Mshale wa Helen Kejo Bisimba kwa Magufuli

Mshale wa Helen Kejo Bisimba kwa Magufuli

Bisimba apewe tu uongozi huko Chadema tujue moja badala kujificha LHRC kufanya siasa
 
Mkuu lets be honesty, nani asiyejisikia fahari na kujisifia akiwa ametekeleza vema wajibu wake kama kiongozi wa familia? Wajibu kama umewasomesha watoto vizuri, umewapa huduma bora ya mavazi na tiba ktk hospital nzuri n.k.? Tuwe wakweli huku mitaani wengi tunajisifia wengi tu, hasa kama waliokutangilia ktk familia au waliokuzunguka wana/wame shindwa?
Kujisifia tunajisiafia baada ya kua umetenda umekamilisha vyoote,kama ulivyosema umeshawasomesha watoto wako vizuri sasa we unataka kila unachofanya uwe unasifiwa asiyekusifu basi ni adui,wakati wa kufanya we fanya ila sifa isiwe kitu cha kutafutwa kwa nguvu ama kigezo cha utendaji wako bali iwe ni matunda ya utendaji wako uliotukuka mwishoni. Otherwise utawaumiza na kuwakashifu wengi wasiokusifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ccm ilitakiwa ipumzishwe kabla hata hatujapata uhuru! Hiki chama ni laana kwa waTz
 
MFANO:
Sisi binaadam tunapaswa kusaidiana. Mwenzio akiwa hatarini ni jukumu lako kumsaidia.

Sasa fikiria bi kizee anavuka barabara na mkongojo wake. Alipofika katikati ya barabara kukawa na fuso (lori) linaporomoka kwa kasi sana. Wewe kuona ajali inayomkabili yule bibi ukamkimbilia, ukamnyanyua na kumtoa barabarani. Ile mguu wako wa mwisho tu unatoka barabarani na fuso nalo linapita kwa kasi ile ile. Umejitolea kumuokoa huyu bi kizee.

Bi kizee ana mambo matatu ya kufanya:

1. Kukaa kimya
2. Kukushukuru kwa kumuokoa
3. Kusema kuwa ule ulikuwa ni wajibu wako, kama binaadam, kumuokoa na hustahili pongezi.

Unafikiri bi kizee anapaswa kufanya kipi katika hivi vitu vitatu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kusaidiana sio wajibu ni mapenzi na mtu husika na roho yake,hivyo bibi kizee ndio ana wajibu wa kumshukuru aliyemsaidia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hasimamii kwa kukataza rushwa hayo maji mtayapata wapi? Umesema mwenyewe ni wajibu wa serikali, hujiulizi mbona miradi haikukamilika mpaka sasa na serikali ikiwepo? Mnachosahau kuwa serikali ni chombo kikubwa kinachojumuisha watu wenue bongo tofauti na kwamba serikali si chama cha siasa pekee. Wezi si wanasiasa tu bali hata watendaji wa serikali na wengine wako vyama pinzani. Yes, kasimamia vyema na watu wameogopa kupiga ni lazima apewe sifa. Nadhani ushanisoma.

Havome
Magu is part and parcel of the scam can't qualify for any credit.
 
Chama hakileti maendeleo bali kinatunga ilani na sera za maendeleo.

Rais alieko madarakani ndie anaeamua ni miradi gani ya maendeleo ipewe kipaumbele. Kwa hiyo chochote kinachofanywa na serikali ni juhudi za kiongozi wake (Rais). Miradi ikifanikiwa sifa zinakwenda kwa Rais. Miradi ikikwama lawama zinakwenda kwa Rais.

Watu wasikomalie kumshutumu Rais na chama chake kwa mabaya tu, bali wawe tayari kumshukuru kwa yale mazuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mazuri yapi hayo we punguani?! Au unazungumiza kuwapima mkojo wanaomkosoa
 
Raisi kufanya kazi yake sawasawa ni wajibu wake wala sio favour anatufanyia au huruma.Kwanza WaTanzania wanasahau kuwa mshahara wa raisi na kila kitu anachotumia ni pesa zao na wala hatumsimangi.
 
"To seek accolades from the great and ignorant public is the vice of a fool" (Saving Faith; by David Baldacci).
 
JF Kwenu,

Akiwa Kigoma, Mh. Rais Magufuli aliongea maneno mengi ya kufurahisha wananchi wakati akizindua mradi wa barabara na maji.
Maneno ya Mama Bisimba kwa Rais Magufuli yanafikirisha, "Wananchi kwa kutoelewa wanaamini serikali inawapendelea kwa kuwapa maji na barabara, bila kujua huo ndiyo wajibu wa serikali iliyo madarakani na maji hayo yalipaswa kuwepo tangu mwaka 1961 tulipoanza kujitawala. Halafu mtu anatumia hiyo kama ngao ya kuwa ni mtendaji kuliko vyama vya upinzani ambavyo huo si wajibu wake hata kidogo".

Kwa tabia yake, Magufuli anaweza kuishiwa uvumilivu akajibu mapigo. Tusubiri wakati tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mama ni punguani tu.

Hapendi anayoyafanya rais?

Yeye anawatumikia vipi Watanzania zaidi ya huo ufataani alo nao?
 
Mkuu Nyangomboli heshima yako. Naona unadadavua vilivyo. Kama yalitakiwa kuwepo 1961 mbona hayakuja hadi leo ndio yanakuja. Kuna wengine wameisimamia serikali miaka 10 mfululizo na hawakufanya hayo matokeo yake wamekimbilia kujificha upinzani wakiwaongopea wananchi.

Hapo unamsema JK au Mkapa au Mwinyi? Umeniacha. Hivi mradi wa maji Kigoma ni mkopo kutoka Exim ya Uchina? Au South Korea? Au ni pesa za ndani za serikali? Pengine Zitto analipwa fadhila kwa kazi nzuri aliyoifanya na anayoendelea kuifanya ya kudhoofisha upinzani nchini.
 
Huyo mama ni punguani tu.

Hapendi anayoyafanya rais?

Yeye anawatumikia vipi Watanzania zaidi ya huo ufataani alo nao?

Hajasema hapendi anayofanya Rais. Ameonesha tu dhana potofu (misconception) na jinsi kiongozi wa kisiasa, kwa makusudi au kwa kutokujua, anatumia dhana hiyo potofu kujijenga kisiasa au kudanganya wananchi. Wito wa Helen Bisimba kwa wapiga kura ni kwamba ni jukumu na wajibu la serikali kuhakikisha huduma za maji, barabara etc. ni za uhakika wakati wote. Si hisani. Si upendeleo. Kama Rais (na wewe) anaamini kuwa huduma za maji, barabara etc. ni upendeleo kwa wananchi walioko kwenye baadhi ya maeneo, then, by definition, he is leading a patrimonial/neo-patrimonial state (i.e. patrons use state resources in order to secure the loyalty of clients in the general population).
 
Ndugu zangu tunachotakiwa kuwa nacho ni katiba mjpya.
Tunafurahi kuwa na Raisi Magufuli lakini akiondoka akaingia mwingine itakuwaje.
Tunayakiwa tuwe nà mfumo wa utawala utakao simikwa na katiba nzuri.
Katiba ambayo haimfanyi raisi kufanya analota bila kuohojiwa na inayo mnyima kinga akifanya makosa
Katiba inayo ruhusu demokrasia ili wananchi wapime uwezo wa serikali na wafanye maamuzi kupitia sanduku la kura. Wengine endeleza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Nyangomboli heshima yako. Naona unadadavua vilivyo. Kama yalitakiwa kuwepo 1961 mbona hayakuja hadi leo ndio yanakuja. Kuna wengine wameisimamia serikali miaka 10 mfululizo na hawakufanya hayo matokeo yake wamekimbilia kujificha upinzani wakiwaongopea wananchi.
Ndg mbona zzk aliandika juzi kwamba hakuna mradi kanda ya magharibi iliyojengwa na serikali hii bali in mbwembwe za uzinduaji tu! Sasa kama anazindua tu si ina maana vimejengwa enzi za Vasco dagama? Ukweli ni kwamba vyote hivyo ni wajibu wa serikali na si vya kujisifu navyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hasimamii kwa kukataza rushwa hayo maji mtayapata wapi? Umesema mwenyewe ni wajibu wa serikali, hujiulizi mbona miradi haikukamilika mpaka sasa na serikali ikiwepo? Mnachosahau kuwa serikali ni chombo kikubwa kinachojumuisha watu wenue bongo tofauti na kwamba serikali si chama cha siasa pekee. Wezi si wanasiasa tu bali hata watendaji wa serikali na wengine wako vyama pinzani. Yes, kasimamia vyema na watu wameogopa kupiga ni lazima apewe sifa. Nadhani ushanisoma.

Havome
Hujaelewa muktadha wa hoja ya Bisimba. Hebu tusaidie, mtukufu Rais yuko sahihi kuzindua mradi huku akiwaambia wananchi wa jimbo fulani kuwa walikosea kuchagua mbunge wa upinzani na kuhusisha uamuzi wao na kuchelewa au kutotimizwa kabisa kwa miradi ya maendeleo ambayo kimsingi inapaswa kutimizwa na serikali na sio mbunge?
 
Back
Top Bottom