Mshahara wa wabunge wapanda mpaka 11,000,000/-

kwa mtindo huu itabidi sisi wa laki na 70 tuwe na nyumba ndogo ambazo ni mabinti wa wabunge ili kuzifaidi hizo 15m
 
Mnyika na Zitto tunaomba m-confirm hii habari? Au na nyinyi mmejiunga na manyang'au?!
 
Maji Marefu darasa La Saba > Mshahara million 15
Daktari Chuo Kikuu Miaka 5 > Laki 6.
 
sekta ipi????labda ya wauza matunda
mkuu mi mkulima wa mchele Bajabiri na fanya mgomo wa kuzalisha mpaka gunia moja liwe laki 5 , sasa kama nyie walimu hamgomi ili mlipwe milion 7 shauri yune, mi nsha likisha kuwa na sisi wakulima tunataka gunia la mpunga liwe laki 5 , lazima tugawane umaskini
 
Last edited by a moderator:
Mnyika na Zitto tunaomba m-confirm hii habari? Au na nyinyi mmejiunga na manyang'au?!

Ifikapo masuala ya mshahara, ni vigumu kusikia neno la mbunge. Si hao uliowataja wala wengine!

Je ni kweli kuwa mishahara yao imeongezwa? Hilo lawezekana manake niliwahi kusikia wakidai posho ya 150,000/= kwa siku haiwatoshi lakini walimu wanalipwa mshahara huo kwa mwezi.

Wabunge wetu ni wachumia tumbo kama wengine wote na ukweli huu uonekana pale wanapojadili masilahi ya wabunge!

 
nangoja watangaze ili na mimi nianze mgomo

Najuta Kusomea fani isiyolipa kwa mgomo, mimi Dr. wa Mifugo nikigoma nani atanisikiliza? Haki ya nani na mimi ningegoma kabisa! Maana huu upumbavu sasa!!!! Kiongozi wetu yule dhaifu anawajibu kunya madaktari lakini anaachia huu upumbavu unapita? Ama kweli TZ ni zaidi ya uijuavyo!!!

Ma-TUCTA nayo yanatudanganya na migomo ya watumishi kumbe kelele za chura Nyamba...ff!!!
 
Wanastahili, wanafanya kazi kubwa sana hawa wawakilishi wetu.

Bravo serikali kwa hilo. Angalau sasa wanakaribia kufanana wabunge wenzao wa EAC.

Hata hivyo wabunge wetu wanapunjwa sana. Yaani kamshahara ka tumilioni 15 tu?! wanastahili angalau milioni 75 kwa mwezi.
 
Wanastahili, wanafanya kazi kubwa sana hawa wawakilishi wetu.

Bravo serikali kwa hilo. Angalau sasa wanakaribia kufanana wabunge wenzao wa EAC.

Ngoromiko, naamini kabisa wewe ni Mbunge na una maslahi ktk hili. Hapa ni ule msemo: "scratch my back and I will scratch yours."
Sasa waongezewe kama wenzao wa EAC, mbona kwa Madaktari haiangaliwi majirani wanawalipaje?
 
Kutoka 7.5 Million to 15 Million.


Asiyetaka anacha.


Shahidi mimi mwenyewe.
mi ningependekeza kufanyike standardization ya mishahara ndani ya serikali na idara zake kwa kutumia kigezo cha elimu hii iwe pamoja na bunge.

Mbunge mwenye elimu ya form four basi apate mshahara ngazi ya Mwalimu wa shule ya msingi and so on

Lakini kwa sasa Daktari wa Binadamu (Dr. of Medicine) kuzidiwa mshahara na Dereva wa BOT - Hili ni tatizo kubwa mno.
 
Mshahara wa wabunge umepanda kutoka Tsh 6,000,000/- kwa mwezi mpaka Tsh 10,000,000/- kwa mwezi mbali na marupurupu mengine!..

Hii inakuja ikiwa wadaktari tayari wameshatangaza mgogoro na serikali na kuipa wiki 2 kutimiza madai yao la sivyo watatangaza mgomo mkubwa nchi nzima kuanzia 23/6/2012...


acha ujuha wewe...hiyo kauli ya hatuwezi kutatua matatizo ni kauli ya albert einstein siyo ya huyo mchungaji wako
Source: Mtanzania ya leo

"Hatuwezi kutatua matatizo kwa akili ile ile ambayo ilisababisha yawepo"..Mch. Peter Msigwa

acha ujuha wewe ni albert einstein ndiye aliyesema hiyo kauli si msigwa
 
Wana JF hiyo ni ujinga sana. WaBUNGE wana hela yakuongeza ila Madaktari ni mzozo sio ???
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom