Mshale wa Helen Kejo Bisimba kwa Magufuli

hiyo miradi inayozinduliwa sasa michakato yake na kuanza kwake ni awamu ya nne au ya tano?
 
Mkuu Nyangomboli heshima yako. Naona unadadavua vilivyo. Kama yalitakiwa kuwepo 1961 mbona hayakuja hadi leo ndio yanakuja. Kuna wengine wameisimamia serikali miaka 10 mfululizo na hawakufanya hayo matokeo yake wamekimbilia kujificha upinzani wakiwaongopea wananchi.
Kumbe na wewe akili umepangishwa?! Kutokuwepo miaka hiyo siyo kwa sababu wengine walishindwa kusimamia bali ni kwa sababu rasilimali fedha na watu vilikuwa havitoshi!! Ndiyo sababu miradi ya maendeleo imekuwa ikijengwa kila wakati kadri fedha zinavyopatikana ama kwa kukopa au kwa vyanzo vya ndani!!
 
Huyu mama
JF Kwenu,

Akiwa Kigoma, Mh. Rais Magufuli aliongea maneno mengi ya kufurahisha wananchi wakati akizindua mradi wa barabara na maji.
Maneno ya Mama Bisimba kwa Rais Magufuli yanafikirisha, "Wananchi kwa kutoelewa wanaamini serikali inawapendelea kwa kuwapa maji na barabara, bila kujua huo ndiyo wajibu wa serikali iliyo madarakani na maji hayo yalipaswa kuwepo tangu mwaka 1961 tulipoanza kujitawala. Halafu mtu anatumia hiyo kama ngao ya kuwa ni mtendaji kuliko vyama vya upinzani ambavyo huo si wajibu wake hata kidogo".

Kwa tabia yake, Magufuli anaweza kuishiwa uvumilivu akajibu mapigo. Tusubiri wakati tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mama huwa simuelewi kabisa, yeye nadhani alishatangaza vita na serikali. Ndiyo ni haki yao kupata hiyo miradi lakini kama hakuna usimamizi makini hiyo miradi itakuwepo na kutekelezwa? Wakati Tundu Lissu anaongea maneno ya shombo kwamba Tanzania itengwe na jumuiya za kimataifa na kunyimwa misaada ya kibinadamu mbona hatukumuona huyo mama akikenua meno yake mabovu hayo kulaani kauli ya Tundu Lissu ila amekuwa mtu wa kumvizia Rais Magufuli kaongea nini ili aje na hoja kinzani. Tunajua hasira zake zimekuwa kubwa baada ya wa kaskazini kushindwa kwenye uchaguzi wa Rais 2015 na kwa kumthibitishia tu ni kwamba tuna imani kubwa na Rais wetu na 2020 tutamchagua tena kuendelea kuongoza Tanzania,kama vipi ajinyonge maana sisi watanzania ndo tunaochagua na si vinginevyo...!!
 
JF Kwenu,

Akiwa Kigoma, Mh. Rais Magufuli aliongea maneno mengi ya kufurahisha wananchi wakati akizindua mradi wa barabara na maji.
Maneno ya Mama Bisimba kwa Rais Magufuli yanafikirisha, "Wananchi kwa kutoelewa wanaamini serikali inawapendelea kwa kuwapa maji na barabara, bila kujua huo ndiyo wajibu wa serikali iliyo madarakani na maji hayo yalipaswa kuwepo tangu mwaka 1961 tulipoanza kujitawala. Halafu mtu anatumia hiyo kama ngao ya kuwa ni mtendaji kuliko vyama vya upinzani ambavyo huo si wajibu wake hata kidogo".

Kwa tabia yake, Magufuli anaweza kuishiwa uvumilivu akajibu mapigo. Tusubiri wakati tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mama ndio yule alievua nguo pale salenda bridge ? Ukivuo gagulo lako hadharani huezi kua mzima namimi huyo mama tayari kuchwani empte
 
Ccm wanatumia matatizo ya wananchi kama mtaji wa kisiasa.
Huduma za kijamii zote zinatakiwa zipatikane nchi nzima,hawataki kwasababu watakosa sababu ya kuombea kura.
 
Kama hasimamii kwa kukataza rushwa hayo maji mtayapata wapi? Umesema mwenyewe ni wajibu wa serikali, hujiulizi mbona miradi haikukamilika mpaka sasa na serikali ikiwepo? Mnachosahau kuwa serikali ni chombo kikubwa kinachojumuisha watu wenue bongo tofauti na kwamba serikali si chama cha siasa pekee. Wezi si wanasiasa tu bali hata watendaji wa serikali na wengine wako vyama pinzani. Yes, kasimamia vyema na watu wameogopa kupiga ni lazima apewe sifa. Nadhani ushanisoma.

Havome
Sasa anapowaambia wananchi waliochagua mbunge asiye wa CCM kwamba chama walichochagua ndicho kiwaletee maji au maendeleo mengine unadhani huyo kiongozi ana nia njema na watu wake au ana interest na chama chake kushika hatamu tu?
 
Tangu serikali hii ya maneno mengi kuliko vitendo iingie madarakani ni miradi gani imetekeleza zaidi ya kuzindua miradi ilifanywa na serikali ya awamu iliyopita, inayotuhumiwa kwa rushwa? Serikali hii ni ya maneno na mbwembwe nyingi, matendo ni sifuri. Wajinga wanaaminishwa kuwa inafanya na imetenda mengi. Yaorodhesheni tuyaone. Hakuna kikubwa kilichofanywa zaidi ya kutumbua kusiko na tija.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli. Waimba pambio waichukue hii challenge yako waorodheshe hiyo miradi iliyoanzisha na kukamilika ili sifa zimwendee kwa uhalali. wasisahau kuorodhesha na ile iliyoanzishwa na kufeli, au waliyoikuta wakaiua wenyewe.
 
