Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

Hili zee limekuwa litumwa fulani hivi.linataka na wengine wawe watumwa kama lenyewe. Jinga kabisa. Ni hivi watu atuwezi kuwa unavyotaka wewe. Ndiyo maana wengine mliwapiga risasi na kuwapoteza baada ya pesa kugonga mwamba.
 
Mkuu hapa umepotosha. Objectives za DA uchaguzi wa mwaka jana ilikuwa kuretain Western Cape na Kuishusha ANC chini ya 50% Gauteng na hilo walifanikiwa so si kweli Maimane alishindwa. Pia Kwa mara ya kwanza DA ilipata kura za watu weusi wengi kuliko wakati wowote ule kwenye historia ssa unaposema alifeli kuwavutia una maana gani? Kwa takwimu zipi?? Mkuu una credibility sana humu JF at least uwe unakuja na facts sio ushabiki.

Kuhusu Mbowe niseme tu ndio mwenyekiti pekee hapa TZ ambaye kila uchaguzi chama chake kinaongeza wingi wa wawakilishi ngazi zote na kura za urais kwahiyo hajafeli kama ulivyotaka kupotosha. CCM wao ndio wanaporomoka kila chaguzi from 88% to 62 to 56 sasa hapo nani failure??

Btw chaguzi za hao uliotaja ni huru na haki ndio maana mtu akishindwa anakubali matokeo ssa huku kwetu mnaharibu chaguzi kma Jecha ssa utasema kweli Maalim au Mbowe wameshindwa kwenye chaguzi?? Case study zako haziendani kabisa

Kiufupi mwanakijiji you are overrated!!
 
Kuna nyakati nyingine watu wawe na angalau aibu, wajisitiri ili wasionekane kwa misimamo yao kuwa wanawaona wenzao wanaosoma wanayoyawasilisha hawana akili kichwani.

Demokrasia hapa nchini ipo wapi ambayo unaweza kuilinganisha na hizo unazoziorodhesha hapo chini.

Hivi vyama vya upinzani vinaendelea kuwepo katika mazingira magumu sana, wewe hayo huyaoni kabisa; unafumba macho na wala kusikia husikii!

Kazi yako ni kulinganisha tu hivyo vyama na wenzao walioko kwenye mazingira tofauti kabisa?

Hakuna haja ya kuandika mengi kwenye mada kama hii.
 
Rubish, I head is too small for this.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wale wanaomjua wanasema jamaa ni mshamba fulani hivi, pamoja na kukaa marekani bado ule ushamba haujamtoka, hapo ujue ameshaingiziwa hela kwenye account yake na team ya akina bashite na tiss,.ndoo maana anatapiga minyoo tu, sasa si bora ungebaki bongo kama sisi, maana anaonekana ana njaa kuliko sisi tunaopigwa na juaa Kali la bongo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
"JokaKuu, post: 34429132, member: 221"]
Mkuu kabla ya kupitia hoja zako, nianze na ya Mzee Mwanakijiji. Sikubaliani na hoja ya Mbowe kujiuzulu kwa sababu zifuatazo
1. Hiwezekani Nahodha akatoboa chombo au kupoteza uelekeo halafu akapewa fursa ya kujitosa kwa kuogelea!

Mbowe anatakiwa aendelee na uongozi hadi pale chama kitakapozimia kama si kumfia mikononi.
MM anafahamu, wengine tulipiga kelele siku nyingi kwamba kunatatizo la uongozi ndani ya CDM

Kule Mabawa na Ngamiani Tangakuna kitu kinaitwa ''Limbwata''.Inasemekana ukikutana nacho huoni wala husikii. Kama kuna hicho kitu, Mbowe amefanikiwa kuwalisha mashabiki na Wapenzi wa CDM. Tuachie hapo
.
..kwasababu kuna wengine wanaamini tangu Mbowe amekuwa mwenyekiti chama kimekuwa kikikua kwa kuongeza idadi ya mashabiki, wanachama, na wabunge.
Kukukua kwa CDM kuna sababu
1. Uongozi wa Mtei, Marehemu Makani, Dr Slaa na Zitto waliojenga chama kama taasisi na kufuata misingi yake
2. Kufa kwa NCCR na kutokomea kwa CUF kuliwalazimu wanaoutaka upinzani kama mbadala kuhamia CDM
Mbowe alipokea chama kikiwa tayari kinakua na kina mizizi yake
..pia ubora na udhaifu wa Mbowe
unaupima vipi?
Ubora wake unahitaji muda kuupima.
Udhaifu wake ni kutofuata taratibu za chama, kutofikiria ushirikiano na wapinzani wenzake na kutaka kuhodhi chama. Hayo yanasababisha chama kiwe mtu lakini kubwa zaidi ni kukosa maono ya muda mfupi na mrefu
Unamlinganisha na wenyeviti waliopita wa CCM?
Haiwezekani kumlinganisha nao, udhaifu wa hao ndio unakuza upinzani. Kwa wenyewe wanasema ''blessing in disguise''
Au unamlinganisha na wenyeviti wa vyama mbalimbali vya upinzani nchini?
Hapana, udhaifu wa viongozi wengine ndiyo ilikuwa fursa kwake kuitumia
Au unajaribu kuona ni wapi angeweza kufika, lakini hakufika, kwa kuzingatia mazingira ya kisiasa na resouces at the disposal of his party?
Katiba mpya ni fyongo kubwa sana. Wakati wa JK CDM ilikuwa na nguvu ya umma haswa.

Mbowe alishangilia tangazo la katiba mpya, hakuona tatizo la katiba kutengenezwa na mwenyekiti wa CCM.

Udhaifu wa kushindwa kuongoza upinzani wakati ukiwa na nguvu ndiyo unawagharimu wapinzani sasa hivi.

Udhaifu wa pili ni kushindwa kutambua mbinu za kutwaa madaraka.
Mwaka 2015 Mbowe aliongoza kundi la ''gia'' za angani akitumaini EL atakuwa Rais.

Tulimweleza kuwa hakuna anayeweza kuwa Rais wa nchi hii chini ya katiba iliyopo na mazingira yaliyopo.

Mbowe alikuwa na fursa ya kutumia nguvu ya umma na mpasuko ndani ya CCM kupata Wabunge zaidi badala ya kuzunguka kumnadi mtu ambaye, kwanza, ilikuwa wazi ni dhaifu.

Pili, umaarufu wake ulijengwa na watu na sisi yeye mwenyewe.
Ndiyo maana wale 20 aliotaka kuondoka nao walipogoma, akabaki Mbowe na EL

Iwe walishinda au walishindwa, jibu moja ni sahihi, kwamba, hakukuwepo uwezekano CCM ikihodhi kila kitu.
Maalim iikuwaje? Jecha si alipata tumbo la kukata kisha kutibiwa TV Zenj.!

Kuna hoja ya kuongeza Wabunge wa Upinzani.

Swali la kujiuliza, Mbowe amekuwa kiongozi kwa muda gani?
Hiwezekani kiongozi kuongoza miaka 15 na kupata wabunge 50.
Hii ina maana itachukua miaka 40 ili kupata majority katika Bunge.

Hapana, kiongozi akishindwa kufikia lengo kwa muda fulani au chaguzi fulani anakaa pembeni.
Hilo halikutokea kwasababu moja, kwamba, hakuna Demokrasia ya kukosoa au kukosoana.

Kwa utaratibu ule wa pale Mlimani City na mauza uza yake, haiwezekani kuwa na mabadiliko yoyote chanya.
Kwa utaratibu wa katiba kutokuwa na ukomo na hilo kufanywa jando, hakuna mafanikio

Udhaifu mwingine ni maamuzi yanayotia shaka. Ile safari ya Kirumba ilikuwa bomu kwa kuanzia

Pamoja na ubomu wake Mbowe kama kionozi wa upinzani hakuwashirikisha wenzake kupata maoni yao.

Leo tunauliza Kirumba imetoa matokeo gani? Je, Mbowe ameweza peke yake bila wapinzani wenzake?

Je, yale ya Meya wa Jiji la DSM ndiyo aliyoenda kuyaomba? Na amefanya nini katika sakata hilo?

Nimalizie kwa kumtetea Mbowe, hapana, asijiuzulu! hiki ni ''kidali po alale nacho''

.
 
Duh... sasa unafikiria kiko wapi; peponi?
You talk of them because you fear them!

Mmejawa na ushauri hovyo, nadhani CDM katika uchaguzi walitaka waazimie kubadili uongozi walivyowaona ninyi wenye midomo mirefu mnawapangia wa kumchagua mkawaudhi.

Tangu lini adui akushauri na kukuchagulia safu ya uongozi hayo ndiyo mliyafanya kwa CUF mkadhani na CHADEMA ni vihiyo.

Mzee Mpumbavu ni hasara kwa jamii yake kwa hili hata mjukuu wako humshawishi.

Mnafiki sana we mzee na ni mnafiki kweli kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe ameonekana kuwa tishio kwao,so wamejaribu kila namna wameshindwa kumdhoofisha!Sasa wamekuja na hii,wanajaribu kuwahamasisha wanaCDM wamuone Mbowe hafai tena!Uzuri mbinu hii ishajulikana na nafurahi majibu wanayoyapata!
Ila jamaa wana roho ngumu,hawakati tamaa licha ya kuona hakuna anayewasikiliza zaidi ya kuwaona wapuuzi tu!
Wameivuruga CUF na sasa wamehamia kwa CDM!
 
Tatizo cdm hawaandai viongozi, na inakuwaje ukubwa wote huu wa chama hakuna viongozi walio andaliwa kushika hatamu?
Hilo nalo neno. Nadhani cdm inatakiwa iwaandalie vijana wa kuchukua hatamu za juu za uongozi e.g. Katibu mkuu wa sasa aliyelewa na cdm ni mfano mzuri wa hayo malezi.
 
Ni kweli Mbowe ajiuzulu chama kimemshinda kabisa. Hafai kuwa kiongozi. Haiwezekani kingozi mzima anashindwa kufanya usajili wa maana chamani zaidi anasajili mafisadi na specialist in failure na kuendekeza ukanda na ukabila Chamani.

Tulitegemea tutapata mabadiliko ndani ya Chadema lakini aa wapi hakuna mabadiliko

Chadema is the worst political part in Tanzania.
Sina chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikio la kufa zibuka usikie hii dawa. Mhe. Mbowe umeivuruga CHADEMA unadhani hawa wanaokulamba miguu hawajui kwamba umefeli! Hashaa wanajua ila wapo upande wako ili watoto wao waendelee kwenda chooni na ma sweetheart wao waendelee kuwakoga mashoga zao mtaani aidha kwa wao wanasubiri hatma iwahukumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pumba tupu! We aint buying shit!
Mwambie Julius Malema aachie ngazi kwenye chama chake kwanza.
Tatizo siyo Mbowe kama nyie wajinga mnavyotaka kuaminisha watu, tatizo ni vyombo vya dola na NEC-ccm.
 
Watu wanafikiria kuwapoteza watu kama Kitila, Mwigamba, ni jambo dogo... wengine tuna maslahi zaidi na CHADEMA kuliko watu wanavyofikiria. Tungeshindwa uchaguzi fair and square 2015 leo tungekuwa kwingine kabisa...
Mzee unateseka sana. Ulimponda Lowasa akiwa CHADEMA< karudi CCM Kimya. Hivyo hivyo kwa Sumaye & Co. Kwa nini unajifanya una uchungu sana na CHADEMA, wamekuomba uwahurumie?? Na kile kijarida chako cha CHECHE vipi cheche zimeisha??
 
Unaandika maneno mengi lkn yasiyo na mantiki yoyote. Hilo la kujiuzulu linakuwa na msingi kama watu mmeshindwa katika uchaguzi unaoandaliwa na kusimamiwa na tume huru ya uchaguzi.

Kushindwa huku tume yenyewe ikiwa ni ya yule mnayeshindana naye sasa huo ushindi una mantiki yoyote kweli hapo, si ni takataka tu hiyo.

Yanga anacheza na Simba kisha Yanga anachapwa 8-0 huku marefa wa mechi wakiwa Haji Manara, Mo Dewji na Zakaria Hans Pope na commissar Aden Rage.

Sasa huo ni ushindi kweli. Mleta mada hauna lolote kwani siku hizi umejiongeza kwenye ile orodha "Infamous" ya Wachumia Tumbo maanake hata reasoning ndogo tu hauna.
You've sunk too low.
 
Mzee Mwanakijiji nadhani unakuza fikra zako juu ya Aina ya siasa za Tanzania na kuona kuwa ni vizuri Mbowe akajiuzulu..... Kwanza hebu jaribu kuangalia haraka ni nani anayeweza kubeba na kusimama imara katika upinzani kama Mbowe. Lakini pia kwa mizania kutokuwa sawa dhidi ya viongozi wa vyama mbadala na wafuasi wao na pia kwa Aina ya siasa kwasasa na kwa faida ya taifa hili Mbowe ndiye anafaa kuwa kiongozi wa CHADEMA na upinzani kwa ujumla hapa Tanzania.
 

Tatizo la a Tanzania ni demokrasia sio vyama vya upinzani. Watanzania wenyewe wamelala na hili ndilo tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…