Msimjaribu Zitto, mtaumia!

Mwanzisha mada umekurupuka kwani hata katiba haimruhusu zito kugombea urais kutokana na umri wake, iweje ukurupuke na kudai atapata kura yeye kama yeye na siyo cdm wakati qualification zake hazimruhusu?
 
Sisi tunatanguliza nchi yetu mbele sio mtu au chama mana vyote hivyo vinapita...cdm sio Zitto ni Taasisi ipo na itakuepo bila Zitto wala wengine wengi...kwani hata sasaiv kazi inafanyika huko kusini Zitto yupo huko?!! wewe vipi bana tafta chakula ule..njaa itakuua...
 

Kikwete atabaki anatamani tu hawezi kutuchagulia Rais. Tunahitaji rais mwenye vision na demonstrated committment ya kuifanya Tanzania kucompete na nchi kama South Africa, Botswana, n.k na sio umri wa mtu.

Mifano halisi tunayo, serikali ya CCM ina vijana kwa wazee lakini hakuna mwenye uzalendo wala committment ya kututoa kwenye umasikini huu wa kutisha.
 
HUYU JAMAA ANAHOJA ZA KIPUMBA FU KWELI. Kama hawakipigii kura za uraisi CHADEMA Bali wanampigia Zito amshauri Zito agombee kupitia ata CCM AU NCCR.

Nafuu tuweke Mbwa CHADEMA KULIKO MROHO WA MADARAKA ZITTO
 
Huwezi ku conclude kuwa zito anakubalika nchi nzima kwa reference ya uchaguzi wa kigoma! Ulishaweka mlinganyo wa slaa na zito jinsi wanavyokubalika countrywide? Zito ni jembe la ukweli chadema lakini chadema sio zito! Chadema ni wananchi! Ni wangapi wamehama vyama vyao kuja chadema kwa sababu ya zitto? Mapenzi yako kwa zito yasiwe conclusion ya hisia na mitazamo ya watu! Nenda kwa takwimu!
 
Haya mambo hayo, vitisho vya kitoto na mbio za uraisi 2015. Mbona hujasema CHADEMA wataumiaje?
 
Simba wanasirikiana katika mawindo,wanafanya coordination katika mawindo. Inakuwaje Chadema wagombane when the enemy is strong?
 

Mkuu zomba ndio zitto kabwe mwenyewe, fuatilia utajua
 
though i am neither a member nor a fan of chadema but i am suddenly a fan of zitto kabwe, if he runs for president and i am still alive, count my vote for him, if he continues the way he is now.


so do i !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
.. wewe na nani mnamtaka Zitto? Au ndo yale yale ya "wakeup sleeping giant!" Cheap!
 

Hapana, mimi si Zitto, mimi ni mnazi wa Zitto ingawa mimi si magwanda ya kijivu, mimi ni gwanda orijino la kijani.
 
Lowassa ni mwamba wa kaskazini hamuwezi nyinyi mlikuwa mnafikiri ni wa bagamoyo sio atawalipua

Huyo wa Bwagamoyo ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Lowassa ameshawahi kuwa Waziri Mkuu wake, au umesahau? wale ni chanda na pete hawakujuana "barabarani".
 
Zombi=zomba upo wapi? Naona huko ccm mnamtamani sana zito kiongozi wetu shupavu CDM. Viongozi wenu ni lowassa mwamba kaskazini jaribuni kumgusa muone moto Pambaf

Sasa ndugu yangu, kama unaona id yangu ni Zomba wewe kunipachika Zombi, huoni kuwa huo ni uchokozi wa wazi wazi? Kama mjadala wa kiungwana unakushida, nakushauri kunywa maji kidogo, upumuwe kisha urudi tena. Tusianze kuitana majina "name calling" ni kinyume na kanuni za JF. Natumai moderators wanakusoma na watakufahamisha zaidi.

Naomba tuongee mada husika tusianze kushambuliana binafsi. Si vyema, au unasemaje kijana?
 
Zombi=zomba umeingia mitini lowassa Mzee wa makanisa Hana mpinzani ndani ya ccm lazima wote mfyate Mkia mpaka Rais wenu

Ni Zomba na si Zombi kama unavyonikejeli. Naomba tuendelee na mjadala wa kuheshimiana. Sijaingia mitini, nipo, kunywa maji halafu urudi, utapunguza Munkar na kejeli zisizo na tija kwako wala kwangu.
 

Hapo kwenye red, wewe na nani? Sasa naona umetumwa, kuna chama kipya kimeanzishwa kinaitwa ADC mshauri zito aende huko mkampee kura zenu. Ama kama hilo litakuwa gumu mshauri asimame kama mgombea binafsi kama katiba itakuwa imepitishwa. Huku CDM asahau kusimama kama mgombea wa urais, hatutakubali hilo litokee, tunahitaji kamanda mpambanaji zaidi bishoo. Pamoja na mtu sisi tunachagua Chadema. Zitto ni mbinafsi na mpenda sifa, ni mroho wa madaraka. Baba wa taifa alitushauri kuwa ukiona mtu anakimbilia Ikilu huyo ni wa kuogopwa kama ukoma. Angekuwa na busara walau kidogo angeacha watu wampeleke kuliko yeye kukimbilia. Angengojea kama Dr Slaa mwaka 2010, sio kujikimbiza kimbiza.

Hapana Zitto anafaa kuendelea kuwa mbunge tu labda huko baadaye akikuwa. Mara natakuwa mwenyekiti wa chama, mara nataka kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, mara nataka kuwa rais; who are you? kusema hivyo si kwamba napuuzia mchango wake katika siasa za mageuzi nchini mwetu, lakini ana kiherehere mno.

Ushauri wa bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…