuta namna ya kuwawekea mziki ili nyinyi msahau shida zenu.

Nisikilizeni Bob Marley anasema hivi sakafu ya baridi jana usiku kilikuwa ni kitanda changu kipande cha tofarikiliwa ni ni mto wangu jana usiku sikupata chakula wala tumaini la chakula ila niliamini ipo siku nitapata ukombozi nenda kasikilize wimbo wa Duppy Conqueror wa Bob Marley.

Maana yake ni nini kuna watanzania ambao usiku ukiingia anachukua boksi analala nje ya duka la muhindi hajui atakula nini anateseka ana matanio ya kuwa na familia pengine kamuacha dada yake yupo amekaa delux anasubiria wa kumnunua sababu amemaliza chuo kikuu hakuna msaada.

Huyu ambae ametoka Sengerema analala kwenye balaza la wahindi mwanae akienda shule anakaa chini kama mlivyokaa chini makamanda anaandika ili siku moja awe daktari kwenye shule za Magufuli anakuja anatuletea zama za mauno kwa watanzania masikini hawa ni dharau.

Mwalimu Nyerere anasema mtu mzima akikudanganya na anajua anakudanganya amekuon mjinga. Niweke msimamo wa mwisho nyakati kama hizi mwambie Mabula kwenye masumbwi kuna watu wenye uzani uzito na uzani mwepesi lakini nyakati hizi wenye uzani mwepesi wanalenga shabaha akamuulize Goliati Daudi alifanya nini. Kama anawapima wagombea wetu kwa fedha itakula kwake.
 
Kampeni za CCM za mwaka huu zimeja vimbwanga tu. Mara wapigane mitama jukwaani, mara wapakatane mbele ya watoto, mara mgombea apigishwe magoti na msanii eti kwa kigezo cha kumuombea marehemu!

All in all, Mgombea wa ccm na chama chake mwaka huu anavuna alichopanda. Watu hawataki tena kusikia kuhusu kununua ndege! wanataka kusikia sera zinazo husiana na maisha mapya na yenye matumaini kwa wote.
 
Katika kinyang'anyiro cha ugombea ubunge, wagombea wengi sana wametoa hotuba zao.

Katika hotuba zote, iliyobora kabisa ni hotuba iliyotolewa na mpiga debe wa mgombea ubunge wa Chadema huko Mwanza katika Jimbo la Nyamagana huko Mwanza.

Kijana huyo amewakumbusha wapiga kura wake kuhusu umuhimu wa uchaguzi huu, amewaasa wote wanaodhani kuwa uchaguzi ni kama vile ushabiki wa mpira wa Simba na Yanga. Amewaambia kuwa uchaguzi unahusu ajira zao, pensheni zao n. k

Pia amewaasa wananchi kuwa Magufuli hana sera za kuwaambia wananchi ndiyo maana anazunguuka na wasanii ili kuwasahaulisha matatizo yao kupitia burudani. Akahoji kuwa kwani mauno ya Diamond yanasaidiaje kwa mfano wazee wetu kupata pensheni zao?

Kwa kweli inafurahisha kuwa TZ tuna baadhi ya vijana vichwa, ambao naamini kama wakiingia bungeni watakuwa na mchango mzuri sana wa mawazo

Kwa taarifa zaidi angalia hotuba yenyewe hapa

 
Ahsante, nyie wasanii ni akina mond tu, VP hao wakata viuno niliowaona pamoja na muimba shairi? Sio wasanii?
 
Aiseee huyo Ni jembe kwelikweli na waliofatia pia Ni majembe yote , Lumumba nzima si Jiwe , Bashiru , Polepole wenye uwezo wa kujibu hizo hoja hakuna , haya kijani kibichi njooni sasa mtuambie mauno ya Diamond , yatalipa wastaafu, yataleta ajira , yatatatua changamoto za huduma duni za afya , ukosefu wa fedha mtaani , umaskini , ukosefu wa madawati n.k.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom