Msimamo wa Rais Samia kuhusu demokrasia ya kisiasa, fujo za kisiasa na fujo za kidini: Tutaelewana tu!

Sawa. Kuna mawili hapo:
1. Umuhimu wa Katiba Mpya
2. Uharaka wa Katiba Mpya

Ushahidi gani unahitajika kwa kila kipengele?

1. Kazi za Wariona na Kisanga ni ushahidi wa kipengele cha kwanza
2. Kipengele cha pili hakina ushahidi hadi sasa, japo Chadema wanakiuma uma midomo tu na kulazimisha kipaumbele cha Chadema kiwe ndio kipamumbele cha Serikali ya CCM.

Mambo hayaendi hivyo.

Tuweke nguvu ya hoja katika kipengele cha pili, cha kwanza kinaeleweka na kukubalika.
2.Uharaka wa Katiba..
Tupo kwenye kipindi ambacho ili tuijenge nchi basi tunahitaji mawazo kinzani na ya kwetu chama tawala,sasa mianya iliyopo kwenye katiba ya sasa inatupa uwezo mkubwa sana hata tusitake wapinzani waseme mawazo yao kinzani..rejea zuio la mikutano ya kisiasa,rejea uwiano wa wabunge wa upinzani bungeni na wa chama tawala,tazama bungeni upitishwaji wa miswada,vifungu vya kisheria spika anasema " wanaopinga waseme hapana,wanaokubali waseme ndiyo" imetupelekea leo tunahaha kuelezea kuhusu hizi TOZO..

Tupo kwenye kipindi mtu anaweza kukausha tu mifuko ya hifadhi na kuamua kuzifanyia pesa jambo jingine bila kushauriana na mtu..

Mimi kama mwana CCM natamani kuiona hali hii na nyingine kama hizi ziondoshwe na wala tusitegemee mbeleko za mapungufu ya Katiba ili tuendelee kuwepo madarakani..
 
Bila ya shaka una utindio wa ubongo. Wahi Mirembe kabla hujaanza kuokota makopo barabarani.
Wewe kama huna mtindio wa ubongo mbona ulirudia darasa la saba, kina Dionise wa CBE wakakuacha nyuma unajivuta kama konokono?
 
Kauli kwamba "Hata ukipiga kura kwingine CCM itaunda serikali" yaweza kuwa ni uchokozi kwa sababu tayari CCM walikuwa wamejihakikishia, sio kura halali za ushindi, bali kura haramu za ushindi.

Lakini, Kauli kwamba"Hata ukipiga kura kwingine CCM itaunda serikali" ilitamkwa kwa sababu tayari CCM walikuwa wamejihakikishia kura halali za ushindi.

Kwa hiyo, Kauli kwamba"Hata ukipiga kura kwingine CCM itaunda serikali" sio kauli ya kichokozi.

Kuna swali jingine?
Mwenye mamlaka ya kumtangaza na kumwakikishia mgombea Urais kuwa ameshinda kwa mujibu wa sheria ni tume ya Taifa ya uchaguzi.CCM ni tume ya uchaguzi ya Taifa hadi itangaze matokeo?

Hizo kura "halali" za ushindi unazozizungumzia ni zipi hizo wakati CCM walipora uchaguzi nchi nzima?Siku hizi wizi wa kura unaitwa ni kura halali?Kuiba kura siyo fujo za kisiasa?

109_20210724_194836.jpg
109_20210724_194739.jpg
109_20210724_194857.jpg
 
Mwenye mamlaka ya kumtangaza na kumwakikishia mgombea Urais kuwa ameshinda kwa mujibu wa sheria ni tume ya Taifa ya uchaguzi.CCM ni tume ya uchaguzi ya Taifa hadi itangaze matokeo?

Hizo kura "halali" za ushindi unazozizungumzia ni zipi hizo wakati CCM walipora uchaguzi nchi nzima?Siku hizi wizi wa kura unaitwa ni kura halali?Kuiba kura siyo fujo za kisiasa?

View attachment 1889193View attachment 1889195View attachment 1889196

Swali: Mwenye mamlaka ya kumtangaza na kumwakikishia mgombea Urais kuwa ameshinda kwa mujibu wa sheria ni tume ya Taifa ya uchaguzi.CCM ni tume ya uchaguzi ya Taifa hadi itangaze matokeo?

Jibu: Naona huna uzoefu na siasa za uchaguzi. Kanuni ya kwanza ya kujiongezea kura ni kuwaaminisha wapiga kura kwamba utashinda, hata kama tayari unaona maji yako shingoni. Kama hili hulifahamu achana na mjadala huu.

Swali: Hizo kura "halali" za ushindi unazozizungumzia ni zipi hizo, wakati CCM walipora uchaguzi nchi nzima? Siku hizi wizi wa kura unaitwa ni kura halali?Kuiba kura siyo fujo za kisiasa?

Jibu: Maneno kwamba "wakati CCM walipora uchaguzi nchi nzima" yanahitaji ushahidi wenye hadhi ya kisheria kuyathibitisha. Mpaka leo jambo hilo limeshindikana. Hata hao kina Mdee pichani pale Bungeni juzi wameadhibiwa kwa kutolewa Bungeni kwa wiki kadhaa kwa sababu ya kushindwa kuyathibitisha ndani ya Bunge. Ukituhumu ni juu yako kuthibitisha. Ukishindwa kuthibitisha unafuta kauli na kulamba adhabu yako.

Mwisho, kumbuka haya mawili:

1. Sheria ya Usalama wa Taifa (1996) ilitungwa na wabunge wote wakiwemo wa upinzani. Wakatoa mamlaka kwa TISS kufanya "covert operations" pale ambapo kuna sababu za kiusalama kufanya hivyo. Sheria hiyo haisemi kuwa "covert operations" hazitafanyika kwenye uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

2. Chadema waliandika Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 wakasema kuwa wataiweka nchi rehani kwa kutumia madini kama dhamana ya mikopo ya kimataifa.

Ukishindwa kulipa mkopo nchi inachukuliwa na mkopeshaji. Kwa maoni yangu, hii ingekuwa sababu nzuri ya kiusalama kuifanya TISS kuchukua hatua zinazofaa kuichinjia baharini Chadema.

Mtu yeyote anayejua kazi za secret service atakwambia hivyo. Hata hivyo, sijui kwa uhakika kilichotokewa katika uchaguzi wa 2020. Utafiti unaoratibiwa na Ngurumo uendelee, labda utatupa majibu sahihi katika siku za usoni.
 
Swali: Mwenye mamlaka ya kumtangaza na kumwakikishia mgombea Urais kuwa ameshinda kwa mujibu wa sheria ni tume ya Taifa ya uchaguzi.CCM ni tume ya uchaguzi ya Taifa hadi itangaze matokeo?

Jibu: Naona huna uzoefu na siasa za uchaguzi. Kanuni ya kwanza ya kujiongezea kura ni kuwaaminisha wapiga kura kwamba utashinda, hata kama tayari unaona maji yako shingoni. Kama hili hulifahamu achana na mjadala huu.
Samia hakuhakikishia wapiga kura kuwa atashinda ila aliwaambia kuwa anaenda kuunda serikali hata kama watu watachagua upinzani.
Swali: Hizo kura "halali" za ushindi unazozizungumzia ni zipi hizo, wakati CCM walipora uchaguzi nchi nzima? Siku hizi wizi wa kura unaitwa ni kura halali?Kuiba kura siyo fujo za kisiasa?

Jibu: Maneno kwamba "wakati CCM walipora uchaguzi nchi nzima" yanahitaji ushahidi wenye hadhi ya kisheria kuyathibitisha. Mpaka leo jambo hilo limeshindikana. Hata hao kina Mdee pichani pale Bungeni juzi wameadhibiwa kwa kutolewa Bungeni kwa wiki kadhaa kwa sababu ya kushindwa kuyathibitisha ndani ya Bunge. Ukituhumu ni juu yako kuthibitisha. Ukishindwa kuthibitisha unafuta kauli na kulamba adhabu yako.
Mihimili yote mitatu ilishiriki katika kuisaidia CCM katika kupora uchaguzi.Huwezi kwenda kulalamika kwa mtu ambae ndiye amekuibia kura.Huwezi kwenda kuomba haki yako ya kisheria kwa yuleyule ambae ameshiriki kukuibia haki hiyo.
Mwisho, kumbuka haya mawili:

