Msikilizeni Waziri mwenye Dhamana

Msikilizeni Waziri mwenye Dhamana

Kauli "Upo na mafundi na mafundi hawasemi hivyo" - inamaanisha maamuzi unayotoa si kwa uelewa wako bali kuna watu wako nyuma yako.

Kwanini wewe na mafundi wako mnafikiri kwamba hoja ikija na mantiki bila cheti, huwa haifai?
Yaani kama hata hili nalo hujui kuwa, wizara zote zinao wataalam ambao, ndiyo kwa taaluma zao hupika njia ya ufundi wa kupita na waziri ni msimamizi wa sera.... basi mjadala hoja yako bado ina safari ndeeefu
 
Jibu swali bwana wewe, una zunguka zunguka tuu😂😂😂

Wanaotekwa ni jamii ipi na wanaobakwa ni jamii gani na wewe ni Waziri wa ustawi wa jamii ipi.
Mbona uko kimyaa

Leo umeyakanyaga
Kwa kweli 🤣 you guys mtanivunja mbavu 🤣🙌
 
🤣🤣🤣 Mtamuua
Yeye ndiye anatuua kwasababu ameweka mpaka wa elimu katika kusikiliza hoja za watu.

Waziri aliyebeba dhamana hawezi kukejeli wananchi ambao hawajasoma kutoa yao ya moyoni.

Waziri aliyebeba dhamana ya wananchi wote waliosoma na ambao hawajasoma anasema hawezi sikiliza hoja za wanachi ambao hawana vyeti.
Huyu Waziri atawasikiliza kweli wananchi wasio na elimu wenye changamoto?

Sijajua wenzangu mnaona nini, ila mimi Ninaiona pride iliyojificha chini ya mwavuli wa dini.
 
Yaani kama hata hili nalo hujui kuwa, wizara zote zinao wataalam ambao, ndiyo kwa taaluma zao hupika njia ya ufundi wa kupita na waziri ni msimamizi wa sera.... basi mjadala hoja yako bado ina safari ndeeefu
Hii ni appeal to authority - kupendelea mamlaka badala ya mantiki ya hoja.

Kama kweli wataalam wapo na wanafanya kazi, kwa nini hoja ya mtu asiye na cheti iwe tishio hadi ihitaji kukejeliwa badala ya kujibiwa?​

Na utazimia kweli kama wewe kwa kuwa tu ni mwananchi unataka utoe ushauri wa kitaalam mfano hiyo sindano choma hapa, halafu ukiulizwa hapo kuna nini na nini unasema hujui ila unataka tu hoja yako izingatiwe tu, hapo si lazima ukaguzi wa yaliyomo kwenye hoja yako ufanyike. Ukifanyiwa ukaguzi unaanza ohhh mimi sitendewi haki. Ndiyo, katika hoja hiyo sahihi kabisa usitendewe haki. Edit hoja yako. Vinginevyo kaa nayo tu.
Kuwa kiongozi ni pamoja na kunyoosha maelezo crystal clear hata kama anayeelezwa ataendelea kubisha. Hiyo sasa itakuwa ni kwa manufaa yake binafsi...
 
Pumbavu wewe hujui kitu. Waziri ni binadamu na hapa pia tunamchangamsha siyo kila wakati afikirie kazi tu. Pia huyu ni waziri wa Jamii na Jamii yenyewe ndo hii. Hujui kitu nyamaza kilaza wewe. Yeye anajua huku anakutana na vichwa vyote na ana handle ndo sababu mpaka leo anakubalika na kupendwa sababu anapokea watu mbalimbali na wengine walipaswa kuwa milembe yeye ana deal nao. We umemwona analalamika? Au unaleta kiherehere chako na kujikomba?
Haya sasa baada ya kumshushia mwenzio matusi umefaidika na Nini?
 
Hii ni appeal to authority - kupendelea mamlaka badala ya mantiki ya hoja.

Kama kweli wataalam wapo na wanafanya kazi, kwa nini hoja ya mtu asiye na cheti iwe tishio hadi ihitaji kukejeliwa badala ya kujibiwa?​

Uelewa wako sasa. Darasa moja mwalimu mmoja matokeo ya mtihani kwenye topiki mmoja huwa tofauti tofauti. Hivyo hivyo na kwenye mijadala mbalimbali.
 
Hakuna kiongozi wa mtume aliyemaliza kila changamoto duniani. Mtume Yesu naye aliishi miaka yake akaondoka bado kijana hakumaliza changamoto na bado kuna waliomkataa alipokuwa akifanya kazi yake, ajabu hao hao wakamkubali baada ya kumaliza kazi na kuondoka.

Aidha, hata wizara kongwe na kubwa za miaka mingi bado hazijawahi kumaliza changamoto na zinaibuka mpya kila leo, itakuwa wizara ya maendeleo ya jamii yenye umri wa miaka 3 na miezi 6.

Tulichofanya tumefanya, ya kuanzisha tumeanzisha, yaliyobakia yataendelezwa kwa kuwa, kazi ya ujenzi wa Taifa haijaisha. Na katika mafanikio hayo yaliyopatikana mfano hapa kwenye bango chini👇, hatuna budi kumshukuru Mungu na kwa shukrani hizo kwa imani yangu mimi, naimba🤗🥰 na wewe ikikupendeza shukuru kwa imani yako na isipokupendeza basi, potezea.

Hii ni kwa kifupi tafadhali....
View attachment 3407353
Kigezo kikuu cha mwanamke yoyote kukosa akili ni kushindana na wanaume...ukiona tu mwanamke anashindana na uwanaume tambua huyo mwanamke ni mpumbavu hata kama ni mama mzazi...hii ni kanuni ya kilimwengu.

MWANAMKE MPUMBAVU UVUNJA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE.
 
Attachments

  • AQNL9KwvgNwOGe3X7iWw35pDYtTgm3PmnnSAtZlH282vFEEJ_TPg63tAkGfJAtwjxiJiImeK_MRsNkKaZyISS6Q3J_m1zj...mp4
    1.1 MB
Na utazimia kweli kama wewe kwa kuwa tu ni mwananchi unataka utoe ushauri wa kitaalam mfano hiyo sindano choma hapa, halafu ukiulizwa hapo kuna nini na nini unasema hujui ila unataka tu hoja yako izingatiwe tu, hapo si lazima ukaguzi wa yaliyomo kwenye hoja yako ufanyike. Ukifanyiwa ukaguzi unaanza ohhh mimi sitendewi haki. Ndiyo, katika hoja hiyo sahihi kabisa usitendewe haki. Edit hoja yako. Vinginevyo kaa nayo tu.
Kuwa kiongozi ni pamoja na kunyoosha maelezo crystal clear hata kama anayeelezwa ataendelea kubisha. Hiyo ni kwa manufaa yake sasa...
Sawa Ahsante kwa ushauri!!

Lakini Kiongozi anayeshindwa kujibu hoja bila kutafuta mafundi nyuma yake huyo ni msemaji na siyo msimamizi.
 
Yeye ndiye anatuua kwasababu ameweka mpaka wa elimu katika kusikiliza hoja za watu.

Waziri aliyebeba dhamana hawezi kukejeli wananchi ambao hawajasoma kutoa yao ya moyoni.

Waziri aliyebeba dhamana ya wananchi wote waliosoma na ambao hawajasoma anasema hawezi sikiliza hoja za wanachi ambao hawana vyeti.
Huyu Waziri atawasikiliza kweli wananchi wasio na elimu wenye changamoto?

Sijajua wenzangu mnaona nini, ila mimi Ninaiona pride iliyojificha chini ya mwavuli wa dini.
Anasema kutoa maoni au kumshauri ni Mpaka uwe na cheti Cha ustawi wa jamii 🤣🤣🙌

Ila hii nchi 🙌
 
Uelewa wako sasa. Darasa moja mwalimu mmoja matokeo ya mtihani kwenye topiki mmoja huwa tofauti tofauti. Hivyo hivyo na kwenye mijadala mbalimbali.
Sahihi uelewa unatofautiana.

Kama uelewa unapotofautiana ndiyo sababu hoja za watu wa kawaida zipuuzwe, basi hatuhitaji uongozi – tunahitaji wataalam wa kujibizana wenyewe.
 
Hakuna kiongozi wa mtume aliyemaliza kila changamoto duniani. Mtume Yesu naye aliishi miaka yake akaondoka bado kijana hakumaliza changamoto na bado kuna waliomkataa alipokuwa akifanya kazi yake, ajabu hao hao wakamkubali baada ya kumaliza kazi na kuondoka.

Aidha, hata wizara kongwe na kubwa za miaka mingi bado hazijawahi kumaliza changamoto na zinaibuka mpya kila leo, itakuwa wizara ya maendeleo ya jamii yenye umri wa miaka 3 na miezi 6.

Tulichofanya tumefanya, ya kuanzisha tumeanzisha, yaliyobakia yataendelezwa kwa kuwa, kazi ya ujenzi wa Taifa haijaisha. Na katika mafanikio hayo yaliyopatikana mfano hapa kwenye bango chini👇, hatuna budi kumshukuru Mungu na kwa shukrani hizo kwa imani yangu mimi, naimba🤗🥰 na wewe ikikupendeza shukuru kwa imani yako na isipokupendeza basi, potezea.

Hii ni kwa kifupi tafadhali....
View attachment 3407353
Binafsi nachokiona matatizo hayatokei from from nowhere bali makosa uzembe wa leo ndio unasababisha shida za kesho, and on that token kuna bomu fulani ambalo litawatafuta awamu za kesho ila ukweli ni mbegu mlizopanda nyie kwa kutokushughulikia hii michicha kabla haijawa mibuyu..., nilishauliza na sitachoka kuuliza (as my civic duty) na suala hili linahitaji ushirikiano wa nyie wote sio kwamba hii ni Wizara yangu basi nifanye yangu pekee... (Nadhani hayo ya Mungu / Imani, Tuyaache kwenye Imani au tuyahifadhi tukiwa kwenye nyumba za Ibada hapa tudeal na ya Kaisari )

Kigezo kikuu cha mwanamke yeyete kukosa akili ni kushindana na wanaume...ukiona tu mwanamke anashindana na uwanaume tambua huyo mwanamke ni mpumbavu hata kama ni mama mzazi...hii ni kanuni ya kilimwengu
Kwa uelewa wako sasa wa yaliyomo ulimwenguni ni sahihi. Ila kwa uelewa wa wengine siyo sahihi. Sasa vema kila mmoja aendelee kunufaika na uelewa wake ili mradi mwisho wa siku atapima mwenyewe je, unampa faida au hasara. Nakutakia asubuhi njeeema kabisa na baraka...
 
Sahihi uelewa unatofautiana.

Kama uelewa unapotofautiana ndiyo sababu hoja za watu wa kawaida zipuuzwe, basi hatuhitaji uongozi – tunahitaji wataalam wa kujibizana wenyewe.
Sasa ili kuthibitisha usahihi wa hoja inayoshikiliwa na mtu kwa madai kuwa yuko sahihi, si inabidi uombe ma CV yake? Kwani kuomba CV kosa? Mbona siku hizi ukiitwa kwenye mikutano mbalimbali kushiriki mijadala unaombwa na CV? Huwa za nini? Dunia ya mijadala imebadilika. Tubadilike, vinginevyo tutakuwa tunaanzisha ligi za chuki chuki tu na personalities kwenye mijadala kumbe uelewa wetu tu. Ndiyo maana wengi wanaamua kutokuwa na akaunti, ila mimi nipo hadi mwisho na tutaenda hivi hivi hadi tuelewane.
 
Jibu swali bwana wewe, una zunguka zunguka tuu😂😂😂

Wanaotekwa ni jamii ipi na wanaobakwa ni jamii gani na wewe ni Waziri wa ustawi wa jamii ipi.
Mbona uko kimyaa

Leo umeyakanyaga
Anaogopa kuambiwa anagwajimanize chama.
 
Sawa Ahsante kwa ushauri!!

Lakini Kiongozi anayeshindwa kujibu hoja bila kutafuta mafundi nyuma yake huyo ni msemaji na siyo msimamizi.
Na mimi bahati mbaya siyo msimamizi bali, mtunga sera. Usimamizi uko huko Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Kwa kawaida, kuingia kwenye mjadala, huwa kunahitaji mtoa hoja ujiandae na mawanda ya hoja yako. Siku ingine, jiandae vema zaidi vinginevyo na wewe unakuwa mtia stori tu mchana ufike jioni ije iwe siku mpya.
 
Yaani kama hata hili nalo hujui kuwa, wizara zote zinao wataalam ambao, ndiyo kwa taaluma zao hupika njia ya ufundi wa kupita na waziri ni msimamizi wa sera.... basi mjadala hoja yako bado ina safari ndeeefu
Kwa hiyvyo sisi tusio na elimu plus wabunge kina Msukuma na Babu Tale hatua cha kukushauri mweshimiwa
 
Sahihi uelewa unatofautiana.

Kama uelewa unapotofautiana ndiyo sababu hoja za watu wa kawaida zipuuzwe, basi hatuhitaji uongozi – tunahitaji wataalam wa kujibizana wenyewe.
Nenda sasa jukwaa la wataalamu. Ni kazi ya mtoa hoja au mshiriki wa mjadala kujua, anashiriki mjadala gani na nani ba hapo ndiyo umuhimu wa kuulizana CV sasa duniani kote. Maana mnaweza kupishana content kwa kuwa, hamjuani nani mwenzangu.
 
Kwa hiyvyo sisi tusio na elimu plus wabunge kina Msukuma na Babu Tale hatua cha kukushauri mweshimiwa
Kila mtu analo la kushauri kwa kuzingatia kona ya hoja na anachotaka kushauri ili mradi, ushauri unaenda sambamba na kona ya hoja. Mtoa hoja wa leo alikuja na kona ya kutaka niijue tafsiri ya ustawi wa jamii na jamii kwa ujumla kwa mujibu wa majukumu yangu. Sasa kasahau kuwa, tasfiri za mambo mbalimbali husajiliwa kitaalam na ni taaluma, anataka tu nielewe anavyoelewa yeye nifute tafsiri iliyosajiliwa na mabaraza ya kitaaluma. Sasa na mimi si nikamuomba CV? Sasa hapo kosa liko wapi kama si nia hapa ya wengine ni kunogesha mjadala tu😃
Haya unoge sasa tusukume siku iende ije mpya.
 
Uliwahi kuingia ukurasa wa wizara ya habari, Utamaduni, Sanaa na michezo ukatoa maoni? Maana huko ndiyo kuna dhamana ya hayo yote. Naona changamoto ya wengi kujua wapi maoni yake yaende kwa usahihi zaidi
Ahaa, kumbe hii Serikali huwa inasikiliza maoni ya wananchi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom