JF Kwenu,
Akiwa Kigoma, Mh. Rais Magufuli aliongea maneno mengi ya kufurahisha wananchi wakati akizindua mradi wa barabara na maji.
Maneno ya Mama Bisimba kwa Rais Magufuli yanafikirisha, "Wananchi kwa kutoelewa wanaamini serikali inawapendelea kwa kuwapa maji na barabara, bila kujua huo ndiyo wajibu wa serikali iliyo madarakani na maji hayo yalipaswa kuwepo tangu mwaka 1961 tulipoanza kujitawala. Halafu mtu anatumia hiyo kama ngao ya kuwa ni mtendaji kuliko vyama vya upinzani ambavyo huo si wajibu wake hata kidogo".
Kwa tabia yake, Magufuli anaweza kuishiwa uvumilivu akajibu mapigo. Tusubiri wakati tu.
Sijamsikia wala kusoma alichokisema Hellen Bisimba ila tuchukulie alichoandika mleta mada ndicho alichosema huyo Hellen,hoja hii ndiyo sehemu ya kazi ya NGO yake? atakapotuhumiwa kuwa kuna watu wanamtumia atajibu nini.Watetezi wataibuka utawala wa kidikteta.Bisimba na wenziwe wanataka binti zetu wapate mimba halafu waendelee na shule.JPM kawaruhusu waanzishe shule kwa fedha za wafadhili zao wawasomeshe hao wanaokataliwa katika shule za Serikali.
Mtetezi mzuri wa haki za binadamu huyafanya kwa vitendo anayoyatetea.Ingekuwa vizuri Hellen na wanaofanana naye wakajenga shule nzuri kuliko za serikali,wakaajiri walimu wenye sifa wawalipe vizuri zaidi ya waliopo serikalini ili matokea ya shule hizo yashindane na Fedha,St Marian na zinazofanana na hizo ili matendo yao yazungumze kuliko maneno yao na serikali ijifunze kwao.
Sent using
Jamii Forums mobile app