Mshahara wa wabunge wapanda mpaka 11,000,000/-

Mshahara wa wabunge wapanda mpaka 11,000,000/-

Mods tafadhali wekeni taarifa hii rasmi ambayo imetoka gazeti la mwananchi kuhusu nyongeza ya mafao:

Wabunge wazidi kuongezewa marupurupu:Monday, 30 July 2012 11:25Boniface Meena, Dodoma

MARUPURUPU ya wabunge ikiwamo mishahara imeongezwa kutoka Sh7.4 milioni kwa mwezi hadi takriban Sh11milioni kwa mwezi, hatua ambayo imeibua mjadala mwingine mzito miongoni mwao.

Tangu mwaka jana, wabunge wamekuwa katika vita ya kupokea au kutopokea posho ya vikao ambayo imekuwa ikikolezwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ambaye alizikataa akisema mbunge anapokuwa kazini hahitaji kulipwa.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba sasa vita kubwa ipo katika marupurupu mapya ambayo pamoja na kuchanganya na mshahara yanafikia Sh11milioni kwa mwezi.

Spika wa Bunge, Anne Makinda alipoulizwa jana alithibitisha kuhusu kuongezeka kwa malipo jumla ya wabunge kwa mwezi lakini akasema hafahamu kiwango halisi kilichoongezwa. Makinda alisema nyongeza iliyopo siyo kwa wabunge tu, bali watumishi wote wa Serikali na ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), wakati wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2012/13.

"Hiyo nyongeza siyo tu kwa wabunge, bali ni kwa watumishi wa Serikali. Tena hiyo ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma). Sasa ukiniuliza kiasi gani hapo ndipo sielewei, ila najua nyongeza ipo," alisema Spika. Lakini, vyanzo kutoka ndani ya Bunge vilisema kwamba nyongeza hiyo ambayo tayari imeingia katika mshahara wa Julai ni Sh3.6milioni, hivyo kufanya jumla ya fedha anazochukua mbunge kufikia kiasi hicho cha Sh11milioni.

"Hiyo ni vita, kuna wabunge wana hasira kweli hawataki wananchi wajue kama marupurupu yameongezeka. Wanaona wananchi wakijua itakuwa ni tatizo kubwa, watapigiwa kelele lakini nyongeza hiyo ipo. Tayari wengine wamechukua tangu Ijumaa," kilisema chanzo kimoja kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi ya wabunge kutoka kundi la wanaopinga posho kwa wabunge wamepinga pia nyongeza hiyo wakitaka fedha hizo zielekezwe katika sekta nyingine za kijamii.

Marupuru ya sasa

Hadi mwezi uliopita, mbunge alikuwa akipokea Sh7.4milioni kwa mwezi ambazo kati ya hizo Sh2.5milioni ni kwa ajili ya mafuta, Sh2.3 mshahara, Sh170,000 kwa ajili ya mshahara wa dereva, 100,000 kwa ajili ya katibu wa mbunge na posho ya jimbo.
Hata hivyo, katika nyongeza hiyo ya sasa haijawekwa wazi kwamba kiasi gani ni kwa ajili ya mshahara, fedha za mafuta ya gari la mbunge, za dereva, katibu na za posho ya jimbo na tayari baadhi ya wabunge wameanza kufuatilia mchanganuo wa nyongeza hiyo.[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Kwa hiyo waalimu wanataka fedha ndogo tu sasa tunafanya nini?
hii mambo inatakiwa tuiangalie vizuri maana ni ngumu saa
 
Mshahara siyo Sh10 milioni ni Sh11 milioni...mods bana.
 
Kasungura kenyewe kadogo Wacha wakubwa washibe kwanza. Hahaha Mimi naandamana rohoni niungeni mkono jamani....
 
Ningekuwa Dodoma ningerusha mawe bungeni. Kwa kuwa niko mbali na Dodoma nitarusha mawe kwenye 'screen' nikiamini yatakuwa yamewapata wabunge. Katika maswala ya mishahara na posho zao sibagui kati ya magamba na wapinzani.
 
Kwa hisabati ya haraka haraka,hizo millioni 10 kuzidishi na idadi ya wabunge wote unapata shiling ngapi kwa mwezi?Pia naomba anayejua mishahara ya ndugu zetu wawakilishi wa bunge lao anijuze.
 
sasa mnalalamika nini???
solution musiwapigie kura tu, lakini kila kukicha mnapigia kampeni vyama vyenu vya siasa na kuwasifia mie nataka wapeane milioni mia kwa siku si washapata mijinga.
 
kwa kiwango hiki HAFIFU cha mwamko wa watanzania acha wabunge wajipangie hadi sh. Bilioni 2 kwa mwezi, sio mbaya.
ALIYELALA USIMWAMSHE.
UJINGA GHARAMA.
 
Scale ya mshahara LSS(P) 2 Ndo shilingi ngapi wadau? Elimu gani inatakiwa ili tucompee na TGS scales wanazolipwa wavuja jasho yet wasomi huko serikalini?
 
