Msimamo wa CHADEMA kuhusu maridhiano

Msimamo wa CHADEMA kuhusu maridhiano

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
917
Reaction score
3,181

Mtangazaji:"Kuhusu maridhiano, hapa nimesikia mwanzoni umezungumza unasema kwamba hakuna maridhiano mpaka wapatikane watu kutoka nje. Unaamini kwamba Tanzania haiwezi kufanya mambo yake bila kushirikisha watu wengine?"

John Heche: "Hivi vitu Farhia si vitu vinavyotokea kwa mara ya kwanza duniani. Na tutachukua mifano ya karibu hivi karibuni kwa uzoefu (experience) wa Kenya iliyotokea kama hii ya kwetu, exactly kama hii, na experience ya Afrika Kusini.

Sasa kama tungekuwa na tume ya ukweli, pande mbili zimeletwa pamoja, tumekubaliana tuunde tume, tuipe hadidu za rejea ambazo zinaenda kwanza kutuchunguza nani, nini chanzo? Nani waliosababisha? Nani walioamuru? Nani waliotekeleza?

Baada ya hapo tuchunguze waliotekwa, waliofanya nini, alafu sasa tuseme kama wanaomba msamaha, je, wakiomba msamaha, ule msamaha wa aina gani? Tuwape total amnesty au wengine wafungwe ili watu sujifunze? Au wengine washtakiwe?

Alafu baada ya hapo tunachunguza, wale waliopata madhara tunawasaidiaje? Pamoja na familia zao tunazisaidiaje?

Tatu, tunafanyaje haya mambo yasijirudie? Tunaunda vyombo gani? Tunabadili jeshi la polisi liwe la aina gani? Mimi nafuatiliwa na gari ambazo zina namba tofauti. Namba EQJ uki-Google unakuta hiyo namba iko kwenye trela la grader, wakati ni namba ambayo hiyo gari unajua kabisa imetoka polisi.

Sasa tunaundaje hivi vyombo vipya? Tunaandika katiba ya aina gani ili mambo haya ya uchaguzi yasije tena yakaleta mgogoro?

Hiyo ndio kitu tunachoweza kushiriki. Hicho! Kitu cha aina hiyo kinachokwenda kuleta ukweli, sio kitu kinachokwenda kuleta uongo. Sisi hatuko tayari kushiriki kwenye uongo.

Kama taratibu (procedures) zote zitafuatwa ambazo zitaweka mambo wazi, mambo ambayo tunaona yana mwanga mbele, yanakwenda kuwapata Watanzania katiba, yanakwenda kuondoa manyanyaso yote, yanakwenda kuwajibisha watu walioumiza watu, yanakwenda kulipa fidia watu ambao wamepata ili kufuta chuki... kwa sababu sasa hivi kuna chuki, tunatengeneza visasi.

Lakini kama tingetengeneza tume ya ukweli—kwanza ukweli, alafu huo ukweli ndio utuletee sasa upatanishi—hiyo tume ingeondoa chuki, ingeondoa hasira, mtu ingesema ni kweli babangu aliuawa, ni kweli ndugu yangu alipotea, ni kweli... lakini watu wamekiri, watu wameomba msamaha, na watu wamelipa fidia. Japo hatarudi, lakini sasa tunaweza kupumzika kwamba ndugu yetu ata damu yake iliyomwagika imeleta matunda kwenye nchi hii, hakuna mtu mwingine atapata hayo matatizo.

Hiyo tungeweza kushiriki."
 
maridhiano ya hiyari miongoni mwa waTanzania yatafanyika kwa wakati muafaka bila kujali misimamo ya waliopoteza uelekeo wa kisiasa nchini 🐒
Jizi na lipenda rushwa limetoa comments
 
Mwenyekiti wa Truth and Reconciliation Commission alikuwa Askofu Desmond Tutu na Makamu wake alikuwa Alex Boraine wote raia wa Afrika Kusini.

Amandla...
 
Mwenyekiti wa Truth and Reconciliation Commission alikuwa Askofu Desmond Tutu na Makamu wake alikuwa Alex Boraine wote raia wa Afrika Kusini.

Amandla...
Ufahamu wako ni mfinyu kuelewa mambo. Mhe. Heche ameshakuambia CCM hawaaminiki kutokana na past history, ndo maana wanataka msuluhishi wa kimataifa. Du! shule hizi za hapa na pale zinashida sana
 
Ufahamu wako ni mfinyu kuelewa mambo. Mhe. Heche ameshakuambia CCM hawaaminiki kutokana na past history, ndo maana wanataka msuluhishi wa kimataifa. Du! shule hizi za hapa na pale zinashida sana
Umejiunga mwaka jana halafu unapata ubavu wa kunitukana. Shida yenu ni kuwa mmeenda shule lakini hamjaelimika.
Heche alitumia mifano ya Kenya na Afrika Kusini katika kujenga hoja ya umuhimu wa kuwa na msuluhishi kutoka nje. Mimi nimesema hapakuwa na msuluhishi kutoka nje Afrika ya Kusini. Ungekuwa umeelimika ungenitajia msuluhishi kutoka nje aliye ongoza Truth and Reconciliation Commission ya Afrika Kusini. Mimi sikuzungumzia hitaji la kuwa na msuluhishi wa nje bali pungufu la kutumia Afrika Kusini katika kujenga hoja yake.

Stupid is as stupid does.

Amandla...
 
Mwenyekiti wa Truth and Reconciliation Commission alikuwa Askofu Desmond Tutu na Makamu wake alikuwa Alex Boraine wote raia wa Afrika Kusini.

Amandla...
Kumbe hata Dr. Bagonza alipaswa kuwa Mwenyekiti wa hiyo tume na si lazima kutuletea upumbavu kutoka Uganda siyo?
 
Mimi ninacho jua nikuwa SAMIA NA ABDUL WANAMILIKI VIKUNDI VYA MAUAJI VIKIWEMO VYA KIDINI
 
Back
Top Bottom