1. Sheria ya Usalama wa Taifa (1996) ilitungwa na wabunge wote wakiwemo wa upinzani. Wakatoa mamlaka kwa TISS kufanya "covert operations" pale ambapo kuna sababu za kiusalama kufanya hivyo. Sheria hiyo haisemi kuwa "covert operations" hazitafanyika kwenye uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

2. Chadema waliandika Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 wakasema kuwa wataiweka nchi rehani kwa kutumia madini kama dhamana ya mikopo ya kimataifa.

Ukishindwa kulipa mkopo nchi inachukuliwa na mkopeshaji. Kwa maoni yangu, hii ingekuwa sababu nzuri ya kiusalama kuifanya TISS kuchukua hatua zinazofaa kuichinjia baharini Chadema.
Sasa kwa nini hiyo unayoiita TISS haikuchinjia chadema baharini?Haijui wajibu wake?Tuna taasisi ambazo hazijui wajibu wake?Tuna taasisi ambazo zinaendeshwa kutokana na mtu alivyoamka siku hiyo na mke wake badala ya taasisi kuendeshwa kwa mujibu wa sheria?

Kama walizembea katika hili ni mangapi mpaka sasa hivi watakuwa wamezembea?Hii inaonyesha kuwa tuna taasisi tasa ambazo muda wowote zinaweza kuuza nchi yetu,na huu ndiyo mfumo ambao CCM imetengeneza kwa miaka yake 60 ya kuongoza nchi hii.Ni muda muafaka sasa CCM kukaa pembeni ili ituachie nchi yetu tuweze kuindesha kwa mujibu wa sheria.
 
Majukumu ya kuheshimu haki za watu baki ni yapi?
Katika haki ya serikali kutekeleza programu zake za maendeleo, hauni umuhimu wa serikali kushirikisha wadau wengine wa maendeleo Kama vyama mbadala(upinzani) katika kushiriki katika hizo programu badala ya kuwaweka pembeni
Hiyo ni hoja nyingine kabisa. Itakayotegemea utashi wa mtu binafsi.

Magufuli aliteua wapinzani kwenye serikali yake. Matokeo yake mkabeza kwamba hao anaowateua ni makanjanja.

Kule Zanzibar nadhani hilo takwa la kushirikishwa kwa vyama vingine kwenye serikali lipo kwenye katiba yao. Sidhani kama kuna impact yoyote positive tangu huo utaratibu uanze kule Zanzibar zaidi ya "kutuliza" wapinzani kwa style ya "tule wote".

Hapa kwetu kama hicho ndicho mnachokitaka baada ya kugundua hakuna namna nyingine yoyote halali au haramu ya kuifanya CCM iachie madaraka basi mseme tena mseme kwa uwazi.

Kwamba "...na sisi wapinzani tunataka kula keki ya taifa mtushirikishe katika kula."

Ila mkianza kuleta pretense zenu kwamba mnapambania maslahi ya watanzania kwa ujumla hivyo muachwe mfanye kila mnachokitaka kwa uhuru sidhani kama uhuru huo mtaupata.

Duniani hakuna kitu kama hicho.
 
Uongo ni jadi yako mpuuzi wewe hunijui sikujui na sijawahi kurudia darasa la lolote lile na wala sijawahi kutia mguu CBE. Ná huyo dionise sijawahi hata kumsikia masikioni mwangu. Muongo mkubwa wewe. Umeshindwa hoja sasa unaleta viroja na kutunga uzushi.
Wewe kama huna mtindio wa ubongo mbona ulirudia darasa la saba, kina Dionise wa CBE wakakuacha nyuma unajivuta kama konokono?
 
Msimamo wa Rais Samia kuhusu demokrasia ya kisiasa, fujo za kisiasa na fujo za kidini ni wa kujadiliwa kwa kina kusudi watu wengi wauelewe na kuukubali.

Tayari kuna maoni kadhaa yametolewa tangu alipofanya mahojiano yake na BBC, na kuuweka bayana.

Kuna maoni ya Askofu Bagonza, Kauli za Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, mawazo ya Godbless Lema na maoni ya watu baki. Nami napenda kutoa maoni yangu leo.

1. Tofauti kati ya "demokrasia ya kisiasa na fujo za kisiasa" haikuanzishwa na Rais Samia.

Ipo siku zote kwa sababu ya mstari unaotenganisha siasa za watu wengi zinazoendeshwa kwa kutumia nguvu ya ushawishi wa hoja (democratic people's power) na siasa za watu wengi zinazoendeshwa kwa kutumia nguvu za ubabe na mitulinga (coercive people's power).

Fujo za kisasa zinazofanywa na vyama vya upinzani huwa ni mkakati wa kuiondoa serikali katika vipaumbele vyake. Hilo jambo halikubaliki popote duniani. Viongozi wa Chadema wanapaswa kuzingatia ukweli huu.

2. Kuna fujo zinazofanywa na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akipinga kauli za Rais Samia. Mnyika anasema kuwa uhuru wa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano hauna mipaka.

Hapana. Hakuna haki isiyo na mipaka. Ni kweli vyama vya siasa vina haki ya kufanya mikutano ya hadhara ili kueneza sera zake.

Lakini pia vinalo jukumu la kujizuia kuikwamisha serikali katika azima yake ya kutekeleza programu ambazo ni vipaumbele vya kitaifa kwa mujibu wa Ilani ya chama tawala.

Kwa mujibu wa
tangazo la Mbowe pale Mwanza, Chadema hawatambui jukumu hilii. Wanapaswa kulazimishwa kulitambua jukumu hili.

3. Kuna viongozi wa Chadema wanafanya fujo za kisiasa kupitia mgongo wa dini makanisani.

Wanazunguka makanisani na kuwaomba viongozi wa makanisa kuingiza katika ratiba zao za kikanisa kumwombea Mbowe ili aachiwe huru.

Kwa kitendo hiki, viongozi wa kidini wanashiriki kutekeleza programu za chama cha siasa. Aidha, kwa njia hii viongozi na wanachama wa Chadema wanatumia dini kufanya siasa.

Naona kwamba hapa inakuja hatari kama ile ya "mitano kwanza" ya Askofu Bagonza dhidi ya "mitano tena" ya Shehe nanihii.

Na bado hadi sasa Askofu Bagonza anaendeleza chokochoko kwa sababu ya
ugonjwa wa theomania unaomsumbua.

Theomania ni ugonjwa wa kichaa cha kidini kinachomfanya mhusika kuamini kwamba yeye ama ni Mungu au mpaka mafuta wa Mungu, na kwamba kwa sababu hiyo, yeye ni mtu mwenye uwezo wa kujua kila kitu, kufanya kila kitu, kusikilizwa na kila mtu, na kupewa utii na kila mtu.

Naye Askofu Mwamakula ametunga novena ya kumwombea Mbowe yenye kibwagizo "Mwanakondoo Ameshinda," na hivyo, kuigeuza CHADEMA kuwa Chama cha Demokrasia na Mwanakondoo Ameshinda"

Hatua za haraka zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi kusimamia kanuni inayokataa jaribio lolote kuanzisha na kuendesha chama cha siasa chenye kutafuta ufuasi kwa kutumia mafundisho ya kidini.

Nawasilisha.

No comment. Nothing to discuss. The thread is empty and heavily biased.
 
Sawa. Kuna haja ya kurejea misingi ya human rights based ideologism (“huribatism”) ambayo imefafanuliwa vizuri na Profesa John Finnis kama ifuatavyo:

"The fundamental postulates of Hohfeld’s system [of human rights] are:

(i) that all assertions or ascriptions of rights can be reduced without remainder to ascriptions of one or some combination of the following four ‘Hohfeldian rights’: (a) ‘claim-rights’, (b) ‘liberty rights’, (c) ‘power rights’, and (d) ‘immunity rights’; and

(ii) that to assert a Hohfeldian right is to assert a [four-term relation] between one person, one act-description, one other person, [and a normative rule R].

