Msichana aliyeingiliwa na mbwa Shinyanga ameharibiwa

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,420
2,337
Matukio ya wanawake kuingiliwa kimwili na mbwa hapa Tanzania yamekuwa yakiripotiwa na vyombo vya habari kwa nyakati tofautitofauti. Kwangu mimi tukio lilitokea huko mgodini Shinyanga ni la tatu kulisikia. Inawezekana kuna mengine mengi ambayo hayaripotiwi.

Wiki iliyopita kulitokea tukio baya kwenye mgodi mmojawapo huko Shinyanga. Mtoto wa kike na anayesoma shule ya msingi aliingiliwa kimwili na mbwa wa mwekezaji mgodini hapo. Inasemekana walinzi, ambao ni Watanzania, walihusika kufanikisha kitendo hicho kiovu na inasemekana wameshafikishwa kwenye vyombo vya usalama (kulingana na Radio Wapo FM kwenye kipindi chake cha Pata Pata (leo 16-04-2008) kinachorushwa kila siku asubuhi kuanzia saa 1:15). Kibaya zaidi madaktari wamesema mtoto huyo ameharibiwa vibaya na imeshindikana kutibiwa hapa nchini na hivyo inabidi apelekwe kutibiwa nje ya nchi.

Kwa nini watu wenye akili timamu na wenye dada au watoto wa kike (au hata kama wao hawana watoto wa aina hiyo) wawe na tabia ya kiovu hivyo? Hivi inamfurahishaje mtu kuona mbwa anamwingilia kimwili mtoto wa mwenzake na yeye akishuhudia kitendo hicho kiovu?

Kwa kweli nasikitika sana na nadhani ipo haja ya kutunga sheria na kuielimisha jamii kuhusu kupiga vita udharirishaji wa kijinsia na hasa kuwadharirisha wanawake au watoto wa kike. Lazima tufike mahali tuwe na uelewa na elimu nzuri na maadili mema. Ujanjaujanja wa kijingakijinga na usio na maana kwetu sisi na kwa taifa letu tuondokane nao.

Mbali na tukio hili, tukio la kwanza kulisikia lilitokea hapa nchini (nadhani Dar es Salaam) mwaka 1986 (kama sichanganyi na 1976). Tukio hilo lilipotiwa kwamba wazungu fulani waliwapa akina dada wawili (nadhani) pesa na hao akina dada wakakubali kuingiliwa kimwili na mbwa waliokuwa wa hao wazungu. Nakumbuka wakati ule kulizuka aina fulani ya fedheha kwa wanawake, watu wakishtumu kwa nini dada zetu wajirahisishe kwa kiasi hicho.

Tukio lingine lilitokea miaka ya 1990 (kama siyo miaka ya 2000). Tukio hilo lilitokea Dar es Salaam. Vyombo vya habari vilihabarisha kuwa wazungu fulani walikuwa wakinywa pombe baa na msichana mmoja. Baada ya kuona kuwa amelewa waliondoka naye na yeye na kumfanya aingiliwe kimwili na mbwa wao, kitendo ambacho kilidharirisha kwa kiwango kikubwa utu wake. Ilisikika kuwa watu hao walipewa notice ya masaa 24 wawe wameshaondoka nchini.

Binadamu wote ni sawa!
 
Hawa ndio wawekezaji wetu, ambao hata huko kwao hawana uwezo wa kupata kazi huku kwetu ni waheshimiwa.

Naomba wananchi tuseme hapana... hapana.. Hii thread naomaba uendelee kutupasha nini kinajiri.

Naomba mwenyezi mungu atujalie subira ili jambo hili lifanyiwe kazi.
 
Watu wanamuona Mugabe mbaya lakini hii rangi nyeupe hii sio kitu ya kuithamini ni watu wabinafsi wasiojali maadili ingawa wao ndio wanaojiona wenye maadili zaidi na ya kuwa wametufundisha sisi waafrika hayo maadili kupitia white collar education lakini si kweli sisi tuna maadili ya kwetu, tamaduni zetu ambazo ni bora kuliko hizo zao. Walitufanya watumwa, wakatutawala, wanajifanya wawekezaji na bado wanamnyanyasa huyo mzawa asiye na hatia. Kuna msemo ambao niliwahi kuisikia ilikuwa ni hadithi ya mti na mwanae ambapo mti analalamika kuwa anakatwa bila kuthaminiwa anatumika katika maisha ya kila siku . Siku moja akaja mtu na shoka akitaka kumkata na shoka hilo mpini wake umetengenezwa kwa mti Mti akamuuliza yule mti mwenzake ambaye ni mpini wa shoka " hata wewe leo unakuja kuniua mimi?" Watu hawa ndio wanaopambwa na viongozi wetu kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa wamejenga zahanati, shule za msingi ambazo hata miminaweza kukiri shule hizo hazifikiii hata robo ya punje ya shule alizojenga MKONO. Sasa wananchi ndio miti inayokatwa kila kukicha, shoka ni mwekezaji na hao wanaojiita akina Sinclair na Mpini ndio hao viongozi wetu.
 
wangewakamata wote si watanzania peke .. hata hao wawekezaji pia .. kwanini msumeno ukate upande mmoja .. wa Tz walikuwa wakitekeleza amri ya bosi wao, leo iweje wawajibishwe hao tu.