Tangu serikali hii ya maneno mengi kuliko vitendo iingie madarakani ni miradi gani imetekeleza zaidi ya kuzindua miradi ilifanywa na serikali ya awamu iliyopita, inayotuhumiwa kwa rushwa? Serikali hii ni ya maneno na mbwembwe nyingi, matendo ni sifuri. Wajinga wanaaminishwa kuwa inafanya na imetenda mengi. Yaorodhesheni tuyaone. Hakuna kikubwa kilichofanywa zaidi ya kutumbua kusiko na tija.

Sent using Jamii Forums mobile app

Yaelekea haupo Tanzania wewe....................... imefanya mengi sana mno
1. watu wengi hawana kazi kwa namna moja ama nyingine
2. Tumbua tumbua asbh saaa sita na mchana
3. kuaminisha watu yeye ndio Alfa na Omega
4 . Hatuelewi kesho ataamka na neno gani
5. Vi-wonder vipo kila baraza
 
Kama hasimamii kwa kukataza rushwa hayo maji mtayapata wapi? Umesema mwenyewe ni wajibu wa serikali, hujiulizi mbona miradi haikukamilika mpaka sasa na serikali ikiwepo? Mnachosahau kuwa serikali ni chombo kikubwa kinachojumuisha watu wenue bongo tofauti na kwamba serikali si chama cha siasa pekee. Wezi si wanasiasa tu bali hata watendaji wa serikali na wengine wako vyama pinzani. Yes, kasimamia vyema na watu wameogopa kupiga ni lazima apewe sifa. Nadhani ushanisoma.

Havome
Ni sawa na wizi ndani ya familia kuzibitiwa na msimamizi wa mirathi anayrtoka ktk familia ya majizi yaleyale je tutaaminije kama kadhibiti ikiwa wale wenye kuidhinisha matumizi ya fedha hawana mamlaka juu ya udhibit wa fedha? Au ni njia ingine ya wizi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KIJO BI SIMBA NI MWANASIASA WA UPINZANI

Na Thadei Ole Mushi.

[HASHTAG]#Wakati[/HASHTAG] Mh Kikwete akiwa Raisi Mama Helen Kijo-Bisimba aliwahi kuandika mabango na kutembea nayo karibu Dar yote akimlazimisha Kikwete kuwavua madaraka mawaziri wake akiwemo waziri wa Afya.

Bi Kijo alifanya hivyo wakati mauaji ya kutisha yakiwa yanafanyika huku Mwanza. Hoja hii ya kuwasimamisha mawaziri iliibuliwa bungeni na upinzani kipindi cha sakata la mawaziri mzigo.

[HASHTAG]#Jana[/HASHTAG] tena katoa tamko la kukosoa Hotuba ya Rais Huko kigoma. Ni sahihi kabisa kwa alichokiongea na ni haki yake kuongea alivyoongea kuhusu Serikali kuhudumia wananchi wote bila ubaguzi wa kisiasa. Kwa mara nyingine anatoa tamko huku akiwa kimya kuhusu mauaji ya kibiti. Sikumsikia pia akitoa Tamko kuhusu Mnyika aliposema mauaji ya kibiti yataenea maeneo mengine. Hapa ndipo napouona unafki mkubwa Bi Simba. Hakuna hata siku moja amewahi kuukosoa upinzani wa nchi hii...

Hii ni mara nyingine watanzania wanahoji nini hasa kazi ya kituo hiki cha haki za binadamu?? Inawezekana malengo ya kituo hiki ni mazuri kabisa tatizo lipo kwenye itikadi na mapenzi aliyonayo mama kijo Bi simba na siasa za Upinzani.

Ni wakati sasa mama Kijo kuachia nafasi aliyonayo na kupewa kadi ya chama cha upinzani maana kwa kaliba yake Fitna za siasa anaziweza zaidi kukiko fitna za kutetea haki za wanyonge.Huyu anafaa kuwa mwenyekiti wa Bawacha zaidi kuliko hapo alipo.

Ole Mushi
 
nadhani kuna wakati hawajisifu kwa kutekeleza wajibu wao ila angalau kwa kuwa na utashi wa kisiasa kuweza kuwahudumiwa wananchi.
 
JF Kwenu,

Akiwa Kigoma, Mh. Rais Magufuli aliongea maneno mengi ya kufurahisha wananchi wakati akizindua mradi wa barabara na maji.
Maneno ya Mama Bisimba kwa Rais Magufuli yanafikirisha, "Wananchi kwa kutoelewa wanaamini serikali inawapendelea kwa kuwapa maji na barabara, bila kujua huo ndiyo wajibu wa serikali iliyo madarakani na maji hayo yalipaswa kuwepo tangu mwaka 1961 tulipoanza kujitawala. Halafu mtu anatumia hiyo kama ngao ya kuwa ni mtendaji kuliko vyama vya upinzani ambavyo huo si wajibu wake hata kidogo".

Kwa tabia yake, Magufuli anaweza kuishiwa uvumilivu akajibu mapigo. Tusubiri wakati tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee
Hii ndo Tanzania
 
Back
Top Bottom