"[Concerning claim-rights and liberty-rights,] if A and B signify persons, F stands for an act description signifying some act, and R signifies a rule that relates the two parties, then, the following logical relations among A, B, [R] and F will obtain:

(1) A has a claim-right that B should F, if and only if [there is a rule R which specifies that] B has a duty to A to F.

(2) B has a liberty (relative to A) to F, if and only if [there is no rule R which negates the claim that] A has no-claim-right (‘a no-right) that B should not F.

(2’) B has a liberty (relative to A) not to F, if an only if [there is no rule R which negates the claim that] A has no-claim-right (‘a no right’) that B should F.

"From the above, one can easily see, in light of these four-term relations that, the most important of the aids to clear thinking provided by Hohfeld’s schema is the distinction between A’s claim-right (which has as its correlative B’s duty) and A’s liberty , which is A’s freedom from duty and thus has as its correlative the absence or negation of the claim-right that B would otherwise have.

"A claim-right is always either, positively a right to be given something (or assisted in a certain way) by someone else, or, negatively, a right not to be interfered with or dealt with or treated in a certain way, by someone else. When the subject-matter of one’s claim of right is one’s own act(s), forbearance(s), or omission(s), that claim cannot be to a claim-right, but can only be to a liberty ."

(Source: John Finnis, Natural Law and Natural Rights. New York/Oxford: Clarendon Press, 1980, p. 199-200.)."

Tafsiri nyepesi ya maneno haya ni kwamba, katika anatomia ya kila haki inayoweza kufikirika kuna sehemu nne muhimu. Sehemu hizo ni: madai, mdai, mdaiwa na sababu ya madai. Ufafanuzi ni huu:
  1. Madai (claim): Haya na madai ya kufanyika au kutofanyika kwa tendo fulani; au madai ya kitu fulani.
  2. Mdai (right-holder): Huyu ni mtu anayedaiwa afanyiwe au asifanyiwe tendi fulani; au anayedai kitu fulani.
  3. Mdaiwa (duty-bearer): Huyu ni mtu anayedaiwa afanye au asifanye tendi fulani; au anayedaiwa kitu fulani.
  4. Sababu ya madai (normative justiification): Hiki ni kifungu cha kanuni, sheria au utaratibu kinachotumika kuonyesha kwamba madai ni halali, mdai ni yupi na mdaiwa ni yupi.
Kwa kuzingatia mwongozo huu wa HURIBATISM,naona kwamba, haki zinazohusiana na DEMOKRASIA zitajadilika vizuri zaidi ikiwa ufahamu wa kategoria anuai za haki zinazojadiliwa katika hoja iliyo mbele yetu utakuwa hudu dhidi ya kosa la kimantiki liitwalo “equivocation,” yaani kutumia neno “haki” katika major premise likiwa na maana “x” na kasha kulitumia neno hilo hilo katika minor premise au katika conclusion likiwa na maana “y”.

Angalizo hili ni muhimu kwani, kwa kuzingatia mwongozo wa profesa John Finnis hapo juu ni wazi kwamba tunazo aina kuu nne za haki za binadamu, ambapo kila haki inazo sehemu nne pia kama ifuatavyo:

  1. Haki ya raia A kufanyiwa tendo T na raia B kwa mujibu wa maagizo ya sheria S inaitwa haki ya madai chanya (POSITIVE CLAIM RIGHT)
  2. Haki ya raia A kutofanyiwa tendo T na raia B kwa mujibu wa makatazo ya sheria S inaitwa haki ya madai hasi (NEGATIVE CLAIM RIGHT)
  3. Haki ya raia A kufanya tendo T bila hofu ya kuhojiwa na raia B kwa mujibu wa ombwe lililo katika makatazo ya Sheria S inaitwa haki ya uhuru chanya (POSITIVE LIBERTY RIGHT).
  4. Haki ya raia A kutofanya tendo T bila hofu ya kuhojiwa na raia B kwa mujibu wa ombwe lililo katika makatazo ya sheria S inaitwa haki ya uhuru hasi (NEGATIVE LIBERTY RIGHT)
Katika muktadha huu wa huribatism, Alan Gewirth, aliandika makala yake “Are there any absolute rights?” kupitia jarida la “The Philosophical Quarterly, Volume 31, Number 122 (Jan. 1981), pg 1-16”, na kufanya uchambuzi murua kwa ajili yetu.

Gewirth (1981) anasema kwamba, mienendo ya watawala na watawaliwa yaweza kuifanya haki ya binadamu kuanguka katika kundi moja wapo kati ya makundi haya manne: FULFILLED, VIOLATED, INFRINGED, AND OVERRIDDEN. Kwa ukamilifu Gewirth anasema:

A right is FULFILLED when the correlative duty is carried out, i.e. when the required action is performed or the prohibited action is not performed.

"A right is INFRINGED when the correlative duty is not carried out, i.e. when the required action is not performed or the prohibited action is performed…

"A right is VIOLATED when it is unjustifiably infringed, i.e. when the required action is unjustifiably not performed or the prohibited action is unjustifiably performed.

"And a right is OVERRIDDEN when it is justifiably infringed, so that there is sufficient justification for not carrying out the correlative duty, and the required action is justifiably not performed or the prohibited action is justifiably performed.

"A right is absolute when it cannot be overridden in any circumstances, so that it can never be justifiably infringed and it must be fulfilled without any exceptions (Gewirth, pg.2).

Kwa kuzingatia mchanganuo huo hapo juu, ni wazi kwamba, utekelezaji wa " POSITIVE LIBERTY RIGHT" unayo mipaka inayotokana na uwepo wa " NEGATIVE CLAIM RIGHT."

Kwa lugha ya walei wa mitaani tunasema kuwa uhuru wa kunyoosha mikono yako hewani na kujizungusha unaishia pale pua ya jirani yako inapoanzia.

Hii ndiyo sababu haki ya mvuta sigara inaminywa na jukumu lake la kuheshimu haki za majirani zake (kwa mfano wagonjwa waliolazwa wodini).

Vivyo hivyo, haki ya mwimbaji inaminywa na jukumu lake la kuheshimu haki za majirani zake (kwa mfani wanafunzi walio darasani wanajisomea).

Na hatimaye, haki ya kuandamana na haki ya kufanya mikutano ya hadhara ni "liberty rights" ambazo urefu wake unaishia pale yanapoanzia majukumu ya kuheshimu haki za watu baki, na katika hoja ya sasa, haki za serikali kutekeleza programu zake za maendeleo.

Nadhani nimejibu dukuduku zako kisheria.

Tunashukuru kuwa umetuonyesha kuwa kweli ulienda shule. Kwa sisi mambumbu, mfano wa sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingetusaidia zaidi kuelewa hoja yako.

Aidha, haujafafanua kwa vipi haki ya mtu baki inaathirika kwa chama kufanya mikutano ya hadhara na kuandamana. Sijawahi kusikia Chadema wakilazimisha watu kuhudhuria mikutano yao lakini kuna mifano mingi ya vyuo na shule kufungwa ili wanafunzi na walimu wakahadhurie mikutano ya hadhara ya viongozi wa serikali. Kwangu mimi hii ni kuingilia haki yao ya msingi ya kupata elimu katika muda uliowekwa. Tumeshuhudia barabara zikifungwa ili viongozi wa serikali wapate nafasi ya kutoa hotuba bila kujali kuwa kuna watu baki ambao wana safari zao muhimu. Sijawahi kusikia ikifanyika hivyo kwa ajili ya mikutano ya Chadema au chama kingine cha upinzani. Hapa guilty party ni huyo unaemtetea.

Sijawahi kusikia Chadema wamezuia serikali kutekeleza programu zao za maendeleo. On the contrary, nimesikia viongozi wa serikali na chama chao wakisema waziwazi kuwa watazito katika programu zao za maendeleo sehemu zote zitakazopigia kura vyama vya upinzani pamoja na kuwa kodi zao zinachangia katika kufanikisha hayo maendeleo. Hapa tena, you are barking up the wrong tree.

Amandla...
 
Msimamo wa Rais Samia kuhusu demokrasia ya kisiasa, fujo za kisiasa na fujo za kidini ni wa kujadiliwa kwa kina kusudi watu wengi wauelewe na kuukubali.

Tayari kuna maoni kadhaa yametolewa tangu alipofanya mahojiano yake na BBC, na kuuweka bayana.

