Kama ni kweli utashangaa jinsi watakavyotengeneza hoja kwanini wao wanastahili kuongezewa hivyo lakini hoja hizo hizo zikipelekwa kwa wengine wataruka...
Mshahara wa wabunge umepanda kutoka Tsh 6,000,000/- kwa mwezi mpaka Tsh 10,000,000/- kwa mwezi mbali na marupurupu mengine!..
Hii inakuja ikiwa wadaktari tayari wameshatangaza mgogoro na serikali na kuipa wiki 2 kutimiza madai yao la sivyo watatangaza mgomo mkubwa nchi nzima kuanzia 23/6/2012...
Source: Mtanzania ya leo
"Hatuwezi kutatua matatizo kwa akili ile ile ambayo ilisababisha yawepo"..Mch. Peter Msigwa
Mshahara wa wabunge umepanda kutoka Tsh 6,000,000/- kwa mwezi mpaka Tsh 10,000,000/- kwa mwezi mbali na marupurupu mengine!....
Najuta Kusomea fani isiyolipa kwa mgomo, mimi Dr. wa Mifugo nikigoma nani atanisikiliza? Haki ya nani na mimi ningegoma kabisa! Maana huu upumbavu sasa!!!! Kiongozi wetu yule dhaifu anawajibu kunya madaktari lakini anaachia huu upumbavu unapita? Ama kweli TZ ni zaidi ya uijuavyo!!!
Ma-TUCTA nayo yanatudanganya na migomo ya watumishi kumbe kelele za chura Nyamba...ff!!!
Zomba ni kweli, wabunge wanachota millioni 10 kwa mwezi sasa...Halafu inashangaza sisi wananchi tunaendelea kupiga makelele CCM Oyee, Chadema Oyee, CUF Oyee wakati hawa watu hakika hawana maana kabisa wala Uzalendo rohoni mwao wakiendesha hoja bungeni za mgomo, Dr.Ulimboka, Muungano na madudu mengine kutupoteza sisi wananchi kuelewa kilichofanyika..Unataka hata mada za uongo tuchangie?
Una uhakika wa mshahara huo wa millioni 10 au unayakinisha udaku?