MWANDAMBO
Member
- Feb 2, 2011
- 19
- 17
Mathalani, China kuivamia Taiwan! Korea kusini kuingia vitani dhidi ya Korea Kaskazini, Rwanda kupigana na Burundi, Rwanda kuingia vitani dhidi ya Congo Drc, Uganda kuivamia Rwanda, AFRIKA kusini kuivamia SwaziLand, Kenya kuivamia Somalia, Senegal kuivamia Gambia, vita vikubwa baina ya mataifa ya Mashariki ya kati, kati ya Israeli na mataifa ya Waarabu, Saudia Arabia dhidi ya Iran, Pakistan dhidi ya Afghanistan, India dhidi ya Pakistan, na unaweza kumalizia dunia nzima. Sababu kuu zote ktk mifano ya nchi hizo ni usalama wa mataifa yao...
2. Ukraine ni Taifa Huru ambalo halipaswi kuwajibika juu ya mtazamo ya kisiasa na kiusalama kwa Taifa Jingine nje ya mipaka ya mfumo wa sheria za kimataifa na kipekee sana kwenye masuala binafsi ya Taifa Jingine. Usalama wa Taifa moja unapaswa kuzingatia uhuru wa Taifa jingine.
3. Hatuwezi kutumia makosa dhaniwa yaliyofanywa na Mataifa mengine hapo nyuma kuhalalisha hatari za kuharibu usalama wa Dunia ambapo hakuna ambae atabaki salama kama tukiacha mwelekeo mpya wa vita na visasi. Makosa yaliyofanywa na mataifa mengine yanapaswa kuwa ushahidi na msingi wa kuimarisha usalama wa kila Taifa kwa misingi ya demokrasia na sheria za haki za kimataifa.
4. Misingi ya usalama wa Taifa fulani, pamoja na kuzingatia sheria za Kimataifa na makubaliano ya Kimijataba ya kikanda, ni muhimu yakazingatia msingi wa Uhuru wa Kila Taifa kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na Taifa jingine.
5. Dunia inahitaji demokrasia ili kuweza kuhimili mikiki ya migogoro ya Kimataifa na mitazamo tofauti baina ya Mataifa mbalimbali. Kama kila Taifa likawa na mfumo wa uendeshaji wa Mambo ya nchi yake kwa misingi ya demokrasia, basi tunaweza kuifanya Dunia kuwa sehemu salama zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule. Kwasababu tofauti zetu na maugomvi yetu yataiishia kwneye mqbishano ya hoja, kukubaliana au kutokukubaliana na kuendelea kubishana na kutofautiana lkn sio kupigana na kuuwana.
Taifa la Urusi (Russia) kupitia kampuni binafsi ya WAGNER PMC, limeendesha vita na ukatili dhidi ya Binadamu maeneo mbalimbali duniani, na kipekee sana waathirika mkubwa amekuwa Afrika. Kimsingi hakuna Taifa kubwa duniani ambalo halijahusisha madhila ya ughadamizaji wa haki za Binadamu kwenye mabara kadhaa.
A. Ndambo