Kuna maoni ya Askofu Bagonza, Kauli za Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, mawazo ya Godbless Lema na maoni ya watu baki. Nami napenda kutoa maoni yangu leo.

1. Tofauti kati ya "demokrasia ya kisiasa na fujo za kisiasa" haikuanzishwa na Rais Samia.

Ipo siku zote kwa sababu ya mstari unaotenganisha siasa za watu wengi zinazoendeshwa kwa kutumia nguvu ya ushawishi wa hoja (democratic people's power) na siasa za watu wengi zinazoendeshwa kwa kutumia nguvu za ubabe na mitulinga (coercive people's power).

Fujo za kisasa zinazofanywa na vyama vya upinzani huwa ni mkakati wa kuiondoa serikali katika vipaumbele vyake. Hilo jambo halikubaliki popote duniani. Viongozi wa Chadema wanapaswa kuzingatia ukweli huu.

2. Kuna fujo zinazofanywa na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akipinga kauli za Rais Samia. Mnyika anasema kuwa uhuru wa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano hauna mipaka.

Hapana. Hakuna haki isiyo na mipaka. Ni kweli vyama vya siasa vina haki ya kufanya mikutano ya hadhara ili kueneza sera zake.

Lakini pia vinalo jukumu la kujizuia kuikwamisha serikali katika azima yake ya kutekeleza programu ambazo ni vipaumbele vya kitaifa kwa mujibu wa Ilani ya chama tawala.

Kwa mujibu wa
tangazo la Mbowe pale Mwanza, Chadema hawatambui jukumu hilii. Wanapaswa kulazimishwa kulitambua jukumu hili.

3. Kuna viongozi wa Chadema wanafanya fujo za kisiasa kupitia mgongo wa dini makanisani.

Wanazunguka makanisani na kuwaomba viongozi wa makanisa kuingiza katika ratiba zao za kikanisa kumwombea Mbowe ili aachiwe huru.

Kwa kitendo hiki, viongozi wa kidini wanashiriki kutekeleza programu za chama cha siasa. Aidha, kwa njia hii viongozi na wanachama wa Chadema wanatumia dini kufanya siasa.

Naona kwamba hapa inakuja hatari kama ile ya "mitano kwanza" ya Askofu Bagonza dhidi ya "mitano tena" ya Shehe nanihii.

Na bado hadi sasa Askofu Bagonza anaendeleza chokochoko kwa sababu ya
ugonjwa wa theomania unaomsumbua.

Theomania ni ugonjwa wa kichaa cha kidini kinachomfanya mhusika kuamini kwamba yeye ama ni Mungu au mpaka mafuta wa Mungu, na kwamba kwa sababu hiyo, yeye ni mtu mwenye uwezo wa kujua kila kitu, kufanya kila kitu, kusikilizwa na kila mtu, na kupewa utii na kila mtu.

Naye Askofu Mwamakula ametunga novena ya kumwombea Mbowe yenye kibwagizo "Mwanakondoo Ameshinda," na hivyo, kuigeuza CHADEMA kuwa Chama cha Demokrasia na Mwanakondoo Ameshinda"

Hatua za haraka zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi kusimamia kanuni inayokataa jaribio lolote kuanzisha na kuendesha chama cha siasa chenye kutafuta ufuasi kwa kutumia mafundisho ya kidini.

Nawasilisha.

Mh!!! Mama Amon!!!!
 
Kazi ya siasa ni mdomo.
Kazi ya chama cha upinzani ni kuangalia mapungufu ya chama tawala na kuyaanika,Kazi ya chama tawala ni kujibu hoja za Wapinzani.
Uwezo wa ccm kujibu hoja ulishakufa,tegemeo lao ni kuwahaidi teuzi baada ya kustaafu wakuu wa police Ili wawasaidie kuzijibu hoja za Wapinzani.
 
Msimamo wa Rais Samia kuhusu demokrasia ya kisiasa, fujo za kisiasa na fujo za kidini ni wa kujadiliwa kwa kina kusudi watu wengi wauelewe na kuukubali.

Tayari kuna maoni kadhaa yametolewa tangu alipofanya mahojiano yake na BBC, na kuuweka bayana.

Kuna maoni ya Askofu Bagonza, Kauli za Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, mawazo ya Godbless Lema na maoni ya watu baki. Nami napenda kutoa maoni yangu leo.

1. Tofauti kati ya "demokrasia ya kisiasa na fujo za kisiasa" haikuanzishwa na Rais Samia.

Ipo siku zote kwa sababu ya mstari unaotenganisha siasa za watu wengi zinazoendeshwa kwa kutumia nguvu ya ushawishi wa hoja (democratic people's power) na siasa za watu wengi zinazoendeshwa kwa kutumia nguvu za ubabe na mitulinga (coercive people's power).

Fujo za kisasa zinazofanywa na vyama vya upinzani huwa ni mkakati wa kuiondoa serikali katika vipaumbele vyake. Hilo jambo halikubaliki popote duniani. Viongozi wa Chadema wanapaswa kuzingatia ukweli huu.

2. Kuna fujo zinazofanywa na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akipinga kauli za Rais Samia. Mnyika anasema kuwa uhuru wa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano hauna mipaka.

Hapana. Hakuna haki isiyo na mipaka. Ni kweli vyama vya siasa vina haki ya kufanya mikutano ya hadhara ili kueneza sera zake.

Lakini pia vinalo jukumu la kujizuia kuikwamisha serikali katika azima yake ya kutekeleza programu ambazo ni vipaumbele vya kitaifa kwa mujibu wa Ilani ya chama tawala.

Kwa mujibu wa
tangazo la Mbowe pale Mwanza, Chadema hawatambui jukumu hilii. Wanapaswa kulazimishwa kulitambua jukumu hili.

3. Kuna viongozi wa Chadema wanafanya fujo za kisiasa kupitia mgongo wa dini makanisani.

Wanazunguka makanisani na kuwaomba viongozi wa makanisa kuingiza katika ratiba zao za kikanisa kumwombea Mbowe ili aachiwe huru.

Kwa kitendo hiki, viongozi wa kidini wanashiriki kutekeleza programu za chama cha siasa. Aidha, kwa njia hii viongozi na wanachama wa Chadema wanatumia dini kufanya siasa.

Naona kwamba hapa inakuja hatari kama ile ya "mitano kwanza" ya Askofu Bagonza dhidi ya "mitano tena" ya Shehe nanihii.

Na bado hadi sasa Askofu Bagonza anaendeleza chokochoko kwa sababu ya
ugonjwa wa theomania unaomsumbua.

Theomania ni ugonjwa wa kichaa cha kidini kinachomfanya mhusika kuamini kwamba yeye ama ni Mungu au mpaka mafuta wa Mungu, na kwamba kwa sababu hiyo, yeye ni mtu mwenye uwezo wa kujua kila kitu, kufanya kila kitu, kusikilizwa na kila mtu, na kupewa utii na kila mtu.

Naye Askofu Mwamakula ametunga novena ya kumwombea Mbowe yenye kibwagizo "Mwanakondoo Ameshinda," na hivyo, kuigeuza CHADEMA kuwa Chama cha Demokrasia na Mwanakondoo Ameshinda"

Hatua za haraka zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi kusimamia kanuni inayokataa jaribio lolote kuanzisha na kuendesha chama cha siasa chenye kutafuta ufuasi kwa kutumia mafundisho ya kidini.

Nawasilisha.
SIASA za FUJO zimeanzishwa na CCM Kwa KUSHIRIKIANA NA Polisi CCM ingeendesha Siasa kwa HAKI hakuna Chama kingeleta FUJO
Kwanini CCM ivizuie VYAMA vingine VISIFANYE SIASA lakini CcM ifanye? Viongozi wa CCM wanazunguka Nchi nzima Wanafanya SIASA wapinzani Wakifanya hata MIKUTANO ya NDANI wanakamatwa kwanini Kusiwe na SIASA ZA FUJO?
Tufike Mahali CCM ikubali Vyama vyote Vina HAKI sawa ya KUFANYA MIKUTANO na POLISI Waache Kuwakamata na Kuwanyima Dhamana Watuhumiwa na Walio Wengi Wanaonewa.
JamiiForums1966179623.jpg

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom