Mstaafu Kulipwa Mafao Ndani ya Siku Saba (7)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,428
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amesema kutokana na maendeleo ya mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), sasa hivi mstaafu anaweza kulipwa mafao yake ndani ya siku saba, licha ya sheria mpya ya Mafao kutaka mstaafu kulipwa mafao yake ndani ya siku 30 baada ya tarehe ya kustaafu.

Naibu Waziri Katambi ametoa kauli hiyo bungeni Jijini Dodoma leo Aprili 29, 2025, wakati akijibu swali la Mbunge wa Sumve mkoani Mwanza, Kasalali Mageni ambaye aliishauri Serikali kutunga sheria kali dhidi ya wanaochelewesha mafao ya watumishi pindi wanapostaafu.

Amesisitiza kuwa yameshafanyika marekebisho ya sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambayo yanamtaka mwajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati, hivyo malipo ya mafao yanatakiwa kufanyika ndani ya muda wa siku 30 baada ya tarehe ya kustaafu.
 
Vipi kwa ambao mda wa kustaafu haujafika na ameacha au kuachishwa kazi?
 
Uongoooo mtupu subiri wajr hapa wastaafu wanasota miaka hawajalipwa
 
Hizi serikali zetu maneno meeeengi. Hivi wasiposema wanajisikiaje? Walisema kujifungua ni bure lakini mmoja akamwambia mjamzito arudi kwa mumewe amzalishe.
 
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amesema kutokana na maendeleo ya mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), sasa hivi mstaafu anaweza kulipwa mafao yake ndani ya siku saba, licha ya sheria mpya ya Mafao kutaka mstaafu kulipwa mafao yake ndani ya siku 30 baada ya tarehe ya kustaafu.

Naibu Waziri Katambi ametoa kauli hiyo bungeni Jijini Dodoma leo Aprili 29, 2025, wakati akijibu swali la Mbunge wa Sumve mkoani Mwanza, Kasalali Mageni ambaye aliishauri Serikali kutunga sheria kali dhidi ya wanaochelewesha mafao ya watumishi pindi wanapostaafu.

Amesisitiza kuwa yameshafanyika marekebisho ya sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambayo yanamtaka mwajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati, hivyo malipo ya mafao yanatakiwa kufanyika ndani ya muda wa siku 30 baada ya tarehe ya kustaafu.
Labda vigogo.Sirikali ikisema kitu huwa ni kinyume chake
 
Back
Top Bottom