Hakika watu kama hao hata wahukumiwe kunyongwa ni sawa tu
 
Hao mmbwa inakuwa wanao uzoefu wamefundishwa kuingilia watu, hivyo mwenye mbwa lazima akamatwe, afunguliwe mashtaka na kufungw amiaka yote aliyobakiza duniani.
Mbwa ahamie polisi.

Mungu akujalie mtoto upone, na urudie uzuri wako mungu aliokuumba nao.
 
Hao mmbwa inakuwa wanao uzoefu wamefundishwa kuingilia watu, hivyo mwenye mbwa lazima akamatwe, afunguliwe mashtaka na kufungw amiaka yote aliyobakiza duniani.
Mbwa ahamie polisi.

Mungu akujalie mtoto upone, na urudie uzuri wako mungu aliokuumba nao.

kweli kabisa hawa mbwa wamefundishwa na binadamu kufanya hivyo na watakua niwenye mbwa hivyo wanapaswa kufunguliwa mashitaka wenye mbwa na walinzi wote kwani wanajua uovu huu na huyu atakua sio mtoto wa kwanza kufanyiwa hivi, hao walinzi wakibanwa watasema ukweli wote.
 
wangewakamata wote si watanzania peke .. hata hao wawekezaji pia .. kwanini msumeno ukate upande mmoja .. wa Tz walikuwa wakitekeleza amri ya bosi wao, leo iweje wawajibishwe hao tu.

Hakika watu kama hao hata wahukumiwe kunyongwa ni sawa tu
Naimaomari
Waswahili wenzio ndio walikuwepo eneo la tukio ndio maana wamekamatwa wao.Wazungu hawakuwepo.
Tatizo ni letu,sisi kama waswahili kwani TUMEKUWA FACILITATORS KWENYE MAMBO MENGI,hao wamemtoa sadaka mswahili mwenzao(mtoto wao).
LAKINI VIONGOZI WETU WANATUTOA SADAKA(WANASIMAMIA) SISI KAMA TAIFA " KUINGILIWA NA MBWA "
 
Huu ulikuwa unyama wa hali ya juu!na hadi leo ni kimya sijui nini kiliendelea!
 
Naimaomari
Waswahili wenzio ndio walikuwepo eneo la tukio ndio maana wamekamatwa wao.Wazungu hawakuwepo.
Tatizo ni letu,sisi kama waswahili kwani TUMEKUWA FACILITATORS KWENYE MAMBO MENGI,hao wamemtoa sadaka mswahili mwenzao(mtoto wao).
LAKINI VIONGOZI WETU WANATUTOA SADAKA(WANASIMAMIA) SISI KAMA TAIFA " KUINGILIWA NA MBWA "

am on the verge of tears ... kweli ndugu yangu
 
Yawezekana ujinga wa watanzania wenzetu wanaotumwa na hiyo mizungu kufanya mambo ya kishenzi ndio wanaochangia kutekeleza huu uchafu may be ni njaa kwa kuahidiwa kitu fulani au ndio ujinga wa kila kitu "ndio mzee". Kwani hao walinzi kama wangekuwa watu makini na wenye utu wangekuwa wa kwanza jaribio la kumfanyia huyo binti hicho kitendo....

Nina wasi wasi na vyombo vyetu vya sheria kama kweli vitachukua hatua zinazostahili kwa watuhumiwa wote vinginevyo linaweza kuishia hewani wakati binti ameshapata kilema.....
 
Jamani hii mbona imewekwa kwenye entertainment? Kuna hata chembe ya entertainment kwenye hii article? Hebu iwekeni inapostahili kuwekwa.
 
Jamani mbona inasikitisha? Watanzania tumekuwa wakatili kiasi hiki? Je hao walinzi waliamrishwa na boss wao kumpatia mbwa starehe hiyo au walijiamulia? Waadhibiwe haraka ingekuwa mimi ningelipa the same
 
Kwani Hii Imefikia Wapi Nakumbuka Ilifika Mahakamani.........na Wale Wazungu Wanatakiwa Washitakiwe Haraka Sana Sanaa............
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom