Matukio ya wanawake kuingiliwa kimwili na mbwa hapa Tanzania yamekuwa yakiripotiwa na vyombo vya habari kwa nyakati tofautitofauti. Kwangu mimi tukio lilitokea huko mgodini Shinyanga ni la tatu kulisikia. Inawezekana kuna mengine mengi ambayo hayaripotiwi.
Wiki iliyopita kulitokea tukio baya kwenye mgodi mmojawapo huko Shinyanga. Mtoto wa kike na anayesoma shule ya msingi aliingiliwa kimwili na mbwa wa mwekezaji mgodini hapo. Inasemekana walinzi, ambao ni Watanzania, walihusika kufanikisha kitendo hicho kiovu na inasemekana wameshafikishwa kwenye vyombo vya usalama (kulingana na Radio Wapo FM kwenye kipindi chake cha Pata Pata (leo 16-04-2008) kinachorushwa kila siku asubuhi kuanzia saa 1:15). Kibaya zaidi madaktari wamesema mtoto huyo ameharibiwa vibaya na imeshindikana kutibiwa hapa nchini na hivyo inabidi apelekwe kutibiwa nje ya nchi.
Kwa nini watu wenye akili timamu na wenye dada au watoto wa kike (au hata kama wao hawana watoto wa aina hiyo) wawe na tabia ya kiovu hivyo? Hivi inamfurahishaje mtu kuona mbwa anamwingilia kimwili mtoto wa mwenzake na yeye akishuhudia kitendo hicho kiovu?
Kwa kweli nasikitika sana na nadhani ipo haja ya kutunga sheria na kuielimisha jamii kuhusu kupiga vita udharirishaji wa kijinsia na hasa kuwadharirisha wanawake au watoto wa kike. Lazima tufike mahali tuwe na uelewa na elimu nzuri na maadili mema. Ujanjaujanja wa kijingakijinga na usio na maana kwetu sisi na kwa taifa letu tuondokane nao.
Mbali na tukio hili, tukio la kwanza kulisikia lilitokea hapa nchini (nadhani Dar es Salaam) mwaka 1986 (kama sichanganyi na 1976). Tukio hilo lilipotiwa kwamba wazungu fulani waliwapa akina dada wawili (nadhani) pesa na hao akina dada wakakubali kuingiliwa kimwili na mbwa waliokuwa wa hao wazungu. Nakumbuka wakati ule kulizuka aina fulani ya fedheha kwa wanawake, watu wakishtumu kwa nini dada zetu wajirahisishe kwa kiasi hicho.
Tukio lingine lilitokea miaka ya 1990 (kama siyo miaka ya 2000). Tukio hilo lilitokea Dar es Salaam. Vyombo vya habari vilihabarisha kuwa wazungu fulani walikuwa wakinywa pombe baa na msichana mmoja. Baada ya kuona kuwa amelewa waliondoka naye na yeye na kumfanya aingiliwe kimwili na mbwa wao, kitendo ambacho kilidharirisha kwa kiwango kikubwa utu wake. Ilisikika kuwa watu hao walipewa notice ya masaa 24 wawe wameshaondoka nchini.
Binadamu wote ni sawa!