Wabunge ndo watetezi wetu ila ndo wala rushwa wakubwa, je tukimbilie wapi?
 
Umeendaa timu ya kujibu matusi?

Nikutie moyo rafiki yangu, Job hatukani tena lakini akija kujaribu kutukan plz ntaarifu nafahamu madudu yake kibao,tutahakikisha anajidhalilisha mwenyewe na jimbo tunamnyag'anya, au vipi mkuu!

Kwa upande wa maposho: Haijalishi kama ni mshahara pa1 na maposhoposho bt generally huu mpunga ni kufuru kwa hali iliyopo ktkt bongo jamani daah! Ukiangalia maisha ya mtz alomchagua huyo mbunge utaona huruma alivyozingirwa na songombingo:Akisogeza pua yake hospital angongwa,akipeleka mwanae kuanza std one anapigwa na mchango wa madawati,hajakaa sawa anadaiwa mchango wa kujenga shule mpya,hajakaa sawa analanguliwa mazao yake kwa soko holela la undefined kipimo aka debe,bakuli sado,lumbesa nk. Sasa waheshimiwa hamjui kuwa huyu mtz siku moja atachukua kwa nguvu hivyo mnavyojilimikzia? Hatokuja kwamba eti utamdhibiti tutakusanyana wakeshahoi wote na kukutaarifu kuwa tumefuata vyetu na kila mmoja atachukua kitachomfaa na tutamtembelea kila tunayeamini kapata mali kiujanjaujanja akiwa madarakani.
 
Mshahara wa wabunge umepanda kutoka Tsh 6,000,000/- kwa mwezi mpaka Tsh 10,000,000/- kwa mwezi mbali na marupurupu mengine!..

Hii inakuja ikiwa wadaktari tayari wameshatangaza mgogoro na serikali na kuipa wiki 2 kutimiza madai yao la sivyo watatangaza mgomo mkubwa nchi nzima kuanzia 23/6/2012...

Source: Mtanzania ya leo

"Hatuwezi kutatua matatizo kwa akili ile ile ambayo ilisababisha yawepo"..Mch. Peter Msigwa


[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Mwalimu na mbuge nani muhumu, Daktari je.
 
Hivi wanaongezwa hii pesa kwa kazi gani wanazofanya??
Tunawatuma kutuwakilisha Bungeni hakuna wanachofanya
Masaa yote ni kusinzia Bungeni,Kufuta vumbi kwenye viatu
Kupiga story za Udaku
Mbona walimu wanaowatoa ujinga hamtaki kuwaongezea hela ?
Mbona madaktari hamtaki kuwasikiliza
Na pesa Zetu za Mafao mnataka kuchukua kwa nguvu
Hivi tuwafanye nini Nyie..?
 
Wajameni jana nimeona ripoti ya mafao ya Wabunge kupanda toka milioni 9 mpaka milioni 11! Cha ajabu leo asubuhi siioni hiyo habari! kwa nini imefutwa naomba kuuliza
 
Sasa jiulize hela zinatoka wapi wakati walimu na madaktari wameambiwa serikali haina hela
 
Kuna tetesi kwamba posho na mishahara wa wabunge imeongezeka, taarifa ni kwamba mishahara ya wabunge sasa itakuwa around 11 million kwa mwezi.

Follower mmoja wa Zitto alianza kwa kumuuliza mhehimiwa, check haya maongezi yao

@wema4life: Mheshimiwa naskia mshahara wenu wabunge saivi ni 11.4m per month hizo habari ni za ukweli au uzushi?
@zittokabwe: Sitaki balaa

@wema4life: na posho kwa siku 350,000, tuwekee bayana mkuu."
@zittokabwe: Nimesema sitasema lolote kuhusu posho wala mishahara mipya

@wema4life: funguka kiongozi, sifa yako mojawapo ni ukweli daima...." .
@zittokabwe:Usiniletee balaa, Huko kusema kweli ndio watu hawapendi

@iLashayo: kwanini Mh?Hii hoja ya #Posho ni yako.Unafaa kuiongelea tuone msimamo wako mpaka mwisho"
@zittokabwe: mnielewe pls


MyTake:

  1. Zitto ni mwanasiasa ninaemwamini, i hope and pray kwamba yote yanayosemwa dhidi yake yawe si kweli na yathibitike hivyo, ikiwa tofauti, nitakua nimevunjwa moyo sana, Zitto atakua kani-let down big time.
  2. Baada ya haya yote ni lazima Zitto anapitia wakati mgumu sana, while i fully understand his position not to talk about mishahara na posho, natamani haya mambo yaishe, natamani nijue msimamo wake kuhusu hii mishahara minono na ma-posho makubwa. Kama kweli ataamua kukaa kimya kwa sababu ya haya mambo, na kama kweli haya mambo ni ya kuzusha tu, basi hawa mafisadi wana nguvu sana, wameweza kumnyamazisha zitto
 
Back
Top Bottom