Msimamo wa Rais Samia kuhusu demokrasia ya kisiasa, fujo za kisiasa na fujo za kidini: Tutaelewana tu!

Kazi ya chama chochote ni kushika dola kwa kuwini mapungufu ya kingine.
With evidence provided, Ukifanya comparative SWOT analysis kati ya CCM na Chadema unaona mizania inaangukia wapi?
 
Theory-Action-Review cycle haikwepeki kama unataka kufanya siasa za kitaifa.
Na theory maana yake ni yale yote uliyoyapata shuleni.
No short cut

Theory zako ni useless, si vibaya maana zinatusaidia kupoteza muda ni kurefresh hapa jukwaani, lakini hazina jipya.
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa, halafu nakuuliza swali. Wakati Dr Slaa na Katibu Mkuu wa CDM uliona mapambana kati ya CDM na dola kama sasa? Tafakari juu sababu zake.

Inaonekana wakati Dr. Slaa akipambana na dola ulikuwa bado mtoto. Maandamano ya Arusha mpaka watu kuuwawa na polisi hujui? Muuza magazeti Ali Zona mpaka anauwawa na polisi ulikuwa hujui? Mwandishi Daudi mwangosi aliuwawa huko iringa kwenye mkutano wa Slaa na bomu la polisi na picha zipo. Acha upotoshaji wa kijinga tafadhali.
 


Msimamo wa Rais Samia kuhusu demokrasia ya kisiasa, fujo za kisiasa na fujo za kidini ni wa kujadiliwa kwa kina kusudi watu wengi wauelewe na kuukubali.

Tayari kuna maoni kadhaa yametolewa tangu alipofanya mahojiano yake na BBC, na kuuweka bayana.

Kuna maoni ya Askofu Bagonza, Kauli za Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, mawazo ya Godbless Lema na maoni ya watu baki. Nami napenda kutoa maoni yangu leo.

1. Tofauti kati ya "demokrasia ya kisiasa na fujo za kisiasa" haikuanzishwa na Rais Samia.

Ipo siku zote kwa sababu ya mstari unaotenganisha siasa za watu wengi zinazoendeshwa kwa kutumia nguvu ya ushawishi wa hoja (democratic people's power) na siasa za watu wengi zinazoendeshwa kwa kutumia nguvu za ubabe na mitulinga (coercive people's power).

Fujo za kisasa zinazofanywa na vyama vya upinzani huwa ni mkakati wa kuiondoa serikali katika vipaumbele vyake. Hilo jambo halikubaliki popote duniani. Viongozi wa Chadema wanapaswa kuzingatia ukweli huu.

2. Kuna fujo zinazofanywa na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akipinga kauli za Rais Samia. Mnyika anasema kuwa uhuru wa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano hauna mipaka.

Hapana. Hakuna haki isiyo na mipaka. Ni kweli vyama vya siasa vina haki ya kufanya mikutano ya hadhara ili kueneza sera zake.

Lakini pia vinalo jukumu la kujizuia kuikwamisha serikali katika azima yake ya kutekeleza programu ambazo ni vipaumbele vya kitaifa kwa mujibu wa Ilani ya chama tawala.

Kwa mujibu wa
tangazo la Mbowe pale Mwanza, Chadema hawatambui jukumu hilii. Wanapaswa kulazimishwa kulitambua jukumu hili.

3. Kuna viongozi wa Chadema wanafanya fujo za kisiasa kupitia mgongo wa dini makanisani.

Wanazunguka makanisani na kuwaomba viongozi wa makanisa kuingiza katika ratiba zao za kikanisa kumwombea Mbowe ili aachiwe huru.

Kwa kitendo hiki, viongozi wa kidini wanashiriki kutekeleza programu za chama cha siasa. Aidha, kwa njia hii viongozi na wanachama wa Chadema wanatumia dini kufanya siasa.

Naona kwamba hapa inakuja hatari kama ile ya "mitano kwanza" ya Askofu Bagonza dhidi ya "mitano tena" ya Shehe nanihii.

Na bado hadi sasa Askofu Bagonza anaendeleza chokochoko kwa sababu ya
ugonjwa wa theomania unaomsumbua.

Theomania ni ugonjwa wa kichaa cha kidini kinachomfanya mhusika kuamini kwamba yeye ama ni Mungu au mpaka mafuta wa Mungu, na kwamba kwa sababu hiyo, yeye ni mtu mwenye uwezo wa kujua kila kitu, kufanya kila kitu, kusikilizwa na kila mtu, na kupewa utii na kila mtu.

Naye Askofu Mwamakula ametunga novena ya kumwombea Mbowe yenye kibwagizo "Mwanakondoo Ameshinda," na hivyo, kuigeuza CHADEMA kuwa Chama cha Demokrasia na Mwanakondoo Ameshinda"

Hatua za haraka zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi kusimamia kanuni inayokataa jaribio lolote kuanzisha na kuendesha chama cha siasa chenye kutafuta ufuasi kwa kutumia mafundisho ya kidini.

Nawasilisha.
Unasumbuliwa njaa na kukosa maadili. Unaishi bila maadili yoyote na akili zako umehamishia tumboni!

Raisi Samia ameaibisha taifa na kujiaibisha mwenyewe kwa kusema uongo dhahiri shairi! Kwa ujumla,amezingua sana. Anachimba kaburi lake la kisiasa mwenyewe kwa kukosa werevu wakubaini njia sahihi ya kufuata.

Katika siku 100 za kwanza za utawala wake,wapenda haki wote walimuamini na kumuunga mkono. Kwa sasa,imani hiyo ameipoteza mwenyewe kwa kutoka hadharani kudanganya taifa na ulimwengu.

Mimi nilikuwa mtetezi mkubwa wa mh raisi. Kwa sasa napata wakati mgumu sana. Niko njia panda.
 
Unasumbuliwa njaa na kukosa maadili. Unaishi bila maadili yoyote na akili zako umehamishia tumboni!
Katika historia ya dunia hakuna maadili mabovu kama haya yanayoanzia kwenye COERCIVE PEOPLE'S POOWER, kama yanayohubiriwa na Chadema. Ondoa boriti kwenye jicho lako kabla ya kuongelea kibanzi kwa wengine.
 
Back
Top Bottom